109. NYANG’WANGU

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Olaliho ngikulu bhulima, lina lyakwe Nyang’wangu. Wikalaga na ng’wana okwe umo, ngosha wikalaga na kalambo ku nsago ha bhulili b’okwe. Kuhayumanila, Nyang’wangu wapandika liganiko lya kuntoja ng’witunja okwe.

Aho ng’winga wagabhuka (kwinga ha kaya na kwiza kwigasha ha ng’wa nina bhuko) na nina bhuko ubhi ali nikub’i ung’winha bhuli dilu ndilo ndoto ilipalagana. Ng’winga agayukumya ulu winhiwa indilo ndoto bhuli dilu ku nguno yalitiho nyanza nulu mongo.

Wibhuja bhuja giki, “uyo wafunya hali ndilo indoto na hangi Nyanza ili kule giko! Lushiku lumo, ngikulu ung’winha ndiko ibhili, ung’winga wandya kukobha hose uko jikafumilaga indilo.

Ulinha ku kano ugayiwa, wingila ng’wifuma ugayiwa, ukundula hiwe lya gushela, ugayiwa, nose ushika ha bhulili. Wahaya ukundula ku nsago, usanga kaliho kalambo. Ndilo jilidamka ningi duhu. Jilib’inab’inila, huna ujishoshaho ijo wali winhagwa, ujisola mhya mo nhale ibhili, ulu alita giko akagikulu kalimana  uku walwa isho alita ukunu kaya.

Ngikulu winga lulu uku walwa. Wiza ushikila kumuja ung’winga okwe, “iki b’uli mayu wanitilaga giko? Nakub’onaga walinhaga kukano yane, nakub’onaga wingila ng’wifuma lyane, nakub’onaga wakundulaga na hiwe lyane na mhayo ndimu gete gete, wadimaga ku nsago gwane? Umu yeniyo nali natali kukwinha shikilo shane, kwinama hiwe lyane lya kushela sha kupinda uku mbele yane bhuli bhuhubhi wingi, iki bhuli wanitilaga giko?” Ng’winga ali sele duhu. uNgikulu gashi okolagwa noi. Atalile shiliwa  isho wazugaga ung’winga.

Nose ubhujiku wila, bhose bhulala. Bhujiku hagati, ngikulu uja hose ha bhulili, ubhucha shikolo shakwe shose, usama guja kulugulu. Ukingila muli shiganga na lishiganga lyenilo lyupilingita kwinga mu lugulu. Liza lyub’itila aha numba ya ng’witunja na ng’winga okwe. Lyubhatobhagula. Bhucha pye. Iwe lyukimila ku mbuga. Na iwe liliho mpaga lelo. Lili hagati ya minzi ku nguno nyanza ikatulwa hagati. Lilitanwa “Nyang’wangu”

Bhubhi bhukafumaga ku bhise bhenekili giko!

KISWAHILI: NYANG’WANGU

Alikuwepo bibi kizee Bulima, jina lake aliitwa Nyang’wangu. Alikuwa na mtoto wake mmoja, mwanamume. Alikuwa na kadimbwi kwenye mto wa kulalila kichwani kwenye kitanda chake. Kushitukia, Nyang’wangu, akapata wazo la kumuoza kijana wake.

Alipoamka mkaa mwana wake (kutoka kwenye familia na kuja kukaa kwa mama mkwe wake) na mama mkwe akawa na huruma ya ukarimu kwa mkaa mwana wake, akawa akimpa kila asubuhi samaki mbichi alirukaruka. Mkaa mwana alishangaa alipopewa samaki wabichi kila asubuhi kwa sababu haikuwepo baharí wala mto karibu nao.

Akajiuliza uliza hivi, “huyu ametoa wapi samaki wabichi na baharí ilikuwa mbali hivyo?” Siku moja, bibi kizee alimpa samaki wawili, mkaa mwana alianza kutafuta pote pale wanapotolewa hao samaki.

Alipanda kwenye dari, akakosa, akaingia sehemu nyingine aliyoidhania kuwepo hao hapo, akakosa, akafungua kwenye jiwe la kusagia, akakosa, mwishowe akafika kwenye kitanda. Alipofungua kwenye mto, akakuta kapo kadimbwi. Samaki wanaruka wengi tu. Wanacheza cheza, ndipo aliwarudisha humo wale samaki wawili, aliokuwa nao, akachukua wale wakubwa wawili. Alipokuwa akifanya hivyo, kabibi kizee kalifahamu kakiwa kule kwenye pombe, alichokuwa anakifanya kule nyumbani.

Basi, bibi kizee aliondoka kutoka kwenye pombe. Akaja kufikia kumuuliza mkaa mwana wake, “kwa nini, mama umenifanyia hivyo? Nimekuona ulipanda kwenye dari yangu, ukaingia kwenye sehemu yangu maalumu, ukafunua kwenye jiwe langu, na neno gumu kabisa kabisa, ukashika kwenye mto wangu?

Kwa hiyo, bado sijakupa maagizo yangu, kuinama kwenye jiwe langu la kusagia, na kupita kwenye sehemu yangu maalumu, ni kukosa kwingi, kwa nini umenifanyia hivyo?” Mkaa mwana alikuwa kimya tu. Kumbe kale ka bibi kizee kalikuwa kamekasilika mno. Hakakula chakula alichopika mkaa mwana wake.

Mwishoni, usiku ulipoingia, wote wakalala. Kwenye usiku wa manane, bibi kizee alienda kwenye kitanda, akabeba vitu vyake vyote, akahama akaenda kwenye milima.

Akaenda kuingia kwenye mwamba na ule mwamba ukavilingika kutoka kwenye miamba mlimani. Ukaja kuipitia ile nyumba ya kijana wake na mkaa mwana wake.

Ukawabonda bonda wakafa wote. Mwamba ukaenda kusimama mbugani. Mwamba huo, bado upo hadi leo. Uko kati kati ya maji kwa sababu, baharí iliwekwe katikati. Unaitwa, “Nyang’wangu.” Hivyo, ubaya huwa unatoka kwetu sisi wenyewe namna hiyo!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s