1049. LYAGUKUNGA MIKOB’A.

Imbuki ya kahayile kenako, ilolile bhukungi bholi ginhu litanda. Lyalihoyi ling’ombe ilo lyalilitanda ugusheng’wa kunguno ya bhuhala bholyo. Abhanhu ulu bhahaya ugulishema lyapelaga lyabhashiga bhaduma ugulishema. Nose bhiyangula gulikunga mikanda umumagulu galyo na lyuzunya lulu ugusheng’wa. Hunagwene abhanhu bhenabho bhalitana iliong’ombe linilo giki, “lyagukunga mikob’a.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinambu ugutung’wa na bhiye umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga alemile ugutung’wa josejose nabhiye na hangi agashoshaga mihayo bho makala ukubhiye kunguno ya nhinda jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguibheja ikaya yakwe kunguno ya bhulambu bhokwe ubho gubhashokeja mihayo ya nhani abhiye, umumahoya gakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ng’ombe inhanda iyo yalemaga ugusheng’wa mpaga yutungwa mikob’a, kunguno nuweyi alinambu uyo alemile ugutung’wa guja kunhimo gosegose na bhiye umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “lyagukunga mikob’a.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja bhulambu bho guzunya gutung’wa na bhiye umuchalo jabho, kugiki bhadule gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, umuchalo jabho jinijo.

Wagalatia 3:1-8.

KISWAHILI: LA KUFUNGA MIKANDA.

Chanzo cha msemo huo chaangalia ufungaji wa mkanda kwenye kitu ambacho ni kikali kuguswa. Alikuwepo ng’ombe mmoja ambaye alikuwa hataki kukamuliwa kwa sababu ya ukorofi wake. Mwishowe watu waliamua kumfunga mkanda miguuni mwake ndipo akakubali kukamuliwa. Ndiyo maana watu hao walimuita ng’ombe huyo kwamba ni “la kufunga mikanda.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mwenye kiburi katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hataki kutung’wa kwenda kufanya chochote na wenzake, na tena huwajibu watu kwa kauli mbaya, kwa sababu ya kiburi chake hicho, maishani mwake. Yeye hushindwa kutengeneza familia yake kwa sababu ya kiburi chake hicho cha kuwajibu wenzake kwa maneno mabaya, katika maongezi yake.

Mtu huyo, hufanana na yule ng’ombe mjeuri aliyekataa kukamuliwa, mpaga akafungwa mkanda miguuni mwake ndipo akakubali, kwa sababu naye hukataa kutumwa na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita kuwa ni “la kufunga mikanda.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia ya kuwa na kiburi kwa kukubali kutumwa na wenzao, ili waweze kusaidiana vizuri katika kuyatekeleza majukumu yao, kijijini mwao.

Wagalatia 3:1-8.

cow-7301439__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.