31. Ngumba Nagache atina Ngunani-methali

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Lusumo lwenulu lulitumanilwa ulu bhabyaji bhakambilijiwagwa na ng’wana wabho mu makoye gabho. Bhadulile kuhaya giki, “Ngumba nakache.”

Ng`wana ulu atabyalilwe, tutina ngunani mu makoye gise. Gashinaga gubyala kulina solobho. Uyo atabyalaga atina solobho. Ulu wacha Ima nalyo lyacha.

Liliho lyimbo lya bhasukuma. “Kubyala mayu kubyala jawiza, nenhele mmzi ng`wana wane, ilinilumbi, kubyala jawiza, ilinilumbi. Ha mashula ga witoji bhatali bhimba lyimbo lyenilo mpaga lelo.

Ulu wacha ulma bhana bhagatulaga iwe (ishigo) ha shigila shizukija sha kwizukila bhana na bhizukulu. Ulu ngumba na akwiza ho ufupa nulu kugabha shizukijo, bhatizujimilwa ho bhaduguye, kujugabha ho nulu kwitongeleja ngumba wa kitinde ngumba ng`wikanza lya kujikwa bhakatulaga ikala lyumile umolushindo.

Hukuhaya giki bhugumba bhushile umuludugu. Na hangi luli lumeng`ho lo giki aje na bhugumba wakwe, bhutizubhadima bhangi umu ludugu lwabho.

Kiswahili: Tasa Na Akafe Hana Wa Kumsaidia- methali

Methali hii hutumika kama wazazi wanasaidiwa na mtoto wao katika taabu zao. Wanaweza kusema kwamba “Tasa na akafe.”

Huwa hatuna msaidizi kwenye matatizo yetu kama mtoto hakuzaliwa. Kumbe kuzaa kuna faida. Yule ambaye hazai hana faida. Kama akifa, watu husema, “sijui mwenyewe amekufa.”

Kuna wimbo wa kisukuma usemao, “Kuzaa mama kuzaa ni kuzuri, niletee maji mtoto wangu, inashukrani, kuzaa ni kuzuri, inashukrani.” Hata siku hizi, kwenye sherehe za kuoana bado wanaimba hivyo.

Kama mtu alikuwa na watoto akifa huwa wanaweka jiwe kwenye kaburi ambalo ni ukumbusho wa watoto wao na wajukuu. Kama ni tasa atakuja pale kutekeleza kadiri ya mila alivyofundishwa, yaani kuweka kumbukumbu, wasije wakapotea pale ndugu zake. Hali hiyo huitwa kugawa pale namna ya kuongozana, tasa kitinde, tasa wakati wa kuzikwa, huwekewa kaa lililokauka matakoni, (walivyoamini wao hapo zamani, kwa sasa wengi wameicha imani hiyo).

Ndiyo kusema kwamba, utasa uishe kwenye undugu. Pia, ni alama ya kwamba, “aende na utasa wake, usiwashike wengine tena kwenye undugu wake.

mother-2262750__340

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.