sayings

1049. LYAGUKUNGA MIKOB’A.

Imbuki ya kahayile kenako, ilolile bhukungi bholi ginhu litanda. Lyalihoyi ling’ombe ilo lyalilitanda ugusheng’wa kunguno ya bhuhala bholyo. Abhanhu ulu bhahaya ugulishema lyapelaga lyabhashiga bhaduma ugulishema. Nose bhiyangula gulikunga mikanda umumagulu galyo na lyuzunya lulu ugusheng’wa. Hunagwene abhanhu bhenabho bhalitana iliong’ombe linilo giki, “lyagukunga mikob’a.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinambu ugutung’wa na bhiye umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga alemile ugutung’wa josejose nabhiye na hangi agashoshaga mihayo bho makala ukubhiye kunguno ya nhinda jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguibheja ikaya yakwe kunguno ya bhulambu bhokwe ubho gubhashokeja mihayo ya nhani abhiye, umumahoya gakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ng’ombe inhanda iyo yalemaga ugusheng’wa mpaga yutungwa mikob’a, kunguno nuweyi alinambu uyo alemile ugutung’wa guja kunhimo gosegose na bhiye umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “lyagukunga mikob’a.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja bhulambu bho guzunya gutung’wa na bhiye umuchalo jabho, kugiki bhadule gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, umuchalo jabho jinijo.

Wagalatia 3:1-8.

KISWAHILI: LA KUFUNGA MIKANDA.

Chanzo cha msemo huo chaangalia ufungaji wa mkanda kwenye kitu ambacho ni kikali kuguswa. Alikuwepo ng’ombe mmoja ambaye alikuwa hataki kukamuliwa kwa sababu ya ukorofi wake. Mwishowe watu waliamua kumfunga mkanda miguuni mwake ndipo akakubali kukamuliwa. Ndiyo maana watu hao walimuita ng’ombe huyo kwamba ni “la kufunga mikanda.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye kiburi katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hataki kutung’wa kwenda kufanya chochote na wenzake, na tena huwajibu watu kwa kauli mbaya, kwa sababu ya kiburi chake hicho, maishani mwake. Yeye hushindwa kutengeneza familia yake kwa sababu ya kiburi chake hicho cha kuwajibu wenzake kwa maneno mabaya, katika maongezi yake.

Mtu huyo, hufanana na yule ng’ombe mjeuri aliyekataa kukamuliwa, mpaga akafungwa mkanda miguuni mwake ndipo akakubali, kwa sababu naye hukataa kutumwa na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita kuwa ni “la kufunga mikanda.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya kuwa na kiburi kwa kukubali kutumwa na wenzao, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza majukumu yao, kijijini mwao.

Wagalatia 3:1-8.

cow-7301439__480

ENGLISH: IT IS OF FASTENING BELTS.

The source of this saying looks at the tying of a belt on something that is hard to touch. There was a cow that did not like to be milked because of its rudeness. Finally the people decided to tie a belt around her legs and then she agreed to be milked. That is why those people said about such cow that “it is of fastening belts.”

This saying is compared to the person who is proud in his life. Such person does not like to be pushed to do anything by his colleagues, and again he answers people with wicked words, because of his pride, in his life. He fails to form well his family because of his pride in answering his colleagues by using ruthless words, in his speech.

This person is similar to the cow that refused to be milked, until when a belt was tied around her legs and then she accepted, because he also refuses to be sent by his companions, in his life. That is why people say about him that, “it is of fastening belts.”

This saying instills in people a clue of abandoning habit of being proud by accepting to be sent by their nobles, so that they can help each other well in carrying out their duties in their village.

Galatians 3:1-8.

1048. LYANG’WANIKI ADALAB’ULAGA.

Imbuki ya kahayile kenako, yingilile ku bhutuji bho mbula bho likanza lilihu gete iyo igalenganijiyagwa na ng’waniki uyo azimizaga bho nduhu ugulabhula inuma.

Aho kale gulihoyi ng’waka uyo mbula nhale igatula ahikanza lya jidiku iyo igasola makanza malihu gete kunguno yaliidoyaga wangu. Imbula yiniyo, igandya gutula haho lyandya duhu ilijidiku bho nduhu ugugata mpaga giki abhanhu bhuyuduma bhangi agulimila ingese kunguno ya mbula yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki imbula ya ung’waka gunuyo, “lyang’waniki adalab’ulaga.”

Akahayile kenako, kagalenjiyagwa kuli munhu uyo agatumama milimo yakwe bho gwigulambija chiza mpaga jashila ijidiku, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, aganguhaga ugumisha ogatumama mimimo yake bho nduhu gwilendeja mpaga oimala chiza, kunguno ya bhukalalwa na bhukamu bhokwe bho guitumama imilimo yiniyo, muwikaji bhokwe.  Uweyi agaponaga majiliwa mingi noyi aha kaya yakwe kunguno ya wigulambija bhokwe ubho gutumama milimo bho bhukamu bhutale chiniko, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mbula iyo igatula mpaga jushila ijidiku bho nduhu ugugata, kunguno nuweyi agigulambijaga gutumama milimo yakwe bho nduhu uguyileka mpaka jashila ijidiku, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki agatumamaga milimo “lya mwaniki adalab’ulaga.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija kutumama milimo yabho chiza, bho gwanguha uguja ukumilimo yabho yiniyo, kugiki bhadule gupandika sabho ningi, umuwikaji bhobho.

 

Mwanzo 2:15.

Mhubiri 11:4.

Mithali 6:9.

 

KISWAHILI: LA MSICHANA ASIYEANGALIA NYUMA.

Chanzo cha msemo huo, chatokea kwenye unyeshaji wa mvua iliyochukua mda mrefu kabisa inayofananishwa na msichana asiyeangalia nyuma katika safari yake kwa sababu ya huleta uhai katika aridhi.

Hapo zamani, ulitokea mwaka ambao mvua kubwa ilinyesha kwa mfuluzo wa siku nyingi bila kukatika wakati wa masika. Mvua hiyo, ilipoanza kunyesha ilindelea hivyo, mpaka watu wakashindwa kupalilia palizi kwenye mashamba ya mazao yao kwa sababu ya ukubwa wake huo. Ndiyo maana watu walisema kwamba mvua ya mwaka huu ni “la msichana asiyeangalia nyuma.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake kwa bidii kubwa mpaka anazimaliza, katika maisha yake. Mtu huyo, huanza kufanya kazi wakati yanapoanza masika kwa kujibidisha katika kuyatunza vizuri mazao yake mpaka anayamaliza vizuri kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kufanya kazi maishani mwake.  Yeye hupata mavuno mengi katika mashamba yake kwa sababu ya kupenda kwake kuyatekeleza vizuri majukumu yake hayo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na mvua ile iliyonyesha kwa mfululizo mpaka kipindi cha masika kikaisha, kwa sababu naye hujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yake mpaka anayamaliza vizuri bila kuyaacha, katika maisha yake hayo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba yeye hufanya kazi “la msichana asiyeangulia nyuma.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao, kwa kuwahi kwenda kazini, ili waweze kupata mafanikio mengi zaidi maishani mwao.

Mwanzo 2:15.

Mhubiri 11:4.

Mithali 6:9.

portrait-11

blue-khruem-1571592__480

 

ENGLISH: IT IS THAT OF A GIRL WHO NEVER LOOKS BACK.

The source of the overhead saying came from the rainfall that lasted for a long time. This rain is compared to a girl who does not look back in her journey because of bringing life to the land.

Once upon a time, there was a year in which heavy rain fell for many days without stopping during the spring season. This rain carried on raining until people were unable to weed their crops because of its non stop. That is why people called that rain that “it is that of a girl who never looks back.”

This saying is compared to the person who does his work with great effort until he finishes it in his life. This person starts working when the spring season starts by taking care of his crops well until he finishes them because of his hard working way in his life. He gets a lot of harvest in his fields because of his love to carry out his duties well in his life.

This person resembles the rain that rained continuously until the end of the spring season, because he also carries out his duties well until he finishes them well without leaving them in his life. That is why people said about his works that, “it is that of a girl who never looks back.”

This saying imparts in people an idea of carrying out their duties well, by working well, so that they can get more success in their lives.

Genesis 2:15.

Ecclesiastes 11:4.

Proverbs 6:9.

 

umbrella-

1047. BHANDYAGA GWILEBHA MAGANDA.

Akahayile kenako, kahoyelile bhanhu abho bhilebyaga maganda muchalo jilebhe. Bhali hoyi bhanhu bhab’ili abho bhali ng’wichobha. Uumo obho agab’iza na jikolo jingi kunebya ung’wiye kunguno ya bhuguji bho sabho bhokwe ubho gutumila mpango go higulya.

Ung’wiye agabhiza na mpango go aha silili, ub’iza giki olebhiwa amaganda nu ng’wiyile ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagayomba giki, “bhandyaga gwilebha maganda.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagajitumilaga inguzu jabho chiza, bho gwikija gutumama milimo, umuwijaji bhobho. Abhanhu bhenabho, bhagipunaga diyu bhaja gujutumama milimo yabho ahikanza lya malima kwa kunguno ya bhukamu bho gutumama milimo bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagapandika sabho ningi noyi bhuli ng’wene kunguno ya wikindi bhobho ubho gutumama milimo yabho bhunubho, umukikalile kabho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nabho wilebhyaga maganda ga gupandika jikolo bho mpango gohigulya ulu bhaligula ijikolo jinijo, kunguno nabhoyi bhagikindaga ugutumama imilimo yabho bho bhukamu bhutale, umuwikaji bhobho. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “bhandyaga gwilebha maganda.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwikomeja gutumama milimo yabho bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika sabho ningi ubhutumami bho milimo yabho bhunubho, umuwikaji bhobho.

Luka 16:11-13.

Warumi 13:8-10.

Yakobo 1:9.

Warumi 15:1-2.

KISWAHILI: WAMEANZA KUZIDIANA UWEZO.

Msemo huo, huongelea juu ya watu waliokuwa wakizidiana uwezo wa kupata mali kwenye kijiji fulani. Walikuwepo watu wawili waliokuwa wakitafuta mali. Mmoja wao alipata mali nyingi kumzidi mwenzake kwa sababu ya ununuaji wake wa bei ya juu.

Mwenzake alikuwa akinunua vitu kwa bei ya chini, akawa amezidiwa uwezo na mwenzake huyo. Ndiyo maana watu walisema kwamba, “wameanza kuzidiana uwezo.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa watu wale ambao huzitumia nguvu zao vizuri kwa kushindana kufanya kazi, katika maisha yao. Watu hao, huamuka asubuhi na kuwahi kwenda kufanya kazi zao unapofika wakati wa kilimo kwa sababu ya bidii yao hiyo ya kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao. Wao hupata mali nyingi sana kila mmoja kwa sababu ya ushindani wao huo wa kufanya kazi kwa namna hiyo, katika maisha yao.

Watu hao, hufanana na wale waliokuwa wakizidiana uwezo wa kupata mali kwa bei ya juu, kwa sababu nao, hushindana katika kufanya kazi zao kwa bidii kubwa, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “wameanza kuzidiana uwezo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa juhudi kubwa, ili waweze kupata mali nyingi katika utekeleji wa majukumu yao, maishani mwao.

Luka 16:11-13.

Warumi 13:8-10.

Yakobo 1:9.

Warumi 15:1-2.

fight-1564959__480

angolan-509593__480

women-5935801__480

ENGLISH: THEY HAVE BEGUN TO SURPASS EACH OTHER IN TERMS OF WEALTH.

This saying talks about people who were competing with one another to get wealth in a certain village. There were two people who were looking for property. One of them got more wealth than the other because of his high-priced purchases.

His colleague was buying things at a low price, he was overwhelmed by that colleague. That is why people said that, “they have begun to surpass each other in terms of wealth.”

This saying is compared to people who nicely use their energy by competing to work in their lives. These people wake up in the morning and go to do their work when it is time to farm because of their hard working situation which is strong enough to carry out their duties well in their lives. They get a lot of wealth each one of them because of their competition to work in that way in their lives.

These people are similar to those who were competing with each other ing using their abilities to get property at a high price, because they, too, compete in doing their works with great effort, in their lives. That is why people tell them that, “they have begun to surpass each other in terms of wealth.”

This saying teaches people about forcing themselves to do their works with great effort, so that they can get a lot of wealth in fulfilling their responsibilities in their lives.

Luke 16:11-13.

Romans 13:8-10.

James 1:9.

Romans 15:1-2.

1046. ONILOLELAGA MUMINZI.

Akahayile kenako, kalolile bhuloleji bho ng’wa munhu munzi. Bhalihoyi bhanhu bhab’ili abho bhayelaga mulitabha. Aho bhashiga hoyi, umo obho agandya gugulola ung’wengeleji go ng’wiye umuminzi ga litabha linilo kunguno oliadahayile ugumanwa nu ng’wiye igiki aling’wilolela moyi. Kihamo ni yiniyo, ung’wiye agambadija igiki alinhola weyi umuminzi genayo. Hunagwene agang’wila giki, “onilolelaga muminzi.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga abhadalahile abhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adabhadegelekaga abhiye ulu bhaliyomba umumahoya gakwe, kunguno ya libhengwe lwake linilo. Uweyi agikalaga bhung’wene aha kaya yake kunguno ya gwiiganikila giki ayimanile pye imihayo kulebha abhiye, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ung’wunuyo, agikolaga nuyo onholelaga mu ng’wengeleji gokwe ugo muminzi ung’wiye, kunguno nuweyi agikalaga abhadalahile abhiye bho gulema ugubhadegeleka ulu bhaliyomba, umumahoya gakwe. Hunagwene uyo ajimanile ing’hungwa jakwe agang’wilaga giki, “onilolelaga umumingi.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka ng’hungwa ja gubhadalaha abhanhu bho gubhadegelaka chiza ulu bhaliyomba umumahoya gabho, kugiki bhadule gwikala chiza na bhanhu bhabho na bho mholele, umuwikaji bhobho.

Mithali 9:10.

Wagalatia 6:10.

Luka 16:9.

KISWAHILI: UMENIANGALIA KWENYE MAJI.

Msemo huo, huangalia ungaliaji wa mtu kwenye maji. Walikuwepo watu wawili waliokuwa wakitembea pembeni mwa dimbwi. Walipofika hapo, mmoja wao akaanza kumwangalia mwenzake kupitia kivuli kilichomo kwenye maji ya hilo dimbwi kwa sababu hakutaka kugundulika naye kuwa anamtazama. Pamoja na hayo, mwenzake huyo, aligundua kuwa mwenzake amekuwa akimwangalia kwenye maji. Ndiyo maana alimwambia kwamba, “umeniangalia kwenye maji.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwadharau wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hawasikilizi wenzake wanapoongea katika maongezi yake kwa sababu ya dharau yake hiyo, maishani mwake. Yeye huishi peke yake kwenye familia yake kwa sababu ya kujiona kwamba anafahamu mambo yote kupita wenzake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyemwangalia mwenzake kwenye maji kupitia kivuli chake, kwa sababu naye huwadharau wenzake kwa kutokuwasikiliza wanapoongea katika maongezi yake. Ndiyo maana yule anayeifahamu tabia yake hiyo, humwambia kwamba, “umeniangalia kwenye maji.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya kuwadharau watu kwa kuwasikiliza vizuri wanapoongea katika maongezi yao, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani na watu wao, maishani mwao.

Mithali 9:10.

Wagalatia 6:10.

Luka 16:9.

pool-424194__480

 ENGLISH: YOU LOOKED AT ME IN THE WATER.

This saying looks at a person’s gaze on the water. There were two people who were walking by the pool. When they got there, one of them started looking at the other through the shadow in the water of that pool because he did not like to be found out that he was looking at him. Despite this, the colleague realized that his associate had been watching him in the water. That is why he told him that, “you looked at me in the water.”

This saying is compared to the person who despises his colleagues, in his life. Such person does not listen to his coworkers when they speak in his conversation because of his contempt in his life. He lives alone in his family because of thinking that he knows all things better than his peers, in his life.

This person resembles the one who looked at his fellow in the water through his shadow, because he also despises his fellows by not listening to them when they speak in their conversation. That is why the one who knows his behavior, tells him that, “you looked at me in the water.”

This saying instils in people a clue on stopping belittling people by listening to them well when they speak in their conversations, so that they can live well and in peace with their people, in their lives.

Proverbs 9:10.

Galatians 6:10.

Luke 16:9.

1044. UDIZUKUNG’UNHA JILATU.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya bhunguji bho jilatu bho ng’wa munhu ngeni ohakaya ndebhe. Ungeni ng’wunuyo, aha oshiga aha kaya iyo alioigeniha, agakungula ijilatu jakwe uhaya gujigung’unha, huna bhunhemeja abhaha kaya yiniyo, kunguno ubhugung’uni bho jilatu bhunubho, bhugolechaga jito ja gubhalekela izumo abhaha kaya yiniyo.  Hunagwene abha hakaya yiniyo, abhang’wila ungeni ng’wunuyo giki, “udizukung’unha jilatu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo aling’wiza nholo aha kaya yake, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhokelaga chiza abhageni abho bhagajaga gujungeniha, aha ng’wakwe henaho, kunguno ya wiza ng’holo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agapandika mbango ja gwikala chiza na bhanhu na gusabha majikolo mingi, aha ng’wakwe henaho, kunguno ya gubhabokela chiza abhageni bhakwe bhenabho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo aganhemeja ungeni okwe unhekela izumo uyo ahayaga gujikung’unha ijilatu jakwe, kunguno nuweyi agalema ugulekelwa ili zumo linilo bho gubhapokela chiza abhageni bhakwe, na gubhagalila chiza chiniko. Hunagwene agang’wilaga ungeni okwe giki, “udizukung’unha jilatu.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza na bhuza ng’holo bho gubhabokela chiza abhageni bhabho, kugiki bhadule gupandika mbango ja gusabha na gwikala chiza na bhanhu bhabho, umuwikaji bhobho.

Marko 6:11 – 12.

Kutoka 3:4 – 5.

Mathayo 10: 14 – 15.

KISWAHILI: USIKUNG’UTE VIATU.

Msemo huo, huongelea juu ya uvuaji wa viatu vya mgeni aliyetembelea familia fulani. Mgeni huyo, alipofika kwenye familia aliyekuwa anaitembelea, alivua viatu vyake akataka kuvikung’uta, wanafamilia hiyo wakamkataza, kwa sababu tendo hilo la kukung’uta viatu huadhiria uachaji wa laana kwenye familia hiyo. Ndiyo maana wanafamilia hao, walimwambia kwamba, “usikung’ute viatu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule aliye na moyo mzuri wa ukarimu katika familia yake, maishani mwake. Mtu huyo, huwakaribisha kwa ukarimu wageni wanamtembelea kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya moyo wake huo wa ukarimu, katika maisha yake. Yeye hufanikiwa kupata Baraka nyingi za kutajirika na kuishi vizuri na watu wake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyemzuia mgeni wake aliyetaka kumuachia laana kwenye familia yake kwa kukung’uta viatu vyake, kwa sababu naye hukataa laana kwa kuwakaribisha kwa ukarimu wageni wanaomtembelea kwenye familia yake hiyo. Ndiyo maana humwambia mgeni wake kwamba, “usikung’ute viatu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwapokea na kuwatunza vizuri wageni wao, ili waweze kupata Baraka za kutajirika na kuishi vizuri na watu, maishani mwao.

Marko 6:11 – 12.

Kutoka 3:4 – 5.

Mathayo 10: 14 – 15.

earth-1280293__480

ENGLISH: DO NOT SHAKE YOUR SHOES.

The above saying talks about shaking shoes of a guest who visited a certain family. This guest took off his shoes and wanted to shake them off after arriving at the family which he visited. The family members forbade him to shake his shoes, because such an act could mean cursing them. That is why they told him that, “do not shake your shoes.”

This saying is compared to a man who has a generous heart in his family life. Such person welcomes guests who visit him in his family, because of his generous heart, in his life. He manages to get many blessings enough to get rich and live well with his people, in his life.

This person is similar to those who stopped their guest who wanted to leave a curse on their family by shaking off his shoes, because he also rejects the curse by welcoming guests who visit him at his family. That is why he tells his guest that, “do not shake your shoes.”

This saying teaches people about being generous enough to receive their guests and take good care of them, so that they can get blessings of getting rich for living well with their societal members in their lives.

Mark 6:11 – 12.

Exodus 3:4 – 5.

Matthew 10: 14 – 15.