Sukuma Riddles

1127. KALAGU – KIZE. NDITO ALIYO ADIMANILE IGIKI NDITO – JIGANGA.

Ikalagu yiniyo ilolile lijiganga liduma ilo libadikile nulu lyimilile. Iliwe linilo ligikalaga haho pye amakanza bho nduhu ugwimana ilyoyi igiki lililidito. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki “ndito aliyo adimanile igiki ndito – jiganga.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu nshiganu uyo alina wimo wiza umukikalile kakwe. Umunhu ung’winuyo agayombaga mihayo ya nhana na adiko gulenva lulu gugaluchiwa na munhu ungi, kunguno ya bhutungilija bhokwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhaha kaya yakwe shimile sha gudimila nhungwa ja wiza kunguno ya bhushiganu bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nili jiganga ilo lidazegejiyagwa kunguno nuweyi alinshiganu umushimilile shakwe pye amakanza, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ndito aliyo adimanile igiki ndito – jiganga.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na shimile jishikanu ija gwikala munhungwa jawiza bhuli makanza, kugiki bhadule kujilanhana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

1Petro 2:3-4.

1Petro 2:8.

1Wathesalonike 4:1-2.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI  –  TEGA.

MZITO LAKINI HAJITAMBUI KWAMBA NZITO –  MWAMBA.

Kitendawili hicho huangalia mwamba ambao umepachikwa au umesimama. Mwamba huo upo pale ulipo wakati wote na haujitambui kuwa ni mzito. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “mzito lakini hajitambui kwamba mzito – Mwamba.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana msimamo mzuri katika maisha yake. Mtu huyo, huongea maneno ya hekima na ya kweli bila kudanganywa wala kugeuzwa na mtu mwingine kwa sababu ya uaminifu wake. Yeye huwafundisha watu walioko kwenye familia yake namna ya kuwa na msimamo wa kuishi katika maadili mema kwa sababu ya kupenda ukweli kwake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule mwamba usiosogezwa kwa sababu naye ana msimamo wa kuishi katika maadili mema muda wote katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mzito lakini hajitambui kwamba mzito – Mwamba.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na msimamo wa kuishi katika maadili mema siku zote, ili waweze kuzilea familia zao katika maadili hayo mema siku zote, maishani mwao.

1Petro 2:3 – 4.

1Petro 2:8.

1Wathesalonike 4:1-2.

stones-7307274__480

mountains-7427724__480

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

HE IS HEAVY BUT HE DOES NOT REALIZE THAT HE IS HEAVY – ROCK.

This puzzle looks at the rock that is embedded or standing. It is there all the time and it does not realize that it is heavy. That is why people tell each other about him that, “he is heavy but he does not realize that he is heavy – Rock.”

This paradox is related to a person who has a good position in his life. Such person, speaks words of wisdom and truth without being deceived or changed by another person because of his honesty. He teaches people in his family on how to have a position of living in good morals because of his love for the truth in his life.

This person is like the unmoved rock because he also has a position of living in good morals all the time in his life. That is why people tell him that, “he is heavy but he does not realize that he is heavy – Rock.”

This riddle imparts in people an idea on having a position of living in good morals all the time, so that they can raise their families in those good morals all the time, in their lives.

1Peter 2:3 – 4.

1 Peter 2:8.

1 Thessalonians 4:1-2.

sharp-2482839__480

1112. KALAGU – KIZE. MUNHU NG’WENUYU NADAMANILE UKO AFUMILE NUKO AJILE – LUYAGA.

Ikalagu yiniyo ihoyelile higulya ya luyaga. Uluyaga lunulo lugahuyembaga lujile mumabala matale aliyo lulu ludamanyikile uko lulifumila nuko lujile. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “munhu ng’wenuyu nadamanile uko afumilile nuko ajile – Luyaga.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo adina shimile ishawiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga uyunga sagala bho nduhu ugulenda aha kaya yakwe kunguno ya bhukokolo bho guduma gutumama milimo yakwe bhunubho. Uweyi agadumaga uguyibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya bhujidalenda ha ng’wakwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu luyaga ulo ludamanyikile uko lufumilile nuko lujile, kunguno nuweyi agikalaga uyunga sagala bho nduhu ugulenda aha kaya yakwe yiniyo, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “munhu ng’wenuyu nadamanile uko afumile nuko ajile – Luyaga.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na jimile ja nhungwa jawiza ijo jidulile gubhambilija ugujilela chiza ikaya jabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Waebrania 7:1-3.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MTU HUYU SIJUI ATOKAKO NA AENDAKO – UPEPO.

Kitendawili hicho huongelea juu ya upepo. Upepo huo huvuma kuelekea sehemu mbalimbali, lakini huwa haujulikani unakotoka na unakoelekea. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu sijui atokako na aendako – Upepo.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa hana msimamo mzuri katika maisha yake. Mtu huyo, hupendelea kutembea hovyo bila kutulia kwenye familia yake kwa sababu ya uvivu wake wa kutokufanya kazi. Yeye hushindwa kuiendeleza vizuri familia yake kwa sababu ya kutokutulia nyumbani kwake huko, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule upepo usiojulikana kule uendako na ulikotoka, kwa sababu naye hudhurura hovyo bila kutulia nyumbani kwake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu huyu sijui atokako na aendako – Upepo.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na msimamo wenye tabia njema ya kuwawezesha kuzilea vyema familia zao, maishani mwao, ili waweze kupata maendeleo makubwa, maishani mwao.

Waebrania 7:1-3.

cyclone-2102397__480

banner-1076214__480

tree-3191872__480

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

I DO NOT KNOW WHERE THIS MAN COMES FROM AND WHERE HE IS GOING – THE WIND.

This riddle talks about the wind. This wind blows in different directions, but no one knows where it comes from and where it is going. That is why people say that, “I do not know where this man comes from and where he is going – the wind.”

This puzzle is compared to the person who does not have a good position in his life. Such person, prefers to walk carelessly without settling well in his family because of his laziness of not working. He fails to bring progress to his family properly because of his unsettled home there in life.

This person is like the wind that one does not know where it is going and where it came from, because he also stays carelessly without working well in his home in life. That is why people tell him that, “I do not know where this man comes from and where he is going – the wind.”

This riddle teaches people about having a good attitude that can enable them to raise their families well, in their lives, so that they can achieve great progress in their lives.

Hebrews 7:1-3.

 

 

1111. KALAGU – KIZE. NAGANG’WIGWAGA ALIYO NADAMONAGA – ILAKA.

Ikalagu yiniyo ilolile ilaka ilo agaligwaga munhu bho nduhu ugulibhona. Olihoyi munhu uyo agigwa ilaka liling’witana bho nduhu ugumhona umunhu uyo alimwitana. Umunhu ng’wunuyo, agidika na gutimija iyo lyang’wilaga ililaka linilo. Hunagwene abhanhu bhagiganila giki, “nagang’wigwaga aliyo nadamonaga – ilaka.”

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhigwaga chiza abho bhagang’wilaga mihayo, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agatumagwa gujutumama milimo na bhiye oja ugaitimija chiza kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe. Uwei agikalaga bho mholele na bhiye kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’winuyo agikolaga nuyo agwigwa ilaka liling’witana widika bho nduhu ugumona umunhu uyo aling’witana, kunguno nuwei agiigwaga chiza imihayo iyo bhaling’wila abhiye, na guyitimija chiza. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nagang’wigwaga aliyo nadamonaga – ilaka.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya nhungwa ja guigwa chiza imihayo ya bhichabho na guitimija, kugiki bhadule kujibheja chiza ikaya jabho.

Luka 3:4-6.

Luka 1: 46-47.

Yohane 1: 29 – 34.

Zaburi 55: 1-6.

Luka 3:22.

Yohane 10:1-5.

Warumi 20:18.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

NAMSIKIA LAKINI SIMUONI – SAUTI.

Kitendawili hicho huangalia sauti ambayo mtu huisikia bila kuiona. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alisikia sauti ikimuita bila kumuona mtu yule anayemuita. Mtu huyo, aliitika na kutekeleza kile alichoambiwa na ile sauti. Ndiyo maana watu walihadithiana kwamba, “namsikia lakini simuoni – Sauti.”

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwasikia vizuri watu wanaompatia ujumbe na kuutekeleza, maishani mwake. Mtu huyo hutumwa kwenda kutekeleza majukumu na wenzake na kuyatii vizuri kwa sababu ya unyofu wake huo, katika maisha yake. Yeye huishi kwa amani na wenzake kwa sababu ya uaminifu wake huo maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeitii sauti iliyomuita bila kumuona mtu aliyemuita, kwa sababu naye huyasikiliza vizuri maneno anayoambiwa na wenzake na kuutekeleza ujumbe aliyopewa. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “namsikia lakini simuoni – Sauti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia ya kuyasikilia na kuyaelewa maneno ya wenzao, ili waweze kuzilea vyema familia zao.

Luka 3:4-6.

Luka 1: 46-47.

Yohane 1: 29 – 34.

Zaburi 55: 1-6.

Luka 3:22.

Yohane 10:1-5.

Warumi 20:18.

woman-6920629__480

parade-2657870__480

dance-5173941__480

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

I HEAR IT BUT I DO NOT SEE IT – VOICE.

The overhead riddle looks at the sound that one hears without seeing. There was a person who heard a voice calling him without seeing the person calling him. Such man responded and did what the voice told him. That is why people told each other that, “I hear it but I do not see it – Voice.”

This paradox is compared to the person who listens well to people who give him a message and implements it in his life. Such person is sent to carry out duties by his colleagues whom he obeys them well because of his sincerity in life. He lives in peace with his colleagues because of his honesty in his life.

This person resembles the one who obeyed the voice that called him without seeing the person who called him, because he also listens well to the words which are said to him by his colleagues and carries out the message that is given to him. That is why he says, “I hear it but I do not see it – Voice.”

This riddle instills in people an idea of having habit of listening and understanding words of their nobles, so that they can courteously raise their families.

Luke 3:4-6.

Luke 1: 46-47.

John 1: 29 – 34.

Psalm 55: 1-6.

Luke 3:22.

John 10:1-5.

Romans 20:18.

 

1110. KALAGU – KIZE. NINA BHANA BHATANO INGOFILA BIYIKOJIJE – NJALA.

Ikalagu yiniyo iholelile higulya ya wiikoji bho njala na katumamila kajo. Injala ijamumakono nija kumagulu jiniyo jigikalaga jiikolile kunguno jili tano ijo jigatumama milimo bho gwiyambilija chiza. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “Nina bhana bhatano ingofila biikojije – Injala.”

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kubhanhu bhanhu bhagikalaga bhidebhile chiza umukatumamile ka milimo yabho. Abhanhu bhenabho bhagikalaga bhutumama milimo bho witogwi bhutale kunguno ya ng’wigwano gobho uyo bhalinago umuwikaji bhobho. Abhoyi bhabhakujije abhichabho kunguno ya nhungwa jabho ijawiza jinijo, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga ni njala ijo jiikojije ni ngofila na kiyambiligije ka bhutumami bho milimo, kunguno na bhoyi bhali na nhungwa jawija pye abhose ijo jigabhambilijaga kutumama milimo yabho chiza. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “Nina bhana bhatano ingofila biikojije – Injala.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwikala na nhungwa jawiza ija gutumama milimo kihamo bho gwiyambilija chiza, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

Yohana 15:9.

Wagalatia 3:27.

Wagalatia 2:20.

 

KISWAHILI: KITENGAWILI –  TEGA.

NINA WATOTO WATANO KOFIA ZAO ZINAFANANA – KUCHA.

Kitendawili hicho huongelea juu ya ufananaji wa kucha na utendaji wake wa kazi. Kucha za miguuni na zile za mikononi zinafanana kwa sababu ni tano ambazo hufanya kazi kwa kusaidiana vizuri. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba “nina watoto watano kofia zao zinafanana – kucha.”

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa watu wale ambaho wanaelewana vizuri katika utekelezaji wa kazi zao. Watu hao hufanya kazi kwa pamoja na kwa upendo mkubwa kwa sababu ya uelewano huo wao maishani mwao. Watu hao huwaheshimu wenzao vizuri kwa sababu ya tabia yao hiyo kuwa nzuri, katika maisha yao.

Watu hao, hufanana na zile kucha zenye kofia za kufanana na ambazo hushirikiana katika kufanya kazi, kwa sababu nao wana tabia njema ambayo huwasaidia kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Ndiyo maana huwaambia kwamba, “nina watoto watano kofia zao zinafanana – kucha.”

Kitendawili hicho hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuwawezesha kuyatekeleza majukumu yao wakisaidiana vizuri, ili waweze kupata mafanikio mengi maishani mwao.

Yohana 15:9.

Wagalatia 3:27.

Wagalatia 2:20.

mug-2568355__480

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

I HAVE FIVE CHILDREN WHOSE HATS ARE THE SAME – NAILS.

The above riddle talks about similarity of nails and their functions. Fingernails and toenails are similar because there are five of them that work well together. That is why people tell each other that “I have five children whose hats are the same – nails.”

This paradox is compared to people who understand each other well in the implementation of their works. These people work together and with great love because of such understanding of one another in their lives. They people respect their nobles well because of their good behaviors in their lives.

These people are similar to those nails of similar hats that cooperate in working, because they also have good behavior that helps them in carrying out their duties well. That is why people say that, “I have five children whose hats are the same – nails.”

This riddle teaches people about having a good attitude enough to enable them carry out their duties by helping each other well, so that they can achieve many successes in their lives.

John 15:9.

Galatians 3:27.

Galatians 2:20.

 

1070. KALAGU – KIZE. MUNHU NAMBU AHA KAYA ODUDUNDUGAJA AYISE – NZUKI.

Imbuki ya kalagu yiniyo ilolile wikaji bho nzuki. Inzuki jinijo jigingilaga na gwikala munumba ja bhanhu abho bhagajizunilijaga kunguno ya gujiganikila giki jili bhudugu nabho. Aliyo lulu, ulushigu jasayaga jigabhalumagulaga mpaga lulu gubhabhulaga gete abhamo bhabho. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagahayaga giki, “munhu nambu ahakaya odudundukaga ayise – Nzuki.”

Ikalagu yiniyo, igalengajiyagwa kuli munhu uyo agikalaga ahumulile aliyo munholo yakwe alina bhuchilu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga kihamo na bhiye umutumami bho milimo yakwe, uyo agakenyiyagwa hadoo duhu opelana na gwandya kutula bhanhu kunguno ya bhuchilu bhokwe bhunubho. Uweyi agabhalabhulaga bhanhu bhingi noyi abho agikalaga nabho kunguno ya bhulambu na bhujidigwa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nzuki ijo jigasayaga jandya gubhaluma abhanhu bhahene aho jigikala, kunguno nuweyi agakenyiyagwa hadoo duhu wandya gubhatula abhanhu abho agikalaga nabho, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagayombaga giki, “munhu nambu ahakaya odudundukaga ayise – Nzuki.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya gwikala na bhanhu chiza bho guleka bhuchilu bho sagara, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwiyambilija gutumama milimo yabho chiza, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 4:10 – 14.

Wagalatia 1:7-8.

Mathayo 26:14 – 16.

Tito 1:5-11.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MTU KICHWA NGUMU HAPA NYUMBANI AMETUSHINDA SISI – NYUKI.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia maisha ya nyuki. Nyuki hao huingia na kuishi kwenye nyumba za watu wale ambao huwaruhusi kwa sababu ya kuwafikiria kuwa ni ndugu zao. Lakini siku wamekasirika huwauma hata mpaka kuwaua kabisa baadhi ya watu hao waishio kwenye nyumba hiyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu kichwa ngumu hapa nyumbani ametushinda sisi – Nyuki.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa kimya lakini ndani ya moyo wake anahasira kali, katika maisha yake. Mtu huyo, huishi pamoja na wenzake katika utekelezaji wa majukumu yao, ambaye akichokozwa kidogo tu hukasirika na kuanza kuwapiga watu wale anaoishi nao kwa sababu ya hasira yake hiyo kali. Yeye huwaumiza watu wengi wale wanaoishi naye, kwa sababu ya kiburi na hasira zake hiyo kali, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na wale nyuki waliokasirika na kuanza kuwauma watu wa kwenye familia ya pale walipo, kwa sababu naye pia huchokozwa kidogo tu na kuanza kuwapiga watu anaoishi nao. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu kichwa ngumu hapa nyumbani ametushinda sisi – Nyuki.”

Kitendawili hiyo, hufundisha watu juu ya kuishi vizuri na watu kwa kuachana na hasira zisizo na maana katika maisha yao, ili waweze kusaidiana katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Mwanzo 4:10 – 14.

Wagalatia 1:7-8.

Mathayo 26:14 – 16.

Tito 1:5-11.

bees-326337__480

bees-345628__480

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

A STUBBORN PERSON WHO HAS DEFEATED US AT HOME – BEE.

The origin of this paradox looks at the life of bees. The bees enter and live in houses of people who allow them because they think that they are their relatives. But when they are angry, they bite them until they completely kill some of the people who stay in that house. That is why people say that, “a stubborn person who has defeated us at home – bee.”

This paradox is compared to the person who stays silent but in his heart he is very angry, in his life. Such person lives with his colleagues in the execution of their duties, who if provoked just in a little matter gets angry and starts beating people whom he lives with because of his strong anger. He hurts many people who live with him, because of his pride and strong anger, in his life.

This person resembles the bees that got angry and started stinging the people who live in that family where they are, because he is also provoked just in a little  matter and starts hitting people whom he lives with. That is why people tell him that, “a stubborn person who has defeated us at home – bee.”

This riddle teaches people on how to live well with people by letting go of unnecessary anger in their lives, so that they can help each other in carrying out their responsibilities well, in their lives.

Genesis 4:10 – 14.

Galatians 1:7-8.

Matthew 26:14 – 16.

Titus 1:5-11.

bees-352206__480