Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)
Mbuki ya kahayile kenako ilolile munhu uyo agacholaga bhuki. Ubhuki jili ginhu jinonu. Kuyiniyo lulu, umunhu uyo ahayile gulya chiza agajicholaga ijawiza na gutumama milimo iyo idulile gung’wambilija ujipandika kugiki abhize na bhuyegi.
Umunhu ng’wunuyo agakwabhaga sabho, nulu jikolo bhogutumama bho nguzu na wiyumilija bhutale. Unchoji o ginhu ijawiza jinijo adanogaga ugujichola mpaka ajipandike. Ukwene huguhaya giki, ‘uyo agacholaga bhuki adanogaga.’
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa nu kuli munhu uyo agacholaga ginhu ijawiza bho wiyumilija bhutale mpaka ajipandike. Iginhu jinijo jilisawa na bhusuluja, bhulimi, nu bhutumami ubho milimo iyo iliyawiza. Umunhu ng’wunuyo agajipandikaga, kunguno, ‘Uyo agacholaga bhuki adanogaga.’
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guchola ginhu ijo jilijawiza bho nduhu ugunoga. Ilichiza abhanhu bhabhize na wiyumilija bhutale ubho uguitumama imilimo iyo iliyawiza mpaka guimala chiza na gupandika matwajo mingi.
KISWAHILI: YULE ATAFUTAYE ASALI HACHOKI
Chanzo cha msemo huo chaangalia mtu atafutaye asali. Asali ni kitu kitamu. Kwa hiyo basi, mtu huyo atakaye kula vitu vizuri hutafuta kilicho kizuri kwa kufanya kazi ambazo zaweza kumsaidia kukipata ili awe na furaha.
Mtu huyo hupata mali au vitu hivyo vizuri kwa kufanya kazi kwa nguvu na uvumilivu wa kutosha kumwezesha kuyafikia mafanikio hayo. Mtafutaji huyo wa kitu kilichokizuri huwa hachopi mpaka atakipata. Ndiyo kusema kwamba, ‘Yule atafutaye asali hachoki.’
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule atafutaye kitu kizuri kwa kuvumilia kukubwa mpaka akipate. Kitu hicho ni sawa na kufanya biashara, kuendesha kilimo na kufanya kazi zingine zilizo nzuri maishani mwa mtu huyo. Mtu huyo hukipata kitu hicho kilichokizuri kwa sababu, ‘Yule atafutaye asali hachoki.’
Msemo huo hufundisha watu juu ya kutafuta kitu kilicho kizuri kwa uvumilivu bila kuchoka. Yafaa watu wawe na uvumilivu mkubwa wa kuwawezesha kufanya kazi zilizonjema kwa bidii kubwa, mpaka kuzimaliza vizuri kiasi cha kutosha kuwapatia mavuno mengi na yaliyo mazuri.
Zaburi 8:10.
Waebrania 10:36.
Mathayo 13:45-46.
ENGLISH: HE WHO SEARCHES FOR HONEY DOES NOT GET TIRED
The above saying talks about a person who searches for honey. Honey is a sweet thing. Thus, anybody who loves eating sweet things will do whatever it takes to find them and be happy.
A person achieves wealth or admirable possessions through hard work and sufficient patience. Such a person never gets tired in the search for those good things until he/she finds it. That is why it is said, “He who searches for honey does not get tired.”
That maxim is compared to the effort of one who searches for an invaluable thing, enduring all the difficulties until one gets it. Such a thing could be an activity like engaging in business, farming or doing other valuable things in one’s life. The person is bound to get that good thing because, ‘He who searches for honey does not get tired.’
The saying teaches people about perseverance in their pursuit of what they value. People ought to possess a lot of patience to enable them undertake their tasks with hard work until they effectively accomplish those tasks and reap bountifully and admirably.
Psalm 8:10.
Hebrews 10:36.
Matthew 13: 45-46.