Usulumo lunulo, lulolile nimo uyo gulindamu ugugutumama mpaga gushila. Ubhudamu bhogo bhuli guti bho chuma. Unimo gunuyo gugabhanojaga noyi abhatumami bhago. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagaguyombaga giki, “ikola guti lya chuma.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali ndamu ugwelelwa imihayo iyo alilangwa na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adaidebhaga wangu imihayo iyo bhalinhanga abhanhu, kunguno ya gwikala aliganika hinghu jingi ahikanza agulangagwa henaho. Uweyi agadumaga nulu uguyibheja chiza ikaya yakwe, kunguno ya gubhiza adaimanile imihayo ya gubhalela chiza abhanhu bhakwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nimo uyo gulindamu ugugutumama, kunguno nuweyi alindamu ugwelelwa imihayo iyo alilangwa na bhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ikola guti lya chuma.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilila bho guitumama chiza imilimo yabho, imukikalile kabho, kugiki bhadule gupandika mafumilo mingi, umuwikaji bhobho.
Zaburi 14:1.
Wakolosai 3:25.
1Petro 1:17.
KISWAHILI: CHUKIZO KAMA LA CHUMA.
Methali hiyo, yaangalia kazi ile ambayo ni ngumu kuitekeleza mpaka kuimaliza. Ugumu wake ni kama wa chuma. Kazi hiyo, huwachosha sana watekelezaji wake. Ndiyo maana watu huisema kwamba ni “chukizo kama la chuma.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mgumu wa kuelewa kile anachofundishwa na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa haelewi upesi maneno anayofundishwa na watu, kwa sababu ya yeye kuwa anafikiria vitu vingine wakati akifundishwa. Yeye hushindwa hata kuendeleza vizuri familia yake, kwa sababu ya kukosa malezi ya kuwafundisha watu wake.
Mtu huyo, hufanana na kazi ile ambayo ni ngumu kuitekeleza, kwa sababu naye ni mgumu wa kuelewa upesi kile anachofundishwa na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu, humwambia kwamba ni “chukizo kama la chuma.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuwawezesha kuyatekeleza vizuri majukumu yao, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.
Zaburi 14:1.
Wakolosai 3:25.
1Petro 1:17.
ENGLISH: AN ABOMINATION LIKE THAT OF AN IRON.
This proverb looks at a task that is difficult to accomplish as it required. Its hardness is like that of an iron. Such task exhausts its performers. That is why people call it “an abomination like that of an iron.”
The above proverb is likened to a person who has a hard time in understanding what others teach him/her in life. This person does not immediately understand words which he/she is taught by people, because of thinking other things during the teaching time. He/she fails to provide the family with basic needs because of his/her hardness to understand what others teach him/her.
Such a person is like a job that is difficult to complete in doing it, because it is difficult for him or her to understand quickly what he or she is learning from his or her people. That is why people say that it is “an abomination like that of an iron.”
This proverb teaches people about having patience that can enable them to fulfill their responsibilities, in their lives, so that they can have more success, in their lives.
Psalm 14: 1.
Colossians 3:25.
1 Peter 1:17.