75. Jigano Ja ngoko Na Ng’hungulume

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Ikale gete muna ngoko na muna ng’hungulume bhali bhati bhana noni bha mukaya. Bhali bhana noni bha mumapolu abho bhigashaga kihamo na noni jingi ija mu mapolu.

Huna lulu, lushiku yutula mbula nhale kwipolu kwenuko. Muna ng’hanga ung’wila umuna ngoko, “Jaga ku makaya ga bhanhu abho bhalitanwa magulu abhili, na makono gabho galabhili, na miso abhili, ukalombe moto twize tupembe twote, nguno ulunyili lwatigwanya.

Muna ngoko uja aho washika kubhanhu, wanukulwa chiza no, bhumuja inguno yakwe. Nang’hwe uyomba, “Unene ndi munhu wa ng’wipolu, nizaga kulomba moto, nguno ukubhise kutiko umoto”.

Aho wayomba giko, bhamagulu abhili bhenabho bhatang’winhile umoto. Bhongeja kung’wanukula chiza, na kung’winha sha kulya. Nang’hwe ubhona giki, magulu abhili alina bhuyegi gete. Wiwila bhangi bhalitobhola tulo niyo ya limi. Magulu abhili atashokile numa ongeja kung’winha shakulya. Muna ngoko aho witilwa giko wib’a nose isho watumagwa.

Bhakwipolu aha bhanoga ukulindila, bhuntuma muna ng’hungulume anondeje. Muna ng’hungulume atalemile uja, aho washika wanukulwa chiza no, kitumo wali witilwa muna ngoko.

Aho wingila mukaya unsanga umuna ngoko aliyuminoga tulo. Kunu atumanaga mhayo gose gose. Muna ngoko umishiwa, aha wamisha muna ng’hungulume umuja, “Ni bhuli icheniki bhageshi, ni bhuli sele duhu?”

Muna ngoko ushosha, “Nene natushokaga hangi ukwipolu, nguno haho nizila magulu abhili alinitila chiza no, ali nashoke kwipolu kwita ki lulu?”

Wakanoga ung’wila hangi giki, “Ni nzu ulye ishiliwa ijo nashijaga bhageshi”. Muna ng’hungulume ulya. Nang’hwe utogwa no, uyomba na kuyornba, “Nunene natujaga ung’wipolu”.

Hi nguno yene muna ngoko ulu aling’wa minzi akalangamilaga ng’wigulya kunumbilija nsumbi uyo akabhenheleja bhiza ng’wa magulu abhili. Aliyo ubhutengeke bho ng’wa magulu abhili bhuliho, aliyo ikanza lingi bhutiho. Bhutina kongeja kubhutongi gete.

Sha lushiku lumo, bhiza bhageni henaho hakaya ya ng’wa magulu abhili. Bhulola bhubhona shiliho ishiliwa, lelo amakubhi nduhu. Huna lulu bhitambuja bhuyomba, “Tutina kukoya koya, nguno isho shikagunanaga munhu shakwe.

Ndimagi umuna ngoko tung’wite ikubhi lya bhageni bhise. Litakulile ikanza muna ngoko uding’wa, nang’hwe ulila, “Natineneee, natinenee”. Kwike atigwilwe usinzwa duhu.

Muna ng’hungulume aho wabhona giko uyoga, “Go go go ligokoo!” Makulu kaho giki, “Muna ngoko wanilemba lemba”. Muna ng’hanga nose unoga ukulindila.

Waganoga wiza hihi na hakaya ya ng’wa magulu abhili. Witanana, “Muna ngoko bhebheee! Nakuwilaga jilaga moto nang’ho uja malali. Aliyo atigwile shilaka isho shilishosha. Witanana hangi. Muna ng’hungulume ushosha, “Yakale itihooo!

Utizingila mu bhuluhi ubhu”. Muna ng’hanga aha wigwa giki bhatushokaga hangi uja ng’wipolu mpaga na lelo aliho guko.

Kiswahili: Hadithi Ya Kuku Na Jogoo

Zamani kuku na Jogoo hawakuwa ndege wa majumbani. Walikuwa ndege wa porini waliokaa pamoja na ndege wengine humo kwenye mapori.

Hivyo, siku moja ilinyesha mvua kubwa sana huko porini. Kanga alimwambia kuku, “Nenda kwenye majumba ya watu waitwao wa miguu miwili, na mikono yao miwili, na macho mawili, ukaombe moto tuje tuwashe kwa ajili ya kuota kwa sababu bariki hii inatutesa mno.

Kuku alienda alipofika kwa watu, walimpokea vizuri mno, wakamuuliza sababu yake ya kuwafikia. Naye akasema, “Mimi ni mtu wa porini, nimekuja kuomba moto, kwa sababu kwetu hakuna moto.”

Aliposema hivyo, hao wa miguu miwili hawakumpa ule moto. Waliongeza kumpokea vizuri kwa ukarimu, na kumpa chakula. Naye akaona kwamba, miguu miwili ana furaha kabisa.

Akasema moyoni, wengine wanakula usingizi tena mchana. Miguu miwili hakurudi nyuma, aliongeza chakula. Kuku alipofanyiwa hivyo, akasahau mishowe kile alichotumwa.

 Wale wa porini walipochoka kusubiri, wakamtuma jogoo amfuate. Jogoo hakukataa kwenda, alipofika walimpokea vizuri sana, kama walivyomfanyia kuku.

Alipoingia ndani alimkuta kuku akifurahia usingizi. Akiwa hajui neno lolote. Kuku aliamshwa. Alipoamka jogoo alimuuliza, “Ni kwa nini hivi jamani, kwa nini kimya tu?”

Kuku akajibu, “Mimi sirudi tena huko porini, kwa sababu tangia nije hapa miguu miwili ananifanyia vizuri mno. Nirudi huko porini kufanya nini basi?”

Mwishowe alimwambia tena kwamba, “Hebu njoo ule chakula kile nilichobakisha ndugu yangu.” Jogoo akala. Naye akapenda mno, akasema na kusema, “Na mimi siendi porini.”

Ndiyo sababu kuku anapokunywa maji hutazama juu kumshukuru Muumba aliyewapeleka hadi akafika kwa wa miguu miwili. Lakini wema wa wa miguu miwili upo, wakati mwingine haupo. Hauna kuongeza mbele kabisa.

Siku moja wakaja wageni hapo nyumbani mwa miguu miwili. Wakaangalia na kuona kuwa chakula kipo, lakini mboga hakuna. Ndipo wakashaulina wakasema, “Hatuna haja ya kuhangaika, kwa sababu kile kinachomsaidia mtu ni chake.”

Shikeni kuku tumfanye mboga ya wageni wetu. Haukupita mda mrefu kuku akashikwa, naye akalia, “Siyo mimiiii, siyo mimiiii.” Lakini hakusikilizwa alichinjwa tu.

Jogoo alipoona hivyo, alipiga kelele, “Go go go go Likuku!” Maana yake hivi, “Kuku alinidanganya.” Kanga mwishowe alichoka kusubiri.

Alipochoka kusubiri akaja karibu na nyumbani mwa watu wenye miguu miwili. Akaita, “Kuku wewe! Nimekuambia fuata moto nawe umeenda kimoja.

Lakini hakusikia sauti inayojibu. Akaita tena. Jogoo akajibu, “Ya zamani haipooo! Usiingie kwenye mateso haya.” Kanga aliposikia kwamba hawarudi tena, akaenda porini mpaka leo yupo huko.

the-hen-

ENGLISH: THE STORY OF THE CHICKEN AND THE ROOSTER.

In the past hens and cocks were not domestic birds. They were wild birds living with other birds in the wilderness.

So one day it rained very heavily in the wilderness.

The Guinea fowl said to the hen, “Go to the two-legged people, with their two hands, and two eyes, and ask for fire so that we can set it and warm ourselves because this cold is torturing us.

The hen went to the people, who received her very well.Then they asked her why she had visited them. And she said, “I am a person from the wilderness. I have come to ask for fire, because there is no fire at our place.”

When she said this, the two legged people did not give her the fire. They gave her a warm welcome, and gave her food. She saw that the two legged people were very happy.

She said in her heart, others eat and some even sleep during the day. The two legged people did not let her go back. Instead, gave her more food. When the hen saw that she was kindly treated, she forgot about what she was sent.

 When the birds in the wilderness got tired of waiting, they sent a cock after her. The cock did not refuse to go.When he arrived they received him very well, as they did for the hen.

When he go tin, he found the hen enjoying the sleep. When she woke up, the cock asked her, “What happened?Why are you just silent?”

The hen replied, “I am not going back to the wilderness anymore.This is because I am comfortable here.The two legged people are treating me very well. What could make me go back to the wilderness?”

Finally,she said to him again, “Come, eat what I have left,my brother.” The cock ate. And he liked it very much, and said, “And I won’t go out into the wilderness.”

That is why when the hen drinks water looks up to thank the Creator who sent her the two legged animals. But it is important to note the two legged are sometimes good and sometimes they are not.

One day, the visitors came to the house of the two legged. They looked and saw that food was available, but no vegetables. Then they adivised each other and said, “We do not need to worry, because what helps a person is his.”

Catch a hen to make her a side dish for our guests. Without much ado, the hen was caught, and she cried, “It’s not me, it’s not me.” But she was just  slaughtered.

When the cock saw it, he screamed, “Go go go go Likuku!” This means, “The hen deceived me.”

Finally,Guinea fowl got tired of waiting. It came closer to the house of the two legged people. It said, “Hen! I have asked you to go and ask for fire and you have gone to stay.”

But he did not hear the answer. He called again. The cock answered, “Old is gone! Do not enter into this persecution.”When Guinea fowl heard that, she went back to the wilderness where she is until today..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.