1505. IMBULI YAPI ICHOLAGE LIMI LIDINALIB’ILA.

Imbuki ya lusumo lunulo ihoyelile munhu uyo agajimija mbuli yakwe iyo yaliyapi. Umunhu ng’wunuyo agandya guyichola imbuli yakwe bhujiku uduma uguyibhona kunguno ya bhupi bho bhoyo ubho wikolile ni giti ya bhujiku bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki “imbuli yapi icholage limi lidinalib’ila.”

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agakelejaga ugutumama imilimo yakwe mpaka lyabhita ilikanza lya guitumamama imilimo yiniyo, umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga wilendejije bho wigwasha ulu lyashiga ilikanza lya gwandya kutumama milimo guti gulima mpaka nose lyapita kunguno ya bhukeleja bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga ugupandika ijiliwa aha kaya yakwe mpaga ogukoya na nzala kunguno ya wilendeja bho gutumama milimo yakwe bhunubho umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agajimija mbuli yakwe yapi uyichola bhujiku mpaka uduma uguyibhona, kuguno nuweyi agakelejaga ugutumama imilimo yakwe mpaga lyapita ilikanza lya guitumama imilimo yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “imbuli iyapi icholage limi lidinalib’ila.”

Ulusumo lunuyo, lolanga bhanhu higulya ya gub’iza na witegeleja bho gwanguya kuitumama imilimo yabho ulu lyashiga ilikanza lyayo, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi, umukaya jabho.

Mathayo 24:42-44.

Mathayo 5:14-16.

Luka 11:33-36.

KISWAHILI: MBUZI MTAFUTE KABLA JUA HALIJAZAMA.

Methali hii ya Kisukuma hutokana na maisha ya kitamaduni ya kijijini ambapo mifugo, hasa mbuzi, walithaminiwa sana. Mbuzi mweusi ni vigumu kumwona, hasa mwanga wa jua unapofifia. Akipotea lazima atafutwe mapema kabla ya jua kutua wakati bado kuna mwanga wa kutosha. Kusubiri hadi giza liingie hufanya kazi iwe ngumu zaidi, kama si haiwezekani. Ndiyo maana watu humwambia yule aliyepoteza mbuzi hiyo kwamba, “tafuta mbuzi mweusi kabla ya jua kutua.”

Methali hii hulinganishwa na mtu anayechelewesha majukumu au maamuzi muhimu kwa kufikiri kwamba kutakuwa na muda zaidi baadaye. Mtu huyu huchelewesha kufanya maamuzi ya kuteyatekeleza majukumu yake kwa kufanya mambo mengine ambayo si ya lazima sana kwa sababu ya kutokuwa mwangalifu sana maishani mwake. Yeye hushindwa kupata mahitaji ya msingi katika familia yake kwa sababu ya kuchelewa kwake kufanya kazi zake maishani mwake.

Mtu huyu hufanana na yule aliyemtafuta mbuzi mweusi baada ya jua kutua hadi wakashindwa kumuona, kwa sababu naye pia huchelewesha kutimiza majukumu yake hadi anashindwa kupata mafanikio katika family yake, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “mtafute mbuzi mweusi kabla jua halijazama.”

Methali hii huwafundisha watu kuhusu kutenda haraka kwa kutochelewesha mambo muhimu ili waweze kutumia fursa zao wakati bado zinapatikana vya kutosha kuwapatia mafanikio katika maisha yao. Zaidi ya hayo, huwataka watu wawe na hekima ya kutosha kupanga na kusimamia majukumu yao kabla hali hazijazidi kuwa mbaya kwa sababu muda uliopotea hauwezi kupatikana.

Mhubiri 9:10 – “Lolote mkono wako utakalopata kulifanya, lifanye kwa nguvu zako zote…”

Yohana 9:4 – “Lazima tufanye kazi zake Yeye aliyenituma maadamu ni mchana; usiku unakuja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.”

Mithali 6:6–8 – Mfano wa chungu akijiandaa mapema

Wagalatia 6:9 – Kutiwa moyo kutochoka kutenda mema kwa wakati unaofaa.

Mathayo 24:42-44.

Mathayo 5:14-16.

Luka 11:33-36.

Maandiko haya, kama methali, yanasisitiza kutenda kwa wakati, bidii, na umuhimu wa kutoahirisha kile kinachopaswa kufanywa.

ENGLISH: FIND A BLACK GOAT BEFORE THE SUN SETS.

This Sukuma proverb comes from traditional village life where livestock, especially goats, were highly valued. A black goat is difficult to see, particularly as daylight fades. If it strays or gets lost, it must be searched for early before sunset while there is still enough light. Waiting until darkness falls makes the task much harder, if not impossible. Thus, the proverb arose as a practical warning about urgency and timing saying “find a black goat before the sun sets.”

This proverb is compared to a person who delays important responsibilities or decisions by thinking that there will always be more time later. This person delays doing his responsibilities by doing other things which are not so necessary because of not being so carefully in his life. He fails to get basic needs at his family because of delaying to do his works in his life.

This person resembles the one who looked for a black goat after sun setting until it was already too late to see it, as conditions had become unfavorable. In the same way, he also delays fulfilling his responsibilities until it is too late in his life. That is why people tell him “find a black goat before the sun sets.”

This proverb teaches people about acting promptly by not delaying important matters so that they can use their opportunities while they are still available enough to be successfully in their lives. Besides, it calls them to be wise enough to plan and manage responsibilities before situations worsen because the time lost cannot be recovered.

Ecclesiastes 9:10 – “Whatever your hand finds to do, do it with all your might…”

John 9:4 – “We must work the works of Him who sent Me while it is day; the night is coming when no one can work.”

Proverbs 6:6–8 – The example of the ant preparing in advance.

Galatians 6:9 – Encouragement not to grow weary in doing good at the right time.

Matthew 24:42-44.

Matthew 5:14-16.

Luke 11:33-36.

These scriptures, like the proverb, emphasize acting in time, diligence, and the importance of not postponing what must be done.

One comment

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.