Sukuma Riddles

1033. KALAGU – KIZE. SHEPAGA NANE NASHEPE DUGUTUNG’WANHILA KUB’UKWINGWA – NSHIBI MKIMBILI.

Ikalagu yiniyo, yihoyelile higulya ya bhuzwaji bho nshibi go mkimbili. Unshibi gunuyo gugabhitiyagwa mumagwasijo ga mbutula nulu ga msulubhale ya ng’wa munhu nhebhe. Unzwaji ogo agajaga ushepya bhuli higwasijo lyene mpaga gwiza go gotung’wanhila kung’humbi. Ing’humbi yiniyo ha hab’ukwingwa lulu. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “shepaga nane nashepe dugutung’wanhila kub’hukwingwa – Nshibi mkimbili.”

Ikalagu yiniyo, yigalenganijiyagwa ku bhana bha myaji umo abho ligashigaga likanza bhaja bhagalumana ahali myaji obho ng’wunuyo, umukikalile kabho. Abhana bhanebho, bhali bha myaji umo abho bhabalasana ahakaya yabho bhuja bhuli ng’wene kumilimo yakwe abho bhagalumanaga bhuli ng’waka ahali myaji obho ng’wunuyo kunguno ya kungisha na gwiyizukiza mihayo ya gwikala chiza na bhanhu. Abhoyi bhaganhanhanaga chiza umyaji obho gung’wambilija na gwidilila chiza kunguno ya likujo lyabho ukuli myaji obho na witogwi bhobho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga nu nshibi go mkimbili uyo gugashepaga mumalungulo ga sulubhale nulu mbutula, gogalumana aha ng’humbi, kunguno nabhoyi bhagalumanaga bhuli ng’waka ahali myaji obho bhang’wambilija na gwiizukija mihayo ya gwikala chiza na bhanhu. Hunagwene bhagiganilaga giki, “shepaga nane nashepe dugutung’wanhila kub’hukwingwa – Nshibi mkimbili.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhalanghana bhabyaji bhabho bho gubhambilija chiza na gwiyizukija mihayo ya gwikala chiza na bhanhu kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

Mwanzo 5:3 – 32.

Mathayo 1: 1-17.

 

KISWAHILI: PENYA NAMI NIPENYE TUTAKUTANA UKWENI – MKANDA KIUNONI.

Kitendawili hicho, chaongelea juu ya uvaaji wa mkanda wa kiunoni. Mkanda huo, hupitishwa kwenye vifunguo vya kaputula au suluali ya mtu fulani. Mvaaji wa mkanda huo, huupitisha kwenye kila fungio mpaka unakutana kwenye tumbo. Tumbo hilo ndipo ukweni. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “penya nami nipenye tutakutana ukweni – mkanda kiunoni.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watoto wale ambao hukutana kwa mzazi wao mara kwa mara, katika maisha yao. Watoto hao, ni wa mzazi mmoja waliosambaa kwenye familia yao kwa ajili ya kufanya kazi ambao hukutana kwa mzazi huyo kila mwaka, kwa lengo la kumsalimia na kukumbushana juu ya maadili ya kuishi vizuri na watu. Wao humtunza vizuri mzazi wao kwa sababu ya heshina walio nayo kwake, na upendo walio kati yao, maishani mwao.

Watu hao hufanana na ule mkanda wa kiunoni unaopitishwa kwenye kila fungio mpaga unakutana kwenye tumbo, kwa sababu nao hukutana kila mwaka kwa mzazi wao kwa lengo la kumtunza na kukumbashana juu ya maadili ya kuishi vizuri na watu. Ndiyo maana wao huhadithiana kwamba, “penya nami nipenye tutakutana ukweni – mkanda kiunoni.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwaheshimu wazazi wao kwa kuwatunza na kukumbushana juu ya maadili ya kuishi vizuri na watu, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Mwanzo 5:3 – 32.

Mathayo 1: 1-17.

I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

ENGLISH: GO IN AND I GO IN AND WE WILL MEET AT OUR IN LAW’S PLACE – WAIST BELT.

The over head riddle talks about wearing a waist belt. This belt is passed through all brooches of a person’s shorts or pants. The wearer of the belt, passes it through each bronch until it meets to the stomach. Such stomach is what is compared to the wife’s parents’ place. That is why people tell each other that, “go in and I go in and we will meet at our in law’s place – waist belt.”

This puzzle is compared to children who meet their parents frequently, in their lives. Those children, spread out in their family for working purposes, who meet at that parents’ place every year, with the aim of greeting them and reminding each other of the values ​​of living well with people. They take good care of their parents because of the love they have for them, and the love they have in their lives.

These people are similar to the waist belt that is passed on every brooch up to the stomach, because they also meet every year at their parents’ house with the aim of taking care of them and arguing about the values ​​of living well with people. That is why they tell each other that, “go in and I go in and we will meet at our in law’s place – waist belt.”

This riddle imparts in people an idea of respecting their parents by taking care of them and reminding each other about the values ​​of living well with people, so that they can achieve many successes in their lives.

Genesis 5:3 – 32.

Matthew 1: 1-17.

 

1024. KALAGU –  KIZE. BHANA BHA NG’WISE B’ISHIGANYA UGUSIMINZA – MAZWI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kasiminzile ka ng’wa munhu. Umunhu ulu alisiminza, amagulu gadajilanijaga lihamo kunguno gagishiganyaga bho gumo gumo. Kuyiniyo lulu, amazwi galikihamo na magulu umo gagishiganijaga. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu bha hakaya iyo bhagishib’ilaga uguyomba, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagilekelaga uguyomba bho gundegeleka bhuli ng’wene mpaga omala uguyomba kunguno bhali nilange lya gwikuja bhuli ng’wene. Abhoyi bhagikalaga bhitogilwe bho gwiyambilija chiza bhuli ng’wene ulubhitana abhiye, kunguno ya wiyigwi bhobho bhunubho, umuwikaji bhobo.

Abhanhu bhanebho, bhagikolaga na mazwi ayo gagishib’ilaga ugusiminza, kunguno nabhoyi bhagishib’ilaga uguyomba, mpaga omala ung’wene na oyomba nu ungi, aha kaya yabho yiniyo. Hunagwene bhagiganilaga giki, “bhana bha ng’wise b’ishiganya ugusiminza – mazwi.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gub’iza nikujo lya gwidegeleka chiza umumahoya gabho bho gwilekela oyomba uumo mpaga omala, na oyomba nuungi lulu, kugiki bhadule gwikala bho mholele chiza, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

WATOTO WA KWETU HUBISHANA KUTEMBEA – MAGOTI.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia utembeaji wa mtu. Mtu anapotembea miguu yake huwa haiendi kwa pamoja kwa sababu hupishana mmoja mmoja. Kwa hiyo basi, magoti nayo yako pamoja na miguu inavyotembea. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wa kwenye familia ile ambayo watu wake huwa wanasikilizana katika maongezi yao kwa kupeana zamu, katika maisha yao. Watu hao, huachiana zamu ya kuongea kwa kumsikiliza kila mmoja wao mpaka anamaliza vizuri kuongea ndipo na mwingine anaanza, kwa sababu ya heshima walionayo kwa kila mmoja wao. Wao huishi katika upendo wa kusaidiana vizuri kila mmoja anapowahitaji wenzake, kwa sababu ya uelewano wao huo mzuri, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na yale magoti ambayo hupeana zamu katika kutembea, kwa sababu nao huachiana zamu ya kuongea mpaka mmoja wao anamaliza ndipo na mwingine anaanza kuongea, kwenye familia yao hiyo. Ndiyo maana watu hao huhadithiana kwamba, “watoto wa kwetu hubishana kutembea – magoti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na heshima ya kusikilizana vizuri katika maongezi yao kwa kuachiana kila mmoja anaongea mpaka anamaliza ndipo anaanza na mwingine kuongea, ili waweze kuishi vizuri na kwa amani, maishani mwao.

Matendo ya mitume 17:25.

1Petro 2:4.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

OUR RELATIVES CHILDREN ARGUE ABOUT WALKING – KNEES.

The source of the above riddle looks at a person’s walking. When a person walks his legs do not move together because they overlap one by one. Therefore, the knees are also with the legs as they move. That is why people say to one another that, “Our relatives children argue about walking – knees.”

This riddle is compared to the members of a family whose people listen to each other in their conversations in their lives. These people take turns talking to each other until they have finished talking and then the other can start doing so, because of the respect they have for each other. They live in love of helping each other well when they are in need, because of their good understanding in their lives.

These people are like the knees that take turns walking, because they also take turns talking until one of them finishes and the other can start talking to their family members. That is why these people tell each other that, “Our relatives children argue about walking – knees.”

This paradox teaches people on how to have a good sense of respect on one another in their conversations by letting each other talk until one finishes and then they can start talking to each other, so that they can live well and peacefully in their lives.

Acts 17:25.

1 Peter 2: 4.

1023. KALAGU – KIZE. IKAYA YISE ILELO BHO GUNUNG’HYA – MHANDE.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ihoyelile higulya ya bhuli bho mhande. Imhande indoto ulu juzugwa abhanhu bhadatondolaga akagula gajo kunguno bhagazigaza bhegeleja haho nomo bhakanza yafuma imhande balya giti balinung’hya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “ikaya yise ilelo bho gunung’hya – mhande.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali na ng’wigwano go wiza aha kaya yabho. Abhanhu bhanebho, bhagilomelaga mihayo ya gwiyambilija gutumama milimo yabho bhizunilija chiza, kunguno ya ng’wigwano gobho gunuyo, umukikalile kabho. Abhoyi bhagaponaga jiliwa noyi umubhutumami bho milimo yabho yiniyo, kunguno ya gujilanija chiza, umuwikaji bhobho bhunubho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga ni mhande ijo bhajilyaga abhanhu bho gwegeleja hanomo bhakanda yafuma guti bhalinunghya, kunguno bhagatumamaga milimo yabho bho gujilanija na ng’wigwano chiza, mpaga bhapandika sabho ningi a hakaya yabho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayombaga giki, “ikaya yise ilelo bho gunung’hya – mhande.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’wigwano go gujilanija chiza umuwigulambija bho gutumama milimo yabho, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila chiza umu kaya jabho.

Matendo ya mitume 10:34-36.

Luka 16:9-10.

Matendo ya mitume 2:42-46.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

FAMILIA YETU LEO WA KUNUSA – NJUKU MAWE.

Chanzo cha kitendawili hicho huongelea juu ya ulaji wa njugu mawe. Njugu mawe hizo, zikipikwa wakati zikiwa mbichi, watu huwa hawamenyi maganda yake, kwa sababu huwa wanasogeza kwenye mdomo na kuminya ambapo njugu mawe hutoka yenyewe kwa kurukia mdomoni na kuila kama wananusa hivi. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “familia yetu leo wa kunusa – njugu mawe.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale walio na uelewano kwenye familia zao. Watu hao, hupanga mipango yao ya kusaidiana katika kufanya kazi kwa kuelewana vizuri, kwa sababu ya uelewano wao huo, katika maisha yao. Wao hupata mavuno mengi katika kazi zao hizo, kwa sababu ya kuendana kwao huko vizuri, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na zile njuku mawe walizokuwa wakizila wale watu kwa kusogeza mdomoni na kuminya halafu inarudia mdomoni wanakula kama wananusa hivi, kwa sababu nao huyatekeleza majukumu yao kwa uelewano mzuri, mpaka wanafanikiwa kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza familia zao. Ndiyo maana wao huwaambia watu kwamba, “familia yetu leo wa kunusa – njugu mawe.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uelewano wa kuendana vizuri katika juhudi zao za kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza vizuri familia zao.

Matendo ya mitume 10:34-36.

Luka 16:9-10.

Matendo ya mitume 2:42-46.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

AT OUR HOME TODAY WE WILL EAT SOMETHING SMELLY – BAMBARA NUTS.

The foundation of the overhead riddle talks about eating of Bambara nuts. If these Bambara nuts are cooked when they are raw, people do not peel their pods, because they tend to bring near to their mouth and squeeze where the Bambara nuts come out by themselves by jumping in the mouth and eating them as if they smell like this. That is why people say to one another that, “at our home today we will eat something smelly – Bambara nuts.”

This riddle is compared to people who have harmony in their families. These people, in turn, make plans to help each other enough to work in harmony with each other, because of their mutual understanding, in their lives. They reap a bountiful harvest in their labors, because of their good arrangement in their lifetime.

These people resemble the Bambara nuts that the people used to eat by bringing them near to their mouths and squeezing enough to let them jump into their mouths, because they also carry out their duties in a good way, until they manage to get enough wealth to take care of their families. That is why they tell people that, “at our home today we will eat something smelly – Bambara nuts.”

This riddle imparts in people an idea on how to have a good sense of belonging in their efforts to fulfill their responsibilities, so that they can have enough wealth to take good care of their families.

Acts 10: 34-36.

Luke 16: 9-10.

Acts 2: 42-46.

hazelnut-2284654__480

nuts-762803__480

peanut-6757556__480

1022. KALAGU – KIZE. GWA KAGAKULAGULAGA – KAGOKO.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile kikalile ka ngoko. Ingoko yiniyo igigalaga yukulagula umugwicholela ijiliwa jayo, umukikalile kayo kenako. Iyoyi igajitagulaga hasi ijiliwa nulu jigikala jitulile mujisema, kunguno ya wigulambija bho gwicholela jagulya. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “gwa kagakulagaulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigulambijaga gwicholela sabho bho gutumama milimo yakwe bhuli lushigu, umukitakile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wigulambija gutumama milimo yakwe bho gwanguha uguyandya uguitumama bhuli lushigu, kunguno ya gutogwa guyibheja chiza ikaya yakwe yiniyo. Uweyi agapandikaga sabho ningi umumilimo yakwe kunguno ya wigulambija bhokwe bhunubho ubho gutumama milimo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nkogo iyo igikalaga yuchola jiliwa bhuli lushigu, kunguno nuweyi agigulambijaga kutumama milimo yakwe chiza, mpaga opandika sabho ningi, umubhutumami bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “gwa kagakulagulaga – kagoko.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bhuli lushigu kugiki bhadule kupandima sabho jagijilanhanila chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

2Wathesalonike 3:10.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KILA SIKU HUPEKUAPEKUA – KUKU.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia maisha ya kuku. Kuku huyo, hupekuapekua kila siku katika kujitafutia chakula chake, katika maisha yake hayo. Yeye hukimwaga chini hata chakula kile kilichomo kwenye chombo kizuri kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kutafuta chakula. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujibidisha kutafuta mali kwa kufanya kazi zake kila siku, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa akijibidisha kufanya kazi zake kwa kuwahi kwenda kazini kila wakati kwa sababu ya kutaka kuitunza vizuri familia yake. Yeye hufanikiwa kupata mali nyingi katika kazi zake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kuyatekeleza vizuri majukumu yake hayo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule kuku aliyejibisha kutafuta chakula kila siku, kwa sababu naye hujibidisha kufanya kazi vizuri, mpaka anafanikiwa kupata mali nyingi za kutosha kuitunza vizuri familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kila siku hupekuapekua – kuku.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kila siku ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzitunza vizuri familia zao, maishani mwao.

2Wathesalonike 3:10.

ENGLISH: I HAVE RIDDLE – LET IT COME.

IT PECKS EVERY DAY – CHICKEN.

The basis of the above riddle looks at the life of the chicken. The chicken search every day for their food in their lives. They even pour out the food that is in the fine container because of their zeal for the food. That is why people say that, “It pecks every day – chicken.”

This riddle is compared to a man who strives to seek wealth by doing his daily work, in his life. This person, in turn, strives to do his job by going to work all the time because he wants to take good care of his family. He succeeds in gaining wealth in his work because of his diligence in fulfilling his responsibilities in his life.

This man is like the hen that had to work hard to get food every day, because he also strives to work hard, until he manages to get enough wealth to take good care of his family. That is why people say to him that, “It pecks every day – chicken.”

This riddle teaches people on how to work hard every day so that they can earn enough money to take good care of their families in their lives.

2 Thessalonians 3:10.

chicken--

1016. KALAGU – KIZE. KAB’ULUB’A KANENEZU KATUNGULE LIDUMU – TULO.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ihoyelile higulya ya tulo. Itulo yiniyo igingilaga hado hado ukuli munhu, niyo bho nduhu ugudebha chiza uweyi, kunguno agwimanila otindilaga duhu, mumo agakulia agulyeha duhu bho gutindila chiniko. Hunagwene umili gugagemanijiyagwa na lidumu ilo litungile bhulubha bho gwiganila giki, “kab’ulub’a kanenezu katungile lidumu – tulo.”

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agilendejaga bho gutindila mpaga okeleja ugujutumama imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agakelejaga noyi ugumisha mpaga oduma ugujutumama imilimo yakwe kunguno ya kutugwa tulo jakwe jinijo, umukikalile kakwe. Uweyi agagayiyagwa ijiliwa ijagulya aha kaya yakwe kunguno ya kutogwa tulo jakwe jinijo ijo agajizunilijaga mpaga janendeja ugujutumama imilimo yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni lidumu ilo ligalendejiwa bho gutungwa na kab’ulub’a kanenezu, kunguno nuweyi agalyehiyagwa na tulo mpaga wilendeja ugujutumama imilimo yakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bha muchalo jakwe bhagang’wilaga giki, “kab’ulub’a kanenezu katungile lidumu – tulo.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu bhigulya ya kuleka wilendeja bho kukindwa tulo mpaga bhakeleja ugujutumama imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika sabho ningi ja gujilisha chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mhubiri 5:11.

Mathayo 25:1-12.

Waefeso 5:14.

KISWAHILI: KITENDAWILI –  TEGA.

UZI MWEMBAMBA UMEFUNGA DUMU – USINGIZI.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaongelea juu ya uzingizi. Usingizi huo, huingia pole pole kwa mtu bila ya yeye kuelewa vizuri, kwa sababu mtu huyo hujikuta amesingia tu, hata kama atakuwa mkubwa kiasi gani, atatulia kwa kusinzia namna hiyo. Ndiyo maana mwili wa mtu huyo hufananishwa na dumu lililofungwa uzi  mwembamba kwa kuhadithiana kwamba, “uzi mwembamba umefunga dumu – usingizi.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujisahau kwa kusinzia mpaka akachelewa kwenda kazini kwake, katika maisha yake. Mtu huyo, huchelewa sana kuamuka mpaka anajikuta amechekewa pia kwenda kufanya kazi zake, kwa sababu ya kupenda sana usingizi wake huo, katika maisha yake. Yeye hukosa chakula mara nyingi katika familia yake, kwa sababu ya kuendekeza usingizi wake huo ambao huuruhusu mpaka unamchelewesha kwenda kufanya kazi zake, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na lile dumu lililo zubaishwa kwa kufungwa na uzi mwembamba, kwa sababu naye huzubaishwa na usingizi mpaga anachelewa kwenda kufanya kazi zake, katika maisha yake hayo. Ndiyo maana watu wa kijijini mwake humwambia kwamba, “uzi mwembamba umefunga dumu – usingizi.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha kuchelewa kwenda kufanya kazi zao kwa kuendekeza uzingizi, ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kuzilisha vizuri familia zao, maishani mwao.

Mhubiri 5:11.

Mathayo 25:1-12.

Waefeso 5:14.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

A THIN THREAD HAS TIED A GALLON – A SLUMBER.

The origin of the overhead riddle talks about a slumber. Such slumber is a sleep that enters slowly into a person without him fully understanding it, because that person finds himself in a deep sleep, no matter how big he is, he will settle down in such a sleep. That is why the body of such person is likened to a gallon which is tied by a thin thread by saying to one another that, “a thin thread has tied a gallon – a slumber.”

This riddle is compared to a person who forgets him/herself by sleeping until he is late to work in his lifetime. This person wakes up so late that he finds himself too lazy to go to work, because he likes his sleep so much, in his life. He often misses food in his family, because of his sleep deprivation that prevents him from going to work in his life.

This man is resembles the person who was bound by a thin thread, because he is also tossed about by sleeping until he goes to work late, in his life. That is why the people in his village tell him that, “a thin thread has tied a gallon – a slumber.”

This riddle imparts in people an idea on how to avoid committing delays by resorting to stalling, so that they can earn enough money to feed their families well in life.

Ecclesiastes 5:11.

Matthew 25: 1-12

Ephesians 5:14.

eyes-5160174__480

baby-2582305__480

sleeping-1317770__480