Sukuma Proverbs

985. JAWIB’I JIDASAB’ILAGWA.

Olihoyi munhu uyo agib’a hela ujituula mumhinda yakwe. Umunhu ng’wunuyo, agandya lugendo lo guja kaya. Aho oshiga ikaya agachala nkono umumhinda yakwe kugiki ajilole ihela jinilo, ujigayiwa kunguno agajigumila mu nzila bho nduhu ugamana uweyi. Gashinaga ihela jinijo, agajigumila haho ojib’ilaga mpaga ujikuga ung’winikili ojo. Hunagwene abhanhu bhagang’wila ung’wib’i ng’wunuyo giki, “jawib’i jidasab’ilagwa.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agib’aga jikolo ijo jidang’wenhelaga solobho yoseyose, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agib’aga jikolo ja bhanhu ogajitumamila sagala duhu kunguno adajinogelile. Uweyi agikalaga ukoya na nzala bhuli makanza kunguno ya gugayiwa jilila ijaguilisha  kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agib’a hela ujigwisha haho ujib’ilaga mpaga jukugwa nu ng’winikili ojo, kunguno nuwei agajikenagulaga sagala ijikolo ijo agajib’aga, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “jawib’i jidasab’ilagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja wib’i bho gwigulambija gutumama milimo yabho chiza, kugiki bhadule gupandika bhusab’i umuwikaji bhobho.

Kutoka 20: 15.

Mithali 15:9-10.

Mithali 16:8.

 

KISWAHILI: ZA KUIBA HAZITAJIRIKIWI.

Alikuwepo mtu aliyeiba hela na kuiweka mfukoni mwake. Mtu huyo, alianza safari ya kuelekea nyumbani. Alipofipa nyumbani kwake, alipeleka mkono mfukoni ili kuikagua hiyo hela, akaikosa, kwa sababu ilidondoka bila ya yeye kufahamu. Kumbe hela hiyo ilidondokea pale alipoiibia mpaka mwenye nayo, akaiokota. Ndiyo maana watu walimuambia yule mwizi kwamba, “za kuiba hazitajirikiwi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayeiba vitu ambavyo havimletei faida yoyote, katika maisha yake. Mtu huyo, huiba vitu vya watu na kuvitumia hovyo, kwa sababu hakuvitolea jasho. Yeye huishi kwa kusumbuliwa na tatizo la njaa kwenye familia yake, kwa sababu ya kukosa chakula cha kuilisha famalia yake hiyo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeiba hela akaidondosha mpaga mwenye nayo akaiokota, kwa sababu naye huvitumia hovyo vitu alivyoviiba, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “za kuiba hazitajirikiwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya wizi kwa kujibidisha kufanya zao vizuri, ili waweze kupata utajiri, maishani mwao.

Kutoka 20: 15.

Mithali 15:9-10.

Mithali 16:8.

woman-112

african-12

 

ENGLISH: STOLEN THINGS DO NOT MAKE ONE RICH.

There was a man who stole money from somebody and put it in his pocket. This man began his journey home. When he got home, he put his hand in his pocket to check it all over, and missed it, because it fell out without him knowing. But the money fell out when he stole it until the owner had it, and he picked it up. That is why people told the thief that “stolen things do not make one rich.”

This proverb is equated to a man who steals things that do not benefit him in his life. This person steals people’s belongings and uses them carelessly, because he does not sweat in earning them. He lives with the problem of hunger in his family because of the lack of food for feeding his family members.

This person is like the one who stole the money and dropped it off at the owner’s presence, because he also misuses the things which he stole from his life. That is why people say to him that, “stolen things do not make one rich.”

This proverb imparts in people a clue on how to stop stealing properties of others. They have to try doing their best enough to earn for their living, so that they can get rich in their families.

Exodus 20:15.

Proverbs 15: 9-10.

Proverbs 16: 8.

 

home-

983. OBYALILWA HA NZALA.

Ugubyaliwa ha nzala ili gubyalilwa hi kanza lwa nduhu ijiliwa kunguno ya mbula kuleka gutula ung’waka gunuyo. Ili gubyalilwa hikanza lya nduhu jiliwa. Hunagwene uyo obyalilwa hikanza linilo, agawilagwaga giki, “obyalilwa ha nzala.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo osangaga bhanhu bhamalaga gulya jiliwa, aha kaya yiniyo. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga nzala kunguno yagusanga jamalagwa guliwa ijiliwa jinijo ijo jali jazugagwa, aha kaya yiniyo. Uweyi agakoyiyagwa na bhutubhu bhunubho, ubho gulindila ikanza lingi ilya guzugilwa jiliwa jingi, kunguno ya gukeleja mpaga usanga jamalaga guliwa ijiliwa ijo jali jalijazugagwa jinijo, aha kaya yiniyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo abyalilwa ha nzala, kunguno nuweyi agasanga abhiye bhajimalaga gujilya pye ijiliwa ijo jalijazugagwa, aha kaya yiniyo. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagang’wilaga giki, “obyalilwa ha nzala.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwanguha gushiga uko bhalalikagwa guja, umubhutumami bhobho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 26:1.

2Wafalme 4:38-39.

KISWAHILI: UMEZALIWA KIPINDI CHA NJAA.

Kuzaliwa kwenye kipindi cha njaa ni kuzaliwa kwenye wakati wa kutokakuwa na chakula kwa sababu ya kutosekana kwa mvua mwaka huo, au sababu zingine. Kipindi hicho ni cha kuzaliwa wakati chakula hakipo. Ndiyo maana yule aliyezalwa kwenye kipindi hicho, watu humwambia kwamba, “umezaliwa kipindi cha njaa.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule aliyekuta watu wamemaliza kula chakula chote, kwenye familia hiyo. Mtu huyo, huwa anashinda njaa kwa sababu ya kukuta wenzake wamekimaliza kukila chakula chote kilichokuwa kimepikwa, kwenye familia hiyo. Yeye husumbuliwa na njaa tumbuni mwake anaposubiri mpaka wakati mwingine watakapo pika chakula kingine, kwa sababu ya kuchelewa kwake mpaga akakuta wenzake wamekula chakula chote, kwenye familia hiyo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyezaliwa wakati wa njaa, kwa sababu naye amekuta wenzake wamekula chakula chote kilichokuwa kimepikwa, kwenye familia hiyo. Ndiyo maana wenzake hao, humwambia kwamba, “umezaliwa kipindi cha njaa.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwahi kufika kule walikoalikwa kwenda katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Mwanzo 26:1.

2Wafalme 4:38-39.

namibia-21

woman-211

 

ENGLISH: YOU WERE BORN DURING FAMINE.

Being born in a famine-stricken period is a time of little or no food due to a lack of rain, or other reasons. Anyone who is born during this period suffers from hunger because food is not available. That is why people say to him/her that, “you were born during famine.”

This proverb is related to a man who finds people having eaten all food in the family. This man remains hungry because he finds his colleagues have finished eating all the food that was cooked in that family. He suffers from hunger in his stomach as he waits until the next time of cooking another meal after delaying to arrive in that family.

This man in like the one who was born during the famine time, because he also found his fellows had eaten all the food that had been cooked in that family. That is why his colleagues tell him that, “You were born during famine.”

This proverb imparts in people an idea on how to get earlier to where they are invited to go in fulfilling their duties, so that they can have more successes in their families.

Genesis 26: 1.

2 Kings 4: 38-39.

 

979. KILI KILI KUB’UTOLWA B’ONG’WIYO.

Ulusumo lunulo, luhoyelile kili kili ya ng’wa munhu uyo ojaga kuwinga bho bhiye. Ikili kili yiniyo, bhuli bhukimbi bho gutumya lub’ub’u ubho owitaga umunhu ng’wunuyo, ukuwinga bho bhiye. Aliyo lulu uweyi oliadatolilwe, kunguno ya gubhatumija lub’ub’u chiniko abhiye. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “kili kili kub’utolwa b’ong’wiyo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli nkima uyo alina nhungwa mb’ib’ib’i, umukikalile kakwe. Unkima ng’wunuyo, adabyedechaga ugutolwa kunguno ya bhukololo bho gutumama milima na nhani jakwe jinijo. Uweyi agajaga ogabhakenaguja ikaya abhiye abho bhatolilwe, kunguno ya nhungwa jakwe jab’ub’i jinijo, umuwikaji bhokwe.

Unkima ng’wunuyo, agikolaga nu munhu uyo witaga kili kili ya gub’atumija lub’ub’u abhiye abho bhatolilwe, kunguno nuweyi agajaga ogabhakenaguja ikaya abhiye abho bhatolilwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “kili kili kub’utolwa b’ong’wiyo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwikala na nhungwa jawiza ija gubhambilija ugwibhegeja bhiniki ikaya jabho, na kuleka bhuyungi bho guyugula kaya ja bhangi, kugiki bhadule gujilela chiza, ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Yakobo 1:26-27.

Yakobo 3:5-6.

Yohana 8:44.

KISWAHILI: MKIKI MKIKI KWA ALIKOOLEWA MWENZIO.

Methali hiyo, huongelea juu ya mkiki mkiki wa mtu mmoja aliyeenda kwenye harusi ya mwenzie. Mkiki mkiki huo, ni utumuaji wa vumbi aliokuwa akiufanya mtu huyo kwenye harusi za wenzake, wakati anacheza.

Lakini yeye alikuwa hajaolewa, kwa sababu ya tabia yake hiyo ya kuwatimulia vumbi hivyo wenzake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “mkiki mkiki kwa alikoolewa mwenzio.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mwanamke yule aliye na tabia mbaya, katika maisha yake. Mwanamke huyo, hafaulu kuolewa kwa sababu ya uvivu, na kiburi chake hiyo. Yeye huenda kuzivuruga familia za wenzake walioolewa, kwa sababu ya tabia yake hiyo mbaya, maishani mwake.

Mwanamke huyo, hufanana na yule mtu aliyeenda kuwatimulia watu vumbi kwenye ndoa za wenzake, kwa sababu naye huenda kuzivuruga ndoa za wale walioolewa, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mkiki mkiki kwa alikoolewa mwenzio.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia njema ya kuziendeleza familia zao wao wenyewe, na kuacha uzururaji wa kuvuruga ndoa wa wengine, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Yakobo 1:26-27.

Yakobo 3:5-6.

Yohana 8:44.

dance-12

music-1

eyes-

ENGLISH: FREQUENT VISITS TO THE PLACE YOUR FELLOW IS MARRIED TO.

This proverb speaks of a woman who went to another woman’s wedding. She jumped while playing to the point of causing dust to audiences. Her fellows were unhappy of her dancing ways because of such dust she made.

Nonetheless she was not married, because of her tendency of causing dust to other’s weddings. That is why people said to her that, “Frequent visits to the place your fellow is married to.”

This proverb is equaled to the immoral woman in her life. This woman is unable to marry because of laziness, and her pride. She normally goes to disrupt families of her married fellows, because of her bad behavior in life.

This woman, in effect, is like the woman who went to cause dust to the weddings of her fellows, because she too may have disrupted the marriages of fellows in her life. That is why people say to her that, “Frequent visits to the place your fellow is married to.”

This proverb teaches people on how to have good attitude for the development of their own families enough to stop disrupting marriage of others, so that they can better raise their families in their societies.

James 1: 26-27.

James 3: 5-6.

John 8:44.

978. UGUSANGWA LWELWE UDINASIMIZA.

Ulusumo lunulo, lulolile ng’wana uyo oliodila ugusimiza. Ung’wana ng’wunuyo, wikalaga wagula bho nduhu ugwimila, kunguno ya bhudito bho magulu gakwe. Uweyi agakeleja noyi ugusimiza nose ilwelwe ijo jili noni ja gwiza ulujilingila ijidiku, jigegela gwiza.

Ulujiza inoyi jininijo, abhanhu bhandya gulima kunguno bhagamanaga giki, mumho jashigaga ijidiku. Hunagwene bhagang’wilaga ung’wana ng’wunuyo giki, “ugusangwa lwelwe udinasimiza.”

Ulusumo lununo, lugalenganijiyagwa kuli ng’waniki uyo atali ugutolwa, umukikalile kakwe. Ung’waniki ng’wunuyo, ahayile atolwe aliyo lulu okeleja kunguno ya nhungwa jakwe ijo jidijawiza. Uweyi adalombaga ukuli Mulungu uyo adulile gumpandikala ntoji o wiza, kunguyo ya nhungwa jakwe jinijo, umukikalile kakwe.

Ung’waniki ng’wunuyo, agikolaga nu ng’wana uyo agakeleja ugusimiza, kunguno nu weyi okeleja ugutolwa, umukikalile kakwek kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ugusangwa lwelwe udinasimiza.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhayanda na bhaniki abho bhalihaya gupandika bhichabho bha witoji, higulya ya kusalila gete, kugiki bhadule gubhapandika abhitoji bhenabho abhawiza, umuwikaji bhobho.

2Wakorintho 6:2.

Wabrania 12:14.

Luka 9:59-62.

KISWAHILI: UTAKUTWA LWELWE HUJATEMBEA.

Methali hiyo, huangalia mtoto aliyechelewa kutembea. Mtoto huyo, alikuwa akitambaa kwa muda mrefu bila kusimama kwa sababu ya uzito wa miguu yake. Yeye alichelewa sana kutembea mwishowe muda wa kufika Lwelwe ambao ni ndege wanaofika kipindi cha masika, ulikaribia kufika.

Ndege hao wakifika watu huanza kilima kwa sababu ya kutambua kuwa masika yamefika. Ndiyo maana watu waling’wambia mtoto huyo kwamba, “utakutwa lwelwe hujatembea.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa msichana yule ambaye hajaolewa, katika maisha yake. Msichana huyo, ana wito wa kuolewa lakini amechelewa kwa sababu ya tabia yake kutokuwa nzuri. Yeye huwa hasali kwa Mungu awezaye kumpatia mchumba mwema, kwa sababu ya tabia yake hiyo mbaya, maishani mwake.

Msichana huyo, hufanana na yule mtoto aliyechelewa kutembea, kwa sababu naye amechelewa kuolewa, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwambia, “utakutwa lwelwe hujatembea.”

Methali hiyo, hufundisha wasichana na wavulana wenye wito wa ndoa, juu ya kusali sana ili Mungu awajalie kupata, wachumba wema, maishani mwao.

2Wakorintho 6:2.

Wabrania 12:14.

Luka 9:59-62.

family-

african-baby

ENGLISH: LWELWE (RAIN SEASONAL BIRDS {STORK BIRD}) WILL ARRIVE AND FIND YOU HAVE NOT WALKED.

This proverb looks at a child who is late to walk. This baby was crawling for a long time without standing up because of heavy weight of his legs. He was too late to stand up at last. The time of stork bird to arrive was near.  This a bird that arrives during the rainy season.

When these birds arrive, people start to cultivate because they realize that the rainy season has arrived. That is why people told the child that, “Lwelwe (rain seasonal birds {stork birds}) will arrive and find you have not walked.”

This proverb is compared to the unmarried girl in her life. This girl who has been called to get married but she is late because of her bad behavior. She prays to God who can give her a good bride without being successful because of her such bad behavior in her life.

This girl is like the child who was late to walk, because she is also too late to get married in her life. That is why people tell her that, “Lwelwe (rain seasonal birds {stork bird}) will arrive and find you have not walked.”

This proverb imparts in young girls and boys who are called to live marriage life to behave, enough to carry on praying earnestly for God who can grant them good brides in their lives.

2 Corinthians 6: 2.

Hebrews 12:14.

Luke 9: 59-62.

977. HAMBO HAMBO GUGALUKA IHANGA GUKILA GUGALUKA NG’HOLO.

Imbuki ya lusumo lunulo, ilolile lihanga na ng’holo ya ng’wa Munhu. Ilihanga linilo, kalikigelele ka ng’wa munhu ako kaliheke ni ng’holo yakwe, kunguno umunhu adulile gubhiza ni hanga lisoga aliyo ing’holo yakwe iliyabhubhi. Ilihanga linilo lidambilija ginhu. Gashinaga lulu mumo ligab’elela ilihanga lwake umunhu ng’wunuyo, ulu ali na ng’holo yabhub’i adulula ugwikala chiza na bhanhu.

Ukulwande ulungi, uong’holo nsoga agikalaga chiza na bhanhu mumo likab’ipila ilihanga lyakwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “hambo hambo gugaluka ihanga gukila gugaluka ng’holo.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina ng’holo ya gwikala chiza na bhanhu, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga bho gudimila nhungwa ja guntogwa Mulungu na bhanhu bhakwe, kunguno atogilwe gwikala na ng’oho yawiza. Uweyi agadulaga gwikala na bhanhu bhingi aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya ng’holo yakwe iyo iliyawiza yiniyo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo alina ng’holo yawiza iyo igang’wambilijaga ugwikala na bhanhu chiza, kunguno nuweyi alina ng’holo yawiza iya guntogwa Mulungu na bhanhu bhakwe, umukikalile kakwe. Uweyi agabhalangaga abhanhu nhungwa jawiza ija gubhambilija gubhiza na ng’holo niza, umuwikaji bhobho. Hunagwene agabhawilaga giki, “hambo hambo gugaluka ihanga gukila gugaluka ng’holo.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gubhiza na ng’holo jawiza ija gubhambilija ugujidimila inhungwa ija guntogwa Mulungu na bhanhu bhakwe, kugiki bhadule gwikala na bhichabho chiza, umubhulamu bhobho.

1Petro 3:8.

1Yohana 4:7.

Waebrania 13:1-2.

1Petro 4:7-11.

KISWAHILI: HERI KUBADILIKA SURA KULIKO KUBADILIKA ROHO.

Chanzo cha methali hiyo, huangalia sura na roho ya mtu. Sura ni muonekano wa nje ambao uko tofauti na roho, kwa sababu mtu anaweza kuwa na sura nzuri lakini roho yake ikawa mbaya. Sura hiyo haimsaidii kitu. Kumbe basi, mtu hata awe na sura nzuri kiasi gani kama roho yake ni mbaya hataweza kuishi vizuri na watu wake.

Kwa upande mwingine, mwenye roho nzuri, huishi vizuri na watu hata kama sura yake ni mbaya. Ndiyo maana watu husema kwamba, “heri kubadilika sura kuliko kubadilika roho.”

Mtu huyo, hufananishwa na mtu mwenye roho nzuri ya kuishi na watu vizuri, maishani mwake. Mtu huyo, huishi kwa kuyashikilia maadili mema ya kumpenda Mungu na watu wake, kwa sababu ataka nao wawe na roho njema. Yeye huweza kuishi na watu wengi vizuri kwa sababu ya roho yake hiyo njema, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mwenye roho njema inayomwezesha kuishi na watu vizuri, kwa sababu naye ana roho njema ya kumpenda Mungu na watu wake, katika maisha yake. Yeye huwafundisha watu maadili mema ya kuwasaidia kuwa na roho njema, maishani mwao. Ndiyo maana huwaambia watu hao kwamba, “heri kubadilika sura kuliko kubadilika roho.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwa na roho njema ya kuwasaidia katika kuyashikilia maadili mema ya kumpenda Mungu na watu wake, ili waweze kuishi vizuri na wenzao, maishani mwao.

1Petro 3:8.

1Yohana 4:7.

Waebrania 13:1-2.

1Petro 4:7-11.

african-church-

ENGLISH: IT IS BETTER TO CHANGE SHAPE THAN TO CHANGE SOUL.

The basis of this proverb looks at the shape and soul of a person. A shape is an outward appearance that is different from the soul, because a person may have a good appearance but his/her soul can become horrible. Such appearance does not help him/her at all. However, no matter how good a person may be if his soul is bad, he/she will not be able to live well with people.

A good person, on the other hand, lives well with people even when he has a bad appearance. That is why people say that, “It is better to change shape than to change soul.”

This proverb is related to a person with a good soul who lives well with people in his life. This person lives by holding to the moral standards of love for God and his people, because he wants them to have a good soul. He can live with many people because of his good deeds to others in his life.

This person resembles the one who has a good soul that enables him to live well with people, because he also has a good soul enough to love God and his people, in his life. He teaches people good manners enough to help them in having a good soul in their lives. That is why he tells them, “It is better to change shape than to change soul.”

This proverb teaches people on how to have a good soul enough to help them in holding to the good values ​​of loving God and his people, so that they can live well with each other in their lives.

1 Peter 3: 8.

1 John 4: 7.

Hebrews 13: 1-2.

1 Peter 4: 7-11.