53. Lung`wando Na Shimba

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Lushiku lumo umuna Shimba agaja aha numba ya ng’wa Lung’wando, usanga alinduhu wajaga (kumilimo) kungese. Wingila umuna Shimba umu kaya yang’wa Lungwando, ung’wibhandila ize annye.

Aho washika ulung’wando ubhona mabhondo ga Shimba gingilaga umu kaya, ushoka hado hado kushika kasegeno. Ukalala kuko.

Kushika wela, uja kumilimo hangi. Aho wamala imilimo wiza pole pole aha numba, usanga mabhondo gigolo galiho, muna Shimba atali ibhandile.

Lung’wando ushoka hangi hado hado kushika kasegeno, wandya kugisha, “Madilo muna numba wane, sele. Ugisha hangi, madilo muna numba wane, sele. Uyomba muna Lung’wando giki hangi, nakagugishaga wazunya, ilelo witaga kinahe utuzunyaga kunigisha. Madilo muna numba wane, nose uzunya muna Shimba, “Madilo bhabha.” Lung’wando useka hii hii! Natinabhona numba yagisha.

KISWAHILI: SUNGURA NA SIMBA
Siku moja Simba alikwenda nyumbani kwa Sungura. Kumbe hakumkuta, kwani alikuwa amekwenda kazini (kwenye palizi). Simba aliingia ndani ya nyumba ya Sungura, akajibanza ili Sungura atakaporudi akija amle.

Sungura aliporudi, aligundua nyayo za Simba zimeelekea ndani ya nyumba yake. Basi akarudi nyuma kwa mwendo wa kasi hadi mbali na kulala huko.

Asubuhi akaenda moja kwa moja kwenye kazi zake. Alipomaliza kazi, alirejea polepole tena nyumbani kwake. Alizikuta nyayo zilezile za Simba kama alivyoziona jana. Hapo Sungura akasalimia, “Umeshindaje nyumba yangu?” Kukawa kimya kitupu kimetawala. Akarudia kusalimia mara ya pili na ya tatu. Akasema “Huwa ninakusalimu unakubali leo umefanyaje umekataa kunisalimu.?” Akarudia “Umeshindaje we nyumba yangu?”
Mwisho Simba akakubali, “Sijambo baba Sungura!” Akacheka hii! hii! “Sijaona nyumba inasalimu!

KISWAHILI: Sungura Na Simba

Siku moja Simba alikwenda nyumbani kwa Sungura. Kumbe hakuwepo, kwani alikuwa amekwenda kazini (kwenye palizi). Simba aliingia ndani ya nyumba ya Sungura, akajificha ili Sungura atakaporudi aje amle.

Sungura aliporudi, aligundua nyayo za Simba zimeelekea ndani ya nyumba yake. Basi akarudi nyuma kwa mwendo wa pole pole hadi umbali wa kutosha na kulala huko.

Asubuhi akaenda moja kwa moja kwenye kazi zake. Alipomaliza kazi, alirejea polepole tena nyumbani kwake. Alizikuta nyayo zilezile za Simba kama alivyoziona jana.

Hapo Sungura akasalimia, “Umeshindaje nyumba yangu?” Kukawa kimya kitupu kimetawala. Akarudia kusalimia mara ya pili na ya tatu. Akasema “Huwa ninakusalimu unakubali leo umefanyaje umekataa kuniitikia?” Akarudia “Umeshindaje we nyumba yangu?”

Mwisho Simba akakubali, “Sijambo baba Sungura!” Akacheka hii! hii! “Sijaona nyumba inasalimu!”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.