1039. KALAGU – KIZE. AGUNSOLAGA ALU GUNSHOSHA NDUHU – JIGILA.

Ikalagu yiniyo, yihoyelile jigila. Ilijigila ili numba ya ng’wa munhu uyo ojikilwa moyi. Inumba yiniyo ili ya bhulunga kele kunguno ulu munhu ucha utulwa mjigila na ufukilwa ibhizaga nduhu igiki agufuma. Ijigila jinijo jidalanshosha umunhu uyo ojikagwa moyi ng’wunuyo. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “agunsolaga alu gunshosha nduhu.”

Ikalagu yiniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasolaga jikolo ya bhiye ogajikalana bho nduhu ugujishosha mpaga winga kuwelelo. Umunhu ng’wunuyo, agiyibhaga ugubhitila ya wiza abhiye iya gubhashokeja ijikola jabho jinijo ulu bhangunana, kunguno ya gwiganika giki adalacha umukikalile kakwe. Uweyi agabhapambulaga abhiye ugungunana hangi ijikolo jabho ulu obhalanda kunguno ya bhujidashosha bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni jigila ijo jidabhashoshaga abho bhajikilwa moyi, kunguno nuweyi adajishoshaga ijikolo ja bhiye ijo agalandaga umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “agunsolaga alu gunshosha nduhu.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwikala chiza na bhanhu bho gubhitila mihayo ya wiza iya gubhashokesha ijikolo jabho chiza, kugiki bhadule gwinga kuwelelo chiza.

Mwanzo 3:19.

Ayubu 1:21.

Mathayo 10:28.

Ufunuo 14:13.

Wafilipi 1:21.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

ANAMCHUKUA LAKINI KUMRUDISHA HAKUNA – KABURI.

Kitendawili hicho, chaongelea kaburi. Kaburi hilo ni nyumba ya mtu aliyezikwa humo. Nyumba hiyo ni ya milele kwa sababu mtu akifa akawekwa kaburini na kufukiwa huwa harudi.

Kaburi hilo halimrudishi mtu huyo aliyezikwa ndani yake kwa sababu lenyewe huchukuwa moja kwa moja. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “anamchukua lakini kumrudisha hakuna – kaburi.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huchukua vitu vya wenzake na kukaa navyo bila kuvirudisha mpaka kufa kwake. Mtu huyo, hujisahau kuwatendea mema wenzake wanaomwamini kwa kumpatia vitu vyao, kwa kuwarudishia vitu vyao hivyo, kwa sababu ya kufikiri kwamba hatakufa katika maisha yake. Yeye huwaogopesha wenzake kumsaidia vitu vyao tena kwa sababu ya kutokurudisha kwake vitu hivyo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na kaburi ambalo halimrudishi mtu yule aliyezikwa humo, kwa sababu naye huwa hurudishi vitu alivyoazima kutoka kwa wenzake, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “anamchukua lakini kumrudisha hakuna – kaburi.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kuwatendea wenzao mema kwa kuwarudishia vitu vyao vizuri, ili waweze kuaga dunia vizuri.

Mwanzo 3:19.

Ayubu 1:21.

Mathayo 10:28.

Ufunuo 14:13.

Wafilipi 1:21.

grave-1412362__480

 

 

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.