heritage

1232. JIDUMULA BHABODO.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile munhu uyo otulaga bhanhu abho abhakile amasala. Umunhu ng’wunuyo, oyelaga na nanha gokwe go guntulila uluumona uyo annebhije amasala kunguno ya miganiko gakwe ayo galigantuula chiniko. Uweyi agakumuka noyi umuchalo jakwe kunguno ya kikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagayung’witana giki, “jidumula bhabodo.”

Akahayile kenako, kagalengijiyagwa kuli munhu uyo agabhibhonelaga abhanhu abho bhali na masala magehu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhibhonelaga abhanhu abho bhali na masala magehu uko alibhitila kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga mamihayo mingi aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya wibhoneji bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo obhatulaga abhanhu abho abhalebhije amasala, kunguno nuweyi agabhibhonelaga abhanhu abha masala magehu umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhang’witanaga giki, “jidumula bhabodo.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuleka gubhibhonela abhanhu abho bhadidujije umumasala gabho, bho gubhambilija chiza, kugiki bhadule gupandika mbango ja gwikala chiza na bhichabho, umukaya jabho.

1Wakorintho 14:11.

Warumi 2:20.

1Wakorintho 14:16.

Wagalatia 3:3.

KISWAHILI: MPIGA WENYE AKILI PUNGUFU.

Chanzo cha msemo huo, huongelea mtu yule aliyekuwa akiwapiga watu aliowazidi akili. Mtu huyo, alikuwa akitembea na fimbo ya kuwapigia watu hao aliowazidi akili kwa sababu ya mawazo yake kumtuma kufanya hivyo. Yeye alijulikana sana katika kijiji chake kwa sababu ya maisha yake hayo. Ndiyo maana watu walimuita jina la “mgiga wenye akili pungufu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwaonea watu wenye akili pungufu, katika maisha yake. Mtu huyo, huwaonea watu hao wenye akili pungufu anakotembelea kwa sababu ya majivuno yakwe ya kuwadharau watu hao, maishani mwake. Yeye hupata matatizo ya kusumbulia na kesi nyingi kwenye familia yake hiyo kwa sababu ya kuwaonea watu hao wasiona hatia, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyewapiga watu aliowazidi akili, kwa sababu naye huwaonea watu walio na akili pungufu, katika maisha yake. Ndio maana watu humuita jina la “mgiga wenye akili pungufu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kuwaonea watu wasiojiweza maishani mwao, kwa kuwasaidia vizuri watu hao, ili waweze kupata Baraka za kuishi kwa amani na wenzao, katika familia, zao.

1Wakorintho 14:11.

Warumi 2:20.

1Wakorintho 14:16.

Wagalatia 3:3.

ENGLISH: A HITTER OF THOSE WHO HAVE LESS INTELLIGENCE.

The source of this saying speaks of the person who used to beat people who were out of their mind. Such man walked with a stick for hitting those people because of his thoughts that caused him to do so. He was well known in his village because of such behavior. That is why people called him “a hitter of those who have less intelligence.”

This saying is compared to a person who oppresses the mentally retarded ones in his life. Such person treats those people who have are slow in thinking where he visits because of his pride. He gets many problems and lawsuits in his family because of oppressing those innocent people in his life.

This person is similar to the one who beat people who had less intelligent, because he also oppresses people who are slow in thinking in his life. That is why people call him “a hitter of those who have less intelligence.”

This saying teaches people to stop oppressing the less fortunate ones in their lives, by helping them well, so that they can receive blessings of living in peace with their people in their families.

1 Corinthians 14:11.

Romans 2:20.

1 Corinthians 14:16.

Galatians 3:3.

zulu-kingdom-3411052_1280

1229. NAGISHA NABHULICHA.

Imbuki ya ulusumo lunulo, ilolile munhu uyo agabhagiisha bhanhu abho bhalibhingi, bhuzunya bhagehu duhu. Hunagwene agayomba giki, “nagisha nabhulicha.” Umunhu ng’wunuyo, agashokela ugugiisha bho lilaka litale, huna bhuzunya bhingi.

Ugubhulicha ili gulima na gubhibha mbiyu juzwa bho kulekule, nulu yuzwa imo duhu. Giko lulu, unimi ng’wunuyo agashokelaga ugubhiza mbiyu huna jazwa nyingi niyo chiza.

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho jelwa ng’holo chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga milimo yakwe bho gumana ushokela aho obhona giki itali ugubhelela chiza, kunguno ya witegeleja na bhukamu bhokwe ubho gutumama milimo yakwe chiza bhunubho. Uweyi agaponaga majiliwa mingi noyi aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya gutumama milimo yakwe bho bhukamu na witegeleja bhutale bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agashokela chiza ugiisha aho bhazunya bhagehu mpaga nose bhuzunya bhingi, kunguno nuweyi agatumama milimo yakwe na witegeleja bho gushokela gutumama aho itali ugubhelela chiza, umumilimo yakwe yiniyo. Hunagwene agayombaga giki, “nagisha nabhulicha.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho na witegeleja bho gushokela chiza aho idinabhelela imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umukaya jabho.

2Wakorintho 9:6.

Wagalatia 6:7-9.

KISWAHILI: NIMESALIMIA WAMEITIKIA WACHACHE.

Chanzo cha methali hiyo huangalia mtu aliyesalimia watu wengi, wakaitikia wachache tu. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimesalimia wameitikia wachache.” Mtu huyo, alirudia kuwasalimia tena hao watu kwa sauti kubwa zaidi kuliko ile aliyoitumia mwanzoni. Yeye alipofanya hivyo, waliitikia watu wengi zaidi kuliko wale wa kwanza.

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi zake kwa ufuatiliaji mzuri sana, katika maisha yake. Mtu huyo, huyatekeleza majukumu yake kwa kurudia kila pale anapoona kuwa hapajaisha vizuri, kwa sababu ya bidii yake na umakini wake huo katika kufanya kazi zake. Yeye hupata mazao mengi sana katika familia yake kwa sababu ya kufanya kazi kwa bidii na umakini mkubwa, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyesalimia watu wengi, wakaitikia wachache, akarudia kuwasalimia watu hao kwa sauti kubwa zaidi, mpaka wakaitikia wengi, kwa sababu naye huyatekeleza majukumu yake kwa kurudia pale anapoona kwamba hapajaisha vizuri, mpaka kazi yote inaisha. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimesalimia wameitikia wachache.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kutekeleza majukumu yao kwa umakini wa kuparudia pale ambapo hapajafanyika vizuri, mpaka kazi yote imalizike vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao.

2Wakorintho 9:6.

Wagalatia 6:7-9.

ENGLISH: I HAVE GREETED A FEW OF THEM HAVE RESPONDED.

The source of the over head proverb looks at a person who greeted many people, only a few of them responded. That is why he said that, “I have greeted a few of them have responded.”

This man repeated to greet them in a louder voice than the one which he used at first. When he did that, they responded to more people than the first ones.

This proverb is compared to a person who does his works with a very good follow-up, in his life. Such person carries out his duties by repeating whenever he sees that it has not ended well, because of his diligence and his focus in doing his works. He gets a lot of crops in his family because of hard working and great focus, in his life.

This person is similar to the one who greeted many people but a few of them responded, and repeated greeting them with a louder voice, until they responded to many, because he also carries out his duties by repeating when he sees that it has not ended well, until all the work is finished. That is why he says that, “I have greeted a few of them have responded.”

This proverb teaches people about increasing enough effort to carry out their duties with the attention to repeat where it is not done well, until all the work is finished well, so that they can get a lot of success, in their families.

2 Corinthians 9:6.

Galatians 6:7-9.

woman-7455964_1280

1226. WIZUKA NG’WENDA GWA GWIKUMBA IKANZA WELAGA.

Oliyohi munhu uyo wikalaga muchalo jilebhe. Umunhu ng’wunuyo, agingila gulala umuchumba jakwe ukija ugwikumba ung’wenda mpaga wela aliyo imbeho yali nhali noyi. Uweyi akalala mpaga wela ubhujiku na wizuka gwikumba ng’wenda gokwe kunguno ya wiyibhu bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “wizuka ng’wenda gwa gwikumba ikanza welaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu ngosha uyo odila gutola nose unamhala na wiganika mhayo gwa gutola, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, wiganikaga mihayo yingi habhuyanda bhokwe mpaga nose unamhala na wandya gwiganika mhayo gwa gutola, kunguno ya gudilila milimo iyo idinasolobho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga ugubhuyegela ubhutoji bhokwe kunguno ya wiyibhu bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, akikolaga nuyo agiyibha gwikumba ng’wenda mpaga wela ubhujiku na wizuka ugugwikumba ung’wenda gunuyo, kunguno nuweyi igiyibha ugutola mpaga nose unamhala na wizuka gutola, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “wizuka ng’wenda gwa gwikumba ikanza welaga.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwanguha gutumama milimo yabho iyasolobho bho gwigulambija na bhukamu bhutale ahikanza lya milimo yabho linilo, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Yoshua Bin Sira 25:3.

KISWAHILI: UMEKUMBUKA SHUKA YA KUJIFUNIKA WAKATI KUMEKUCHA.

Alikuwepo mtu aliyekuwa akiishi kwenye kijiji fulani. Mtu huyo, aliingia chumbani mwake kulala bila kujifunika shuka wakati baridi ilikuwa kali sana. Yeye alilala mpaka asubuhi ndipo akakumbuka kujifunika shuka kwa sababu ya usahaurifu wake huo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umekumbuka shuka ya kujifunika wakati kumekucha.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mwanamume yule aliyechelewa kuoa mpaka akazeeka ndipo akafikiria kuoa, katika maisha yake. Mtu huyo, alikuwa akifikiria mambo mengine wakati wa ujana wake mpaka akazeeka ndipo akaanza kufikiria kuoa, kwa sababu ya kujali mambo yasiyo na faida, maishani mwake. Yeye alishindwa kuifurahia ndoa yake hiyo kwa sababu ya kujisahau kwake huko, wakati wa ujana wake, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejisahau kujifunika shuka wakati wa baridi kali, mpaka asubuhi ndipo akakumbuka kujifunika, kwa sababu naye alijisahau kuoa mpaka akazeeka, ndipo akakumbuka kuoa, maishani mwake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umekumbuka shuka ya kujifunika wakati kumekucha.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwahi kuyatekeleza majukumu yao ambayo ni muhimu kwa bidii kubwa unapofika wakati wake, ili waweze kuyafikia malengo yao vizuri na kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Yoshua Bin Sira 25:3.

ENGLISH: YOU HAVE REMEMBERED THE SHEET TO COVER YOURSELF WHEN IT WAS MORNING.

There was a man who lived in a certain village. He went into his room to sleep without covering himself with a sheet when it was very cold. He slept until morning then he remembered to cover himself with a sheet because of his forgetfulness. That is why people told him that, “you have remembered the sheet to cover yourself when it was morning.”

This proverb is related to the man who delayed marrying until he was old and then he thought about marrying, in his life. Such man was thinking about other things during his youth until he got old and then he started thinking about getting married, because he cared about useless things in his life. He failed to enjoy his marriage because of his self-forgetfulness there, during his youth, in his life.

This is like the one who forgot to cover himself with a sheet during the cold winter, until morning then he remembered to cover himself, because he also forgot to marry until he was old, then he remembered to marry, in his life. That is why people told him that, “you have remembered the sheet to cover yourself when it was morning.”

This proverb imparts in people an idea of carrying out their duties which are important with great effort when the time comes, so that they can achieve their goals well and achieve many successes in their lives.

Joshua Bin Sira 25:3.

girl-347850_1280

1225. DAGELALA GUBHONA KALYETO DUHU.

Bhalihoyi bhanhu abho bhalibhaja gujunlola ngeni uyo obhitilaga umuchalo jabho. Abhanhu bhenabho bhagaduma ugumona na gundebha chiza ungeni ng’wunuyo, kunguno agabhita wangu wangu aho bhasangwa bhiyebhaga. Hunagwene bhagayomba giki, “dagelela gubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagiyebhaga ugutumama imilimo yabho, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagajaga ugujutumama imilimo yabho bhagalendela yingi duhu iyo idina solobho kunguno ya wiyebhu bhobho bhunubho, umubhutumami bho milimo yabho. Abhoyi bhagakelaga bhuli ng’waka umukaya jabho kunguno ya gwiyebha kutumama milimo yabho yiniyo, bho gulendela yingi iyo idina solobho yoseyose, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nabho bhagaja gujunola ngeni bhugiyebha mpaga ubhita bhadamonile chiza, kunguno nabhoyi bhagajaga ugutumama imilimo yabho bhagiyibha bho gulendela iyo idina solobho yoseyose umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagayombaga giki, “dagelega kubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka gwiyebha gutumama milimo yabho bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale, kugiki bhadule kupandima matwajo mingi, umukaya jabho.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

KISWAHILI: TUMEKOMEA KUONA NUSU TU.

Walikuwepo watu walioenda kumuona mgeni aliyekuwa akipita katika kijiji chao. Watu hao, hawakuweza kumuona na kumfahamu vizuri mgeni huyo kwa sababu yeye alipita haraka wakati wao wakiwa wamejisahamu. Ndiyo maana walisema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hujisahau kufanya kazi zao, katika maisha yao. Watu hao, huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote kwao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko, katika utekelezaji wa majukumu yao. Wao hukosa chakula kila mwaka kwenye mashamba yao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko kufanya kazi zao, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na wale walioenda kumuona mgeni wakajisahau na kukomea kumuona nusu, kwa sababu nao pia huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote, maishani mwao. Ndiyo maana wao husema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kujisahau katika kuyatekeleza majukumu yao kwa kujibidisha kuzifanya kazi hizo kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

ENGLISH: WE HAVE ONLY SEEN HALF.

There were people who went to see a stranger who was passing through their village. Those people could not see and get to know the stranger well because he passed quickly while they were busy. That is why they said that, “we have only seen half.”

This saying is compared to people who forget to do their works, in their lives. Those people go to do their works by wasting their time caring about things that are of no benefit to them, because of their self-indulgence in the implementation of their duties. They lack food every year in their fields, because of their indulgence in doing their works, in their lives.

Those people are like those who went to see a stranger and forgot themselves by wasting their time in useless things until they ended up seeing him only half way, because they also go to do their works and waste their time worrying about things that have no benefit in their lives. That is why they say that, “we have only seen half.”

This saying imparts in people an idea of stopping from wasting their time in useless things themselves enough to carry out their responsibilities by forcing themselves to do those tasks with great effort, so that they can get a lot of success, in their families.

Habakkuk 1:11.

Luke 19:1-3.

africa-5274086_1280

 

 

 

1218. LIKOLO LIGULU NULU UGULINYAMANGA NA OLIKANGILA.

Yaliyohi nholo iyo yalidigwaga uguhang’wa na bhadimi bhayo. Inholo yiniyo yajaga gujulya jiliwa ja jamumigunda ya bhanhu bho nduhu ugushoka nulu ilitulwa na bhadimi bhayo, kunguno ya bhugulu bhoyo bhunubho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayomba giki, “likolo ligulu nulu ugulinyamaga na olikangila.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alemile uguhang’wa na bhiye ulu ohubhaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agahadikijaga gwita iyo alitogwa bho nduhu ugushoshiwa ijina guhang’wa nabhiye nulu ibhize ya bhubhi adoyaga kunguno ya bhujidahang’wa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga ukoya na mihayo yagwikenya na bhiye aha kaya yakwe kunguno ya gubhiitila yabhubhi yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni likolo iligulu ilo lyalemaga uguhang’wa na bhadimi bhalyo, kunguno nuweyi alemile uguhang’wa na bhiye uluohubhaga, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “likolo ligulu nulu ugulinyamaga na olikangila.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza bhigwi ulu bhalilemejiwa gwita miito gabhubhi na bhichabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Yahana 10:1-4.

Zaburi 115:6.

1Petro 5:5-7.

Isaya 6:10.

KISWAHILI: KONDOO KIZIWI HATA UNAMRUDISHA NDIO UNAMSINDIKIZA.

Alikuwepo kondoo aliyekuwa hazikii anaporudishwa na wachungaji wake. Kondoo huyo, alikuwa akienda kula mazao ya chakula cha watu bila kukubali kurudishwa hata kama akipigwa na wachungaji hao aliendelea na safari yake ya kwenda kula mazao hayo, kwa sababu ya kutokusikia kwake huko. Ndiyo maana watu hao walisema kwamba, “kondoo kiziwi hata unamrudisha ndio unamsindikiza.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukataa kuong’wa na wenzake anapokosea, katika maisha yake. Mtu huyo, hulazishimisha kufanya jambo bila kuacha hata kama litakuwa ovu kwa kutokubari kuong’wa au kushauriwa na wenzake hao, kwa sababu ya kutokusikia kwake huko, maishani mwake. Yeye huishi katika mahangaiko ya ugonvi na watu kwenye familia yake, kwa sababu ya kuwatendea maovu wenzake hao, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule kondoo kiziwi aliyekataa kurudishwa na wachungaji wake, kwa sababu naye hukataa kushauriwa na wenzake anapoamua kutenda maovu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kondoo kiziwi hata unamrudisha ndio unamsindikiza.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na usikivu wanaposhauriwa kuacha kutenda maovu, ili waweze kutenda mema yawezayo kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Yahana 10:1-4.

Zaburi 115:6.

1Petro 5:5-7.

Isaya 6:10.

ENGLISH: A DEAF SHEEP EVEN IF YOU BRING IT BACK, YOU ARE JUST ESCORTING IT.

There was a sheep that was not hearing when it was returned by its shepherds. Such sheep normally went to eat people’s food crops without accepting to be returned even if it was beaten by the shepherds. It continued his journey to eat those crops, because of his deafness. That is why those people said that, “a deaf sheep even if you bring it back you are just escorting it.”

This saying is related to a person who refuses to be told by his nobles when he is wrong, in his life. Such person forces to do something without stopping even if it is an evil one by not accepting to be persuaded or advised by those colleagues, because of his lack of hearing in his life. He lives in worries of conflict with people in his family, because of his evil treatments to his family members in life.

This person is like a deaf sheep that refused to be taken back by its shepherds, because he also refuses to be advised by his people when he decides to do evil in his life. That is why people tell him that, “a deaf sheep even if you bring it back you are just escorting it.”

That saying, teaches people to be attentive when they are advised to stop doing evil, so that they can do good things that can develop their families well, in their lives.

John 10:1-4.

Psalm 115:6.

1 Peter 5:5-7.

Isaiah 6:10.

sheep-7723970_1280