11. Ng`hingi ya Ndumbulila

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Lushiku lumo ikatula mbula nduma gete, usayayi nunke, bhali bhadini pandi lya gwigasha. Ulu idigiki kupelela ng’wipilinga ling’ong’ho ili lilibihi.

Bhakalibhona lyochi lilifumila ung`wipilinga bhakabhona giki ahenaho nahi pande lya bhupanga wabho. Bhakaja bhalipela. Aha bhashika mo bhisanga ndamhala ya mbiti na nkima wayo na bhana bhabho bhalota moto. Abhoyi bhali bhadibhonaga imbeho.

Yubhakaribhusha indamhala ya mbiti. Duliho Lung’wando. Yuyomba, “Hii, ilelo tapandika na shiliwa ja nyama.” Ulung`wando nang`hwe ushosha, “Muzidubhiza na mayange ilikubi ilya nyama ng`walipandikaga. Tulindagi tume tamu nang’wite umo mulitogelwa.

Ikanza litakulile, Lung`wando nu nke bhuma. Ulung’wando wimila, uyomba, “Lolagi ilipilinga lise lyina makoye, lilihaya gugwa. Tujagi pye abhose tukalihande iliwe lizidutugwila.” Ahenaho unamhala wa Mbiti na bhiye kihamo nu Lung’wando nu nke bhuja kujulihanda iliwe wa nguzu lizutubhagwila.

Aha ikanza lyabhita idoo ulung’wando ung’wila unke, “ Nke wane unimo, gwenuyu ndamu dugumala inguzu na gulumila kushisha nose tugucha. Nalibhona hambo hambo upele wangu wangu ukenhe ng`hingi ya ndumbulila.”

Nke wa Lung’wando upela na atigelile hangi. Lyubhita ikanza ulung’wando uhaya, “Ni bhuli unkima wane wadila ukushoka, nalibhona hambo hambo nankubhije na kiyenhe ing’hingi ya ndumbulila. Aliyo muzidulilekela iliwe likumumala.” Unamhala wa Mbiti uzunya, “Nahene jaga.” Haho na haho Lung´wando upela nhambo gete, atashokile. Ukunu numa umuna Mbiti nabhiye bhulihandatila iliwe lizitugwa. Bhunoga abhangi bhuyucha bhalidimilile iliwe.

Nosage indamhala ya Mbiti yuyomba, “iii! Gong’hana ulung`wndo ali nsala gete, watuwilaga uweyi nu Nke bhaje bhakenhe ng`hingi ya ndumbulila. Gashinaga bhalumbulilaga gete.

Kiswahili: Nguzo Ya Mfululizo

Ilitokea siku moja, mvua kubwa ilinyesha, Sungura na mkewe hawakuwa na mahali pa kwenda kujistiri isipokuwa kukimbilia pangoni katika mlima uliokuwa karibu.

Waliona moshi umefuka wakasema, “Huko ndiko mahali pa usalama wao,” wakaenda mbio. Kufika huko wakamkuta mzee Fisi na  mkewe na watoto wao wanaota moto, bila wao kuona baridi.

“Karibuni akina Sungura.”  Mzee Fisi akasema, “Ama kweli tutapata kitoweo kizuri cha nyama.” Sungura akajibu, “Msiwe na wasiwasi kitoweo cha nyama mtapata, subirini kwanza tupate joto ndipo mwaweza kufanya mtakavyo.”

Haukupita muda Sungura na mkewe walipopata joto mwilini, Sungura akasimama akasema, “Angalieni kuna hatari pangoni petu, litaanguka. Twendeni tushirikiane kuzuia mwamba wa jiwe usituponde.”

Hapo mzee Fisi na wengineo pamoja na Sungura  na mkewe wakaenda kushika jiwe kwa nguvu, lisiwaangukie. Punde Sungura akamwambia mkewe, “Mke wangu kazi hii ni ngumu, tutakosa nguvu za kuinua na hatimaye kufa. Naona ni heri tukimbilie upesi ukalete nguzo ya mti wa mfululizo.”  Bi Sungura akaenda zake mbio, asionekane.

Baada ya muda, bwana Sungura akasema, “Mbona Mke wangu amechelewa kurudi? Naona ni bora nami nimfuate nikalete hiyo nguzo ya mfululizo.”

Mzee Fisi akasema, “Haya nenda.” Hapo Sungura akakimbia mbio  asirudi. Huku nyuma  wakina Fisi na wenzake wakaendelea  kuzingatia maelezo ya kulizuia jiwe lisianguke. Wakachoka baadhi yao wakafa huku wakilishikilia lile jiwe.

Hatimaye Mzee Fisi akasema, “Ama kweli Sungura ni mjanja, alituambia yeye na mkewe wanaenda kuleta nguzo ya mti wa mfululizo, kumbe wamefululiza kweli kweli.”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.