Tanzania

1257. ILYOCHI ALINGIKULU NKAMU UYO ADIMAGA NULU ILITULA MBULA.

Imbuki ya kahayile kenako ilolile katumamile ka lyochi. Ilyochi linilo ligazukaga nulu igutulaga mbula bho nduhu ugwima guti ngikulu uyo alinkamu gutumama milimo yakwe bhuli makanza. Hunagwene abhanhu bhagalitanaga giki, “ilyochi alingukulu nkamu uyo adimaga nulu ilitula mbula.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinkamu gutumama milimo ya ng’wa Mulungu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agabhutumilaga ubhudula ubho bhunhwa nu Mulungu bho gutumama milimo yake na gunamya Weyi chiza, kunguno ya bhukamu bhokwe bhunubho. Uweyi agapandikaga mbango ja gusabha na gwikala na bhanhu chiza, kunguno ya bhukamu bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni lyochi ilo ligazukaga nulu mbula igutulaga bho nduhu ugwima, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe na ya gunamya Mulungu bho bhukamu bhutale, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhaganhayaga giki, “ilyochi alingukulu nkamu uyo adimaga nulu ilitula mbula.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho na gunamya Mulungu bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule kupandika mbango ya gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Ayubu 8:5.

Zaburi 78:34.

Yohana 6:67-68.

Wafilipi 2:28.

KISWAHILI: MOSHI NI BIBI KIZEE MWENYE BIDII ASIYESIMAMA HATA WAKATI INANYESHA MVUA.

Chanzo cha msemo huo, huangalia utendaji kazi wa Moshi. Moshi huo, hufuka hata wakati mvua inanyesha bila kukoma kwa sababu una bidii kama ya bibi kizee afanyaye kazi wakati wote. Ndiyo maana watu huuita kwamba, “moshi ni bibi kizee mwenye bidii asiyesimama hata wakati inanyesha mvua.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana bidii ya kufanya kazi ya Mungu, katika maisha yake. Mtu huyo, huutumia uwezo aliopewa na Mungu kwa kuyatekeleza majukumu yake na yale ya kumwabudu Mungu, kwa sababu ya bidii yake hiyo. Yeye hupata Baraka za kuwa na mali nyingi na kuishi vizuri na watu, kwa sababu ya bidii yake hiyo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ule moshi unaofuka kwa bidii hata wakati wa kunyesha mvua, kwa sababu naye ana bidii ya kuyatekeleza vizuri majukumu yake, na yale ya kumwabudu Mungu, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuongelea kwamba, “moshi ni bibi kizee mwenye bidii asiyesimama hata wakati inanyesha mvua.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuyatekeleza vizuri majukumu yao na yale ya kumwabudu Mungu kwa bidii kubwa, ili waweze kupata Baraka za kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Ayubu 8:5.

Zaburi 78:34.

Yohana 6:67-68.

Wafilipi 2:28.

ENGLISH: THE SMOKE IS A DILIGENT OLD LADY WHO DOES NOT STOP EVEN WHEN IT IS RAINING.

This saying looks at a performance of smoke. Such smoke burns even when it rains non-stop because it is as diligent as an old lady who works all the time. That is why people say that, “the smoke is a diligent old lady who does not stop even when it is raining.”

This saying is compared to a person who is diligent enough to do God’s work in his life. Such person uses the power given to him by God for carrying out his duties and those of worshiping God, because of his diligence. He gets blessings of having a lot of wealth and living well with people, because of his hard working life.

This person resembles the smoke that burns diligently even when it rains, because he is also diligent enough to carry out his duties well, and those of worshiping God, in his life. That is why people say that, “the smoke is a diligent old lady who does not stop even when it is raining.”

This saying teaches people about using great enough effort to carry out their duties well and that of worshiping God, so that they can get blessings for nurturing their families well, in their lives.

Job 8:5.

Psalm 78:34.

John 6:67-68.   

woman-5949729_1280

cooking-8911937_1280

pot-550482_1280

    

1256. BHUTONGI IPOLU NI NUMA IPOLU.

Aho kale olihoyi munhu uyo ali na makoye mingi umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo, ojizukaga ishuku yakwe ijo jabhita osunduhala umu moyo gokwe kunguno ya makoye mingi ayo agabhitila. Uweyi agayugiganika amakoye genayo gabhiza guti obhitilaga ng’wipolu mpaga nose ni shiku jakwe ja bhutongi oyujibhona jili na makoye guti ajile ng’wipolu, kunguno ya mayange ayo ogiyumilijaga genayo umukikalille kakwe. Hunagwene agayomba giki, “bhutongi ipolu ni numa ipolu.”

Akahahile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agiyumilijaga gugamala makoye mingi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga ukoya na makoye mingi ayo agagamala chiza bhuli makanza ulu gigela kunguno ya wiyumilija bhokwe bhunubho. Uweyi agailelaga chiza ikaya yakwe bho gwigunana ugugamala amakoye kihamo kunguno ya wiyumilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo okoyiyagwa na makoye mingi wiyumilija mpaga ogamala chiza, kunguno nuweyi agapandika makoye wiyumilija oguginja mpaka gashila chiza, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “bhutongi ipolu ni numa ipolu.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhumo bho gwiyambilija na gwiyumilija kihamo ugugamala amakoye gabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

1Petro 5:8-9.

Yeremia 10:19.

Yakobo 5:7.

2Timotheo 1:8.

KISWAHILI: MBELE PORI NA NYUMA PORI.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyekuwa na matatizo mengi maishani mwake. Mtu huyo, alikuwa akizikumbuka siku zake zilizopita anahuzunika moyoni mwake kwa sababu ya matatizo mengi aliyoyapitia. Yeye aliyafikiria matatizo hayo yakawa kama alipitia kwenye pori mpaka mwishowe na siku za mbele zinakuwa za matatizo kama anaenda kwenye pori, kwa sababu ya mahangaiko hayo aliyoyavumilia, katika maisha yake. Ndiyo maana alisema kwamba, “mbele pori na nyuma pori.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia matatizo mengi katika maisha yake. Mtu huyo, huhangaika katika kuyatatua matatizo yanayompata mpaka anayamalia vizuri, kwa sababu ya uvumilivu wake huo. Yeye huilea vizuri familia yake kwa kusaidiana katika kuyatatua kwa pamoja matatizo yanayowakumba, kwa sababu ya uvumilivu wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeyatatua kwa uvumilivu matatizo yaliyokuwa yakimsumbua, kwa sababu naye huyamaliza kwa uvumilivu matatizo yanayomkumba katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “mbele pori na nyuma pori.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na ushirikiano wa kuyatatua kwa uvumilivu matatizo yanayowakumba katika maisha yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

1Petro 5:8-9.

Yeremia 10:19.

Yakobo 5:7.

2Timotheo 1:8.

ENGLISH: FRONT WILD AND BACK WILD

Once upon a time there was a man who had numerous problems in his life. Such person used to remember his past days until he became sad in his heart because of a number of problems which he went through. He thought of these problems as if he went through the forest until the end and the days ahead become difficult as if he goes to the forest, because of worries he endured in his life. That is why he said that, “front wild and back wild.”

This saying is equaled to a person who endures many problems in his life. Such person struggles to solve problems that happen to him until he finishes them well, because of his patience. He takes care of his family well by helping each other to solve together problems which they face, because of his patience in life.

This person relates to the one who patiently solved the problems that were bothering him, because he also patiently solves the problems that plague him in his life. That is why he says that, “front wild and back wild.”

This saying imparts in people an idea of having strong cooperation enough to solve with patience the problems which they face in their lives, so that they can bring progress to their families, in their lives.

1 Peter 5:8-9.

Jeremiah 10:19.

James 5:7.

2 Timothy 1:8.

male-4673194_1280

africa-209332_1280

1255. UNG’WUNUYU NSEBHEJI DUHU NAWE.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile munhu uyo otumamaga nimo uyo guti gokwe. Umunhu ng’wunuyo, ogutumamaga chiza unimo gunuyo mpaga nose abhanhu bhuyuhaya giki, unimo gunuyo guli gokwe, kunguno ya gugudilila chiza chiniko. Nose nuweyi agaiganika giki unimo gunuyo guli gokwe aho obhigwa bhanhu bhingi bhalihaya chene. Hunagwene abhanhu abho bhabhumanile ubhunhana bho nimo gunuyo, bhagayomba giki, “ung’wunuyu nsebheji duhu nawe.”

Akahayike kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agigimbilaga milimo iyo idiyakwe, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga jibalubha uyihaya giki alimungunda gokwe kunguno ya wigimbi bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguyibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya gutumama mumajipande na wigimbi bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo otumamaga nimo go bhangi uyiganika giki, guligokwe, kunguno nuweyi agatumamaga mujibalubha uyuhaya giki, alimungunda gokwe. Hunagwene abhanhu bhaganhayaga giki, “ung’wunuyu nsebheji duhu nawe.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gutumamila bhutengeke imilimo ya bhanhu, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Zaburi 33:4.

2Samweli 22:7.

Maombolezo 3:23.

Mathayo 25:20-23.

Wagalatia 5:22.

Tito 2:10.

KISWAHILI: HUYU NAYE NI DALALI TU.

Chanzo cha msemo huo, huongelea mtu aliyekuwa akifanya kazi isiyo yake. Mtu huyo, alikuwa akiifanya vizuri kazi hiyo mpaka baadhi ya watu wakaanza kufikiria kwamba, kazi ile ni yake kwa sababu ya kuijali vizuri. Naye aliposikia watu wengi wakimsifia hivyo, alianza kuifikiria kazi hiyo kama ni yake mwenyewe. Ndiyo maana wale walioufahamu ukweli wa kazi hiyo walisema kwamba, “huyu naye ni dalali tu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujivunia kazi isiyo yake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi kwenye kibarua na kusema kwamba, anafanya kazi kwenye shamba lake, kwa sababu ya majivuno yake hao, maishani mwake. Yeye hushindwa kuiendeleza vizuri familia yake kwa sababu ya kufanya kazi kwenye vibarua vya mashamba ya watu na majivuno yake hayo, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyefanya kazi ya mtu mwingine, akafikiria kuwa ni yake, kwa sababu naye hufanya kazi kwenye vibarua na kusema kwamba, anafanya kazi kwenye Shamba lake. Ndiyo maana watu husema juu yake kwamba, “huyu naye ni dalali tu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kufanya kazi za watu kwa uaminifu na unyofu wa kweli, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Zaburi 33:4.

2Samweli 22:7.

Maombolezo 3:23.

Mathayo 25:20-23.

Wagalatia 5:22.

Tito 2:10.

ENGLISH: THIS ONE IS JUST A BROKER.

The source of this saying speaks of a person who was doing a job that did not belong to him. That person was doing the job well until some people started thinking that the job was his because he cared about it well. And when he heard many people praising him like that, he began to think of the work as his own. That is why those who knew the truth of such work said that, “this one is just a broker.”

This saying is equated to a person who is proud of a job that is not his, in his life. Such man works as a laborer and says that he works on his farm, because of his pride, in his life. He fails to develop his family properly because of working in the fields of people and his pride in his life.

This person is similar to the one who did someone else’s work, and thought it was his, because he also works on the laborers and said that, he is working on his Farm. That is why people say about him that, “this one is just a broker.”

This saying teaches people about doing people’s work with honesty and sincerity, so that they can raise their families well in their life.

Psalm 33:4.

2 Samuel 22:7.

Lamentations 3:23.

Matthew 25:20-23.

Galatians 5:22.

Titus 2:10.

hiring-2402042__480

1254. MAYU NIHOLELE.

Bhalihoyi bhakima abho bhahoyaga umuchalo ja Ng’watuma. Umo obho agilembekejiwa na ng’wiye giki witaga ginhu jilebhe aliyo uweyi adajitile. Umayu ng’wunuyo agashosha giki, “nadajitile iginhu jinijo.” Ung’wiye aganhadikija bho guyomba, “ojiita ulilema duhu.” Hunagwene uyo wilembekejiyagwa agayomba giki, “mayu niholele.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agilembekijiyagwa mihayo ya bhulongo wiyumilija bho guyomba bhunhana, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikomejaga guyomba bhunhana bhuli ikanza ulu wilembekejiwa mihayo iyo adayimanile, kunguno ya bhutungilija na wiyumilija bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga na bhanhu chiza aha kaya yakwe kunguno ya bhutungilija na wiyumilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’winuyo agikolaga nuyo agilembekeji limhaho ilo adalimanile wiyumilija bho guyomba bhunhana, kunguno nuweyi agilembekejiyagwa mihano iyo adayimanile wiyumiliga bho guyomba bhunhana, umukikalile kakwe. Hunagwene agayombaga giki, “mayu niholele.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuleka gubhilembekeja bhichabho mihayo iyo bhadaitile, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

2Samweli 19:27-28.

Zaburi 15:3.

Warumi 1:30.

Yakobo 4:11.

KISWAHILI: MAMA KUMURADHI.

Walikuwepo wakinamama waliokuwa akiongea kwenye kijiji cha Mwatuma. Mmoja wao alisingiziwa na mwenzake jambo ambalo hakulitenda. Mama yule aliyesingiziwa, alielewa kuwa “sikulifanya na silijui.” Mwenzake huyo alilazimisha akisema, “ulilifanya unakataa tu.” Ndiyo maana yule aliyesingiziwa alisema kwamba, “mama kumuradhi.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvumilia kwa kusema ukweli anaposingiziwa maneno ya uongo, katika maisha yake. Mtu huyo, huendelea kusema ukweli kila wakati anaposingiziwa jambo asilolifahamu, kwa sababu ya unyofu na uvumilivu wake huo. Yeye huishi na watu vizuri kwenye familia yake kwa sababu ya unyofu na uvumilivu wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyevumilia kwa kusema ukweli aliposingiziwa jambo na mwenzake, kwa sababu naye huvumilia kwa kusema ukweli anaposingiziwa maneno asiyo yafahamu, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “mama kumuradhi.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kuwasingizia wenzao maneno ambayo hawakuyatenda, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

2Samweli 19:27-28.

Zaburi 15:3.

Warumi 1:30.

Yakobo 4:11.

ENGLISH: PLEASE MOTHER.

There were women who were talking in the village of Mwatuma. One of them was hypnotized by the other, which she did not do. The mother who was accused, said, “I did not do it and I do not know.” The colleague forced her by saying, “You did it, you just refuse.” That is why the one who was insulted said that, “please mother.”

This saying is compared to a person who endures sufferings by telling the truth when he is accused of false words, in his life. Such person continues to tell the truth every time he is accused of something which he does not know, because of his honesty and patience. He lives well with people in his family because of his honesty and patience in life.

This person resembles the one who endured hardships by speaking the truth when she was slandered by her colleague, because he also endures sufferings by speaking the truth when he is slandered by deceitful words in his life. That is why he says that, “please mother.”

This saying imparts in people an idea of stopping gossiping about their people in their lives, so that they can develop their families well in their societies.

2 Samuel 19:27-28.

Psalm 15:3.

Romans 1:30.

James 4:11.

girl-8918049_1280

1253. UDIZUKILILA AHA JAZWILA NOGE UGUNWELA.

Olihoyo munhu uyo ohadikijaga gukila mongo uyo galigonyama. Umunhu ng’wunuyo, ohadikijaga gugukilila umongo gunuyo, aha jazwila noge, kunguno ya bhujidigwa bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “udizukilila aha jazwila noge ugunwela.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agahadikilaga gwita mihayo ya bhubhi umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agitaga mihayo iyo idulile gung’wenhela makoye umubhutumami bhokwe kunguno ya bhujidigwa bhokwe bhunubho. Uweyi agapandikaga makoye ga guduma uguilela chiza ikaya yakwe kunguno ya bhujidigwa bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agahadikija gugukilila mongo aha shimu, kunguno nuweyi agahadikijaga gwita mihayo iyo idulile gung’wenhela makoye umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “udizukilila aha jazwila noge ugunwela.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guzunya guhang’wa na bhichabho ulu bhahubhaga, kugiki bhadule gujilabhila chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

1Samweli 12:20-21.

2Wafalme 17:13.

Mwanzo 3:1-19.

Mwanzo 19:15-26.

KISWAHILI: USIVUKIE PALE ZILIPOVUJIA DAMU PUANI UTAZAMA.

Alikuwepo mtu aliyelazimisha kuvuka mto uliokuwa umemzuia. Mtu huyo, alilazimisha kuvukia pale zilipovujia damu puani, maana yake penye kina kirefu, kwa sababu ya kutokukubali kuonywa kwake na wenzake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “usivukie pale zilipovujia damu puani utazama.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hulazimisha kufanya mambo yanayoweza kumletea matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya mambo yawezayo kumletea matatizo katika utekelezaji wa kazi zake kwa sababu ya ugumu wake wa kukubali kushauriwa na wenzake, maishani mwake. Yeye hupata matatizo ya kushindwa kuilea vizuri familia yake hiyo, kwa sababu ya ugumu wake huo wa kupokea ushauri wa wenzake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyelazimisha kuvukia mto penye kina kirefu, kwa sababu naye hufanya mambo yawezayo kumletea matatizo katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “usivukie pale zilipovujia damu puani utazama.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kukubali kushauriwa na wenzao wanapokosea katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuzitunza vizuri familia zao, maishani mwao.

1Samweli 12:20-21.

2Wafalme 17:13.

ENGLISH: DO NOT CROSS WHERE THE NOSE BLEED YOU WILL DROWN.

There was someone who forced to cross the river that had prevented him. Such man forced to cross where the nose bleed, which means where it is deep, because of not accepting warning from his colleagues. That is why people told him that, “do not cross where the nose bleed you will drown.”

This proverb is equated to as person who forces himself to do things that may cause problems in his life. That person does things that can cause him problems in fulfilling his responsibilities because of his being hard in accepting advice from his colleagues in his life. He finds problems in not being able to properly raise his family, because of his hardness in accepting advice of his colleagues, in his life.

This person is similar to the one who forced to cross a deep river, because he also does things that can bring him problems in his life. That is why people tell him that, “do not cross where the nose bleed you will drown.”

This proverb teaches people to accept advice from their nobles when they make mistakes in fulfilling their duties, so that they can take good care of their families in their lives.

1 Samuel 12:20-21.

2 Kings 17:13.

passengers-in-a-small-boat-3845514_1280