810. NYANGO GUMO GUDAGINYAGA NVA.

Yalihoyi nva iyo yaliyasugwa ahakaya ya ng’wa munhu nhebhe. Inva yiniyo, yakamilagwa bhuli lushigu, aliyo yalidigutaga, kunguno yingaga ahakaya yiniyo, yagacholeleja jiliwa mumakaya gangi.

Iyoyi yajaga yujilya ijiliwa ijo bhajiponyaga kihamo na maguha ayo gaponyiyagwa, umumakaya genayo, mpaga iguta na yashoka aha kaya iyo ikalaga. Aho bhayibhona abha hakaya yiniyo igwitaga chene bhagayomba giki, “nyango gumo gudaginyaga nva.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo ali na nzala uyo agajaga gujuchola jiliwa mpaga ojipandika ijaguimala inzala yiniyo, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajaga gujusuma bhuli kwene uko jiligelela ijiliwa jinijo, kugiki adule gujipandika ja gudula kumpiga inzala yiniyo. Uweyi agadulaga iguisumila ikaya yakwe mpaga yapila, kunguno ya wigulambija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni nva iyo yajaga yulya jiliwa mumakaya mpaga iguta, kunguno nuweyi, agaisumilaga ikaya yakwe bho guicholela jiliwa mpaka oipija nzala, umukikalile kakwe. Hunagwene agabhawilaga abhanhu giki, “nyango gumo gudaginyaga nva.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwigulambija guchobhalela jiliwa ja gubhapija nzala abhanhu bhabho, umukikalile kabho, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mathayo 13:45-46.

KISWAHILI: MLANGO MMOJA HAUNENEPESHI MBWA.

Alikuwepo mbwa mmoja aliyekuwa amefugwa kwenye familia fulani. Mbwa huyo, alilishwa chakula kila siku, lakini alikuwa hashibi kwa sababu alikuwa akiondoka kwenye familia hiyo, na kwenda kutafuta chakula kwenye familia zingine.

Yeye aliendelea kutafuta mifupa na chakula kilichotupwa na kula, kwenye familia mbalimbali, mpaka aliposhiba ndipo alirudi nyumbani. Walipoona hivyo, wana familia hao, walisema kwamba, “mlango mmoja haunenepeshi mbwa.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hupata tatizo la njaa na kuanza kuzunguka akitafuta chakula mpaka anakipata chatosha kuimaliza hiyo njaa, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa anaenda kuhemea kila sehemu anakosikia kwamba, kuna chakula ili aweze kujipatia chakula cha kuwatosha watu wake. Yeye huweza kuitafutia chakula familia yake mpaka anakipata cha kutosha kuwalisha wanafamilia wote, kwa sababu ya bidii yake ya kuwasaidia wake hao, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na mbwa aliyeenda kula chakula kwenye familia za watu, kwa sababu naye huitafutia chakula familia yake mpaka anakipata cha kutosha kuimaliza njaa hiyo, katika maisha yake. Ndiyo maana yeye humwaambia watu kwamba, “mlango mmoja haunenepeshi mbwa.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kuwatafutia chakula cha kutosha kuwaponyesha njaa watu wao, katika maisha yao, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mathayo 13:45-46.

dog-1

dog and door

dog-

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.