9. Bhana Bhapina Bhadatu

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Shilaka jingi jilihaya mulagagi. Wogoha ulabhula, haho na haho ugaluka ubhiza itale lyapi. Ukukaya bhalolela shiku ningi nduhu kumona. Nose nu ungi ubhuka kuja ko, nang’hwe ukalabhula ubhiza itale lyapi. Ilumbu lyabho usaga ing’wene duhu. Wakanoga ubhuka nang`hwe ajile ko. Uzwala mnyenda ya nyagosha, ushika haho kagikulu. Kung’wila, “Ubhebhe ulibhiza giti ulinkima ukuduja gete. Mazuli zuli duhu bhabhitile bhayanda bhabhili aliyo bhatinashoka na lelo.”

Sumbagwe nu bhebhe, nahene yiyi inhega uje. Ng’hana ng’waniki uja ukashika, aho washika wika ha Nzobhe yakwe, usola bhuluba uchibha amatu.

Wandya kuja kunoni yakwe. Nawe wigwa shilaka shilihaya, “Ndimagi, mulagagi.” Ng’waniki ajile duhu, nose wipandika. Aho wipandika wiwila nakupandika noni yane. Usanga noni ningi jikwimbaga. Iyo yalimukapundu kasoga wisola.

Aho alika uyiwila, “Bhadugu bhane bhajimilila henaha, nakubhabhona kinahe?” Noni yung’wila, “Solaga guyu ntumba gwa minzi uje usamagulila bhakumisha duhu.” Ng`hana wita gitumo wawililagwa. Bhuyufuma bhanhu bhingi, kushisha ubhapandika na bhasisayi. Bhanhu bhingi bhakayega no. ung’waniki bhunkuja.

Bhubhiza bhashoka bhuja kukagikulu, bhukasanga kachaga. Bhukajika bhusambala bhuli ng`wene kaya yakwe. Abhoyi nabho bhuja kaya nu ilumbu lyabho. Ng’hana inoni yeniyo yubhalang`hana mubhupanga wabho.

Kiswahili: Watoto Watatu Yatima

Walikuwapo watoto watatu, wavulana wawili na dada yao. Wazazi wao wote wawili walifariki dunia. Waliachwa peke yao katika nyumba ambayo ilikuwa ni nzuri sana. Waliishi kwa furaha. Walipokua, vijana hao wakawa wawindaji wa wanyama pori. Walikuwa wakimwacha dada yao nyumbani. Siku moja yule msichana alijiwa na jitu pale nyumbani. Jitu likamwuliza,

“Wewe msichana hapa una nani?”

“Tupo watatu, mimi na kaka zangu,” msichana alijibu.

“Kaka zako wamekwenda wapi?”

“Wamekwenda porini kuwinda wanyama!”

Jitu likasifia, “Mmependeza sana. Nyumba yenu ni nzuri. Ila kunakosekana kitu kimoja.”

“Ni kitu gani hicho kilichokosekana?”

“Ikiwa mtampata ndege wa kuimba, nyumba yenu itakuwa nzuri kabisa. Tena atawasaidia katika shida zenu.”

“Tutampata wapi ndege wa aina hiyo?”

“Ndege huyo yuko mbali kidogo, na kupatikana kwake ni vigumu, kwa sababu ana walinzi wake. Anaishi katikati ya pori na njia ya kumfikia ina vikwazo vingi.”

Jitu lile lilipomaliza kusema hayo likatoweka. Msichana hakuliona tena. Waliporejea kaka zake, walimkuta dada yao amehuzunika na kukosa raha kabisa.

“Kwa nini umehuzunika vile dada?” kaka walimwuliza.

Dada aliwasimulia kaka zake yote aliyoelezwa na Jitu. Ila aliwafafanulia kuwa itakuwa vigumu sana kumfikia ndege  yule. Kaka mkubwa akasema, “Mimi nitakwenda kumleta ndege huyo.” Dada yake akamkatalia, “Usiende huko kuna matatizo hutarudi.”

“Hapana lazima nitakwenda, ilimradi uniandalie chakula.” Chakula kilipokuwa kimeandaliwa kweli, kaka mkubwa akaanza safari, alipanda punda. Alipofika mbali, aliiona nyumba, akabisha hodi. Akakubaliwa na bibi kizee. Baada ya kusalimiana, yule kaka alimwuliza yule bibi   kizee, “Tafadhali nionyeshe njia iendayo kwa yule ndege.”

Bibi kizee alitia mashaka kama kweli angeweza kufika huko.  Wengi wameshindwa, na hawakurudi.”

Mama, tafadhali unionyeshe tu njia hiyo ili niende,”kaka alibembeleza. Mwishowe, bibi kizee alimkumbalia. Akamkabidhi mpira (nhega) na kumwambia, “mpira huu ndio utakaokufikisha huko, na mahali utakaposikia ndege wakiimba, ujue kuwa umefika. Hapo ndipo utakaposikia sauti ya kukujaribu na kukudhihaki. Usisikilize wala kuangalia nyuma. Ukigeuka na kuangalia nyuma utakuwa jabali jeusi.”

Kijana aliutumia ule mpira hadi akafika mahali ambapo ndege atapatikana. Hapo aliyaona majabali meusi mengi  sana, na huku  ndege wakipiga kelele kwa mbali kidogo. Akaanza kupanda juu ya jabali. Alipokuwa katikati aliisikia sauti kutoka pande tofauti ikiuliza,  “we kijana, unakwenda wapi?” sauti nyingine ikafoka, “mpigeni kijana huyo!” sauti nyingine iliamuru, “muueni huyo! Muueni huyo!” Baadaye kijana yule aliangalia nyuma na papo hapo akageuka jabali jeusi.

Huku nyumbani walingoja siku nyingi  bila kumuona. Mwishowe na mwingine alianza safari na kwenda huko. Naye aliangalia nyuma, akawa jabari jeusi. Dada yao akabaki peke yake tu.

Baadaye aliondoka naye kwenda huko. Akavaa nguo za kiume. Akafika pale kwa bibi akamwambia wewe si unafanana kama mwanamke utaweza kweli? Juzi juzi wamepita vijana wawili lakini hawakurudi. “Sembuse na wewe.” Haya huu mpira uende.

Kweli akaenda huyo msichana. Alipofika akatelemka kwenye punda yake, akachukuwa pamba akajaza kwenye masikio, akaanza kwenda aliko ndege. Ikaanza kelele tena. Mkamateni, muuweni, mchomeni. Aliposikia  hivyo, msichana alienda tu.

Mwishowe akaipata akaiambia “nimekupata ndege wangu.” Alikuta ndege wengi wanaimba mwenyewe alikuwa kwenye katundu kazuri  akamchukua. Pale alipokuwa akishuka akaiambia “ndugu zangu  wamepotelea hapa nitawaona namna gani?” Ndege akamwabia chukua kibuyu cha maji uende kunyunyuzia wataamka tu.”

Kweli alifanya kama alivyoambiwa. Wakatoka watu wengi, mpaka akawapata na kaka zake. Watu wengi walifurahi mno. Wakamtukuza msichana yule.

Wakawa wamerudi kwenda kwa yule bibi kizee, wakakuta amefariki. Wakamzika, wakasambaa kila mmoja akaenda nyumbani kwake. Wao nao wakaenda nyumbani na dada yao. Kweli yule ndege aliwalinda katika uhai wao.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.