Olihoyi munhu uyo agigumha gugulu ulab’uka. Umunhu ng’wunuyo, agagulagula ugugulu gokwe gunuyo bho gugukandila minzi maseb’u mpaga gupila kunguno ya bhudiliji bho mmili gokwe bhunubho. Uweyi agapandika bhageni bhingi abhagungisha aho wigunha henaho. Hunagwene agabhawila giki, “hambo hambo gwigumha gugulu gukila gwigumha kululimi.”
Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayombaga mihayo yakwe bho witegeleja bhutale, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agamanile amakoye ayo gagenhelejiyagwa na lulimu ulu munhu uyomba mihayo mibhi ukubhiye, kunguno imihayo yiniyo yigabhaminyaga bhanhu bhingi. Abhangi bhagashidakagwa kunguno ya kuyomba mihayo yagubhaminya bhichabho yiniyo, iyo bhagayiyomba bho gugayitegeleja. Uweyi agikalaga na bhanhu chiza kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho, umukayombele kakwe.
Umunhu ng’unuyo, agikolaga nuyo agigumha gugulu ugulagula bho witegeleja bhutale mpaga gupila, kunguno nuweyi agayombaga mihayo yakwe bho witegeleja bhutale, umumahoya gakwe genayo. Hunagwene agabhawilaga abhanhu bhakwe giki, “hambo hambo gwigumha gugulu gukila gwigumha kululimi.”
Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuyomba mihayo yabho bho witegeleja bhutale, kugiki bhadule gujilang’hana chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.
Yakobo 3:5-6.
Waefeso 4:29.
1Petro 3:10-11.
Zaburi 50:14-20.
KISWAHILI: NI AFADHALI KUJIKWAA MGUU KULIKO KUJIKWAA ULIMI.
Alikuwepo mtu aliyejikwaa mguu wake mpaka ukaumia. Mtu huyo, aliuuguza mguu wake huo kwa kutumia maji ya moto mpaka ukapona, kwa sababu ya umakini wake mkubwa wa kuujali mwili wake huo. Yeye alipata wageni wengi wa kumsalimu na kumpa pole kwa kuumia mguu wake huo. Ndiyo maana aliwaambia kwamba, “ni afadhali kujikwaa mguu kuliko kujikwaa ulimi.”
Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule anayeongea maneno yake kwa umakini mkubwa, katika maisha yake. Mtu huyo, anazifahamu hasara za kuutumia ulimi kwa kusema maneno mabaya kwa wengine, kwa sababu maneno hayo huwaumiza watu wengi. Wengine hushitakiwa kwa sababu ya kuongea maneno yaliyowaumiza wengine katika maisha yao. Yeye huishi na watu vizuri kwa sababu ya umakini wake huo katika kuongea maneno yake, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyejikwaa mguu wake akauuguza kwa umakini mkubwa mpaga ukapona, kwa sababu naye huongea maneno yake kwa umakini mkubwa ili asije akawaumiza wenzake, katika maongezi yake. Ndiyo maana huwaambia watu wake kwamba, “ni afadhali kujikwaa mguu kuliko kujikwaa ulimi.”
Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuongea maneno yao kwa umakini mkubwa, ili waweze kuzilinda vizuri familia zao, maishani mwao.
Yakobo 3:5-6.
Waefeso 4:29.
1Petro 3:10-11.
Zaburi 50:14-20.
ENGLISH: IT IS BETTER TO STUMBLE YOUR FOOT THAN SLIP OF THE TONGUE.
There was a man who tripped on his leg and was injured. This man, in turn, treated his leg with hot water until he recovered due to his intense concern for his body. He received many visitors at his family for greeting him as well as apologizing for injuring his leg. That is why he told them that “it is better to stumble your foot than slip of the tongue.”
This proverb is compared to a person who speaks his words very carefully in his life. This person is aware of the disadvantages of using the tongue for saying wicked things to others because those words hurt many people. There are some people who are accused of saying words that hurt others in their families. He lives well with people because of his focus in speaking his constructive words to others in his life.
This man is like the one who stumbled his feet who was healed, because he also spoke constructive words to others so that he would not hurt his fellows with his words. That is why he tells his people that, “it is better to stumble your foot than slip of the tongue.”
This proverb imparts in people a clue on speaking their words very carefully, so that they can nicely protect their families in their lives.
James 3: 5-6.
Ephesians 4:29.
1 Peter 3: 10-11.
Psalm 50: 14-20.