Fr. Joe Healey

840. NADIDUJIJE.

Akahayile kenako, kalolile bhukuji bho ng’wa munhu nhebhe. Ubhukuji bhunubho bhugabhizaga bho namhala, nulu ngikulu uyo omala inguzu jakwe ija guitumama imilimo yakwe bho weyi ng’winikili. Unkuji ng’wunuyo, agikalaga bho gwambilijiwa na bhiye abho bhatali najo inguzu jabho. Hunagwene agayombaga giki, “nadidujije.”

Akahayile kenako, kagalenagnijiyagwa kuli munhu uyo adadulile ugwikala bho nduhu gwambilijiwa na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adidulije kunguno ya bhusatu, nulu jika josejose ijo jiganemejaga uguitumama imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Uweyi agikalaga bho gukoyakoya ugupandika ijiliwa ni jizwalo jakwe, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu namhala, nulu ngikulu uyo agikalaga bho gwambilijiwa na bhiye, kunguno nuweyi agikalaga bho gwambilijiwa na bhiye chiniko, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “nadidujije.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gubhambilija ugugamala wangu amakoye gabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala bho bhuyeji, shigu jose.

Mathayo 14:34-36.

Mathayo 5:3-9.

KISWAHILI: SIJIWEZI.

Msemo huo, huangalia kukua kwa mtu fulani. Kukua huko ni ile hali ya kufikia uzeeni kwenye hatua ambayo mtu hukosa nguvu za kujitegemea mwenyewe. Mzee huyo, huwa anaishi kwa kusaidiwa na wenzake ambao bado wanazo nguvu hizo. Ndiyo maana huwa anasema kwamba, “sijiwezi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hawezi kuishi bila kusaidiwa na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hawezi kujitegemea kwa sababu ya ugonjwa, au kilema fulani ambacho humzuia kuyatekeleza majukumu yake, katika maisha yake. Yeye huwa anaishi kwa kuhangaika katika kupata chakula, na mavazi yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mzee yule aliyeishiwa nguvu za kumwezesha kujitegemea mwenyewe, kwa sababu naye huwa anaishi kwa kusaidiwa na wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana huwa anasema kwamba, “sijiwezi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu wa kuwasaidia katika kuyatatua matatizo yao, maishani mwao, ili waweze kuishi kwa furani siku zote.

Mathayo 14:34-36.

Mathayo 5:3-9.

elderly-

old-

elder-

ENGLISH: I AM INCAPABLE.

This saying looks at the growth of a person. Growing up is the process of reaching old age at a time when a person lacks self-reliance in life. The old person lives with the help of others who still have that power. That is why this person often says, “I am incapable.”

This saying is likened to the person who cannot live without the help of others in life. Such person is not able to stand on his/her own because of an illness, or disability that prevents him/her from fulfilling the responsibilities in life. He/She lives by hardly getting food, and clothes in life.

This person is like the old person who had lost the ability to be self-supporting in life, because he/she too lives with the help of others in life. He/she does not depend on him/herself.  That is why he/she often says, “I am incapable.”

This saying teaches people on how to be patient enough to help each other in solving their problems in lives, so that they can live happily in their societies.

Matthew 14: 34-36.

Matthew 5: 3-9.

 

 

839. GWIMA BHO GUNENEKEJA.

Akahayile kenako, kingilile kuwimiji bho gutumila gugulu gumo. Uwimiji bhunubho, bhudi bho gwisendamija hanhu, kunguno bhudi bho magulu abhili. Ubhoyi bhudi bho gwima higiki, kunguno bhuli bho gugulu gumo duhu uyo gudadulile ugugubhucha umili ngima kulikanza lilihu. Hunagwene abhanhu bhagawitanaga giki, “gwima bho gunenekeja.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adimaga higiki bho gubhutumila chiza ubhudula ubho alinabho, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adagatumilaga chiza amasala gakwe ni nzugu ijo alinajo ijinagwiyenhela maendeleo aha kaya yakwe, kunguno ya gusendamila gwambilija na bhangi, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uyibheja chiza ikaya yakwe, kunguno ya gukija ugujitumila chiza inguzu jakwe, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oliwimila bho gugulu gumo, kunguno nuweyi adabhutumilaga chiza ubhudula bhokwe ijinagwima higiki, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki atogilwe, “gwima bho gunenekeja.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwima higiki bho gujitumamila chiza pye inguzu jabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwimila bho magulu abhili, ijinagujibheja chiza ikaya jabho.

Marko 1:46-52.

KISWAHILI: KUSIMAMA KWA KUNING’INIA.

Msemo huo, ulitokea kwenye usimamaji wa kutumia mguu mmoja. Usimamaji huo, siyo wa kuegemea kwenye kitu chochote, kwa sababu hautumii miguu miwili. Wenyewe siyo wa kuwa imara kwa sababu ni wa kutumia mguu mmoja ambao hauwezi kuubeba mwili mzima kwa muda mrefu. Ndiyo maana watu huuita kwamba, ni “kusimama kwa kuning’inia.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hautumii vizuri uwezo wake wote, kwa kujitegemea, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hazitumii vizuri akili zake wala uwezo alionao katika kujiletea maendeleo kwenye familia yake, kwa sababu ya kujijengea tabia ya kuwategemea wengine, maishani mwake.  Yeye hushindwa kuindeleza vizuri familia, kwa sababu ya kutokutumia vizuri nguvu zake, katika utekelezaji wa majukumu yake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyesimama kwa kutumia mguu mmoja, kwa sababu naye huwa hautumii vyema uwezo wake katika kujiletea maendeleo, kwenye familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, anapenda “kusimama kwa kuning’inia.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia uwezo wao wote, na akili zao katika kuyatekeleza vyema majukumu yao, maishani mwao, ili waweze kusimama kwa miguu miwili katika kuziendeleza vyema familia zao.

Marko 1:46-52.

masai-1

river-trading-

standing-

ENGLISH: TO STAND UNSTEADILY.

This saying came from one-legged way of standing of somebody. Such a standing is not dependent on anything, because it does not use two legs. It is not strong enough to support the body because it is of one leg that cannot carry the whole body for a long time. That is why people call it, “to stand unsteadily.”

This saying is applied to a person who does not make good use of all his/her abilities, independently in life. Such person does not make good use of his or her intelligence or ability to bring about development in his or her family, because he or she builds a habit of relying on others in his or her life. He/she fails to properly develop the family, because of misusing power, in fulfilling his/her daily duties in life.

This person is like the one who stood on one leg, because he/she also does not make good use of his/her ability enough to bring about development to the family. That is why people tell him/her that he/she has “to stand unsteadily.”

The saying imparts in people an idea on how to use their full potentials and their minds in fulfilling their responsibilities in their lives, so that they can stand on their own two feet in taking caring of their families.

Mark 1: 46-52

838. LILAKA LYATINIKAGA.

Akahayile kenako, kalolile bhutiniki bho lilaka lya ng’wa munhu nhebhe. Ililaka linilo, ligolechaga bhudamu bho mili gokwe, umunhu ng’wunuyo, umukikalile kakwe. Aliyo lulu, ulu munhu alisata, nulu onogaga, ililaka lyakwe ligalemaga ugufuma. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “lilaka lyatinikaga.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agikalaga ahumulile ahikanza lyaguyomba mhayo uyo bhalihaya bhagwigwe abhiye, umubhutumami bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agahumulaga kunguno aganogelaga milimo iyo idinasolobho, mpaga nose oduma uguyitumama iya solobho, umukikalile kakwe. Uweyi agadumaga ugubhatumamila chiza abhanhu bhakwe, kunguno ya gugayiwa ililaka lya bhubhalangila abhanhu bhenabho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsatu uyo agatina ililaka, kunguno nuweyi agikalaga ahumulile aho yigelelilwe afunye ilaka lya kuwabhalangila abhanhu bhakwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhang’wilaga giki, “lilaka lyatinikaga.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza ni laka lya gubhalumanya chiza abhichabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gubhalela chiza abhanhu bhabho bhenabho, umuwikaji bhobho.

Marko 1:29-31.

KISWAHILI: SAUTI IMEKATIKA.

Msemo huo, huangalia ukatikaji wa sauti ya mtu fulani. Sauti hiyo huonesha uimala wa mwili wake, mtu huyo. Lakini basi, mtu huyo akiwa mgonjwa au akiwa amechoka, sauti yake hukataa kutoka vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, “sauti imekatika.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa anakaa kimya anapotakiwa kuwaeleza wenzake jambo fulani, katika utekelezaji wa majukumu yake. Mtu huyo, hukaa kimya kwa sababu ya kujichosha kwa kujishugulisha na kazi zisizo na faida, mpaga anashindwa kuyatekeleza majukumu yenye faida kwa familia yake, katika maisha yake. Yeye hushindwa kuwatumikia vyema watu wake kwa sababu ya kukosa sauti ya kuwalelea vyema watu hao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule mgonjwa aliyekata sauti, kwa sababu naye huwa anakaa kimya anapotakiwa kuwaeleza watu wake jambo lililo la muhimu, kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “sauti imekatika.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na sauti yenye kauli ya kuwaunganisha wenzao, katika maisha yao, ili waweze kuwalea vyema watu wao, maishani mwao.

Marko 1:29-31.

female-

black-woman-

child--1-

ENGLISH: VOICE HAS BEEN CUT OFF.

This saying looks at the sound of someone. This sound reflects healthy of the body of that person. But then, if such person is sick or tired, his voice does not nicely come out. That is why people say, “the voice has cut off.”

This saying is applied to a person who is always silent even when he/she is asked to explain something to others in daily activities. This person is normally silent because of an exhaustion which is caused by engaging in unproductive works in fulfilling the daily responsibilities that can benefit his/her family.  Unfortunately he/she fails to serve the family members because of lacking the voice to take good care of them.

This person is like the patient who cut his/her voice, because he/she also keeps quiet when he/she is asked to tell the family members what is important enough to bring them progress in their lives. That is why people say, “the voice has cut off.”

This saying teaches people about having a voice that unites others in their families, so that they can take good care for their people in societies.

Mark 1: 29-31.

837. KUHUBHA NZILA HU GUMANA NZILA

Ulusumo lunulo, lwangila kuli munhu uyo uli mulugendo, ilina lwake Nsimizi. Nsimizi agandwa lugendo lokwe gufumila Ng’watuma guja Badi, iyo ili muwilaya ya Jishabu, Nkoa go Shinyanya, musi ya Tanzania.

Olina bhusiminzi bho masaa atandatu, umulegendo lunulo. Umunhu ng’wunuyo, agasiminza mpaga agati gati ya lugendo lokwe,  ugashiga hi bara ilo inzila yakwe jigabhiza ibhili. Nsimizi agalondeja nzila iyo iganchala Iboja badala ya Badi. Kubahati ya wiza, agatung’wana na Matogoro, uyo oli umo o bhanwani bhakwe bha kale.

Matogoro agamuja, “Nsimizi, ujile heyi?” Nsimizi agashosha, “Oh! najile Badi.” Matogoro agayomba “Loo! Ojimilaga inzila kunguno ijiniji jili chalo ja Iboja.” Nsimizi agabhuja, “nalondeje nzila ki iyo igunisha Badi?”

Matogoro agantongela bho guyomba, “Iki ojimilaga inzila, ugubhiza nhuguku noyi gwandija haha na guja bhutongi, kulebha umo oli igwandya. Londeja inzila iyi iyo ijile limo na limo mpaga Badi.”

Nzimizi agashosha, “Obheja noyi nwani one Matogoro ugunambilija. Lyehaga nailondeje inzila yiniyi bho nduhu uguileka mpaga inishishe Badi.”

Matogoro agashosha, “obheja gulumba, siminzaga na lubhango.”  Nsimizi agaja limo na limo gufuma Iboja mpaga ushiga Badi bho nduhu uguijimiza inzila yakwe imhya yiniyo, kunguno agapandika nzila mhya iyo ili ya ng’hana na yunshisha mpaga Badi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “guhubha nzila hugumana nzila.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhidohya bho gubhuja kubhichabho imihayo iyo bhadayimanile, umukikalile kabho, kugiki bhadule, gubhupandika ubhung’hana ubho gubhashisha uko bhajile, umuwikaji bhobho.

Yohana 14: 6:

Yohana 12:24:

1Wathesalonike 5:10:

Luka 15: 11-32.

KISWAHILI: KUKOSEA NJIA NDIYO KUJUA NJIA.

Methali hiyo hapo juu ilitokea kwa msafiri ambaye jina lake aliitwa Nsimizi. Nsimizi alianza safari yake kutoka Mwatuma kwenda Badi, ambayo inapatikana katika Wilaya ya Kishapu Mkoa wa Shinyanga nchini Tanzania.

Ilibidi atembee kwa masaa sita katika safari yake hiyo.  Mtu huyo, alipotembe karibia nusu ya safari yake, alifika mahali ambapo njia yake iligawanywa katika njia mbili. Nsimizi alifuata njia iliyompeleka Iboja badala ya Badi. Kwa bahati nzuri, alikutana na Matogoro, ambaye alikuwa mmoja wa marafiki zake wa zamani.

Matogoro akamuuliza, “Nsimizi, unaenda wapi.” Matogoro akajibu, “Oh! Naenda Badi. ” Matogoro alisema, “Loo! Umepotea njia kwa sababu hiki ni kijiji cha Iboja. ” Nsimizi aliuliza, “nifuate njia gani itakayonifikisha Badi?”

Matogoro alimwongoza kwa kusema, “Kwa kuwa umepotea njia, utakuwa makini zaidi kuanzia sasa kuliko vile ulivyokuwa hapo awali. Fuata njia hii ambayo inaenda moja kwa moja hadi Badi. ”

Nzimizi alijibu, “Asante sana rafiki yangu Matogoro kwa kunisaidia. Ngoja niifuate barabara hii kwa umakini nishikamana nayo hadi nitakapofika Badi. ”

Matogoro alijibu, “asante kushukuru, uwe na safari yenye baraka.”

Nsimizi alienda moja kwa moja kutoka Iboja hadi Badi bila kuipoteza njia yake hiyo mpya, kwa sababu alipata njia mpya ya kweli iliyomfikisha hadi Badi. Ndio maana watu husema kwamba, “kupoteza njia ndiyo kujua njia.”

ULINGANIFU WA KIBIBLIA

 Yohana 14: 6: “Yesu alisema:‘ Mimi ndimi njia, ukweli na uzima.’”

Yohana 12:24: “Amin, amin, nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa huzaa mbegu nyingi.”

1Wathesalonike 5:10: “Alikufa kwa ajili yetu ili tuishi pamoja naye.”

Luka 15: 11-32 “Yesu akaendelea kusema: “Kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na wana wawili. 12Yule mdogo akamwambia baba yake, ‘Baba, nipe urithi wangu.’ Hivyo akawagawia wanawe mali yake.

‘‘Baada ya muda mfupi, yule mdogo akakusanya vitu vyote alivyokwa navyo, akaenda nchi ya mbali na huko akaitapanya mali yake kwa maisha ya anasa. Baada ya kutumia kila kitu alichokuwa nacho, kukawa na njaa kali katika nchi ile yote, naye akawa hana cho chote. Kwa hiyo akaenda akaajiriwa na mwenyeji mmoja wa nchi ile ambaye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe. Akatamani kujishibisha kwa maganda waliyokula wale nguruwe, wala hakuna mtu aliyempa cho chote. ‘‘Lakini alipozingatia moyoni mwake, akasema, ‘Ni watumishi wangapi walioajiriwa na baba yangu ambao wana chakula cha kuwatosha na kusaza, bali mimi hapa nakufa kwa njaa! Nitaondoka na kurudi kwa baba yangu na kumwambia, ‘Baba, nimetenda dhambi mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili tena kuitwa mwanao, nifanye kama mmoja wa watumishi wako.’

Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake. “Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu. “Yule mtoto akamwambia baba yake, ‘Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’ “Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, mkamvike pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake. Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi. Kwa maana huyu mwanangu alikuwa amekufa na sasa yu hai tena, alikuwa amepotea na sasa amepatikana!’ Nao wakaanza kufanya tafrija. “Wakati huo, yule mwana mkubwa alikuwa shambani. Alipokaribia nyumbani, akasikia sauti ya nyimbo na watu wakicheza.

Akamwita mmoja wa watumishi na kumwuliza, ‘Kuna nini?’ Akamwambia, ‘Mdogo wako amekuja, naye baba yako amemchinja ndama aliyenona kwa sababu mwanawe amerudi nyumbani akiwa salama na mzima.’ Yule mwana mkubwa akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi baba yake akatoka nje na kumbembeleza.

Lakini yeye akamjibu baba yake, ‘Tazama! Miaka yote hii nimekutumikia na hata siku moja sijaacha kutii amri zako, lakini hujanipa hata mwana mbuzi ili nifurahi na rafiki zangu. Lakini huyu mwanao ambaye ametapanya mali yako kwa makahaba aliporudi nyumbani, wewe umemchinjia ndama aliyenona!’

“Baba yake akamjibu, “‘Mwanangu, umekuwa nami sikuzote na vyote nilivyo navyo ni vyako. Lakini ilitubidi tufurahi na kushangilia kwa sababu huyu mdogo wako alikuwa amekufa na sasa yu hai, alikuwa amepotea naye amepatikana.’ ””

MATUMIZI YA KISASA NA MATUMIZI YA KIDINI

 Methali hiyo inafundisha watu juu ya kuwa na mnyenyekevu wa kuwauliza watu wengine kwa ajili ya kuwafahamu yale ambayo hawajue. Hivyo, wakipotea njia, lazima waulize kwa wale wanaoihamu njia hiyo. Ni vizuri kuingalia hali hiyo na kufanya utafiti wakati umekosea kitu fulani maishi au umekoteza lengo lako. Usione aibu kwa kukaa kinya wakati haujui kitu.

Methali hiyo, inatumika kuwaelewesha watu ambao wamefanya makosa katika maisha yao, ili wawe waangalifu zaidi hadi kufikia hatua ya kutorudia kile kilichowasababisha kufanya vibaya. Hivyo, watu hao, wanapaswa kudumisha hali yao mpya ya maisha siku zote za maisha yao.

Methali hiyo hutumika kwa kuongeza ubunifu katika kuishi maisha mapya, ambayo mtu alipata baada ya Ubatizo na kupokea Sakramenti ya Upatanisho.

Kabla ya Ubatizo mtu huwa anaishi njia ambayo inaongoza kwenye upotevu isiyokuwa na uhakika. Lakini baada ya Ubatizo Mkristo hupata njia ya kweli ya kwenda kwenye uzima wa milele.

Kumbe, tunapotenda dhambi tunapotea njia; tunapokiri dhambi hizo, tunaipata njia ya kuelekea kwenye uzima wa milele.

Methali hiyo, hutumika katika kuongeza ujasiri kwa wale ambao wanakatishwa tamaa na kushindwa kwao kwa hapo awali, kwa kuwakumbusha nafasi yao ya pili ya kufurahiya maisha ya furaha kupitia toba.

Hivi ndivyo hadithi ya Mwana Mpotevu inavyotuambia. Methali hii ya Wasukuma inahimiza watu kuwa na nguvu ya kutosha kutimiza malengo yao ya kiroho kwa kutumia talanta na miradi yao licha ya shida zao ambazo zinaweza kupatikana maishani.

Methali hiyo inahimiza watu kuanza miradi mpya ya kiroho, kiuchumi na kijamii ambayo inaweza kuwapa mahitaji ya kiroho, na yale ya msingi kama vile chakula, malazi na nguo, njiani kuelekea kwenye ufalme wa mbinguni.

Inatukumbusha wanadamu kuwa majaribu na makosa yalisababisha uwepo wa Watakatifu katika Kanisa. Waanzilishi wa mashirika ya kitawa walitumia talanta zao kiasi cha kutosha kumchukua Yesu na kumpeleka kwa wenzao kwa kuiishi imani yao kwa vitendo na kutuonyesha mifano mizuri ya kufuata.

Methali kama hiyo inatumika pia katika uvumbuzi wa kisayansi wanauweza kuupata wanadamu. Maendeleo ya kilimo, magari, ndege, meli, uvumbuzi mpya na kadhalika, ni matokeo ya majaribio na makosa ambayo tunaita “majaribio ya kisayansi.”

Kwa hiyo, ni kweli kwamba kupotea njia ni kujua njia, kwa sababu maisha yetu ya kiroho ni mchakato endelevu wa kurekebisha maisha yetu ili tuweze kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu.

KUMBUKA: Methali hii ya wasukuma ni kwa heshima ya Padri wa kimishonari wa shirika la Maryknoll, Don Sybertz, MM. Alikuwa akitafuta maana ya methali hii kabla ya kifo chake mnamo 19 Aprili, 2020.

ENGLISH: TO LOSE THE WAY IS TO FIND THE WAY.

The above proverb originated from a traveler whose name was Nsimizi. Nsimizi started his journey from Mwatuma to Badi that is found in Kishapu District of Shinyanga Region in Tanzania. He had to walk for six hours.  Half-way he reached a place where his way was divided into two ways. Nsimizi followed a way that led him to Iboja instead of Badi.

Fortunately, he met Matogoro, who was one of his old friends. Matogoro asked him, “Nsimizi, where are you going.” Matogoro replied, “Oh! I am going to Badi.” Matogoro said, “Oh! You have lost your way because this is Iboja village.”

Nsimizi asked, “which way should I follow to Badi?” Matogoro directed him by saying, “Since you have lost your way, you will become more carefully from now on than how you were before. Follow this way that goes directly to Badi.”

Nzimizi responded, “Thanks a lot my friend Matogoro for helping me. Let me seriously follow this road by sticking to it until I reach Badi.” Matogoro responded, “you are welcome, have a blessed journey.”

Nsimizi went straight from Iboja to Badi without losing his new way because he found the true new way to Badi. That is why people say, to lose the way is to find the way. Or losing the way is finding the way.

Biblical Parallels

John 14:6: “Jesus said: ‘I am the way, the truth and the life.’”

John 12:24: “Unless a grain of wheat falls into the earth and dies, it remains alone; but if it dies, it bears much fruit.”

1 Thessalonians 5:10: “He died for us so that we may live together with him.”

Luke 15:11-32: Parable of the Prodigal Son.

Contemporary Use and Religious Application

Be humble and ask other people. If you lose the way, you have to ask. Check out the situation and do research when you are wrong or off target. Don’t be disappointed when you do not know something.

It is applied to giving awareness to people who have done mistakes in their lives so that they become more careful to the point of not repeating what caused them to do wrong. They should maintain their new status of life throughout their lives.

It is applied to increasing creativities in living a converted life that one got after Baptism and the Sacrament of Reconciliation. Before Baptism one lives a way that leads to uncertainty After Baptism a Christian finds the true way to eternal life. When we commit sins we lose the way; when we confess those sins, we find the way to eternal life.  It is used to increase confidence in those who become discouraged by their previous failures, by reminding them of their second chance to enjoy a happy life through repentance. This is what the Prodigal Son story tells us.

This Sukuma proverb encourages people to be strong enough to actualize their spiritual goals by using their various talents and projects despite their difficulties that can be found in life. It encourages people to start new spiritual, economic and social projects that can provide them with spiritual needs, as well as their basic needs such as food, shelter and clothes, on the way to the heavenly kingdom.

It reminds us human beings that trials and errors led to the presence of the Saints in the Christian Churches. The founders of religious congregations applied their talents enough to take Jesus to their fellow human beings by putting their faith into practice and expressing good examples to us.

Such a proverb is also applicable to scientific discoveries of human beings. Agricultural developments, cars, airplanes, ships, new inventions and so on, are the results of trials and errors that we call “scientific experiments.”

Therefore it is true that to lose the way is to find the way. Or losing the way is finding the way because our spiritual life is a continuous process of adjusting our lives to live according to the will of God.

NOTE: This Sukuma Proverb is in honor of Maryknoll missionary priest Father Don Sybertz, MM. He was researching the meaning of this proverb before he died on 19 April, 2020. See more information on the:

Maryknoll Africa Region Website
https://maryknollafrica.org

Similar examples can be found on the:

African Proverbs, Sayings and Stories Website
https://www.afriprov.org

Text by:

Rev. Donald Sybertz, MM (deceased)
Maryknoll Fathers and Brothers.

black-1

kenya1

smile-

836. BHUDUGU BHO GUGULU NA NKONO.

Ubhudugu bho gugulu nu nkono bhuli bho gwigunana bhuli ng’wene ulu opandikaga makoye. Ugugulu gugasiminzaga goguchala unkono hanhu uko bhuli ubhutumamilo, kunguno gulinabho ubhudula bhunubho.

Giko lulu, nu nkono nago gugagudimaga ugugulu ulu gulihaya gugwingija makoye ayo gulinago. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “bhudugu bho gugulu na nkono.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa ku bhanhu abho bhagiyambilijaga bhuli ng’wene ulu opandikaga mayange, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhalina bhumo ubho bhugabhinhaga nguzu ja gugingija makoye gabho genayo. Abhoyi bhagagamalaga wangu amakoye gabho genayo, kunguno ya bhukihamo bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nu wiyambilija ubho gugulu nu nkono, kunguno nabhoyi bhagiyambilija halumo uguginja amakoye ayo bhaligo, umukikalile kabho. Hunagwene abhanhu bhagabhitana giki, “bhudugu bho gugulu na nkono.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kubhiza na bhumo bho gwiyambilija chiza, uguginja makoye gabho pye nu uguyitumama chiza imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

1 Wakorintho 12:12-14.

KISWAHILI: UNDUGU WA MGUU NA MKONO.

Undugu wa mguu na mkono ni wa kusaidiana katika kutatuliana matatizo. Mguu huwa unatembea kwa kuupeleka mkono kule ambako utafanyia kazi, kwa sababu unao uwezo huo.

Vivyo hivyo, na mkono nao huwa unaushiga mguu unapotaka kuutatulia matatizo yalioukumba, kwa sababu nao unao uwezo huo. Ndiyo maana watu huuita ushirikianao huo kuwa ni wa, “undugu wa mguu na mkono.”

Methali hiyo, hulinagnishwa kwa watu wale ambao huishi kwa kusaidiana kila mmoja anapokumbwa na matatizo, katika maisha yao. Watu hao, huwa na umoja ambao huwapatia nguvu za kuyatatua matatizo yao kwa pamoja. Wao hufanikiwa kuyatatua matatizo yao mapema kwa sababu ya huwafundisha pia watu wao namna ya kushikiriana vizuri katika kuleta maendeleo yao, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na ushirikiano wa mguu ya mkono, kwa sababu nao husaidiana kwa pamoja katika kuyatatua matatizo yao, maishani mwao. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba wana “undugu wa mguu na mkono.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na umoja wa kusaidiana vizuri katika kuyatatua matatizo yao, na katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

1 Wakorintho 12:12-14.

foot-

child--1

african-mother-and-child-

ENGLISH: LEG AND HAND KIN.

The leg and hand union are mutually supportive in solving problems. The leg walks for moving the hand to where it is going to work because of having that ability.

In the same way, the hand can also support the leg when it wants to solve problems, because it also has such ability. That is why people call this partnership a “leg and hand kin.”

This proverb is applied to people who live by supporting each other when they are in distress in their lives. These people have a unity that gives them strength for solving their problems together. They succeed in deciphering them early because they also teach their people on how to work together enough to bring about development to their societies.

These people, in turn, resemble the mutual supportive relationship of the leg and hand in disentangling hitches, because they also support each other in unraveling their glitches in their lives. That is why people tell them that they have a “leg and hand kin.”

This proverb teaches people on how to be united together enough to support each other better in cracking their difficulties while they carry out their daily responsibilities, so that they can have more success in their lives.

1 Corinthians 12: 12-14.