812. NATUNG’WANA NA SUNGWA JILIFUMA GUJUSUMA NAGULILA NYAMA.

Isungwa jilijisumva ijo jigatumamaga milimo bho gwiyambilija kihamo. Ijoyi jigabhuchaga nigo bhuli yene guti giki jifumilile gujusumo jililwa. Umunhu uyo utung’wana ni sungwa jinijo jibhuchije milimo, agwisagilwa gupandika mbango ja gulya jiliwa ja wiza guti nyama, ukoajile. Hunagwene agayombaga giki, “natung’wana na sungwa jilifuma gujusuma nagulila nyama.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapandikaga mbango bho gutumama milimo kihamo na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhizaga atogilwe gwiyambilija na bhiye kunguno ya jigongo jakwe ija gubhagunana abho bhali na makoye. Uweyi agapandikaga matwajo mingi umuwikaji bhokwe kunguno ya mbango ijo alinajo jinijo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni sungwa ijo jigiyambilijaga kihamo uguitumama imilimo, kunguno nuweyi, agapandikaga mbango ja matwajo mingi, bho gutumama milimo kihayo na bhiye, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “natung’wana na sungwa jilifuma gujusuma nagulila nyama.”

Kahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwiyambilija gutumama kihamo na bhichabho, kugiki bhadule gupandika matwazo mingi, umuwikaji bhobho.

Mithali 28:20.

Ufunuo 5:12.

Luka 19:37-38.

KISWAHILI: NIMEKUTANA NA SUNGUSUNGU WANAOTOKA KUHEMEA NITAKULA NYAMA.

Sungusungu ni viumbe ambavyo hufanya kazi kwa kusaidiana pamoja. Kila mmoja wao hubeba mzigo wake, unaonesha kama wanatoka kuhemea chakula. Mtu ambaye atakutana na sungusungu hao waliobeba mizigo, atatumaini kupata Baraka za kula chakula kizuri, kama vile nyama, kule anakoelekea. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “nimekutana na sungusungu wanaotoka kuhemea nitatakula nyama.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hupata baraka kwa kufanya kazi pamoja na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, hupenda kusaidiana na wenzake hao kwa sababu ya huruma yake ya kuwasaidia wale walioko kwenye matatizo. Yeye hupata mafanikio mengi maishani mwake kwa sababu ya Baraka hizo alizonazo.

Mtu huyo, hufanana na sungusungu wale walioshirikiana katika kufanya kazi, kwa sababu naye hupata Baraka za mafanikio mengi, kwa kuyatekeleza majukumu yake akishirikiana na wenzake, maishani mwake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “nimekutana na sungusungu wanaotoka kuhemea nitatakula nyama.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kushirikiana pamoja na wenzao wanapoyatekeleza majukumu yao, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Mithali 28:20.

Ufunuo 5:12.

Luka 19:37-38.

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.