Author: Sukuma legacy

797. DIMA NZOKA UDIZUDIMA JIKOLO JA BHANGI.

Ulusumo lululo, lulolile bhuhambohambo bho gudima nzoka gukila ugudima ijikolo ja bhangi. Ubhudimi bho nzoka bhugikalaga niyange lya gulung’wa ni  nzoka yiniyo, kunguno inzoka iningi jigikalaga na bhusungu.

Aliyo lulu, ugudima ijikolo ja bhangi gugabhizaga niyange itale kukila ugwidima nzoka, kunguno undimi adulile guding’wa na gutulwa mpaga ucha. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “dima nzoka udizudima jikolo ja bhangi.”

Ulusumo lunulo, lugalenaganijiyagwa kuli munhu uyo agamanaga usola jikolo ja bhangi bho nduhu uguzunilijiwa, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agitanagwa nsambo kunguno agabhib’ilaga abhiye ijikolo jabho. Uweyi adamanile igiki agiyenhelejaga kupandika makoye ayo galikihayo na guding’wa utulwa mpaga ucha.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agogoha gudima nzoka bho gusola jikolo ja bhangi wiyenheleja gutulwa mpaga ucha, kunguno nu weyi agibhaga jikolo ja bhangi abho bhadulile gundina na kumulaga. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “dima nzoka udizudima jikolo ja bhangi.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka nhungwa ja bhusambo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gubhulang’hana chiza ubhupanda bhobho, uwikaji bhobho.

Mambo ya Walawi 19:11-13.

1Wathesalonike 4:6.

KISWAHILI: SHIKA NYOKA USISHIKE VITU VYA WENGINE.

Methali hiyo, huangalia urahisi wa kushika nyoka kuliko kushika vitu vya wengine. Ushikaji huo wa nyoka huwa ni wa hatari sana kwa sababu ya uwepo wa nyoka wengi wenye sumu ya kuweza kuua mtu.

Lakini kushika vitu vya wengine huwa ni kitendo cha hatari kubwa zaidi ya kushika nyoka kwa sababu akikamatwa huyo aliyeshika vitu hivyo aweza kupigwa hadi kufa. Ndiyo maana watu husema kwamba, “shika nyoka usishike vitu vya wengine.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa anachukua vitu vya wengine bila ya kuruhusiwa, katika maisha yake. Mtu huyo, huitwa mwizi kwa sababu ya kuwaibia wengine vitu vyao. Yeye huwa haelewi kwamba, kwa kitendo hicho, hujiletea matatizo mbalimbali yakiwemo yale ya kukamatwa na kupigwa hadi kufa.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeokopa kushika nyoka, kwa kudiriki kushika vitu vya wengine, kwa sababu naye huiba vitu vya wengine wanaoweza kumkamata na kumuua. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “shika nyoka usishike vitu vya wengine.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya wizi katika maisha yao, ili waweze kuulinda vizuri uhai wao, maishani mwao.

Mambo ya Walawi 19:11-13.

1Wathesalonike 4:6.

snake catching

snake catching1

snake catching2

ENGLISH: CATCH SNAKE DO NOT SNATCH OTHERS’ THINGS.

This proverb focuses at an ease way of catching snakes rather than grabbing things of others. These snake bites are very dangerous because of the presence of many venomous snakes that can kill a person.

But snatching belongings of others is a far more dangerous act than catching snakes because if one is caught doing so can be beaten to death. That is why people say, “catch snake do not snatch others’ things.”

This proverb is compared to a person who tends to take other people’s belongings without permission, in life. This person is called a thief because he robbed others of their belongings. He does not understand that, in doing so, he inflicts various hardships on himself, including arrest and beatings to death.

This person is like the one who is afraid of catching a snake, by daring to grab the things of others, because he also steals the things of others who can catch and kill him. That is why people say to him, “catch snake do not snatch others’ things.”

This proverb imparts in people an idea of stopping a habit of theft in their lives, so that they can better protect their lives, in their societies.

Leviticus 19: 11-13.

1Thessalonians 4: 6.

796. YENIYO YAPONYA BHABHIJI.

Ikale aho bhadinamana ugwilagula imbiji, abhanhu abhambiji bhatulagwa lwande, kunguno ya gogoha gubhalekaja abhangi. Kuyiniyo lulu, abhanhu bhenabho nulu agazumalika, abhangi bhogohaga ugujubhajika. Ulu munhu uja kujubhajika na umanyika chine, otulagwa lwande.  Hunagwene abhanhu bhagiwilaga giki, “yiniyo yaponya bhabhiji.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhuchaga ginhu jibholile, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adadebhile ugugulang’hana chiza umili gokwe, kunguno ya gugulekanija mumakoye ga gupandika bhusatu.  Uweyi agikalaga ukoyiwa na sata ja mbika ningi, kunguno ya gubhucha ginhu ijo jigikalaga na madudu kunguno ya bhubhozu bhojo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agaponya bhabhiji ukumuka kunguno nuweyi agakumukaga bho gubhucha ginhu ijo jibholile, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagiwilaga giki, “yiniyo yaponya bhabhiji.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kuyilang’hana chiza imimili yabho, bho gwiganika na gwita miito ga wiza, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwikala chiza na bhichabho, shigu jose.

Marko 7:14-23.

KISWAHILI: HUYO AMEZIKA WAKOMA.

Hapo zamani, wakati watu hawajagundua matibabu ya ukoma, watu wenye ugonjwa huo walitengwa mbali na jamii. Kwa hiyo basi, watu hao hata wakifariki wengine waliogopa kwenda kuwazika. Mtu akijulikana kwamba alienda kuwazika alitengwa naye ili asiwaambukize wengine. Ndiyo maana watu waliambiana kwamba, “huyo amezika wakoma.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huchukua vitu vilivyooza katika maisha yake. Mtu huyo, huwa haelewi namna ya kuitunza vizuri afya ya mwili wake kutokana namna yake ya kuitelekeza kwa kugusa vitu vyenye wadudu. Yeye huutelekeza mwili wake huo kwa kuuweka katika mazingira ya kupata magonjwa ya aina mbalimbali kwa sababu ya wadudu anaowashika kwenye vitu hivyo vilivyooza.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyetengwa na watu baada kujulikana kwamba alienda kuwazika wakoma, wakiogopa kuambukizwa naye, kwa sababu naye huyahatarisha maisha yake kwa kuchukua vitu vilivyooza katika maisha yake. Ndiyo maana watu huambiana juu yake kwamba, “huyo amezika wakoma.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuilinda vizuri miili yao, kwa kufikiri na kutenda matenda mema, katika maisha yao, ili waweze kuishi vizuri na wenzao, siku zote.

Marko 7:14-23.

african-1

african2

ENGLISH: THAT ONE HAS BURIED LEPERS.

In the past, when people had no knowledge of the cure of leprosy, people with such disease were excluded from their societies. Therefore, even when these people died, some were afraid to go to bury them. A person who was known to have gone to the funeral was isolated from their societal members so that he could not infect others. That is why people said to one another, “that one has buried lepers.”

This saying is likened to a person who picks up rotten things in his life. This person does not understand how to take good care of his or her body due to the way he or she abandons it by touching insects. He abandons his body by exposing it to various insects because of the parasites which he catches on the decaying materials.

This person is like the one who was separated from the people after it was known that he went to bury lepers, fearing that he infecte others, because he also endangers his life by taking the rotten things in his life. That is why people say to one another, “that one has buried lepers.”

This saying teaches people on how to properly protect their bodies by preventing them from being infected by various diseases in their lives, so that they can live happly with their societal members all the time.

Mark 7: 14-23.

795. GUYOMBA GWIJUKULA GUHUMULA GWIJIKA.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya wijukuji bho ng’wa munhu na wijiki bhokwe. Bhalihoyi bhanhu bhabhili abho bhikalaga muchalo jilebhe. Abhanhu bhenabho, bhagamala ijiliwa jagulya.

Uumo agaja gujulanda habhuzenganwa aliyomba, “naliomba munigunane jiliwa nagalye nagucha na nzala kunguno natubhaga noyi.” Abhazengangwa bhakwe bhagang’wila, “solaga lulu jiji aha ugalye.” Umunhu ng’wunuyo, agapila ugucha na nzala kunguno ya guyomba bho gulomba jiliwa kubhiye.  Uweyi agijukula bho gulomba jiliwa jinijo kubhiye bhenabho.

Aliyo lulu, ung’wiye oduka ahumulile duhu alukunhu inzala ilinabhula, nose agananuka bho gucha na nzala. Umunhu ng’wunuyo, agabhiza wijika weyi bho guhumula gokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “guyomba gwijukula guhumula gwijika.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapandikaga makoye obhabhile wangu abhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, ijinagugemela, ulu usada agayombaga kubhiye kunguno adebhile igiki bhadulile gung’wambilija bho gunchala kusitali. Uweyi agagamalaga wangu amakoye gakwe kunguno ya gubhawila abhiye abho bhagang’wambilijaga haho gatali ugugula, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agapila nzala bho gulomba jiliwa habhuzenganwa bhokwe, kunguno nuweyi agalombaga wambilijiwa kubhiye, ulu opandikaga makoye. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “guyomba gwijukula guhumula gwijika.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gugamala wangu amakoye gabho bho gulomba wambilijiwa kubhichabho, kugiki bhadule gutumama milimo yabho mhola, umuwikaji bhobho.

Luka 18:1-5.

Mathayo 11:28.

KISWAHILI: KUONGEA KUJIFUFUA, KUNYAMAZA KUJIZIKA.

Methali hiyo, huongelea juu ya kujifufua kwa mtu na kujizika kwake. Walikuwepo watu wawili katika kijiji fulani. Watu hao walimaliza chakula wakawa katika hatari ya kufa.

Mmoja alienda kuomba msaada kwa jirani zake akisema, “naomba munisaidie chakula nikale nitakufa kwa njaa, kwa sababu najisikia njaa sana.” Majirani zake walimwambia, “chukula hiki hapa ukale.” Mtu yule alijiponya kufa kwa njaa kwa sababu ya kuomba chakula kwa wenzake. Yeye akawa amejifufua kwa kuomba chakula hicho kutoka kwa wenzake hao.

Lakini, yule mwingine alibaki kimya tu huku akiumizwa na nzaa ile, mwishowe alipoteza maisha yake kwa kukosa chakula. Mtu huyo, akawa amejizika mwenyewe kwa kukaa kimya wakati ana tatizo kubwa linaloweza kutatuliwa kwa kuwashirikisha wenzake. Ndiyo maana watu walisema kwamba, “kuongea kujifufua, kunyamaza kujizika.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hupata matatizo na kuwashirikisha wenzake mapema, katika maisha yake. Mtu huyo, kwa mfano, akiugua, huwaambia wenzake kwa sababu anafahamu kwamba, wale wanaweza kumsaidia kwa kumpeleka hospitalini mapema. Yeye hupata utatuzi wa matatizo yake mapema kwa sababu ya kuwashirikisha wenzake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyepona kufa kwa njaa kwa kuomba chakula kutoka kwa wenzake, kwa sababu naye akipata matatizo, huomba msaada unaoweza kumsaidia kutoka kwa wenzake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kuongea kujifufua, kunyamaza kujizika.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyamaliza mapema matatizo yao kwa kuomba msaada kutoka kwa wenzao, ili waweze kuendelea kuyatekeleza majukumu yao salama, maishani mwao.

Luka 18:1-5.

Mathayo 11:28.

people-talking1

people-talking

talking

ENGLISH: TO SPEAK OUT IS TO RESURRECT ONESELF TO REMAIN SILENT IS TO BURY ONESELF.

This proverb speaks of a person’s resurrection and burial. There were two people in a certain village. These men finished food and were in danger of dying.

One of them went to ask for help from his neighbors, saying, “Please help me to eat otherwise I will starve to death, because I am so hungry.” Her neighbors told her, “Take this and eat it here.” The man saved himself from starvation by begging for food from his companions. He became self-reliant by asking for food from his companions.

However, the other man remained silent while he was hurt by the hunger, eventually lost his life for lack of food. The man became obsessed with keeping quiet when he had a serious problem that could be solved by involving his colleagues. That is why the people said, “to speak out is to resurrect oneself to remain silent is to bury oneself.”

This proverb is compared to a person who gets into trouble and shares it with others early in life. This person, for example, when he or she is sick, tells his or her colleagues because he or she knows that those are the ones who can help him or her by taking him or her early to hospital. He finds a solution to his problems early because of an involvement of his colleagues in looking for solutions to various tribulations in life.

This person is like the one who survived a starvation by begging for food from his fellows, because when he gets into trouble, he also asks for help from his fellows. That is why people say to him, “to speak out is to resurrect oneself to remain silent is to bury oneself.”

This proverb instills in people an idea on how to solve their problems early by asking for help from their neighbors, so that they can continue carrying out their daily responsibilities safely in their lives.

Luke 18: 1-5.

Matthew 11:28.

794. MHELA IDUGAYIWA BHUSHEMELI.

Imhela ili ndimu iyo igikalaga ya danhagwa, nulu yalumagwa ng’hundya umu mili goyo. Kuyiniyo lulu, inoni ijo jigitanagwa bhushemeli na jingi ja mbika ningi, jigamanaga julya ng’hundya umu mili go mhela yiniyo.

Inoni jinijo, jigamanaga juchalanijiwa ni mhela yiniyo uko ijile, kugiki jimane jujilya ing’hundya jinijo. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “mhela idugayiwa bhusehemeli.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinsabhi o majikolo mingi, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhizaga na jiliwa ja gudula gubhalisha bhanhu bhingi abho bhagatumamaga milimo aha kaya yake. Uweyi agikalaga na bhanhu bhingi kunguno ya kupandika bhatumami bha milimo yakwe, abho nabho bhagamanaga bhulya jiliwa ja ha kaya yiniyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni mhela iyo idagayiwagwa bhushemeli, kunguno nu weyi adagayiwagwa abhanhu abha gutumama milimo yakwe na gulya jiliwa jakwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mhela idugayiwa bhushemeli.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwikala na gwiyambilija bho gutumama milimo chiza, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Marko 2:1-2.

Yohana 6:26.

KISWAHILI: FARU HAKOSI NDEGE.

Faru ni mnyama poli ambaye huwa ameng’atwa na kupe mwilini mwake. Kwa hiyo basi, ndege wanaokula kupe hao huwa hawaishi mwilini mwake kwa sababu ya wao kuendelea kufaidika kwa kuwala hao kupe.

Ndege hao, huendelea kupelekwa na mnyama huyo kokote anakoenda kwa lengo la kuendelea kuwala hao kupe. Ndiyo maana watu husema kwamba, “Faru hakosi ndege.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni tajiri wa vitu vingi katika maisha yake. Mtu huyo, huwa na chakula kingi kiasi cha kutosha kuwalisha watu wote wanaofanya kazi kwenye familia yake.

Tajiri huyo, huishi na watu wengi kwa lengo la kupata wafanya kazi katika familia yake, ambao nao hufaidika kwa hula chakula cha pale, kama vile ndege wanavyofaidika kwa kula kupe mwilini mwa Faru.

Mtu huyo, hufanana na Faru yule asiyekosa ndege mwilini mwake, kwa sababu naye huwa hakosi watu wa kufanya kazi na kula chakula katika familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “Faru hakosi ndege.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuishi kwa kusaidiana katika kuyatekeleza vizuri majukumu yao, katika maisha yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Marko 2:1-2.

Yohana 6:26.

rhonoceros mhela

rhinoceros-mhela

rhino-mhela

ENGLISH: THE RHINO DOES NOT LACK BIRDS.

The Rhino is a wild animal that is been bitten by ticks on its body. Therefore, birds which eat those ticks do not leave its body because they continue to benefit from eating those ticks.

These birds continue to be carried by this animal wherever it goes with an aim of continuing to eat the ticks. That is why people say, “the Rhino does not miss birds.”

This proverb is compared to the man who is rich of many things in his life. This person, in turn, has enough food to feed all people who work in his family.

This rich man lives with many people in order to find workers in his family, who also benefit from eating local food, just as birds benefit from eating ticks on the body of a Rhino.

This man is like the Rhino which does not miss birds in its body, because it also has people who work and eat food in his family. That is why people say to him, “the Rhino does not miss birds.”

This proverb teaches people on how to live by helping each other in fulfilling their daily responsibilities, in their lives, so that they can better develop their families in their societies.

Mark 2: 1-2.

John 6:26.

 

793. AHO BHAGALILAGA BHADINGAGA HOYI.

Ahabhulilo bho jiliwa lilipande lya gubhabhilinga bhose abho bhagapandikilaga jiliwa hoyi. Olihoyi munhu uyo ahayaga gubhilinga lugiko kugiki adule guhoya chiza na bhanhu bhingi.

Umunhu ng’wunuyo, agabhasanga bhanhu bhalilya jiliwa abho bhagang’wila, “nzugu dulye japyagaga jiliwa ahenaha.” Uweyi agashosha, “nahene naliza dulye kihamo.” Uweyi agapandika wasa bho gubhalomela abhanhu bhenabho imihayo yakwe, kunguno bhali bhingi noyi.

Aho omala ugulya agabhuja, “gulihoyi nimo ki nayi ahenaha iki ng’wakwilaga chiniki?” Abhazengi bha hene bhagashosha, “Ahenaha bhadingaga abhanhu, kunguno jigazugagwa jiliwa bhuli lushigu ja gulya bhose abho bhatubhaga.” Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “aho bhagalilaga bhadingaga hoyi.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo, agaitumamaga mpaga oyimala imilimo iyo inganpandikilaga jiliwa, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agaidililaga chiza imilimo yiniyo, kunguno yigananhanijaga chiza ikaya yakwe. Uweyi agabhalangaga na bhanhu bhakwe inzila ja gwigulambigija uguitumama imilimo yabho, kugiki nabho bhabhapandikile jiliwa abhanhu bhabho.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhanhu abho bhadingaga aho bhagalilaga jiliwa, kunguno nuweyi adailekaga imilimo iyo igampandikilaga jiliwa ja guilisha ikaya yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “aho bhagalilaga bhadingaga hoyi.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija guitumama chiza imilimo yabho, iyo igabhapandikilaga jiliwa, umukikalile kabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Yohana 6: 26-27.

Yohana 6:68.

KISWAHILI: WANAPOLIA HAWAONDOKI HAPO.

 Sehemu ya kulia chakula ni mahali pa kujikusanyia wote wanaojipatia chakula pale. Alikuwepo mtu mmoja ambaye alitaka kuitisha mkutano ili aweze kuongea na watu wengi.

Mtu huyo, alikuta watu wakila ambao walimkaribisha wakisema, “njoo tule chakula kimeiva hapa.” Yeye alijibu, “sawa nakuja tule pamoja.” Yeye alipata nafasi ya kuwasimulia watu wale yale aliyokuwa amepanga kuwaeleza, katika mkutano huo, kwa sababu walikuwa wengi sana.

Alipomaliza kula, aliuliza, “kuna kazi gani hapa, ambapo wamekuja watu wengi hivi?” Wananchi wa hapo, walijibu, “hapa watu huwa hawaondoki kwa sababu, hupikwa chakula kila siku cha kuwalisha wale wanaojisikia njaa.” Ndiyo maana watu husema kwamba, “wanapolia hawaondoki hapo.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzitekeleza vizuri kazi zile zinazompatia chakula, katika maisha yake. Mtu huyo, huzijali kazi zake hizo, kwa kuzitekeleza vizuri, kwa sababu hizo ndizo zimpatiazo mahitaji ya familia yake. Yeye huwafundisha watu wake namna ya kuongeza bidii ya kuyatekeleza vizuri majukumu yao, ili waweze nao kujipatia mahitaji yao ya kila siku.

Mtu huyo, hufanana na watu wale wasioondoka pale wanapopatia chakula, kwa sababu naye huzitekeleza mpaka huzimaliza vizuri kazi zile zinazompatia mahitaji yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “wanapolia hawaondoki hapo.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yale yawapatiayo chakula, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Yohana 6: 26-27.

Yohana 6:68.

eating place

baobab fruit

ENGLISH: WHERE PEOPLE EAT DO NOT MOVE OFF THERE.

 The dining room is a place for gathering all those who get food there. There was one person who wanted to convene a meeting so that he could talk to a good number of people.

Such man found people eating who welcomed him by saying, “Come, let us eat some food here.” He replied, “Ok, I will come and eat with you.” He had an opportunity to tell the people what he had planned to tell them, at the meeting, because there were so many of them.

When he finished eating, he asked, “What work is there, as so many people have come?” The local people replied, “People do not leave here because, they cook food every day to feed those who are hungry.” That is why people say, “where people eat do not move off there.”

This saying is compared to a person who performs well the tasks that feed him, in his life. This man takes care of his responsibilities by doing them well, because they are the ones which provide his family with basis needs. He teaches his people on how to be diligent in fulfilling their responsibilities, so that they may be able to meet their daily needs.

This person is like the people who did not leave when they got food, because he also fulfills his responsibilities until he has successfully completed the tasks that provide his family with basic needs. That is why people say, “where people eat do not move off there.”

This saying imparts in people an idea on how to work hard enough to fulfill their daily responsibilities that give food to them, in their lives, so that they can have more success in their families.

John 6: 26-27.

John 6:68.