Sukuma Proverbs

967. UMUNHU NG’WENUYU ADACHAGULILE NULU ADAYANGULAGWA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile Welelo uyo adulile jose. UWelelo ung’wene adachagulaga nulu guyangulwa giki ansole nani, kunguno agamulaga weyi dulu. Uweyi nulu yubhiza nzala agamulaga Weyi duhu igiki mbula yize, kunguno ya bhudula bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhaganyombaga giki, “Umhunhu ng’wenuyu adachagulile nulu adayangulagwa.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo mpaga opandika sabho ja gubhambilija bhanhu bhakwe chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga gutumama milimo yakwe chiza, kunguno alina bhutogwa bho gubhambilija bhanhu bhingi bho gutumila sabho jakwe. Uweyi agapandikaga sabho ningi ijo agajitumilaga bho gubhagunana abhanhu bhakwe gitumo atogelilwe weyi, kunguno ya bhutogwa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu Welelo uyo alina bhudula bho guyangula yose gitumo atogelilwe, kunguno nuweyi alina bhutogwa bho gujitumila isabho jakwe, bho gubhambilija bhanhu bhakwe gitumo atogelilwe weyi, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhaganyilaga giki, “umhunhu ng’wenuyu adachagulile nulu adayangulagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza bhakamu wa kutumama milimo na bhutogwa bho gubhambilija bhichabho bhose abho bhali na makoye, kugiki bhagule kujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Luka 1:35-38.

1Wakorintho 6:14.

Waefeso 2:1, 4-6.

2Wakorintho 5:17-18.

 

KISWAHILI: MTU HUYU HACHAGUI WALA HASHAURIWI.

Methali hiyo, huongelea juu ya Mungu awezaye yote. Mungu Mwenyewe hachagui wala hashauriwi kwamba amchukue nani, kwa sababu yeye huamua lolote atakalo yeye. Yeye hata ikitokea njaa kubwa, Aweza kuamua mvua inyeshe wakati wowote, kwa sababu ya uwezo wake huo mkubwa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu hachagui wala hashauriwi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi kwa bidii mpaka anapata mali za kumwezesha kuwasaidia watu wengi, katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake vizuri, kwa sababu ana upendo wa kuwasaidia wengi kwa kutumia mali zake. Yeye hupata mali nyingi ambazo huzitumia katika kuwasaidia watu wake hao, kama atakavyo yeye, kwa sababu ya upendo wake huo kwao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na Mungu atumiaye uwezo wake atakavyo, kwa sababu naye ana upendo wa kutumia mali zake katika kuwasaidia watu wake wote, kama atakavyo yeye, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtu huyu hachagui wala hashauriwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na bidii ya kufanya kazi, wakiwa na upendo wa kuwasaidia wenzao wote, walioko kwenye matatizo, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Luka 1:35-38.

1Wakorintho 6:14.

Waefeso 2:1, 4-6.

2Wakorintho 5:17-18.

 

ethiopia-21

ENGLISH: THIS PERSON DOES NOT HEED TO ADVICE.

This proverb speaks of the almighty God. God Himself does not choose or need an advice from anyone about whom to take, because He decides whatever He wills. Even in the time of a severe famine, He may decide that it will rain at any time, because of His great power. That is why people say that, “This person does not heed to advice.”

This proverb is related to a man who works hard until he finds wealth that will enable him in helping many people in his life. Such person, in turn, strives to do his best, because he loves to help many people by using his resources. He finds numerous treasures that he uses for supporting his people, as he wills, because of his love to them, in life.

This person resembles to God who uses his power for doing good things, because he loves to use his wealth for supporting all his people, as he wills, in his life. That is why people say to him that, “This person does not heed to advice.”

This proverb teaches people about being hard workers enough to have wealth for supporting all their people who are in trouble, so that they can develop well their families in their lives.

Luke 1: 35-38

1 Corinthians 6:14.

Ephesians 2: 1, 4-6.

2 Corinthians 5: 17-18.

966. B’UDIMU B’O LIGEMBE GULINDILA GU NGESE.

Iligembe jili jitumamilo ja gulimila ukuli nimi. Iligembe linilo, ligamanyikaga ubhudamu bholyo ahikanza ilya gulilimila ingese, kunguno ilidimu lidakolokaga. Aliyo lulu, iligembe ilinegu ligakokolokaga nulu wandya duhu unimi ugulilimila ingese yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “b’udimu b’o ligembe gulindila gu ngese.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyitilaga bhukengeji bhutale imilimo na mihayo hayo atali uguyandya nulu uguitumamila, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agitakaga bhukengeji bho kujilola chiza, inhungwa ja bhanhu abho bhali nhomela, kunguno ya gutogwa gubhudebha chiza ubhumhana bho milimo nulu imihayo yiniyo. Uweyi agayombaga mihayo ya nhana na kupatandika matwajo mingi umumilimo yakwe, kunguno ya gutumama milimo iyo wiyitilaga bhukengeji bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ligembe ili ligikalaga na bhudamu ahikanza ilya gulilimila ingese, kunguno nuweyi agapandikaga matwajo mingi umumilimo yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu bhakwe inzila ja guyidebha chiza imilimo yabho, haho bhatali uguyandya uguitumama. Hunagwene agabhawilaga giki, “b’udimu b’o ligembe gulindila gu ngese.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guyitila bhukengeji bhutale imilimo yabho haho bhatali uguyandya uguyitumama, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umubhutumami bhobho.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 12:33-37.

KISWAHILLI: UGUMU WA JEMBE KUSUBIRI KWENYE PALIZI.

Jembe ni kitendea kazi cha kulimia kwa mkulima. Jembe hilo, hujulikana ugumu wake wa kulilimia wakati huo wa kulifanyia kazi, kwa sababu lile lililo gumu huwa halikongoloki. Lakini lile lililolegea hukongoloka pale mkulima anapoanza tu kulilimia. Ndiyo maana watu husema kwamba, “ugumu wa jembe kusubiri kwenye palizi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzifanyia utafiti mkubwa kazi zote kabla hajaanza kuzifanya, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya utafiti wa kufahamu tabia za wale anaoongea nao kabla ya kuyapokea maneno yao, kwa sababu ya kutaka kuufahamu ukweli wa kazi hizo na maneno hayo. Yeye huongea ukweli na hupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukumu yake, kwa sababu ya kufanya kazi njema alizozifanyia utafiki wa kina, kabla ya kuzianza, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na lile jembe lililoendelea kuwa gumu hata wakati wa kulilimia, kwa sababu naye hupata mafanikio mengi katika kazi zake, maishani mwake. Yeye huwafundisha pia watu wake namna ya kuzifanyia utafiti wa kina kazi zao, kabla ya hawajaanza kuzitekeleza. Ndiyo maana huwaambia watu hao kwamba, “ugumu wa jembe kusubiri kwenye palizi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzifanyia utafiti wa kina kazi zao, kabla ya kuanza kuzitekeleza, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika utekelezaji wa majukumu yao, maishani mwao.

Mathayo 7:15-20.

Mathayo 12:33-37.

africa-121

black-12

ENGLISH: THE DIFFICULTY OF THE HOE IS TO WAIT FOR WEEDING TIME.

A hoe is a farming tool for the farmer. It is known to have a hard time in cultivating at the time of working, because the hard one does not bend. But the loose ends when the farmer begins to week. That is why people say that, “The difficulty of the hoe is to wait for weeding time.”

This proverb is likened to a man who conducts a thorough study of all the works before he begins to do them, in his life. This person, in turn, conducts research that is good enough to understand the behavior the people to whom he is speaking before accepting their words, out of an aim of understanding the truth of their works and words. He speaks the truth and finds great success in the discharge of his duties, because of the good works that he has done in-depth research, before starting to work them out, in his life.

This person is like the hoe that continues to be difficult even when it is weeding, because he also finds great success in his work, in his life. He also teaches his people on how to do their research thoroughly, before they start doing their works. That is why he tells them that, “The difficulty of the hoe is to wait for weeding time.”

This proverb imparts in people a clue on how to do a thorough research on their works, before they start implementing them, so that they can be more successful in fulfilling their responsibilities, in their societies.

Matthew 7: 15-20.

Matthew 12: 33-37.

 

 

 

963. OPALA NVA HANKIMBILI.

Ulusumo lunulo, lulolile bhupaji bho mva hamkimbili bho ng’wa munhu nheb’e. Oliyohi nfugi o mawa aha kaya yakwe, uyo wikalaga mu chalo ja halebhe. Lushigu lumo agayidima inva yakwe wandya guyipala ahamkimbili, mpaga abhanhu bhukumya noyi. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “opala nva hamkimbili.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli ng’waniki uyo obyala ng’wana omumabala, umukikalile kakwe. Ung’waniki ng’wunuyo, adatolilwe aliyo ogetwa nda ya mumabala kunguno ya gulala na bhagosha, aho atali ugutolwa. Uweyi agakoyaga ugutolwa kunguno ulu bhigela abhatoji, bhagawilwa giki, ‘opala nva hamkimbili’, mumho obyalila ng’wana mumabala, umukikalile kakwe.

Ung’waniki ng’wunuyo, agikolaga nu nsugi onva uyo agayipala ahamkimbili inva yakwe, kunguno nuweyi ubyala ng’wana omumabala, haho adinatolwa. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “opala nva hamkimbili.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhaniki higulya ya kubhiza bhib’embu, umukikalile kabho, kugiki bhadule kutolwa wangu haho bhadina byajiwa bhana bha mumabala, umuwikaji bhobho.

Luka 1:46-56.

Mathayo 5:27-30.

KISWAHILI: AMEMPIGA MBWA KIUNONI.

Methali hiyo, huongelea juu ya upigaji wa mbwa kiunoni wa mtu fulani. Alikuwepo mfugaji wa mbwa kwenye familia yake aliyeishi kwenye kijiji fulani. Siku moja alimshika mbwa wake mmoja na kumpiga kiunoni mpaga watu wakashangaa sana. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “amempiga mbwa kiunoni.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa msichana yule aliyezaa mtoto kabla ya kuolewa, katika maisha yake. Msichana huyo, hajaolewa lakini omepata ujauzito kwa sababu ya kulala wa wanaume kabla ya kuolewa. Yeye hupata shida ya kuolewa kwa sababu wale wanaotaka kumuoa huambiwa na watu kwamba, msichana yule ‘amempiga mbwa kiunoni’, katika maisha yake.

Msichana huyo, hufanana na yule mfugaji aliyempiga mbwa wake kiunoni, kwa sababu naye alizaa kabla ya kuolewa, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “amempiga mbwa kiunoni.”

Methali hiyo, hufundisha wasichana juu ya kuwa watulivu katika maisha yao, ili waweze kuolewa mapema kabla ya kuzalishwa watoto wa mapolini, maishani mwao.

Luka 1:46-56.

Mathayo 5:27-30.

massai-1

people-11

african-2

ENGLISH: YOU HAVE SLAPPED A DOG ON ITS WAIST.

This proverb speaks about slapping the waist of a dog. There was a dog keeper in her family who lived in a certain village. One day she grabbed one of her dogs and slapped one of the on the waist. The people who saw such event were shocked. That is why they told her that, “You have slapped a dog on its waist.”

This proverb is compared to the girl who gave birth to a child before marriage, in her lifetime. Such girl is unmarried but has become pregnant because of premarital sex. She finds it difficult to get married because those who want to marry her are told by people that the girl has ‘beaten a dog in the waist’, in her lifetime.

This girl is like the dog keeper who slapped her dog on the waist, because she also gave birth before marriage, in her lifetime. That is why people say to her that, “You have slapped a dog on its waist.”

This proverb instills in girls an idea on how to be calm in their lives, so that they can get married early before being impregnated, in their lifetime.

Luke 1: 46-56.

Matthew 5: 27-30.

956. NG’HINGI YANEGA ITAB’ANYA B’ASIMBIJI.

Ulusumo lunulo, luhoyelile ng’hingi iyo yanega. Ing’hingi yiniyo, igamanaga yusimbililwa na bhasimbiji bhayo, yandra gunega duhu hangi. Iyoyi igabhanojaga nose abhanhu abho bhagayisimbilaga kunguno, ulu bhayisimbila yanega duhu hangi. Hunagwene bhagayombaga giki, “ng’hingi yanega itab’anya b’asimbiji.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa ku kaya iyo yigayogaga bhuli makanza umukikalile kayo. Ikaya yiniyo, yigamanaga yuyoga bhuli makanza kunguno abhanhu bhayo bhadishibhaga ulu bhalilomela. Abhoyi bhagabhizaga bhuli ng’wene nkali duhu uyo alemile ugubhadegeleka abhiye. Iyoyi ikabhakoyaga nose abhayanguji bhayo, kunguno ulu bhayiyangula yayoga duhu hangi, kunguno ya bhikaji bhayo gugayiwa wiyumilija, umukikalile kabho.

Ikaya yiniyo igikolaga ni ng’hingi iyi inegile iyo igatabhanya bhasimbiji, kunguno niyoyi igabhatabhanyaga abhayanguji bhayo. Hunagwene abhanhu bhenabho bhagiyombaga giki, “ng’hingi yanega itab’anya b’asimbiji.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhitoji higulya ya gubhiza na wiyumilija bho gwitogwa na gwilekeja ulu bhidumaga, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikiji bhobho.

1Yohane 3:18.

Marko 10:5-8.

Wakolosai 3:18-19

Mathayo 18:15.

KISWAHILI: NGUZO ILIYOLEGEA HUTATANISHA WACHIMBIAJI.

Methali hiyo, huongelea juu ya nguzo iliyolegea. Nguzo hiyo, huwa inachimbiwa na wachimbiaji wake, lakini huanza kulegea tena. Yenyewe mwishawe huwachosha wale wanaoichimbia, kwa sababu ya kuendelea kulegea kila wanapoichimbia. Ndiyo maana watu huisema kwamba, “nguzo iliyolegea hutatanisha wachimbiaji.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwenye familia ile ambayo huwa inazozana kila wakati, katika maisha yake. Familia hiyo, huzozana kila wakati kwa sababu ya wakazi wake kutokuwa na hali ya kusikilizana wanapoongea. Watu hao, huwa ni wakali wasiokubali kuwasikiliza wenzao, kwa sababu ya kutokuwa na uvumilivu katika maisha yao. Yenyewe huwachosha waamuzi wake kwa sababu ya kuendelea kuzozana tena kila wanapomaliza kuwapatanisha, maishani mwao.

Familia hiyo, hufanana na ile nguzo iliyolegea ambayo iliwashinda wachimbiaji wake, kwa sababu nayo huendelea kuzozana kila inapopatanishwa mwishowe huwashinda wale wapatanishi wake. Ndiyo maana watu hao huisema kwamba, “nguzo iliyolegea hutatanisha wachimbiaji.”

Methali hiyo, hufundisha wana ndoa juu ya kuwa na uvumilivu wa kupendana na kusameheana wanapokoseana, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

1Yohane 3:18.

Marko 10:5-8.

Wakolosai 3:18-19

Mathayo 18:15.

zanzibar-11

ENGLISH: A POST THAT HAS BECOME LOOSE CONFUSES THE DIGGERS.

This proverb speaks of a loose post. This post is dug by its diggers, but it begins to loosen again. It eventually exhausts those who dig its hole for strengthening it, because it continues to falter every time after being fixed. That is why people say that, “a post that has become loose confuses the diggers.”

This proverb is compared to the family that is constantly at misunderstanding, in its life. This family is continually at conflict because of its lack of listening ability to its members. These people are harsh and unwilling to listen to one another, because of their impatience in their lives. It exhausts its judges because of such constantly arguing with them every time after reconciling them, in their lives.

This family resembles the loose pillar that overcame its diggers, because it also continues to quarrel with each other and eventually overcomes its mediators. That is why people say that “a post that has become loose confuses the diggers.”

This proverb teaches married couples on how to have patience that is strong enough to love and forgive each other when they offend each other, so that they can nicely raise well their families, in their lives.

1 John 3:18.

Mark 10: 5-8.

Colossians 3: 18-19.

Matthew 18:15.

949. NAWE JANHILILA BHUGOTA BHUGAMANAGWA NA BHASAJI.

Ulusumo lunulo, luhoyelile bhuhililwa bho ng’wa munhu uyo amanile bhugota aliyo adinapandika solobho nabho. Umunhu ng’winuyo, agawilagwa giki janhilila kunguno inhungulume jili ngoko ng’osha ijo jigahilaga golecha giki ubhujiku welaga.

Ulu munhu alina lugendo ujigwa jahila agumana igiki okelejaga ugwandya ulugendo lokwe lunulo. Hunagwene umunhu uyo adinapandika solobho ya bhugota ubho abhumanile agawilagwa giki “nawe jamhilila bhugota bhugamanagwa na bhasaji.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo amanile bhugota aliyo akatumamile kakwe kali kab’i, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhinhaga bhanhu sagala ubhugota bhokwe bhunubho, bho nduhu gwinhiwa josejose. Uweyi agashililagwa nose inguzu ja gubhubhegeja ubhugota ubho abhumanile bhunubho, bho nduhu ugupandika josejose, kunguno ya gubhiza adina witegeleja, umumilimo yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nu nsaji uyo agaponyaga sagara ijikolo, kunguno nuweyi gabhinhaga bhanhu sagala ubhugota bhokwe bhunubho, bho nduhu gwinhiwa josejose. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “nawe jamhilila bhugota bhugamanagwa na bhasaji.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza ni kujo lya gubhutumila ubhumani bhobho bho gujibheja chiza ikaya jabho, kugiki bhadule gupandika solobho ningi, umubhumani bhobho.

Mhubiri 4:7-12.

KISWAHILI: NAYE ZIMEMUWIKIA DAWA HUFAHAMIWA NA WEHU.

Methali hiyo, huongelea uwikiwaji wa mtu anayefahamu dawa lakini hapati faida nayo. Mtu huyo, huambiwa kuwa amewikiwa kwa sababu jogoo ni kuku dume ambaye huwika kuonesha kwamba usiku umekucha.

Mtu akiwa na safari akisikia jogoo hao wanawika huelewa kwamba amechelewa kuianza safari yake hiyo. Ndiyo maana mtu yule ambaye hapati faida ya dawa anayoifahamu huambiwa kwamba, “naye zimemuwikia dawa hufahamiwa na wehu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayefahamu dawa fulani lakini huitumia vibaya, katika maisha yake. Mtu huyo, huwagawia watu hovyo ile dawa yake bila kupewa chochote. Yeye, mwishowe huishiwa nguvu za kuendelea kuitengeneza dawa yake hiyo, bila kupata faida yoyote, kwa sababu ya kutokuwa na umakini katika kazi zake.

Mtu huyo, hufanana na yule kichaa ambaye hutupa hovyo mali, kwa sababu naye huwagawia watu hovyo dawa hiyo, bila kupewa chochote katika kazi yake hiyo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “naye zimemuwikia dawa hufahamiwa na wehu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na busara ya kuitumia elimu yao kwa kuziendeleza vizuri familia zao, ili waweze kufaidika vizuri kutokana na elimu hiyo, maishani mwao.

Mhubiri 4:7-12.

Jogoo3

 

ENGLISH: THE COCKS HAVE CROWED FOR HIM/HER, MEDICINAL HERBS ARE KNOWN BY MAD ONES!

This proverb speaks of the roosters which crowed before benefiting from medicine which a particular man knew. This man is told so because he has finished his medicine without making anything out of it.  

The rooster is a male chicken that crows to show that the night is over. A person who has a journey, for instance, when he hears the roosters crowing, he realizes that he is late to start his journey. That is why the person who does not get the benefit of the medicine which he knew is told that, “the cocks have crowed for him/her, medicinal herbs are known by mad ones!”

This proverb is compared to a man who is familiar with a particular drug but who abuses it, in his life. This man, in turn, distributes his medication comprehensively without being given anything. He/she, in the end, loses the ability to continue making this medicine, to no avail, because of a lack of concentration in his work.

This man is like the madman who did not benefit from his medicine, because he also distributes the drug to people without being given anything in his work. That is why people say to him that, “the cocks have crowed for him/her, medicinal herbs are known by mad ones!”

This proverb teaches people on how to be wise enough to use their education for the betterment of their families, so that they can benefit well from it, in their lives.

Ecclesiastes 4: 7-12.