1050. SAMA YATINDIKWA NGOKO.

Akahayile kenako, kalolile bhukeleja bho ng’wa munhu uyo ahayaga gusama bho gulindila gumishiwa na ngoko ulujihila. Umunhu ng’wunuyo, ahayaga gusama bho gulindila gumishiwa na ngoko ulu jahila kunguno oli na tulo nyinghi. Uweyi oduka alalile duhu mpaga nose wela ubhujiku kunguno jalijakeleja uguhila inkogo ulushugu lunulo. Hunagwene abhanhu bhagang’ila giki, “sama yatindikwa ngoko.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agilendejaga uguja tumama imilimo yakwe, mpaga nose lyashila ilikanza lya milimo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikala wiyibhiye bhuli makanza uguja ugujutumama imilimo yakwe kunguno ya kutogwa tulo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agachelelagwa ugulima bhuli ng’waka kunguno ya wilendeja bhokwe bhunubho ugujutumama imilimo yakwe yiniyo, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsami uyo olindilaga gumishiwa na ngoko mpaga nose ukeleja ugusama, kunguno nuweyi agilendejaga ugutumama imilimo yakwe mpaga nose lyashila ilikanza lya guitumama imilimo yiniyo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “sama yatindikwa ngoko.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya guleka gwilendeja guja gujutumama milimo yabho bho gwanguha ugumisha, kugiki bhadule gutumama milimo mitale iyagubhapandikila sabho ningi jagubhambilija chiza, umuwikaji bhobho.

Mathayo 25:1-13.

Luka 21:36.

KISWAHILI: UHAMAJI ULICHELEWESHWA NA KUKU.

Msemo huo, huangalia uchelewaji wa mtu kuhama aliyesubiri kuamushwa na kuku wanapowika.  Mtu huyo, alitaka kuhama kwa kusubiri kuku wawike ndipo aamuke na kuanza safari yake hiyo ya kuhama. Yeye aliendelea kulala tu mpaka asubuhi kwa sababu jogoo nao walichelewa kuwika siku hiyo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “uhamaji ulicheleweshwa na kuku.”

Msemo huyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayejisahau kwenda kufanya kazi zake, mpaka muda wa kufanya kazi hizo unapita, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa amejisahau kila wakati kwenda kuyatekeleza majukumu yake kwa sababu ya kupenda kwake usingizi, maishani mwake. Yeye huchelewa kulima kila mwaka kwa sababu ya kujisahau kwake huko, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule mhamaji aliyesubiri kuamushwa na kuku wanapowika, mpaka mwishowe akachelewa kuhama, kwa sababu naye hujisahau kwenda kuyatekeleza majukumu yake, mpaka muda wa kufanya kazi hizo unapita, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “uhamaji ulicheleweshwa na kuku.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha uchelewaji wa kwenda kufanya kazi zao, kwa kuwahi kwenda kuzitekeleza kazi zao hizo, ili waweze kufanya kazi kubwa za kuwapatia mali za kutosha kuwasaidia maishani mwao.

Mathayo 25:1-13.

Luka 21:36.

rooster-5544252__480

animal-3242121__480

rooster-233898__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.