Sukuma Riddles

1206. KALAGU – KIZE. MUMO UGANENGELA UDUNASA UNG’WANA NG’WUNUYO – BHUNYENYA.

Imbuki ya kalagu yiniyo ililola kabhunyenya ako kali kadoo noyi nulu ugiyina kugalasa udukadula kunguno ya bhudoni bhogo bhunubho. Ubhunyenya bhunubho  bhuli bhudodo aliyo bhukikalaga bhunoyi noyi ugubhulya. Ukwene huguhaya giki, iginhu jigikalaga na solobho yajo mumho jigadohela. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “mumo uganengela udunasa ung’wana ng’wunuyo – kabhunyenya.”

Ikalagu yuniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhadahalaga abhanhu kunguno ya bhudoni bho mimili yabho umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo adaibhonaga isolobho ya bhanhu abho bhali hasilili yakwe, kunguno ya libhengwe yakwe linilo umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguyibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya gubhadalaha sagala abhanhu bhakwe bhenabho, aha kaya yakwe yiniyo.

Umunhu ng’wunyo, agikolaga nuyo abhudalaha ubhunyenya bho gulola bhudoni bhobho, kunguno nu weyi agabhadalahaga abhanhu abho bhali hasilili yakwe, umuwikaji bhokwe mpaga oduma uguibhona isolobho yabho, aha kaya yakwe yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mumo uganengela udunasa ung’wana ng’wunuyo – kabhunyenya.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya kuleka libhengwe lya gubhadalaha sagala abhanhu abho bhali hasilili yabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umubhutumami bho milimo yabho, umukaya jabho.

Marko 4:30-32.

1Wakorintho 1:27-28.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

HATA UJITAHIDI KUMLENGA KWA MSHALE NAMNA GANI MTOTO HUYO HUTAMPIGA – UFUTA.”

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia ufuta ambao ni mdogo sana. Ufuta hata mtu ajitahidi kuulenga kwa mshale ili aupige hataweza, kwa sababu ya udogo wake huo. Wenyewe ni mdogo lakini ni mtamu kwa kuula. Ndiyo kusema kwamba, kitu hata kikiwa kidogo namna gani, kinafaida yake katika maisha ya mwanadamu. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “hata ujitahidi kumlenga kwa mshale namna gani mtoto huyo hutampiga – ufuta.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwadharau watu walioko chini yake kwa sababu ya udogo wa miili yao. Mtu huyo, huwa haioni faida ya watu walioko chini yake, kwa sababu ya dharau aliyo nayo kwao, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake kwa sababu ya kuwadharau hovyo watu waliopo kwenye familiya yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliudahau ututa kwa kuangalia udogo wa umbo la zao hilo, hata akashindwa kuona faida yake, kwa sababu naye huwadharau watu walioko chini yake mpaga anashindwa kuona faida yao kwenye familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hata ujitahidi kumlenga kwa mshale namna gani  mtoto huyo hutampiga – ufuta.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha kuwadharau hovyo watu walioko chini yao, ili waweze kupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukuku yao, katika familia zao.

Marko 4:30-32.

1Wakorintho 1:27-28.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

EVEN IF YOU TRY TO TARGET WITH AN ARROW YOU WILL NOT HIT THAT CHILD – SAMSAM.

The basis of this paradox looks at a very small crop which is known as samsam. Even if someone tries to aim at it with an arrow, he will not be able to hit it, because of its small size. They themselves are small but they are sweet to eat. That is to say that, no matter how small something is, it is useful to human life. That is why people tell each other that, “even if you try to target with an arrow, you will not hit that child – Samsam.”

This puzzle is equated to a person who despises people who are under him because of smallness of their bodies. Such person never sees benefit of people who are under him, because of a contempt that he has to them, in his life. He fails to raise his family well because of his carelessness to his people.

This person relates to the one who underestimated the small size of that small crop, until he failed to see its benefit, because he also despises the people who are under him to the point of failing to see their benefit in his family. That is why people tell him that, “even if you try to target with an arrow, you will not hit that child – Samsam.”

This riddle teaches people about stopping belittling the people who are under them, so that they can achieve a lot of success in raising their children, in their families.

Mark 4:30-32.

1 Corinthians 1:27-28.

family-2563889_1280

mother-and-daughter-668167_1280

woman-1320103_1280

1193. KALAGU – KIZE. KANISHISHA KULE – MPILYA.

Umpilya jili jitumamilo ijo jigang’wanguhyaga umunhu ugushiga wangau uko ajile umulugendo lokwe. Umunhu ng’wunuyo, agibakilaga umpilya gokwe opela na gushiga wangu uko ajile kunguno ya bhupeji bho mpilya gunuyo. Hunagwene agayombaga giki, “kanishisha kule – mpilya.”

Ikalagu yiniyo igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumilaga ginhu ja gupelela uko ajile ija kunshisha wangu, umulugendo lokwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumila ginhu guti lori, basi, ndege na jingi ijo jikolile na jinijo, kunguno ya kuhaya kushiga wangu uko ajile umulugendo lokwe nululo. Uweyi agadulaga ugushiga wangu uko ajile umulugendo lokwe na kutumama milimo yingi, kunguno ya gutumila jikolo ya kupelela ija kunshisha wangu jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agatumila mpilya mpaga ushiga kule, kunguno nuweyi agatumilaga ginhu ja gupelela na kushiga wangu uko ajile, umulugendo lokwe. Hunagwene agayombaga giki, “kanishisha kule – mpilya.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya gutumila ginhu ja gupelela umukikalile kabho, kugiki bhadule gushiga wangu, uko bhagile, umuludondo lobho.

Matendo ya mitume 27:1-3, 13.

Kutoka 14:17.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KAMENIFIKISHA MBALI – BAIKELI.

Baisikeli ni chombo cha usafiri ambacho humwezesha mtu kufika haraka kule anakoenda. Mtu huyo, hupanda baiskeli yake na kukimbia mpaka anafika haraka kule anakoenda, kwa sababu ya ukimbiaji wa baiskeli hiyo. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “kamenifikisha mbali – baiskeli.”

Kitendawili hicho hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutumia vyombo vya usafari kwa ajili ya kumfikisha haraka kule anakoenda, katika maisha yake. Mtu huyo, hutumia vyombo vya usafiri kama vile gari, basi, ndege na vingine wingi, kwa sababu anataka kufika haraka kule anakoenda, katika safari yake. Yeye hufanikiwa kufika haraka kule anakoenda mpaka anafanya kazi zingine, kwa sababu ya kutumia usafiri huo wa haraka, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyetumia baiskeli mpaka akafika mbali katika safari yake, kwa sababu naye hutumia vyombo vya usafiri na kufika haraka kule anakoenda, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “kamenifikisha mbali – baiskeli.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kutumia vyombo vya usafiri katika safari zao, ili waweze kufika haraka kule wanakoenda, maishani mwao.

Matendo ya mitume 27:1-3, 13.

Kutoka 14:17.

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

IT HAS BROUGHT ME FAR – THE BICYCLE.

A bicycle is a means of transportation that enables a person to reach his destination quickly. Such person gets on his bicycle and runs until he reaches his destination quickly, because of the speed of such bicycle. That is why he says that, “it has brought me far – the bicycle.”

This paradox is equaled to the person who uses good means of transportation to get him quickly to where he is going, in his life. Such person uses good means of transport such as car, bus, plane and many others, because he wants to get to his journey’s end quickly, in his trip. He manages to get to his last stop quickly until he does other jobs, because of using that fast transport, in his life.

This person resembles to the one who used a bicycle until he got far in his journey, because he also uses good means of transport enough to enable him quickly reach where he is going, in his life. That is why he says that, “it has brought me far – the bicycle.”

This riddle teaches people about using good means of transport in their travels, so that they can quickly reach their destinations, in their lives.

Acts 27:1-3, 13.

Exodus 14:17.

 

man-471192__480

bicycle-7798227__480

old-man-2584620__480

 

1172. KALAGU –  KIZE. UMYAJI ALI NA MAGULU ALIYO UMYALWA ADINA MAGULU – NGOKO NI GI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola kikalile ka ngoko na bhulanhani bho bhana bhayo. Ingoko yiniyo ligashigaga likanza yatela bho gunyela magi na gugalela bho gugabhandila mpaga gapya. Ulu gapya amagi genayo gagatandukaga kafuma kana umu bhuli ligi lyene, kunguno ya bhudiliji wiza ubho ngoko yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “umyaji ali na magulu aliyo umyalwa adina magulu – ngoko ni gi.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli myaji uyo agabhalelaga chiza abhana bhakwe mpaga bhakula, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiyumilila ugubhalela abhana bhakwe bhenabho bho guhoya nabho bhuli lushigu, kunguno ya bhutogwa bhokwe ukubhana bhakwe bhenabho. Uweyi agabhakujaga mpaga bhadula gung’wambilija chiza aha kaya yake kunguno ya gubhalela chiza chiniko, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nkola iyo iyanyelaga magi yagabhandila chiza mpaga gapya na gufuma kana umu bhuli ligi lyene, kunguno nuweyi agabhalelaga chiza abhana bhakwe mpaga bhadula gung’wambilija chiza aha kaya yake yiniyo, umiwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “umyaji ali na magulu aliyo umyalwa adina magulu – ngoko ni gi.”

Ikalagu yiniyo, yalangu bhabyaji higulya ya kubhalanhana abhana bhabho bho gubhalela chiza, kugiki bhadule gubhambilija chiza umu kaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 1:24-31.

Hekima ya Sulemani 7:6.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

MZAZI ANA MIGUU LAKINI MZALIWA HANA MIGUU – KUKU NA YAI.

Chanzo cha kitendawili hicho, huangalia maisha ya kuku na utunzaji wa vifaranga vyake. Kuku huyo, hufika muda wa kutaga mayai na kuyalea kwa kuyakumbatia vizuri mpaga yanaiva. Mayai hayo yakiiva hupasuka na kutoa kifaranga kila moja kwa sababu ya utunzaji mzuri wa kuku huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mzazi ana miguu lakini mzaliwa hana miguu – kuku na yai.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mzazi yule ambaye huwalea vizuri watoto wake mpaga wanakua, katika maisha yake. Mtu huyo, huvumilia katika kuwalea watoto wake hao kwa kuongea nao kila siku, kwa sababu ya upendo wake huo kwao. Yeye huwakuza vizuri watoto wake hao, mpaka wanaweza kumsaidia vizuri katika familia yake, kwa sababu ya kuwatunza kwa kuwapatia malezi mema, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule kuku aliyetaga mayaji akayatunza vizuri mpaka yakaiva na kutoa mtoto kila moja, kwa sababu naye huwatunza watoto wake kwa kuwalea vizuri mpaka wanaweza kumsaidia vizuri katika familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mzazi ana miguu lakini mzaliwa hana miguu – kuku na yai.”

Kitendawili hicho, hufundisha wazazi juu ya kuwatunza watoto wao kwa kuwalea vizuri, ili waweze kuwasaidia vyema katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 1:24-31.

Hekima ya Sulemani 7:6.

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

THE PARENT HAS LEGS BUT THE CHILD HAS NO LEGS – THE CHICKEN AND THE EGG.

The foundation of this paradox, looks at the life of chickens and the care of their chicks. The hen spends time to lay eggs and nurture them by hugging them well until when they are ripe. When the eggs are ripe they crack and give out a chick each one because of the good care of her. That is why people say that, “the parent has legs but the child has no legs – the chicken and the egg.”

This paradox is compared to the parent who takes good care of his children as they grow up, in his life. Such person perseveres in raising his children by talking to them every day, because of his love for them. He raises his children well, until they can help him well in his family, because of taking care of them by providing them with good upbringing in life.

This person resembles the hen that laid eggs and took good care of them until they ripen and give birth to each one, because he also takes care of his children by raising them well until they can help him well in his family. That is why people say about him that, “the parent has legs but the child has no legs – the chicken and the egg.”

This riddle teaches parents on how to take care of their children by raising them well, so that they can help them better in their families in their societies.

Genesis 1:24-31.

Wisdom of Solomon 7:6.

 

chicken-1867521__480

1168. KALAGU – KIZE. KAYA YA NG’WISE IDAMALAGA LUGENDO – SUNGWA/MISWA.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ilolile Sungwa/miswa. ISungwa jilijisunva ijo jidamalaga lugendo kunguno jigajaga gujusuma jiliwa jagiza jilumile liswa bhuli jene, nulu ginhu josejose ijo jigachala hawikalo bhojo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “kaya ya ng’wise idamalaga lugendo – Sungwa/miswa.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa ku bhanhu abho bhagatumama milimo yabho bho bhukamu bhutale na guchala kaya yabho, amatwajo gabho, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho bhagajaga gujigulambija gutumama milimo yabho bhuli lushugu na gujichala kukaya jabho ijo bhagajipandika umubhutumami bhobho, kunguno ya bhutungilija bhobho bhunubho. Abhoyi bhagikalaga na sabho ningi aha kaya yabho kunguno ya gwigulambija bho gutumama milimo yabho yiniyo bhuli lushigu na gujichala aha kaya yabho, ijo bhagajipandikaga umubhutumami bhobho bhunubho, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho bhagikolaga ni Sungwa kihamo ni miswa ijo jigigulambijaga gusuma jiliwa na guchala hawikalo bhojo ijo jigapandikaga, kunguno nabhoyi bhagigulambijaga gutumama milimo yabho bhuli lushigu na gujichala ahawikalo bhobho ijo bhagajikwabhaga, umubhutumami bhobho. Hungwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “kaya ya ng’wise idamalaga lugendo – Sungwa/miswa.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bhuli lushugu, na kujichala kukaya jabho ijo bhagajipandikaga umubhutumami bhobho, kugiki bhadule gupandika sabho ningi imuwikaji bhobho.

Mathayo 10:5-15.

Marko 6:7-13.

Luka 10:1-2.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

FAMILIA YA KWETU HAIMALIZI SAFARI – SIAFU/MCHWA.

Chanzo cha kitendawili hicho huangalia chungu chungu/siafu/ mchwa. Chungu chungu hao ni viumbe wadogo wagodo weusi ambao ni jamii ya siafu na mchwa. Viumbe hao hawamalizi safari kwa sababu huenda kuhemea chakula na kuleta nyumbani kwao kila mmoja kile alichokipata. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “familia ya kwetu haimalizi safari – siafu/mchwa.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa watu wale wambao hufanya kazi kwa bidii kubwa na kukipeleka nyumbani kwao kile walichokipata, katika maisha yao. Watu hao, huenda kujibidisha kufanya kazi zao kila siku na kupeleka nyumbani kwao kile walichokipata katika kazi zao, kwa sababu ya uaminifu wao huo. Wao hutajirika sana kwenye familia yao, kwa sababu ya kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao vizuri kila siku na kukipeleka nyumbani kwao, kile walichokipata, katika kazi zao, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na wale siafu na mchwa ambao hujibidisha kuhemea chakula na kukipeleka nyumbani kwao kile walichokipata, kwa sababu nao hujibidisha kufanya kazi zao kila siku, na kukipekeleka nyumbani kwao kile walichokipata, kwenye utekelezaji wa majukumu yao. Ndiyo maana wao husema kwamba, “familia ya kwetu haimalizi safari – siafu/mchwa.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kujibidisha kutekeleza vizuri majukumu yao, na kukipeleka nyumbani kwao, kile wakipatacho kwenye kazi zao hizo, ili waweze kupata mali nyingi za kutosha kutumia maishani mwao.

Mathayo 10:5-15.

Marko 6:7-13.

Luka 10:1-2.

nature-5898812__480

 

 

 

1155. KALAGU – KIZE. NTOLWA ALILAB’AGILA MUNGUNDA – LIZETI.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola lizeti. Ilizeti yiniyo, lilinti ilo ulu giki lyuhola ligafunyaga wilab’u b’ulab’agizu guti ntolwa uyo alifumanija kunguno nang’hwe agazwalaga jizwalo jilab’agizu chiza. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “ntolwa alilab’agila mungunda –  lizeti.”

Ikalagu yiniyo, igalenganiyagwa kuli ntolwa uyo agayilelaga chiza ikaya yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agatumamaga milimo yakwe chiza na gubhalanga bhanhu bhakwe nzila ja gwika chiza na bhanhu kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho. Uweyi abhalumanyaga chiza abhanhu abho bhidumaga bho guhoya nabho chiza kunguno ya nhungwa jakwe ijawiza jinijo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga ni lizeti iyo igalab’agilaga mungunda, kunguno nuweyi alina nhungwa niza ijo jigang’wambilijaga ugubhalela chiza abhanhu bhakwe, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ntolwa alilab’agila mungunda –  lizeti.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhitoji higulya ya gubhiza na nhungwa ja gubhalela chiza abhanhu bhabho, kugiki bhadule gwikala chiza, umu kaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Wimbo ulio bora 3:11.

Wimbo ulio bora 4:1.

Wimbo ulio bora 5:1’

Isaya 61:10-11.

 

KISWAHILI: KITENDAWILI –  TEGA.

BIBI HARUSI ANAMEREMETA SHAMBANI – ALIZETI.

Chanzo cha kitendawili hicho kinaangalia alizeti. Alizeti hiyo, ni mti ule ambao ukichanua hutoa maua ya kumeremereta kama bibi harusi anayeolewa kwa sababu naye huvaa mavazi ya kumetameta vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, “bibi harusi anameremeta shambani – alizeti.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa bibi harusi yule ambaye huilea vizuri familia yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake vizuri na kuwafundisha watu wake njia za kuishi vizuri na watu, kwa sababu ya uaminifu wake huo. Yeye huwapatanisha watu waliokosana kwa kuongea nao vizuri, kwa sababu ya tabia hiyo njema aliyo nayo, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na ile alizeti iliyokuwa ikimeremeta shambani, kwa sababu naye ana tabia njema ambayo humsaidia katika kuwalea vizuri watu wake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “bibi harusi anameremeta shambani – alizeti.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuwalea vizuri watu wao, ili waweze kuishi vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Wimbo ulio bora 3:11.

Wimbo ulio bora 4:1.

Wimbo ulio bora 5:1’

Isaya 61:10-11.

sunflower-1627179__480