78. Namhala Na Bhana Bhadatu

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho namhala walina bhana bhadatu bhagosha bhike. Lushiku lumo abhayanda bhuja gwipolu, unyanda undo bhalibhadantogagwa abhakuluye. Bhushika ung’wipolu bhuntunga halinti abhakuluye bhunyamka kaya.

Bhuneka guko unzuna wabo. Yagashika mhindi ingoye ijo agatungilwa juma, unyanda ujitina.

Walala mumo ng’wipolu bhogela lyabhiza isana nyanda ulibhona iyoka liduma gete, aliyo liliteng’wa Inanda, nyanda ubhona jisa, usola mawe uliluta ilinanda nzoka yupila.

Nzoka igalumba yung’wila unyanda linhaga aha ngongo gone duje uko duzengile ugamane. Nyanda ulinha ha ngongo gwa Nzoka bhuja mpaga uko izengile inzoka. Nyanda usanga mayoka mingi gete, ‘Nzoka yubhawila abhichayo giki, “Nyanda uyu wanigunanaga, nandaguliwa na Nanda. Huguhaya dung’winhagi manong’ho.”

Nzoka pye ijose juzunya, haho na haho bhuli nzoka yuja mung’obho goyo na gufuma ilina manong’ho. Inzoka iyo agigunana yung’winha mhigi (ng’hilizi), nyanda uwilwa, “Ulu ulashike ha weja ugwilomba imhigi (ing’hilizi) ijo ulitogwa.”

Nyanda ushiminza ushika haweja wigasha uilomba imhigi (ihilizi) yung’winha manumba ga simenti mingi, yung’winha nkima, yung’winha bhanhu bhingi no, yung’winha sabho na ng’ombe ningi gete, ubhiza na kaya nhale.

Lushiku lumo ubheja lugendo uja kubhabyaji bhakwe ushika unsanga Ise nu Nina bhalihoya hakaya.

Bhabyaji bhagansung’wanha na bhuyegi bhutale. Bhagamuja waliwaja he ng’wana wise.” Nyanda ubhawila, “Nali natungilwa halinti na bhakulu bhane.” Bhabyaji bha nyanda bhagapinihala gete ikanza idoo unyanda wandya gufunya hela nyingi ja manoti, ise na nina bhumuja, “Alihela ningi giki ugafunya hali?” Nang’hwe ubhawila, “Unene nasabha no.”

Ubhinha Ise na Nina hela hanuma ubhabhuja ala abhakulu bhane bhaja hali? Bhung’wila bhagwiza duhu bhajaga kujuyela. Ikanza ido abhakuluye bhiza bhunsanga unzuna wabho alihoyi wizaga.

Ng’holo jabho bhogoha no nguno bhalibhamanile giki nzuna wabho wachila ng’wipolu, uko bhagantungila.

Nyanda agabhayegela no abhakuluye, ubhawila, “Duliho bhakulu bhane.” Agabhinha makono bhigisha na bhuyegi bhutale. Aliyo abhakuluye mnomo bhazongile. Imhindi hakikome ubhawila Ise na Nina kihamo na bhakuluye giki, “Dusamagi duje uko nazengile unene.”

Mungu akazidi kumpa baraka akawa na familia kubwa katika maisha yake na utajiri ukaongezeka maradufu.

Kiswahili: Mzee Na Watoto Watatu

Alikuwepo mzee aliyekuwa na watoto watatu wanaume wote. Siku moja Vijana hawa walienda porini. Kijana mdogo alikuwa hapendwi na kaka zake. Walipofika porini wakamfunga mdogo wao kwenye mti, kaka zake wakarudi nyumbani.

Walimuacha huko mdogo wao. Ilipofika jioni kamba zile alizofungwa zilikauka kijana akazikata.

Alilala humo porini. Kulipokucha kajua ka asubuhi kakaoneka, kijana akaona Joka kubwa kabisa. Lakini lilikuwa linakatwa na ndege mkubwa aina ya tai. Kijana aliona huruma. Akachukua mawe akampiga ndege yule, nyoka akapona.

Joka lile lilishukuru likamwambia kijana apande mgongoni mwa Joka waende kule linakoishi akapafahamu. Kijana alipanda mgongoni mwa Joka lile.

Wakaenda mpaka kule linakoishi lile Joka. Kijana alikuta majoka mengi kabisa. Lile Joka likawaambia wenzake hivi, “Kijana huyu amenisaidia, kidogo niliwe na ndege aina ya tai. Ndiyo kusema, tumpeni zawadi.”

Nyoka wote wakakubali. Hapo hapo kila nyoka akaenda kwenye shimo lake akatoka na zawadi. Joka lile alilolisaidia likampa hirizi, likamwambia kijana, “Ukifika sehemu iliyowazi, utaiomba hirizi kile unachopenda.”

Kijana akatembea akafika mahali peupe akakaa akaiomba ile hirizi, ikampa majumba mengi yaliyojengwa kwa matofali ya sumenti, ikampa mwanamke, watu wengi mno, mali na ng’ombe wengi kabisa. Akawa na familia kubwa.

Siku moja alifunga safari kwenda kwa wazazi wake, akafika na kuwakuta Baba na Mama wakiongea  pale nyumbani.

Wazazi walimpokea kwa furaha kubwa sana. Wakamuuliza, “Ulikuwa umeenda wapi mtoto wetu?” Kijana akawaambia, “Nilikuwa nimefungwa kwenye mti na kaka zangu.”

Wazazi wa kijana walihudhunika kabisa, kwa muda mfupi kijana akaanza kutoa pesa nyingi za noti, Baba na Mama wakamuuliza, “Hela nyingi hivi umezipata wapi?” Naye akawaambia, “Mimi nimetajirika mno.”

Akawapa Baba na Mama hela baadaye akawauliza, “Kaka zangu wameenda wapi?” Wakamwambia, watakuja tu wameenda kutembea. Baada ya muda mfupi, kaka zake wakaja wakamkuta mdogo wao yupo amekuja.

Waliogopa sana mioyoni mwao kwa sababu walikuwa wanafahamu kwamba, mdogo wao alishakufa porini, kule walikomfunga.

Kijana akawachangamkia sana kaka zake, akawaambia, “Tupo kaka zangu.” Akawapa mkono kwa maana ya kuwashika mkono kwa furaha kubwa.

Lakini kaka zake wakawa midomo wazi huku wakihudhunika. Jioni kwenye sehemu ya kuongea wakiota moto, akawaambia Baba na Mama waende kule anakoishi. Akawa na familia kubwa katika maisha yake na utajiri wake ukaongezeka maradufu.

people-2

  English: An Elder And Three Children

three-children

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.