1127. KALAGU – KIZE. NDITO ALIYO ADIMANILE IGIKI NDITO – JIGANGA.

Ikalagu yiniyo ilolile lijiganga liduma ilo libadikile nulu lyimilile. Iliwe linilo ligikalaga haho pye amakanza bho nduhu ugwimana ilyoyi igiki lililidito. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki “ndito aliyo adimanile igiki ndito – jiganga.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu nshiganu uyo alina wimo wiza umukikalile kakwe. Umunhu ung’winuyo agayombaga mihayo ya nhana na adiko gulenva lulu gugaluchiwa na munhu ungi, kunguno ya bhutungilija bhokwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhaha kaya yakwe shimile sha gudimila nhungwa ja wiza kunguno ya bhushiganu bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nili jiganga ilo lidazegejiyagwa kunguno nuweyi alinshiganu umushimilile shakwe pye amakanza, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ndito aliyo adimanile igiki ndito – jiganga.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gubhiza na shimile jishikanu ija gwikala munhungwa jawiza bhuli makanza, kugiki bhadule kujilanhana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

1Petro 2:3-4.

1Petro 2:8.

1Wathesalonike 4:1-2.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI  –  TEGA.

MZITO LAKINI HAJITAMBUI KWAMBA NZITO –  MWAMBA.

 

Kitendawili hicho huangalia mwamba ambao umepachikwa au umesimama. Mwamba huo upo pale ulipo wakati wote na haujitambui kuwa ni mzito. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “mzito lakini hajitambui kwamba mzito – Mwamba.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana msimamo mzuri katika maisha yake. Mtu huyo, huongea maneno ya hekima na ya kweli bila kudanganywa wala kugeuzwa na mtu mwingine kwa sababu ya uaminifu wake. Yeye huwafundisha watu walioko kwenye familia yake namna ya kuwa na msimamo wa kuishi katika maadili mema kwa sababu ya kupenda ukweli kwake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule mwamba usiosogezwa kwa sababu naye ana msimamo wa kuishi katika maadili mema muda wote katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mzito lakini hajitambui kwamba mzito – Mwamba.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na msimamo wa kuishi katika maadili mema siku zote, ili waweze kuzilea familia zao katika maadili hayo mema siku zote, maishani mwao.

1Petro 2:3 – 4.

1Petro 2:8.

1Wathesalonike 4:1-2.

stones-7307274__480

mountains-7427724__480

sharp-2482839__480

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.