Sukuma

988. KENAKO HA KAMANILO.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya kamanilo. Akamanilo kenako jili jimanyikijo ja hape iji jigengelekile kunguno jili jagulolela bhuli munhu uyo ulolela koyi. Ijoyi jigang’wambilija nulu munhu uyo alija lugendo bho gwinhiwa lumeng’ho ulo lulihoyi kunguno lugikalaga lumanyikile ukubhanhu abho bhagikalaga koyi. Hunagwene abhanhu bhayombaga giki “kenako ha kamanilo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina nhungwa ja wiza ijo jili lumeng’ho lukwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga amanyikile uku abhanhu bha umuchalo jakwe, kunguno ya nhung’wa ja gubhagunana abhiye abho bhali na makoye. Uweyi agikalaga na bhageni bhingi aha kaya yakwe, kunguno ya lumeng’ho lokwe lunulo, ulo gwikala na bhanhu chiza, umuchalo jakwe jinijo.

Inhungwa ijawiza jinijo, jikolile nuyo alina jimanyikijo ja gubhambilija bhanhu ugumpandika wangu, kunguno ni joyi jigang’wambilija umunhu uyo alinajo, ugushigilwa wangu na bhageni bhakwe. Hunagwene abhanhu bhagajiyombaga giki, “kenako ha kamanilo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubhiza na nhungwa jawiza bho gubhambilija abho bhalina makoye, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya yabho, umuwikaji bhobho.

Luka 6:43-45.

2Wakorintho 12:12.

KISWAHILI: HIKI NDICHO KIJULISHO.

Methali hiyo, huongelea juu ya kijulisho. Kijulisho hicho, ni kitambulisho cha wazi ambacho kinajulikana kwa sababu ya kumuonesha mtu jinsi alivyo alinayekiona. Chenyewe humsaidia hata mtu aliyeko safarini kukitumia kama alama ya kumfikisha kwa haraka kule aendapo kwa sababu ya kujulikana kwake kwa watu wanaoishi huko. Ndiyo maana watu husema kwamba, “hiki ndicho kijulisho.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana tabia njema ambayo ni kitambulisho chake, katika maisha yake. Mtu huyo, huishi na watu vizuri katika kijiji chake kwa sababu ya tabia yake hiyo ya kuwasaidia wenzake walio na matatizo. Yeye huishi na wageni wengi kwenye familia yake kwa sababu ya kitambulisho chake hicho, cha kuishi na watu vizuri, katika kijiji chake hicho.

Tabia hiyo njema, hufanana na kile kijulisho kilichomsaidia msafiri kufika haraka alikokuwa akienda, kwa sababu nacho, huwasaidia watu kumfikia haraka yule aliye nacho. Ndiyo maana watu husema kwamba, “hiki ndicho kijulisho.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuwasaidia wenzao walioko kwenye matatizo, ili waweze kuziendeleza vizuri, familia zao, maishani mwao.

Luka 6:43-45.

2Wakorintho 12:12.

cow-121

goat-

ENGLISH: THIS IS THE SIGN.

This proverb speaks of a distinctiveness. This distinctiveness is a clear identifier that identifies a person for what he or she sees. It even helps the traveler to use it as a sign to get him to his destination quickly because of his popularity with the people who live there. That is why people say that, “This is the sign.”

This proverb is compared to a person who has a good character that is his identity in his life. This man lives well with the people in his village because of his habit of helping his fellows who are in great need. He lives with many visitors in his family because of his good identity in living well with people in his village.

This positive attitude is similar to that of a traveler who helps a tourist to get to his destination quickly, because it also helps people to reach their destination quickly. That is why people say that, “This is an identity.”

This proverb imparts in people a clue on how to have a good attitude enough to help others who are in great need, so that they can better develop themselves in their families.

Luke 6: 43-45.

2 Corinthians 12:12.

sheep-21

987. NKUB’IJA FULO.

Akahayile kenako kahoyelile higulya ya jisumva ijo jigakub’ijaga fulo. Ijisumva jinijo, jili kihamo na ng’holo na danga ijo jigakub’ijaga minzi ga gung’wa na gwikala moyi ijingi. Hunagwene abhanhu bhagajitanaga giki, “nkub’ija fulo.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajaga gujisuga ha bhasab’i umukikalile kakwe. Ijikolo ja ha bhasab’i, jigikolanijiyagwa na fulo iyo agipandikaga umunhu uyo wisuga hoyi, kunguno agamanaga ujilya ijiliwa ija ha kaya yiniyo. Umunhu ng’wunuyo, agamanilaga aha kaya yiniyo, bho gutumama milimo ya henaho na gujilya ijiliwa ja hene, kunguno ya fulo iyo agaipandikaga yiniyo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhizaga guti ng’wana o hakaya iya ha bhasab’i yiniyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni jisumva ijo jigakub’ijaga fulo, kunguno nuweyi agakub’ijaga jiliwa a ha kaya ya bhasab’i bho gwisugilija hoyi, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “nkub’ija fulo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kutumama milimo ya gubheng’hela jikolo ja kutuula hakibha ya gutumila aha shigu ija bhutongi, kugiki bhadule kujilang’hana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 11:25-30.

Yohana 6:67-69.

Mwanzo 46:1-6.

Luka 12:35-40.

KISWAHILI: MFUATA UNYEVU.

Msemo huo, huongelea juu ya viumbe ambavyo hufuata unyevu. Viumbe hivyo, ni pamoja na kondoo na vyura ambavyo hufuata maji ya kunywa na vingine huishi ndani ya maji hayo. Ndiyo maana watu humuita kiumbe hiyo kwamba ni “mfuata unyevu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huenda kujifuga kwa matajiri, katika maisha yake. Mali za matajiri hao hufananishwa na unyevu anaoupata mtu huyo aliyejifuga hapo, kwa sababu ya kuendelea kula chakula cha kwenye familia hiyo. Mtu huyo, huzoea kwenye familia hiyo kwa kuendelea kufanya kazi za pale na kula chakula cha hapo, kwa sababu ya unyevu huo anaoupata, maishani mwake. Yeye huwa kama mtoto wa kwenye familia hiyo ya matajari.

Mtu huyo, hufanana na vile viumbe vifuatavyo unyevu, kwa sababu naye hufuata chakula kwa kwenda kufugwa kwenye familia ya matajiri hao, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni “mfuata unyevu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi ziwezazo kuwaletea mali za kuweka akiba itakayo wasaidia kwenye siku za mbeleni, ili waweze kuzilinda vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 11:25-30.

Yohana 6:67-69.

Mwanzo 46:1-6.

Luka 12:35-40.

frog-

sheep-1

ENGLISH: A PERSON WHO IS AFTER GOOD THINGS.

The overhead saying speaks of creatures that follow moisture. These creatures, include: sheep and frogs, because they follow moisture for drinking water and some of them live in water areas. That is why people refer to that creature as being “a person who is after good things.”

This saying is related to a man who goes to stay in families of rich people for eating some food. The wealth of the rich one is likened to the humidity which that man gets because he continued to eat the food of that family. This person becomes familiar to that rich family by continuing to work there and eat local food, because of the moisture which he gets in his life. He becomes like a child in that rich family.

This man is like the creatures that followed moisture, because he also follows the food by going to be raised in the rich families. That is why people refer to him as “a person who is after good things.”

This saying imparts in people a clue on how to do work that can bring them savings enough to help them in the future, so that they can better protect their families in their lives.

Matthew 11: 25-30.

John 6: 67-69.

Genesis 46: 1-6.

Luke 12: 35-40.

faroe-islands-

986. JIDIGWA.

Ujidigwa ali munhu uyo alina matu gachib’ile. Umunhu ng’wunuyo, adinabho ubhudula ubho gwigwa mhayo uyo guliyombwa na bhiye kunguno ya bhuchib’i bho matu gakwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “jidigwa.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina nhungwa ja jab’ub’i, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agahugulagwa ng’hangala ningi na abhiye ulu ohub’a, aliyo ugwigwa nduhu, kunguno agashokelaka gwita mihayo ya bhubhi yiniyo. Uweyi agapandikaga makoye ga guyisalambanya sagala ikaya yakwe, kunguno ya bhudijigwa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oli na matu gachib’ile, kunguno nuweyi adigwaga ugujileka inhungwa ija bhub’i jakwe jinijo, ulu ohugulwa na bhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “jidigwa.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuzunya guhugulwa na bhichabho, bho kuleka nhungwa ja bhub’i, umubhutumami bhobho, kugiki bhadule kujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Wagalatia 3:1-14.

KISWAHILI: ASIYESIKIA.

Asiyesikia ni mtu yule ambaye ana masikio yaliyoziba. Mtu huyo, hana uwezo wa kusikia neno analoambiwa na wenzake, kwa sababu ya kuziba kwa masikio yake hayo. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni mtu “asiyesikia.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana tabia mbaya katika maisha yake. Mtu huyo, huwa anatenda maovu na kuonywa wenzake, mara kwa mara, lakini huwa hasikii kwa sababu ya tabia yake hiyo ya kurudia kutenda maovu. Yeye hupata matatizo ya kuisambalatisha familia yake, kwa sababu ya kutokusikia kuacha kutenda maovu hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwa na masikio yaliyoziba, kwa sababu naye huwa hasikii kwa kuacha kutenda maovu anapoonywa na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuita kuwa ni mtu ‘asiyesikia.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kukubali kuonywa na wenzao, kwa kuacha tabia ya kutenda maovu, katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Wagalatia 3:1-14.

woman-22

market-

ENGLISH: THE ONE WHO DOES NOT HEED.

The deaf is the one whose ears cannot hear. This person is unable to hear the word which is being spoken to him by his companions, because of such disabilities of his ears. That is why people call him “the one who does not heed.”

This saying is compared to a person who has evil habit in his life. This person often does evil things and is warned by others, but he does not listen because of his recurring behavior. He breaks up his family because of his unwillingness to stop doing these evil things in his life.

This person resembles the one who had ears’ disability, because he also does not listen enough to stop doing evil when he is warned by his fellows in life. That is why people call him “the one who does not heed.”

This saying teaches people about accepting warnings of their fellows, by refraining from committing evil deeds in fulfilling their duties, so that they can well raise their families in their lives.

Galatians 3: 1-14.

ferry-1

985. JAWIB’I JIDASAB’ILAGWA.

Olihoyi munhu uyo agib’a hela ujituula mumhinda yakwe. Umunhu ng’wunuyo, agandya lugendo lo guja kaya. Aho oshiga ikaya agachala nkono umumhinda yakwe kugiki ajilole ihela jinilo, ujigayiwa kunguno agajigumila mu nzila bho nduhu ugamana uweyi. Gashinaga ihela jinijo, agajigumila haho ojib’ilaga mpaga ujikuga ung’winikili ojo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila ung’wib’i ng’wunuyo giki, “jawib’i jidasab’ilagwa.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agib’aga jikolo ijo jidang’wenhelaga solobho yoseyose, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agib’aga jikolo ja bhanhu ogajitumamila sagala duhu kunguno adajinogelile. Uweyi agikalaga ukoya na nzala bhuli makanza kunguno ya gugayiwa jilila ijaguilisha  kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agib’a hela ujigwisha haho ujib’ilaga mpaga jukugwa nu ng’winikili ojo, kunguno nuwei agajikenagulaga sagala ijikolo ijo agajib’aga, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “jawib’i jidasab’ilagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wib’i bho gwigulambija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gupandika bhusab’i umuwikaji bhobho.

Kutoka 20: 15.

Mithali 15:9-10.

Mithali 16:8.

 

KISWAHILI: ZA KUIBA HAZITAJIRIKIWI.

Alikuwepo mtu aliyeiba hela na kuiweka mfukoni mwake. Mtu huyo, alianza safari ya kuelekea nyumbani. Alipofipa nyumbani kwake, alipeleka mkono mfukoni ili kuikagua hiyo hela, akaikosa, kwa sababu ilidondoka bila ya yeye kufahamu. Kumbe hela hiyo ilidondokea pale alipoiibia mpaka mwenye nayo, akaiokota. Ndiyo maana watu walimuambia yule mwizi kwamba, “za kuiba hazitajirikiwi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayeiba vitu ambavyo havimletei faida yoyote, katika maisha yake. Mtu huyo, huiba vitu vya watu na kuvitumia hovyo, kwa sababu hakuvitolea jasho. Yeye huishi kwa kusumbuliwa na tatizo la njaa kwenye familia yake, kwa sababu ya kukosa chakula cha kuilisha famalia yake hiyo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeiba hela akaidondosha mpaga mwenye nayo akaiokota, kwa sababu naye huvitumia hovyo vitu alivyoviiba, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “za kuiba hazitajirikiwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya wizi kwa kujibidisha kufanya zao vizuri, ili waweze kupata utajiri, maishani mwao.

Kutoka 20: 15.

Mithali 15:9-10.

Mithali 16:8.

woman-112

african-12

 

ENGLISH: STOLEN THINGS DO NOT MAKE ONE RICH.

There was a man who stole money from somebody and put it in his pocket. This man began his journey home. When he got home, he put his hand in his pocket to check it all over, and missed it, because it fell out without him knowing. But the money fell out when he stole it until the owner had it, and he picked it up. That is why people told the thief that “stolen things do not make one rich.”

This proverb is equated to a man who steals things that do not benefit him in his life. This person steals people’s belongings and uses them carelessly, because he does not sweat in earning them. He lives with the problem of hunger in his family because of the lack of food for feeding his family members.

This person is like the one who stole the money and dropped it off at the owner’s presence, because he also misuses the things which he stole from his life. That is why people say to him that, “stolen things do not make one rich.”

This proverb imparts in people a clue on how to stop stealing properties of others. They have to try doing their best enough to earn for their living, so that they can get rich in their families.

Exodus 20:15.

Proverbs 15: 9-10.

Proverbs 16: 8.

 

home-

984. LUKWA LO JIHUNDI.

Ijihundi ili ngume iyo yolechije wikenya bho bhanhu abho bhatumamaga nimo go gulimila lukwa lo ngese. Abhanhu bhenabho, bhagayoga na gwikenya mpaga bhuyangulwa na bhanhu abho bhagiyigwa iyombo yabho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “lukwa lo jihundi.” Ulukwa lunulo luli lukwa lo gwitulila.

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kukaya iyo ili na bhanhu bhagumana bhuyoga bhuli makanza. Ikaya yiniyo, yigiyojaga bhuli makanza kunguno ya kugayiwa ng’wigwano. Iyoyi idalamaga shigu ningi kunguno ya gugayiwa ililange ilya gwidegeleka chiza linilo, umuwikaji bhobho.

Ikaya yiniyo, igikolaga na bhalimu abho bhagikenya mpaga bhuyileka ingese yabho, kunguno ni yoyi, abhanhu bhayo bhagayogaga mpaga bhaduma uguyibheja chiza ikaya yiniyo, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagaitanaga giki “lukwa lo jihundi.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka bhupelanu umutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule gutumama milimo yabho chiza, bho nduhu ugwikenye, umuwikaji bhobho.

1Petro 4:7-8.

1Yohana 3:11-18.

1Yohana 4:7-21.

Marko 12:28-31.

 

KISWAHILI: MUKWA WA NGUMI.

Mukwa wa ngumi ni ugonvi wa watu waliokuwa wakipalila mukwa wa palizi. Watu hao, walizozana na kugombana mpaga wakaja watu waliousikia ugonvi huo kuwaamulia. Ndiyo maana watu hao waliita kwamba ni “mukwa wa ngumi.” Huo ni mukwa wa kupigana.

Msemo huo, hulinganishwa kwenye familia ile ambayo watu wake hugombana mara kwa mara. Familia hiyo, huzozana mara kwa mara kwa sababu ya watu wake kukosa uelewano. Yenyewe, huwa haidumu kwa sababu ya kukosa maadili ya kuwawezesha kuishi kwa pamoja, maishani mwao.

Familia hiyo, hufanana na wakulima wale waliogombana wakati wakipalilia palizi, kwa sababu nayo huzozana mara kwa mara, wakati watu wake, wanafanya kazi. Ndiyo maana watu huiita familia hiyo kuwa ni “mukwa wa ngumi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha hasira katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

1Petro 4:7-8.

1Yohana 3:11-18.

1Yohana 4:7-21.

Marko 12:28-31.

farming-

ENGLISH: A FIST’S PORTION TO CULTIVATE.

The fistfight is the quarrel of the people who were weeding the weed in a farm. These men started arguing after misunderstanding of each other took place which causes them to start quarreling between them. The people who heard their noise and saw them quarreling went to reconcile them. That is why these people called it “a fist’s portion to cultivate.”

This saying is applied to a family whose members are not at odds with one another. The family, in turn, quarrels frequently because of the lack of understanding among its members.  This family disintegrates because its members do not have values which can unite them enough to live together in their family.

This family is like the farmers who quarreled when they were weeding in the farm, because its members also quarrel often while are working. That is why people call that family that “a fist’s portion to cultivate.”

This saying teaches people about letting go of anger in fulfilling their duties, so that they can better fulfill their responsibilities in their societies.

1Peter 4: 7-8.

1John 3: 11-18.

1John 4: 7-21.

Mark 12: 28-31.