1102. IKULU IBISI.

Akahayile kenako, kahoyelile higulya ya jiliwa jibhisi. Ijililwa jinijo, jigikalaga jidapile chiza, ijo jili guti numbu, jibabayu na jingi ijo jikolile na jinijo. Abhanhu bhagadumaga ugujilya kunguno ya bhubhisi bhojo bhunubho. Hunagwene bhagajitanaga giki, “ikulu ibisi.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo adajilanijaga chiza na bhiye umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga bhung’wene uko aliyelela kunguno ya kajile kakwe ako katikawiza, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga ugwikala na bhanhu aha kaya yakwe kunguno ya bhujitadilila bhiye bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga ni jiliwa ijibhisi ijo jidijawiza uguliwa, kunguno nuweyi adajilanijaga chiza na bhiye umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “ikulu ibisi.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na nhungwa ja gujilanija chiza na bhichabho, bho gwiyambilija uguitumama imilimo yabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umubhulamu bhobho.

Yohana 13:36-38.

Luka 22:31-34.

Zaburi 53:1-4.

Marko 14:66-72.

KISWAHILI: CHAKULA KIBICHI.

Msemo huo, huongelea juu ya chakula kilicho kibichi. Chakula hicho, hakijaiva vizuri, ambacho ni kama vile viasi, papayi, na vingine vinavyofanana na hivyo. Watu hushindwa kuvila kwa sababu ya ubichi wake huo. Ndiyo maana wao huviita kwamba ni “chakula kibichi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwa haendani vizuri na wenzake katika maisha yake. Mtu huyo, hupendelea kuishi peke yake anakotembelea, kwa sababu ya tabia yake hiyo ya kutopenda kuwa pamoja na wenzake. Yeye hushindwa kuishi na watu kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya tabia yake ya kutokujali wenzake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na chakula kile kibichi kisichokuwa kizuri kuliwa, kwa sababu naye huwa haendani na wenzake katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni “chakula kibichi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na tabia ya kujali wenzao kwa kuendana nao vizuri, ili waweze kusaidiana vyema katika kuyakamilisha vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Yohana 13:36-38.

Luka 22:31-34.

Zaburi 53:1-4.

Marko 14:66-72.

sweet-potato-5318960__480

sweet-potato-1248078__480

potatoes-6528754__480

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.