Akahayile kenako, kingilile kuwimiji bho gutumila gugulu gumo. Uwimiji bhunubho, bhudi bho gwisendamija hanhu, kunguno bhudi bho magulu abhili. Ubhoyi bhudi bho gwima higiki, kunguno bhuli bho gugulu gumo duhu uyo gudadulile ugugubhucha umili ngima kulikanza lilihu. Hunagwene abhanhu bhagawitanaga giki, “gwima bho gunenekeja.”
Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adimaga higiki bho gubhutumila chiza ubhudula ubho alinabho, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adagatumilaga chiza amasala gakwe ni nzugu ijo alinajo ijinagwiyenhela maendeleo aha kaya yakwe, kunguno ya gusendamila gwambilija na bhangi, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uyibheja chiza ikaya yakwe, kunguno ya gukija ugujitumila chiza inguzu jakwe, umukikalile kakwe.
Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oliwimila bho gugulu gumo, kunguno nuweyi adabhutumilaga chiza ubhudula bhokwe ijinagwima higiki, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki atogilwe, “gwima bho gunenekeja.”
Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwima higiki bho gujitumamila chiza pye inguzu jabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwimila bho magulu abhili, ijinagujibheja chiza ikaya jabho.
Marko 1:46-52.
KISWAHILI: KUSIMAMA KWA KUNING’INIA.
Msemo huo, ulitokea kwenye usimamaji wa kutumia mguu mmoja. Usimamaji huo, siyo wa kuegemea kwenye kitu chochote, kwa sababu hautumii miguu miwili. Wenyewe siyo wa kuwa imara kwa sababu ni wa kutumia mguu mmoja ambao hauwezi kuubeba mwili mzima kwa muda mrefu. Ndiyo maana watu huuita kwamba, ni “kusimama kwa kuning’inia.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hautumii vizuri uwezo wake wote, kwa kujitegemea, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hazitumii vizuri akili zake wala uwezo alionao katika kujiletea maendeleo kwenye familia yake, kwa sababu ya kujijengea tabia ya kuwategemea wengine, maishani mwake. Yeye hushindwa kuindeleza vizuri familia, kwa sababu ya kutokutumia vizuri nguvu zake, katika utekelezaji wa majukumu yake, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyesimama kwa kutumia mguu mmoja, kwa sababu naye huwa hautumii vyema uwezo wake katika kujiletea maendeleo, kwenye familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, anapenda “kusimama kwa kuning’inia.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuutumia uwezo wao wote, na akili zao katika kuyatekeleza vyema majukumu yao, maishani mwao, ili waweze kusimama kwa miguu miwili katika kuziendeleza vyema familia zao.
Marko 1:46-52.
ENGLISH: TO STAND UNSTEADILY.
This saying came from one-legged way of standing of somebody. Such a standing is not dependent on anything, because it does not use two legs. It is not strong enough to support the body because it is of one leg that cannot carry the whole body for a long time. That is why people call it, “to stand unsteadily.”
This saying is applied to a person who does not make good use of all his/her abilities, independently in life. Such person does not make good use of his or her intelligence or ability to bring about development in his or her family, because he or she builds a habit of relying on others in his or her life. He/she fails to properly develop the family, because of misusing power, in fulfilling his/her daily duties in life.
This person is like the one who stood on one leg, because he/she also does not make good use of his/her ability enough to bring about development to the family. That is why people tell him/her that he/she has “to stand unsteadily.”
The saying imparts in people an idea on how to use their full potentials and their minds in fulfilling their responsibilities in their lives, so that they can stand on their own two feet in taking caring of their families.
Mark 1: 46-52