Ilipilinga lili lilugulu ilo lilina lukumbi lo gwingila nulu ndimu nulu munhu umugati yalyo. Umunhu uyo wingila moyi adutulwa nulu mbula nulu adubishiwa limi kunguno ilyoyi ligankigijaga chiza. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “ali ng’wipilinga/mumahalo.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali bhambilija umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adiko gukoya na makoye gosegose kunguno agwambilijiwa chiza na bhambilija bhakwe bhenabho. Uweyi agikalaga na bhuyegi aha kaya yakwe kunguno ya kugamala wangu amakoye ulu gampadika, umuwikaji bhokwe bhanubho.
Umunhu ng’unuyo, agikolaga nuyo ali ng’wipilinga uyo agibhisa mbula na limi, kunguno nuweyi alina bhambilija abho bhagagamalaga wangu amakoye gakwe umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhangang’wilaga giki, “ali ng’wipilinga/mulihalo.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kuchola wambilijiwa kufumila kuli Mulungu uyo adulile gugamala wangu amakaye gabho, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi umu kaya jabho, shigu jose.
Mathayo 7:7-8.
Mathayo 11:28-30.
Yohana 6:67-68.
KISWAHILI: YUKO KWENYE JABARI/NGOME YA MAWE.
Jabari ni jiwe lile ambalo lina mlango wa kuingia ndani yake ambamo hata wanyama au mtu huweza kuingia ili kujificha. Mtu akiingia kwenye pango hilo hatanyeshewa mvua wala kupigwa jua, kwa sababu Jabari hilo humkinga vizuri. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “yuko kwenye Jabari/ngome ya mawe.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana watu wa kumsaidia katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hahangaishwi na matatizo yoyote kwa sababu ya uwepo wa watu hao ambao humsaidia katika kuyatatua matatizo yake kila yanapojitokeza. Yeye huishi kwa furaha kwenye familia yake hiyo kwa sababu ya kuyamaliza haraka matatizo yake kila yanapojitokeza, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule aliyekuwemo ndani ya Jabari lililomkinga kunyeshewa mvua na kupigwa jua, kwa sababu naye ana watu wanaomsaidia katika kuyatatua matatizo yake kila yanapojitokeza, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwambia, “yuko kwenye Jabari/ngome ya mawe.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutafuta msaada kutoka kwa Mungu ambaye aweza kuyamaliza matatizo yao kwa haraka, ili waweze kuishi kwa furaha, katika familia zao, siku zote.
Mathayo 7:7-8.
Mathayo 11:28-30.
Yohana 6:67-68.