84. Bhusimbi bho Lwinzi- Lung’wando na Ndimu

Collected by: Don Sybertz,  

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Aho Kale, jaliho ndimu ningi. Imo yajo yali Lung’wando. Bhasi, bhagiigwa gusimba lwinzi la minzi. Aho bhandya ugusimba ulwinzi, Ulung’wando uhaya, “Bhabehi, igwigelelwa dulombe giki mbula ipandike gutula. Ulu idishena igubhiza bhule.” Ibhujiku Ulung’wando wiza agwimbaga;

“Oo ndemle bhamayu ndemle,” “Oo ndemle Lung’wando Lung’wando aliza.” Agahodisha aho lwinzi, alihaya, “Hodii.”

Lidakulile ikanza Ulung’wando wingila umuminzi, wandya goga. Aho omala, unya mashi mumo. Uja lokwe. Intondo yaho bhagasanga mashi umu lwinzi.

Bhiyangula guntuula mnambiti ubhiza nindi o lwinzi lwobho. Ubhujiku Ulung’wando agashika hangi na kunu alimba lwimbo lwakwe lwenilo. Agahodisha, Mbiti agatima tochi na kubhuja, “Bhebhe uli nani?” “Nene aha!”

“Bhebhe uli lung’wando idishene?” “Ehee, jiliho ki?” “Bhebhe lung’wando huna uyo agubhipyaga a minzi gise, enh?”

Ulung’wando agashosha, “Iiii! Unene nadagamanile aminzi ging’we. Unene ninaminzi gane ayo galimasoga noi. Dujage nagagwinhe!”

Imbiti yuhaya, “Haya dujage.” Bhasi, ulung’wando na mbiti bhuja.

Aho bhashika aha lwande fulani ulung’wando ung’wila umnambiti, “Nahene, ubhebhe ikalaga aha si, unene nalinhe ng’wigulwa.”

Ulung’wando agandya kung’wikija. Inhalikilo, mbiti agiyibha, wandya kuntunga lugoye. Aho omala ugwita chiniko, Ulung’wando agiponeja mugati ya lwinzi lwobho, wandya goga. Aho omala goga, unya mashi, na kuja lokwe. Intondo yaho diyu, bhagibhuja, “Ng’wigisu ojaga hei?”

Imbiti yushosha, “Naliho kunu bhabehi, natungagwa lugoye na lung’wando!” Ulushigu ulo lugafuada, bhuntuula grumati giki alinde ulwinzi lwobho.

Bhung’winha bhulangeti na tochi. Bhujiku ulung’wando agashiga na gatolo/gajisabho ako kina bhuki na kunu aliimba lyimbo lwakwe linilo. Aho omala ugupiga ihodi, grumati agikala sele.

Ulung’wando agingila na gwigasha hahigula ya ng’wa grumati. Aho grumati wibhakila, agabhuja, “Ulinani ubhebhe? “Nali nene Lung’wando!” “Ahaa! Gashanaga nu bhebhe lung’wando!”

Aheneho grumati ufula mhembe. Ndimu pye jiza na mapanga. Uluwang’wando agabhawila, “Unene nadadulile gubhulagwa na mapanga.” Bhasi ndimu jigantunga lugoye umnalung’wando na guntuma gujila moto.

Aho lidakulile ikanza, ingoye ijo bhalibhantungila jutinika, na lung’wando agatoloka na gwandya gupela ukunu aliimba.

Lung’wando kanyama kadoo, aliyo kanyama kabhalaganu,

Ulung’wando kanyama kadoo, aliyo kanyaga kabhalaganu.

 Kiswahili: Uchimbaji Wa Kisima-Sungura Na Wanyama

Hapo zamani, kulikuwa na wanyama wengi. Mmoja wa wanyama hao alikuwa Sungura. Basi walikubaliana kuchimba kisima cha maji. Walipoanza kuchimba kisima, Sungura akasema, “Jamani, itafaa tuombe ili mvua ipate kunyesha. Vinginevyo itakuwa ni bure.” Usiku Sungura akaja akiimba;

“Oo ndemle wakina mama ndemle,

“Oo ndemle Sungura Sungura anakuja.”

Akapiga hodi pale kisimani, akisema, “Hodii!”

Mara Sungura akaingia katika kisima, akaanza kuoga, alipomaliza, akanya mavi humo humo. Akaenda zake. Kesho yake walikuta mavi katika kisima. Wakaamua kumweka Fisi kuwa mlinzi wa kisima chao. Usiku Sungura alifika tena na huku akiimba wimbo wake ule ule. Alipobisha hodi, Fisi akamulika tochi na kuuliza, “Wewe ni nani?”

“Mimi hapa!”

“Wewe ni Sungura sivyo?”

“Ndiyo, kulikoni?”

“Wewe Sungura ndiye unayechafua maji yetu, enh?”

Sungura akajibu, “Iiii! Mimi sichezei maji yenu. Mimi nina maji yangu ambayo ni safi sana. Twende nikakupe!”

Fisi akasema, “Haya twende.” Basi, Sungura na Fisi wakaenda. Walipofika mahali fulani Sungura akamwambia Fisi,  “Haya, wewe kaa chini na mimi nipande juu.”  Sungura akaanza kumdondoshea.

Mwisho, Fisi akajisahau, akaanza kumfunga kamba. Alipomaliza kufanya hayo, Sungura alijitumbukiza ndani ya kisima chao, akaanza kuoga. Kisha kuoga, akanya mavi, na akaenda zake. Kesho yake asubuhi, walijiuliza, “Mwenzetu amekwenda wapi?”

Fisi akajibu, “Niko huku jamani, nimefungwa kamba na Sungura!”  Siku iliyofuata, wakamweka Kobe ili alinde kisima chao. Walimkabidhi blanketi na tochi.

 Usiku Sungura akaja na kibuyu chenye asali na huku akiimba wimbo wake uleule. Baada ya kupiga hodi, Kobe akakaa kimya. Sungura akaingia na kukaa juu ya gamba la Kobe. Hapo Kobe akastuka, akauliza,  “Nani wewe?”

“Ni mimi Sungura!”

“Ahaa! Kumbe ni wewe Sungura!”

Hapo Kobe akapiga filimbi. Wanyama wote wakaja na mapanga. Sungura akawaambia, “Mimi siwezi kuuawa kwa mapanga.” Basi wanyama wakamfunga kamba Sungura na kumtupa kwenye moto. Mara kamba  walizomfunga zikakatika, na Sungura alichupa na kuanza kukimbia huku akiimba;

        “Sungura kanyama kadogo, lakini kanyama kajanja,

        “Sungura kanyama kadogo, lakini kanyama kajanja.

English: Drilling Of Wells – Rabbit And Animals

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.