Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu
With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)
Jimala bhupambo – Dede
Pambo na Wilu – Dede
Shingilima, shingilima ndala migunda Dede
Ndala migunda shenene jabhita ibhili Dede
Jabhita ibhili jijile mangaliginja – Dede
Mangaliginja ngoko yalema kubhicha – Dede
Yalema kubhicha, ibhikije ng’wa nyamhanu – Dede
Ng’wa nyamhanu, mhanu mhanukile kunu – Dede
Mhanukile kunu wize umanga – Dede
Akudukile jaso na noko – Dede
Nyanyi gangi yanya dufulo fulo – Dede
Dufulo fulo dongoma nkima Wa bashi – Dede
Nkima wa bashi waja wigonda Dede
Wigonda Sala yita mabhele Dede
Waliho nkima umo walinda, uja kujukanza myenda yakwe hllambo. Wakahayimanila lyamila ililambo lyenilo.aliyo akabhiza alimpanga duhu umugati yilambo.
Gubhiza nzengo gwakwee mo. Iki wali nda akabyala bhana bhabhili bha mabasa, bha Kulwa na Doto. Bhukulila nabho nu ng’wilambo lyenilo bhubhiza bhaniki bha jaluko.
Lushiku lumo bhakafumila nuninabho gukanza myenda yabho. Bhahayimanila gashika mang’ong’oli abhili. Gandya kwimba lyimbo; “Ng’ong’o1i wane udoto jiwangala tukila manyanza, doto jiwangala hiiii!!
Abhaniki aho bhigwa chene bhulibhila ng’wilambo. Wakanoga umayu ng`wenuyo ubhonwa na bhaduguye. Bhunjila kung`wenha kaya. Gaganoga giza hangi amang’ong’oli giza gimba ilyimbo lyago. Ng’ong’o1i wane udoto. Bhupela mukaya bhuyunseka abhiye alihaya kutolwa na ling’ong’oli.
Bhaki manila lushiku lumo giza mang’ong’oIi mingi kwiza kununja ung’waniki udoto. Ubhi watolwa udoto na ling’ong’oli. Ibhujiku Wigaluchaga wabhiza munhu ili mi ng’ong’oli.
Kulushiku lumo, akadoto gukapemba amabhoya gakwe bhujiku. Aha gabhaka jufuma mo ng’ombe, mbuli, ngholo na bhanhu bhingi gete. Gashinaga ing’ong’oli yeniyo yali iti noni. Wali munhu, niyo wali nsabhi na walina bhana bhingi. Bhakigasha nunke na bhanhu bhabho na mitugo jabho. Bhakigala mubhuyegi bhutale.
Kiswahili: Kimaliza Mapambo- Dede
Kimaliza mapambo- Dede
Pambo na wivu – Dede
Shujaa, shujaa, ndala mashamba- Dede
Ndala mashamba senene zimepita mbili- Dede
Zimepita mbili zikienda Mangaliginja – Dede
Mangaliginja kuku aliyekataa kuatamia- Dede
Aliyekataa kuatamia, akiwa amewekeza kwa Nyamhanu- Dede
Kwa nyamhanu, mhanu aliyejiandaa huku- Dede
Aliyejiandaa huku aje mganga – Dede
Aliyekutukana za babako na mamako – Dede
Iliyokunya tena imekunya tupovu povu – Dede
Tupovu povu tumemgonga mwanamke wa bashi – Dede
Mwanamke wa bashi ameenda akiwa amejikunja – Dede
Amejikunja suala akamwaga maziwa – Dede
Alikuwepo mwanamke mmoja wa walinda, akaenda kufua nguo zake kwenye dimbwi. Alishitukia likammeza lile dimbwi. Lakini alibakia kuwa mzima tu ndani ya dimbwi hilo.
Ikawa ndiyo sehemu yake ya kuishi ndani ya dimbwi hilo. Kwa vile alikuwa mjamzito, alijifungua watoto wawili mapacha, Kulwa na Doto. Walikulia nao ndani ya dimbwi hilo wakawa wasichana waliofikia umri wa kuolewa.
Siku moja walitokea nje kufua nguo pamoja na mama yao. Walishitukia wakafika ng’ong’oli wawili. Wakaanza kuimba wimbo: “Ng’ong’oli wangu doto kibeba tukavuka mabahari, doto kibeba hiiiiii!!”
Wasichana waliposikia hivyo, walididimia kwenye dimbwi. Mwishoe mama yule akaonwa na ndugu zake. Wakamwendea wakamleta nyumbani.
Baadaye wakaja tena wale ng’ong’oli wakaja kuimba tena wimbo wao. “Ng’ong’oli wangu doto…” Wakakimbia ndani, wakawa wanamcheka wenzake, kuwa, anataka kuolewa na ling’ong’oli.
Walishitukia yakaja mang’ong’oli mengi kuja kumchumbia doto. Akawa doto ameolewa na ling’ong’oli (ni aina ya ndege). Usiku alikuwa anajigeuza kuwa binadamu, mchana, aligeuka kuwa ng’ong’oli.
Siku moja kadoto kakayachoma manyoa yake usiku. Yalipowaka yale manyoa walitoka humo ng’ombe, mbuzi, kondoo, na watu wengi kabisa.
Kumbe ng’ong’oli huyo hakuwa ndege. Alikuwa mtu, tena alikuwa tajiri na alikuwa na watoto wengi. Walikaa na mke wake na watu wao na mifugo yao. Waliishi maisha yenye furaha kubwa.
ENGLISH: FINISHER DECORATIONS- DEDE
Finisher decorations – Dede
Beautification and jealousy – Dede
Hero, hero, finisher of farms- Dede
Finisher of farms two grasshoppers have passed- Dede
Two of them have passed to Mangaliginja – Dede
Mangaliginja where hen refused to take care of her eggs- Dede
The one who refused to care of her aggs, while invested to Nyamhanu – Dede
To nyamhanu, who has prepared himself- Dede
The one has prepared himself to come with a doctor- Dede
The one who met with your father and mother – Dede
One which ficored has ficored again soft ficore foam foam – Dede
Foam has hit a woman of Bashi- Dede
The woman of Bashi has gone away and while been bending – Dede
She has bent susala has poured milk – Dede
There was a woman in the guard, and she went to wash her clothes in the pool. She happened to be swallowed up the pool. But she remained alive just in the pool.
It became her place of living in that pool. Because she was pregnant, she gave birth to twins, Kulwa and Doto. They grew up as girls to an age of marriage in the pool.
One day they came out to wash dresses with their mother. Suddenly two birds of red heads came to them. They began to sing: “My ng’ong’oli (crane) Doto, the carrier, we shall crose up on the ocean, Doto the carrier hiiiii!!”
When the girls heard about it, they slipped into the pool. Lastly the mother was seen by her relatives. They went to her and brought her home.
Later those cranes came back and sang their song again. “My Ng’ong’oli Doto…” They run away, and they laugh at her fellows, that, she wants to get married with a ng’ong’oli.
They suddenly came many ng’ong’oli to engage Doto. She became married to Ng’ong’oli (crane bird). The night he was transformed into being a man, at noon, turned into a ng’ong’oli (bird).
One day Dodo burned his feathers at night. As soon as the furnace came out, cattle, goats, sheep, and many people came out of it.
Nonetheless the ng’ong’oli was not a bird. He was a man, and he was rich and had many children. They stayed with his wife and their people and their livestock. They lived a happy life.