46. Sayayi, Mbiti Na Mhuli

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho ngosha umo wali na ngunda jigijigi gwa wiza no. Aho ng’waka gwingila wandya gugulima, ubhibhamo bhusiga, mandege, shili na masindi, shose shuponeka, no no no na masindi.

Kuhayimanila shilonga shilili shayugalya masindi, ung’wenekili ngunda wandya kulinda. Bhahayimanila jadula Mhuli jubhandanija kubhalya abha na masindi niyo umbehi wita iyanga gete. Ugugaswagamo umu ngunda gung’ogohya umbehi unyenyeka ajile ku kaya. Ushika ubhitila guja kulinsumba ng’wiye Sayayi, ng’wana Kang’wa. Unsombolela iliyanga lyakwe lyenilo.rabbit

Sayayi uhaya giki, “Agaya, wa mayu gashinaga bhana Mhuli duhu, bhana Mhuli duhu, bhobha no kufilimbi lulu tubhasange!” Huna bhitonja bhajile kungunda mu ng’wa noni. Aho bhashikako, bhusanga Mhuli jitimo jajaga, aliyo abha na masindi lwiyugaga kibhi.

Huna ng’wana Kang’wa wilalangijamo isindi itale gete, lyubhejiwa nomo gwa kudula kwingilamo uSayayi. Ng’wana Kang’wa wisokela ng’wisindi ulibhilamo gete nifilimbi yakwe mu nhingo, ung’wila unsumba ng’wiye giki,”lugalagaho lulu aha nyango gwane.” Huna ulibhucha ilisindi ulitula uko bhagizilaga. Ubhebhe usegenele ukalinhe mu linti wilolele ulu bhalize.”

Umbehi wita gitumo walagililwa. Kuhayimanila, bhana Mhuli bhadula uyo walatongelile ulishikila ilisindi ulishona uliponeja mu nomo ulimila.

Aho bhakwilika milomo umo ngunda, filimbi yukana, bhana Mhuli bhimila pye. Filimbi yuhalala hangi, bhana Mhuli bhunyula nhambo bhalolile muli dakama bhukimila. Filimbi yung’ang’ala, Mhuli hangi jusimila jilolile ng’weli, bhukimila. Filimbi hangi yangilija “Felefele” Mhuli jusimila hangi jilollile muli bhukelebhe. Jukimila jandya kwibhuja bhuja jiwila giki. “Aliyo, muli kiya, aho jakimila jandya kwibhuja hangi filimbi ili lilila mu bhise?”

Kuhayimanila munda ya ng’wichabho “Felefele” Mhuli jandya kwiwila twite kinehe lulu?” Ilitale lyabho lyita lubhanza lyuhaya, “Tundimagi tumulage!” Huna uding’wa ubhulagwa na miye.

Huna bhutandula umunda bhulolwa mo, ubhonwa mo ng’wana Kangwa wabhulyaga miso. Ubhujiwa, “Alu bhebhe nang’ho kinehe?” Sayayi ushosha, “Unene nalung’wambilija nsumba ng’wichane kulinda Mhuli jilimala masindi gakwe.” Mhuli juhaya, “Ubhebhe lulu, ung’wambilija wako wa wiza lulu igiko iki nose umo mu bhise wamulaja?

Niyo igete tukubhulage nang’ho.” Ng’wana Kang’wa udaya alihaya giki, “Nu nene nazunyaga ukubhulagwa, nahene mutizunipandagila numho nakugayaho naka nyenye, lunganyelephant3agi lugoye lulihu gete lwa kulemlelwa na kwibhona.” Mhuli juzunya.

Jandya kuchenula malugoye miselya, mitinje, milumbaga, mihoja mitulwa ngoye lyulungwa lilugoye limo. Ng’wana kang’wa uludima ulugoye alihaya giki, “Naje nalo ulugoye, ning’we ukunung’wa ludimilaga. Ulu lukakalika nakulija filimbi yane, ning’we mukwandya lulu kuluduta wangu wangu ukubhanga naka kunu nachaga kale kale.

Ng’wana Kang’wa bhumanhya na muna Mbiti. Muna Mbiti aliyungula unung’hya na kunung’hilija kunu na kunu. Sayayi umuja, “Kinehe muna Mbiti, ulichobha ki?” “Ndichobha nyama nishoshe isho nalabhone.” Ng’wana Kang’wa ushosha, “Nyama wajipandikaga lulu, jiti ja kumala.

Ubhebhe lulu nagugukunga ili lugoye lyenili, huna likukuchala mpaga aho nyama jili.” Huna muna Mbiti utungwa lugoye ha kugulu gwa ku numa, huna filimbi yulila, jandya lulu kuduta lugoye, muna Mbiti wandya kuhaya, “Wa mayu, nite kinehe lulu? Yuuu!” ilidutwa duhu, ilibhitiwa mu masanzu na mu malambo sagala sagala, nose ushikaho Mhuli jili.

Mhuli julola, jubhona Mbiti aho lugoye. Alu ng’wana kangwa atiho!! Mhuli jumuja muna Mbiti giki, “Alu bhebhe nang’ho? Unene naluchobha nyama. Huna ng’wana Kang’wa unikunga lugoye, angu lukunenha ku nyama.

Mhuli jumuja, bhebhe muna Mbiti uli ng’waka gete u kunyama. Bhugatu. Huna Mbiti usonelwa mimba gwa mhuli, uwilwa giki, “lyaga lulu mpaga ugumale,” muna Mbiti wandya kulya. Wahayimanila ing’humbi yalema, aliyo aliwilwa lyaga duhu. Nose muna Mbiti utanduka lwahi ucha.

KISWAHILI: SUNGURA, FISI, NA TEMBO

Alikuwepo mwanamume mmoja alikuwa na shamba kubwa na zuri mno. Ulipoingia mwaka akaanza kulilima, aliivisha humo mtama, mahindi, Kunde, na (matikiti pori) mamung’unya “masindi” vyote viliiva vizuri, mamung’unya (matikiti pori) yalipatikana zaidi kuliko mazao mengine.

Kushitukia wameingia wadudu wakaanza kuyala mamung’unya, mwenye shamba akaanza kulinda. Alishitukia wanatokea Tembo wakaanza kuyala mamung’unya,  Bwana wa hilo shamba alipata mahangaiko makubwa kweli.

Kuwafukuza watoke   shambani mwake aliwaogopa, akaamua kwenda nyumbani. Alifika na kupitiliza kwenda kwa rafiki yake Sungura, mwanakang’wa. Akamweleza tatizo lake hilo.

Sungura alisema, “Aaa, mtoto wa mama kumbe ni tembo tu, tembo tu, waoga mno wakisikia filimbi basi twende!” Ndipo wakaongozana kuelekea shambani  sehemu iitwayo, Mwanoni. Walipofika huko walikuta Tembo hawapo wameondoka, lakini mamung’unya (matikiti pori) yamekatwa vibaya.

Ndipo Sungura alitazama na kuona limung’unya kubwa kabisa, akatengeneza mdomo wa kutosha kuingia Sungura ndani yake. Sungura akaingia ndani ya mung’unya akapotelea humo na filimbi yake shingoni, akamwambia rafiki yake kwamba, “Funga basi kwenye mlango wangu.” Ndipo akalibeba limung’unya, na kwenda kuliweka kule wanakoingilia Tembo. Akamwambia, “Wewe uende mbali ukapande kwenye mti uangalie kama watakuja.”

Jamaa alifanya kama alivyoagizwa, Kushitukia, tembo wakaja aliyekuwa ametangulia aliliparamia lile mung’unya na kulitoa maganda yake kwa meno. Akalitupia kwenye mdomo akalimeza.

Walipokuwa wengi shambani wakiendelea kula, filimbi ikapulizwa, tembo wote wakasimama. Filimbi ikapulizwa tena, tembo wakakimbia mbio wakielekea upande wa kusini wakaenda kusimama.

Filimbi ikapulizwa tena, tembo tena wakakimbia kuelekea magharibi, wakaenda kusimama. Filimbi ikapulizwa tena, “Felefele” Tembo wakatimua mbio kuelekea Ukelewe. Wakasimama na kuanza kuulizana wakielezana kwamba, kuna filimbi inapulizwa. “Lakini mashariki, waliposimama wakaanza kuulizana filimbi inapulizwa kwetu.”

Kushitukia ndani ya tumbo la mwenzao “Felefele” tembo wakaanza kuambiana “tufanye nini basi”? Mkubwa wao akafanya kikao akasema, “Tumshike tumuue!” Ndipo akashikwa akauliwa na wenzie.

Ndipo wakachana tumboni wakaangalia humo na kumuona Mwana Kang’wa ametoa macho. Akaulizwa, “Na wewe nawe vipi?” Sungura alijibu, “Mimi nilikuwa namsaidia rafiki yangu kulinda Tembo wanaomaliza mamung’unya yake.  Tembo wakasema, “Wewe basi msaidizi wako ni mzuri hivi mwishowe amesababisha mmoja wetu tumemuua?”

“Hivyo kweli tukuue nawe.” Mwana Kang’wa alisema hivi, “Na mimi nimekubali kuuliwa, hivyo msinikanyage nisije nikosekana hata kipande kidogo. Fungeni kamba ndefu kabisa ya kushindwa hata kuonana.” Tembo walikubali.

Wakaanza kuaandaa kamba kutoka kwenye miti, miselya, mitinje, milumbaga, mihoja, mitulwa kamba ikafungwa moja. Mwana Kang’wa akaishika hiyo kamba akisema hivi, “Niende nayo kamba, nanyi huku nyuma mkiwa mmeishikilia. Kama ikifikia mwisho nitapiga filimbi yangu, nanyi mtaanza basi kuivuta haraka haraka kwa hali hiyo nitakuwa nimekufa zamani.

Mwana Kang’wa wakakutana na Fisi. Fisi alikuwa akizunguka akinusa huko na huko. Sungura akauliza. “Vipi Fisi, unatafuta nini?” “Natafuta nyama chochote kile nitakachoona. Mwana Kang’wa akarudisha. “Nyama umezipata basi. Siyo za kumaliza na kumaliza, siyo za kumaliza.

Wewe basi nitakufunga kamba hii, ndiyo itakupeleka kule ambako nyama ipo.” Ndipo fisi akafungwa kamba mguuni, ule wa nyuma. Filimbi ikapulizwa, wakaanza basi kuvuta kamba.

 Fisi akaanza kusema, “Nifanye nini basi wa mama”? Yuuu!” inavutwa tu. Inapitishwa kwenye miti ya miba vichaka mbalimbali, kwenye madimbwi hovyo hovyo, mwishowe akafika pale ambapo Tembo wapo.

Tembo waliangalia, na kuona fisi kwenye kamba. Lakini Mwana Kan’gwa hayupo!! Tembo walimuuliza fisi kwamba, “Na wewe nawe?” “Mimi nilikuwa natafuta nyama. Mwana Kang’wa akanifunga kamba eti itanileta kwenye nyama.”

Tembo wakamuuliza, “wewe fisi ni mlafi kabisa kwenye nyama? Sawa. Ndiyo fisi akaoneshwa mzoga wa tembo, akaambiwa hivi, “ule mpaka uumalize.” Fisi akaanza kula. Alishitukia tumbo limekataa, lakini anaambiwa “ule tu.” Mwishowe Fisi alipasuka kwa ulafi akafa.

spotted-hyena-2798926__340

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.