94. Ntegi Wa Dundo

Collected by: Don Sybertz,

With special thanks to Rev Joe Healey  (African proverbs,Sayings and stories)

Waliho bhabha umo otegaga noni ulina na ng’wana okwe, ilina lwakwe witanagwa, Masemba. Otegaga Malwabhu, ung’wila giki ung’wana okwe,  “Jugaloleje inoni jise.” Ugasanga lyapujiwagwa inoni Lidundo.

Lyung’wila giki, “Nkoyi nilekelage nagugupija nane.” Ushoka kaya ugabhujiwa nu Ise uhaya giki, “Dudapujije.” Uja hangi unamhala ugatega,  bhagaja gujulindila hangi ntondo, uwilwa hangi ntondo ugujuloleja, aha ukaloleja usanga lyapujiwagwa inoni itale lina lyalyo Nkaganga.

Aho ulidima lyung’wila giki, “nilekelage nkoyi nunene nalagupija.” Na ulilekela ng’hana ushoka kaya. Ugabhujiwa hangi nu Ise, ginehe nkoyi uko dugutegelaga, uhaya “Nugumo.”

Unamhala wiza ubhuka uja koyi uko bhagutegelaga. Aho oshika koyi ugasanga jifuluguto na jitobhango, wibhuja unamhala, aliyo ginehe icheniki. Wandya gugisilija lulu unamhala. Uwilwa na bhanhu, “Iki umasemba agumanagu ujilekela ulu opuja.”

Namhala ukolwa gete niyo,  ushoka kaya. Giko lulu ung’wila giki, “Dujage dugatule mandu ilibhuluma lyakulile no.” ung’wila giki, “dupunzage mambo.”

Bhupunza ng’hana, intondo bhubhuka lulu bhajile gujukoma imambo.  Bhulinha lulu unamhala utongela ugulinha ukwigulya. Na ung’wila lulu masemba, “Linhaga nang’ho dutone amandu. Ng’hana ulinha nawe unabhandya lulu ugutula amandu, aha bhakwija uhaya giki, “Dikage duje kaya.”

Utongela hangi unamhala ugwika, omana ulu agwikaga, unamhala  ulinalipuo omana ujitula imambo janegela ojidubula, nose ung’wana ubhuja giki, “Bhabha ugujikomolaga bhuli imambo?”

Nang’hwe unamhala uhaya giki, “Ambu janegelaga ize najikome bhupya jidame.” Namhala lulu wandya gusolela na mandu duhu, adajikomile. Aho wamala ugusolela ung’wila lulu ung’wana okwe giki, “Ubhebhe lulu omanaga ujilekela inoni jane ohayaga ugubhejaga, unene naje kaya, chaga naha linti linili.”

Uja ng’hana kaya unamhala, uyukumya duhu ung’wana, alibhuja, “nakwita ki lulu iki inoni jang’wa bhabha najilekelaga?” Uyugwisha agulyaga mandu nose ugamala.

Naulizuka ilinoni ilitale ilo oliolilekela ili Kaganga wandya gulitana lulu bholyimbo akwimbaga giki;

“Nkaganga noni nkulu nzugu umbone nene,” Lyuditima lulu ijilaka jalyo lilikule. Ulala lulu, ntondo hangi dilu ulitana,

“Nkaganga noni nkulu nzugu umbone nene.” Lyuditima hangi lyegela. Ulala hangi, iza ulitana hangi ahawela umuakwitanilaga.

“Nkaganga noni nkulu nzugu umbone nene.” Lyegela lulu aliyo uliotubha gete ni nota yankola no. uyulitana lulu agulilaga umana giki akucha. Lyuditimila lulu  haha bihi. Ntondo dilu lulu lyushika, aha lyashika aha ng’wandu lyung’wila, “Masemba ginehe?” Nang’hwe uhaya, “Nene bhabha naluha,  nijagulya nagayiwa kunguno ya giki nakulekela, ubhabha okolwa no igiki nakulekela.

Lyuyomba giki, “faga mate,” amate genayo lulu iza lyugaguba, lyung’wila hangi giki, “subhalaga.” Usubhala amine nagene lyugaguba. Lyung’wila  logadatu, giki, “Nyaga” Aho onya mashi lyugaguba. Na lyung’wila lulu giki, “fungumukaga, aha ofungumuka iza lyunguba nu weyi nalyumpeja lulu kunchala kaya, lyang’wibhalaga kungongo.

Aha lyang’wegeleja umchalo lyung’wila giki, “Jaga lulu kaya, ugabheja ugunipija. Masemba ugashinga hakaya, ugabhina ntungilija gukila abhana abhangi.

Kiswahili: Mtegaji Wa Dundo

Kulikuwa na baba mmoja aliyekuwa akitega ndege na alikuwa na mtoto wake jina lake aliitwa Masemba. Alikuwa akitega Malwabu, alimwambia hivi mtoto wake, “Nenda ukaangalie ndege wetu.” Akakuta amenaswa ndege aliyeitwa Dundo.

Akamwambia kwamba “Bwana nisamehe nami nitakusalimisha.” Akarudi nyumbani na kuulizwa na baba yake hivi, “Hatukukamata?”  Mzee alienda tena kutega, wakaenda tena kwenda kusubilia kesho yake.   Akaambiwa tena, kesho utakwenda kuangalia. Alipoenda kuangalia akakuta amenasa ndege mkubwa jina Nkaganga.

Alipomshika akamwambia kwamba, “Nisamehe na mimi nitakuponya.” Akamwachia kweli akarudi nyumbani. Akaulizwa tena na baba yake, vipi bwana huko tunakotega, akasema “Lile lile.”

Mzee akaja akaenda kule wanakotegea. Alipofika kule, akakuta alama za kuonesha kuwa mtego ulikamata. Mzee akajiuliza, lakini vipi hivi. Akaanza kuulizia, akaambiwa na watu, “Hivi yule Masemba mwanao huwa anawaachia ukikamata.”

Mzee akakasilika kweli, akarudi nyumbani. Hivyo basi, akamwambia hivi, “Twende tukaangue ubuyu hii hali ya kukosa mboga imetuchosha mno.”  Akamwambia kwamba, “tutengeneze vijiti vya kupigilia.”

Wakavitengeneza kweli, wakaanza kupanda huku wakivipigilia vijiti hivyo kwa ajili ya kupandia kwenye miti ya ubuyu. Wakapanda huku mzee akiwa ametangulia kupanda juu. Akamwambia Masemba, “Panda nawe tuchume ubuyu. Kweli alipanda naye ndipo wakaanza kupiga ubuyu.  Walipotungua mwingi, alisema kwamba, “Tushuke basi tuende nyumbani.”

Alitangulia tena mzee kushuka. Wakati akishuka alikuwa na chuma la kuvipiga vijiti vinalegea na kuvichomoa. Mwishoe mtoto akauliza hivi, “Baba, kwa nini unavichomoa vijiti vya kupandia?”

Naye mzee akasema kwamba, “Vimelegea nije nivipigilie upya viimalike.”  Basi, mzee akaanza kuokota ubuyu tu, hakuvipigilia. Basi, alipomaliza kuokota akamwambia mwanae hivi, “Wewe ulipokuwa unawaachia ndege wangu, ulifikiri unafanya vizuri, mimi naenda nyumbani, ufe hapa kwenye mti huu.”

 Mzee akaenda kweli nyumbani. Mtoto akaanza kushangaa tu, akijiuliza, “nitafanya nini sasa, kwa vile nilikuwa nawaachia ndege wa Baba?” Akawa akila ubuyu kwa kutwa nzima, mwishowe akaumaliza ubuyu.

Akamkumbuka yule ndege mkubwa aliyemwachia Nkaganga akaanza kumuita kwa wimbo akiimba hivi:

“Nkaganga ndege mkubwa njoo unione mimi,”

Basi likatoa sauti ya lenyewe likiwa mbali. Basi, akalala kesho yake asubuhi akaliita tena.

“Nkaganga ndege mkubwa njoo unione mimi,”

Likatoa sauti tena likasogea. Akalala tena, akaja kuliita tena kesho yake, alivyokuwa analiita.

“Nkaganga ndege mkubwa njoo unione mimi,”

Likasogea basi, lakini alikuwa ana njaa kweli na kiu ilimkamata sana. Akawa analiita huku akilia akijua kwamba atakufa.

Sauti yake ikasikika hapa karibu. Kesho yake asubuhi likafika. Lilipofika kwenye mbuyu huo, likamwambia, “Masemba vipi?”  Naye alisema, “Mimi baba nilishateseka. Hata chakula nilishakosa kwa sababu ya kwamba nilikuachia. Baba alikasilika sana kwamba nilikuachia.

Likasema kwamba, “tema mate,” mate hayo basi yakaja likayadaka. Likamwambia tena hivi, “kojoa.” Akakojoa ule mkojo nao likaudaka. Likamwambia mara ya tatu, hivi, “Kunya” alipokunya mavi likayadaka.

Basi, Likamwambia hivi, “Polomokaga, alipopolomoka lilikuja likamdaka naye. Basi likamkimbiza kumpeleka nyumbani, huku nimembeba mgongoni.

Lilipomsogeza kwenye kijiji hicho, likamwambia hivi, “Nenda basi nyumbani, ulifanya vizuri kuniokoa. Masemba akashinda nyumbani, akawa mkweli kupita watoto wengine.

turkey

English: A Traper Of “Dundo” (a local name given to one of the Big Birds).

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.