Sukuma Proverbs

784. NYAMA YA NG’HOLO UGUIKOLELWA KUBHOYA.

Inyama ya ng’holo ilindoni noyi uguilwa aliyo lulu, ubhoya bhoyo bhudibhowiza ugubhulola. Gashinaga lulu, ubhoya bhunubho bhudulile gunhecha munhu guilya nyama yiniyo uyo alagelele guwilolela bhoyi duhu bho nduhu ugubhonja iyoyi. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “nyama ya ng’holo uguikolelwa kubhoya.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo abhudebhile uwiza bho mioyo ya bhanhu ubho bhuli heke na mahanga gabho. Umunhu ng’winuyo, agikalaga na bhanhu bhose bho nduhu ugubhakomanya kunguno ya mahanga gabho. Uweyi agapandikaga matwajo mingi umutumami bho milimo yakwe, kunguno ya gwikala kihamo chiza na bhanhu bhakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nyama ya ng’holo iyo iliyawiza kukila ubhoya bhoyo, kunguno nuweyi, alina miito ga gawiza, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, ““nyama ya ng’holo uguikolelwa kubhoya.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gulola wiza bho miito ga bhanhu gukila ugugalola mahanga gabho duhu, kugiki bhadule gwikala chiza na bhichacho, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 1:24.

2Wakorintho 10:7.

KISWAHILI: NYAMA YA KONDOO UTAICHUKIA KWENYE MANYOYA.

Nyama ya kondoo ni tamu sana kwa kuila. Lakini manyoya yake siyo mazuri kwa kuyaangalia. Kumbe basi, manyoya hayo yaweza kumuachisha kuila nyama hiyo yule anayeishia kuyangalia hayo tu bila kuamua kuionja nyama ya mnyama huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “nyama ya kondoo utaichukuia kwenye manyoya.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye anauelewa uzuri wa mioyo ya watu ambao hutofautiana na sura zao. Mtu huyo, huishi na watu kwa amani bila kuwabagua kwa sababu ya sura zao. Yeye hupata mafanikio mengi maishani mwake, kutokana na ushirikiano wake mzuri alio nao kwa watu wake.

Methali hiyo, hufanana na nyama ya kondoo ambayo ni nzuri kupita manyoya yake, kwa sababu naye ana matendo mema yanayomuwezesha kutambua pia nia njema za watu wake, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “nyama ya kondoo utaichukua kwenye manyoya.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuangalia matendo mema ya watu wao badaya kuangalia muonekano wa sura zao tu, ili waweze kuishi kwa amani na wenzao, maishani mwao.

Matendo ya Mitume 1:24.

2Wakorintho 10:7.

sheep1

sheep2

meat1

ENGLISH: YOU WILL HATE SHEEP MEAT ON THE WOOL (THERE IS NO ROSE WITHOUT A THORN).

Sheep meat is very sweet to eat. But its wool are not good to look at. In fact, they may stop eating the meat from the one who ends up looking at them without even deciding to taste the meat. That is why people say, “you will hate sheep meat on the wool.”

This proverb is compared to people who understand the kindness of people’s hearts that differ from their appearances. These people live with others in peace without discriminating against them because of their appearances. They find many successes in their lives, and appreciate good cooperation which they have with others.

These people are like sheep, which is better than its wool, because they also have good deeds that enable them to recognize the good intentions of their people who live with them. That is why they tell others that, “you will hate sheep meat on the wool.”

This proverb teaches people to look at the good deeds of their people instead of just looking at their appearances, so that they can live in peace with each other, in their lives.

Acts 1:24.

2 Corinthians 10: 7.

783. KAWE KAGOSHA KADAKOMANGAGWA.

Ulusumo lunulo, lwingila kubhanhu abho bhilomelaga higulya ya bhukomangi bho liwe. Uumo agang’wila ung’wiye, “likamangage iliwe linilo.” Ung’wiye agabhuja, “nibhuli nalikomange iliwe iligosha linilo?”  Nang’hwe agashosha, “ulu ulikomanga ligubhela gukila igwandya.” Ung’wiye ushobha, “nadudula ugukakomanga akawe kenako kunguno kali kagosha.” Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “kawe kagosha kadakomangagwa.”

Usulumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhadalahijaga abhana abhagosha abha mimili midoo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adajidebhile chiza inguzu ijo bhalijo abhana abhagosha bhenabho. Uweyi agaigayiyagwa ibahati ya gwandilijiwa ugutumama imilimo yakwe imidimu iyo bhaidulile guitumama abhanhu bhenabho, kunguno ya libhengwe lyakwe.

Akawe akagosha kagikolaga nu munhu ngosha uyo bhagandalahaga abhanhu aliyo adulile kutumama nimo ndamu, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagabhawilaga giki, “kawe kagosha kadakomangagwa.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka gubhadalaha abhanhu kunguno ya bhudoo bho mimili yabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwiyambilija chiza uguitumama imilimo yabho, umuwikaji bhobho.

Luka 19:1-10.

KISWAHILI: JIWE DUME HALIGONGWI.

Methali hiyo, ilianzia kwa watu waliokuwa wakiongelea juu ya ugongaji wa jiwe. Mmoja alimwambia mwenzake, “ligonge hilo jiwe.” Mwenzake aliuliza, “kwa nini niligonge hilo jiwe dume?”

Naye akajibu, “unatakiwa kuligonga ili liwe zuri kuliko mwanzani.” Mwenzake huyo, alimjibu, “siwezi kuligonga kwa sababu jiwe hilo ni dume.” Ndiyo maana watu husema, kwamba, “jiwe dume haligongwi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwadharau watoto wa kiume wenye miili midogo, katika maisha yake. Mtu huyo, hazielewi vizuri nguvu walizo nazo watoto hao wa kiume. Yeye hukosa msaada kutoka kwa watu hao kutokana dharau yake hiyo.

Jiwe dume hufanana na mtoto wa kiume ambaye watu humdharau pamoja na kwamba anao uwezo wa kufanya kazi ngumu, katika maisha yake. Ndiyo maana watu huwaambia kwamba, “jiwe dume haligongwi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha kuwadharau watu kwa sababu ya miili yao kuwa na maumbo madogo, katika maisha yao, ili waweze kupata mafanikio mengi katika ushirikano wao wa kuyatekeleza vizuri majukumu yao, maishani mwao.

Luka 19:1-10.

grinding stones

grinding stones.jpg1

stone-grinding.1.jpg3

ENGLISH: A MALE STONE IS NEVER STRUCK.

The above proverb began with people who were talking about hitting a grinding stone. One said to the other, “Hit that stone.” A colleague asked, “Why should I hit it?”

The other replied, “You have to hit it for enabling it to grind grains easily.” His companion replied, “I cannot hit it because it a male stone.” That is why people say that, “a male stone is never struck.”

This proverb is likened to a person who despises small boys in his lifetime. Such man does not fully understand the power of these boys. He lacks support from those people who can help him due to his contempt.

This stone is like a baby boy whom people despise even though he has the ability to work hard, in his life. That is why people say to them, “a male stone is never struck.”

This proverb instills in people an idea of stopping despising others because of their small bodies, in their lives, so that they can have more success in their partnership enough to easily fulfill their responsibilities in their lives.

Luke 19: 1-10.

782. BHAJIKUJA MBITA.

Bhalihoyi bhanhu abho bhatumamaga nimo. Umuluganda lobho, abhingi bhatumamaga chiza imilimo yiniyo. Aliyo lulu, abhagehi bhabho, bhikalaga bhigashije duhu kunguno bhalibhadatumamaga chiza imilimo yiniyo. Abhoyi bhakujaga luganda duhu. Hunangwene  abhanhu bhagabhitanaga giki, “bhakuja mbita.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kubhanhu abho bhali bhagokolo ugutumama imilimo, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagisanjaga  muchibho abho bhagatumamaga milimo bho bhukamu bhutale. Abhoyi bhagisanjaga mubhatumami kugiki bhahayiwe nabho bhatumami bha nhana, gashinaga bhali bhalomolomo duhu.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nabho bhagisanjaga muligele lya bhatumami aliyo bhali bhagokolo, kunguno na bhoyi bhali bhagokolo ugutumama imilimo, aliyo bhagisanjaga mubhatumami. Hunagwene abhanhu bhagabhitanaga giki, “bhakuja mbita.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka bhugokolo bho gutumama milimo, umukikalile kabho, kugiki bhadule gwigulambija chiza uguitumama imilimo yabho, mpaga bhapandike mafumimo mingi, umuwikaji bhobho.

Mathayo 7:22.

Luka 13:26-30.

Mathayo 22:11-14.

KISWAHILI: WAJAZA KUNDI.

Walikuwepo watu waliokuwa wakifanya kazi.  Wengi wao, walifanya kazi vizuri  na kwa bidii sana. Lakini baadhi yao, walipenda kukaa tu bila kuyatekeleza vizuri majukumu yao. Watu hao ambao hawakufanya kazi vizuri, walikuwa wakiliza kundi tu. Ndiyo maana watu waliwaita kwamba ni, “wajaza kundi.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa watu wale ambao ni wavivu wa kufanya kazi, katika maisha yao.  Watu hao, hujichanganya kwenye kundi la watu wenye bidii ya kufanya kazi. Wao hufanya hivyo ili watu wawafikirie kuwa nao ni wachapa kazi wa kweli, kumbe ni waongo tu.

Watu hao, hufanana na wale waliojichanganya kwenye kundi la wenye bidii ya kufanya kazi, kwa sababu nao hujificha kwa wenzao wanaofanya kazi vizuri, kumbe wao ni wavivu. Ndiyo maana watu huwaita kwamba, ni “wajaza kundi.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha uvivu wa kuyatekeleza makujumu yao, katika maisha yao, ili waweze kujibidisha kufanya kazi za kuwaeletea maendeleo, maishani mwao.

Mathayo 7:22.

Luka 13:26-30.

Mathayo 22:11-14.

watu

watu1

bhabhini bha benini

ENGLISH: THE GROUP FILLERS.

There were people who were working in a certain village. Most of them worked well and very hard. But some of them preferred resting by sitting down without fulfilling their responsibilities. Those people, who did not work well, were just filling the group. That is why people called them, “the group fillers.”

This proverb is compared to people who are lazy to work, in their lives. These people, in turn, join a group of hardworking ones. They do this to make people think that they are real hard workers, but they are just liars.

These people are like those who are lazy ones who just filled a group of hard workers, because they are also lazy in their lives. They just pretend to be hard workers but in real sense they not. That is why people call them that they are “the group fillers.”

This proverb teaches people to stop being lazy enough to actively carry out their daily responsibilities, in their families, so that they can bring progress to their societies throughout their lives.

Matthew 7:22.

Luke 13: 26-30.

Matthew 22: 11-14.

781. GUKOMELA GUMICHA.

Ulusumo lunulo, lulolile bhukomeji bho nyama. Inyama igakomelagwa  mpaka yuma kugiki idule gwikala makanza malihu bho nduhu ugubhola. Abhanhu ulu bhuhaya gutuula nyama bhagaikomelaga mpaga yuma. Hunagwene abhanhe bhenabho bhagayombaga giki, “gukomela gumicha.”

Usulumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agaibhugilijaga imihayo mpaga oyidebha chiza, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agayidililaga chiza imihayo yakwe bho guitila bhukengeji bhutale. Uweyi agayidebhaga chiza imihayo yiniyo tamu na wandya ugabhalemela abhiye.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga na bhanhu abho bhagakomelaga nyama mpaga bhumicha, kunguno nu weyi agaibhugilijaga chiza imihayo mpaga oyidebha. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “gukomela gumicha.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya guitila bhukengeji tamu imihayo yabho bho guibhugilija chiza, mpaga bhayidebha, huna bhayichala ukubhichabho, kugiki bhadule gubhalela chiza abhanhu bhabho, umuwikaji bhobho.

Matendo ya mitume 15:5-11.

1Wakorintho 7:18-24.

Waefeso 2:1-10.

KISWAHILI: KUBANIKA KUKAUSHA.

Methali hiyo, huangalia ukaushaji wa nyama. Nyama hubanikwa mpaka ikakauka ili iweze kutunzwa kwa muda mlefu bila kuoza. Hivyo basi, watu wakitaka kutunza nyama huwa wanaibanika mpaka ikakauka. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kubanika kukausha.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huyaulizia maneno mpaka anayaelewa vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, huzijali vizuri kazi zake, kwa kuzifanyia utafiti wa kina. Yeye huyaelewa vizuri maneno hayo, kabla ya kuanza kuwaeleza wenzake.

Mtu huyo, hufanana na watu wale waliobanika nyama mpaka wakaikausha, kwa sababu naye huyaulizia vizuri maneno yake mpaka anayaelewa vizuri katika maisha yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, “kubanika kukausha.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuyafanyia kwanza utafiti maneno yao kwa kuyaulizia vizuri, mpaka wayaelewe, katika maisha yao, ndipo waanze kuyafanyia kazi, ili waweze kuwaelezea vizuri watu wao, maishani mwao.

Matendo ya mitume 15:5-11.

1Wakorintho 7:18-24.

Waefeso 2:1-10.

kigali

dried meat.jpg2

dried meat.jpg1

dried meat

ENGLISH: PATIENCE PAYS.

This proverb focuses on a process of preserving meat by drying it. Such meat is roasted until it is dry so that it can be stored for a long time without rotting. Thus, people who want to preserve it tend to roast it until it is dry. That is why people say, “Patience pays.”

This proverb is compared to a person who asks questions during conversation until he/she understands correctly the central message of it. This person, in turn, takes good care of his or her works by conducting extensive research. He/she understands words well before he begins to use them to his/her colleagues.

This person is like the one who roasted meat until it was dry, because he/she also inquires carefully about his/her words until he/she understands them well before using them. That is why people say, “Patience pays.”

This proverb imparts in people an idea on how to research first their words until they understand before using them, then they start working on them, so that they can better use to their people in their daily lives.

Acts 15: 5-11.

1 Corinthians 7: 18-24.

Ephesians 2: 1-10.

780. NG’HOMBA YA NG’WISONZO UDIKOMBA WIMALE.

Ilisongo jiliseme ijo jigabhejiyagwa bho gutumila madala. Amadala genayo, gagalyenhelejaga gubhiza na tujishepo, umo idulie gwingila inhomga ulu yuditilwa moyi. Giko lulu, umunhu uyo aliyikomba imhomba yiniyo aduyimala. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “Ng’homba ya ng’wisonzo udikomba wimale.”

Usulumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga nimo uyo adagudebhile chiza, umukikalile  kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agadumaga uguimala chiza imilimo yakwe, kunguno ya gwandya guitumama bho nduhu uguitila bhukengeji. Uweyi agapandikaga makoye mara hingi ahakaya yakwe, kunguno ya guduma ugubisha ijiliwa, umukikalile  kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agakomba ng’homba ng’wisonzo uduma uguimala, kunguno nuweyi agadumaga uguimala chiza imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ng’homba ya ng’wisonzo udikomba wimale.”

Usulumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuidebha chiza tamu imilimo yabho, na bhandye uguitumama, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Marko 6:40-44.

KISWAHILI: UJI WA KWENYE KISONZO HUWEZI UKAUKOMBA UUMALIZE.

Kisonzo ni chombo ambacho hutengenezwa kwa majani fulani yaitwayo ‘madala.’ Madala hayo, husababisha kuwepo kwa vitundu vidogo vidogo ambavyo vinaweza kuruhusu uji upenye ndani yake. Hivyo basi, mtu anayekomba uji ule hawezi kuumaliza. Ndiyo maana watu husema kwamba, “uji wa kwenye kisonzo huwezi ukaukomba uumalize.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi ambayo haielewi vizuri, katika maisha yake. Mtu huyo, hushindwa kuzimaliza vizuri kazi zake hizo, kwa sababu ya kuanza kuzitekeleza bila ya kuzifanyia utafiti. Yeye huwa anapata matatizo mara nyingi kwenye familia yake, kwa sababu ya kushindwa kuivisha chakula, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekomba uji wa kwenye kisonzo, akashindwa kuumaliza, kwa sababu naye hushindwa kuzimaliza kazi zake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “uji wa kwenye kisonzo huwezi ukaukomba uumalize.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuzielewa vizuri kazi zao kwanza kabla ya kuanza kuzitekeleza, katika maisha yao, ili waweze kupata maendeleo mengi, maishani mwao.

Marko 6:40-44.

porridge uji1

porrdge uji2

porridge uji3

basket uji

ENGLISH: YOU CANNOT GET RID OF BASKET’S PORRIDGE BY FINGER (NEVER CRY OVER SPLIT MILK).

A basket is a container that is made of certain leaves which are called ‘madala.’ This, in turn, results in the formation of small holes that can allow some porridge to enter into it. Thus, the person who takes porridge from it by using a finger cannot finish it. That is why people say, “you cannot get rid of basket’s porridge by finger.”

This proverb is compared to a person who does a job that he/she does not understand it well in life. Such person fails to complete that task properly, because of starting to perform it without researching it well. He/she often faces problems in the family, because of failing to get enough food for running it.

This person is like the one who failed to finish some porridge from the basket by using a finger, because he/she also fails to finish his/her works in life. That is why people say to him/her, “you cannot get rid of basket’s porridge by finger.”

This proverb teaches people on how to understand their works accurately before they start doing them, in their lives, so that they can make a lot of progress in their lives.

Mark 6: 40-44.