127. MUNHU UYOAGAGULA BHASKELI

Collected by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey  (African Proverbs, Sayings and Stories)

Olihoi munhu umo uyoagasumba lugendo lo gujugula bhasikeli ng’widuka lya Nyanga. Aho oshiga ukunuko agagula Bhasikeli. Hanuma ya henaho agagula na ginhu jinghi; Isandiko, miguto ya gwikumba idatu, supana ibhili ja ligogoteni lyakwe, supana ya gwegeleja, na supana nhale ya jijerumani.

Aho omala ugugula iginhi jose ijo, agagaiwa ubhusafiri ubhogushoka ikaya. Kulwa nguno ibhasi yaliyabhachala bhatuji bha mpila ku nkoa gungi.

Agiyangula gushoka kaya bho gutumila bhasikeli yakwe imhya. Makanza ga sa kenda ya limi agandya lugendo. Aho yashika saa ikumi na ibhili ya mhindi, agabhona giki niadadujije ugushika ikaya.

Agiyangula guja gujulala kulindugu okwe uyo uli bhukule bho kilomita makumi adatu. Gashinaga aho adinashiga ukulindugu okwe, agavamilwa na masambo adatu ayo galinajilanga ja aina nyingi. Amasambo gagantula noi na guntaja ibhasikeli ni lisandiko.

 Bahati ya wiza agafyaduka aho alina chupi na sokisi umumagulu, upela nhambo mpaga kuchalo jilebhe ijo agashiga koyi mu saa sita ya bhujiku, ugota moto uyo gulihanze ni numba.

Agiyangula gwingila mu jibhanda ijo jali ng’waje, aliyo adadulile ugulala kulwa nguno ya gwiigwa umili gulisata kulwa gutulwa na malonda ayogagenhelejiwa na majambazi.

Agakeyula wigashije na gwisendamija handugu. Oganoga wigwa jilaka ja bhanhu abhobhahayaga nabho gwiza ahenaho njini. Ahoobhasula, agabhabhona bhalina bhasikeli ni isandiko ijo jali sabho jakwe ijo gansojaga amasambo gene.

  Bhagapiga hodi mu imo ya numba jinijo. Lidakulile ikanza saabho omasambo gene ugalugulila unyango na gufuma hanze. Usaabho agabhabhuja, “Ee, ng’wapandika kiyi na kiyi?”

 Abhana bhagashosha, “Dapandika bhasikeli iyi mhya na ni sandiko ili.” “Ee, umugati ya lisandiko jilihoi kiyi?” Agabhuja usaabho. “Dudina likundula dutali,” abhana bhunshokeja usaabho.  Ibhasikeli na lisandiko linilo bhagajituula mu numba iyo yaliyagubhisila isabho jabho na gugulugala unyango bholigufuri.

Umunhu ng’wunuyo agadegeleka pye imihayo. Gung’wizila miganiko ga kuja gujulomba wambilijiwa kukaya ya ng’wa bhalozi. Aho oshiga akaya imo, bhagampinihalila, bhung’winha ng’wenda, surubhale na ngwanda na bhung’olekeja ukulibhalozi.

Aho oshika ahakaya ya ng’wa bhalozi, aganomela yose iyo yaliyampandika. Ubhalozi agayomba, “dujagi kujituo ja polisi, dugafunye mbhola.” Abhapolisi bhagawilwa nu ojikolo giki agatajiwa bhasikeli mhya ni sandiko. Hangi bhulomela iginhu jose ijobhajituula umugati ya lisandiko linilo. Agolekeja ulufungulo ni lisiti ya gugulila isabho jinijo.

Abhapolisi bhagasola loli na guja gujivamila ikaya iniyo. Aho bhashika ukunuko bhagagadima amasambo gene, saabho ni sabho jinijo ijawibhi. Bhagasombwa na guchalwa kujituo ja polisi gujandikisha na gulugulilwa bhushidakiwa. Aho bhashishiwa ahaibhanza, bhagalamulwa jifungo ja miaka itano mujela na milimo midimu.

KISWAHILI: MTU ALIYENUNUA BAISKELI

Kulikuwa na mtu mmoja aliyefunga safari kwenda kununua baiskeli katika duka la Nyanga. Alipofika huko, alinunua baiskeli. Halafu akanunua vitu vingine; Sanduku, shuka tatu, spana mbili za mkokoteni wake, spana ya sogeza, spana kubwa kutoka Ujerumani.

Baada ya kumaliza kununua vitu hivyo vyote, alikosa usafiri wa kurudi nao nyumbani. Maana basi liliwapeleka wachezaji wa mpira katika mkoa mwingine. Akaamua kurudi nyumbani kwa kutumia baiskeli yake mpya.

Mnamo saa tisa alasiri, alianza safari. Ilipofika saa kumi na mbili ya jioni, aliona kuwa asingefaulu kufika nyumbani. Akaamua kwenda kulala kwa ndugu yake umbali wa kilometa thelathini.

Kumbe kabla hajafika nyumbani kwa ndugu yake, alivamiwa na majambazi watatu wakiwa na siraha mbalimbali. Majambazi walimpiga sana na kumnyang’anya baiskeli na sanduku.

Bahati nzuri alifyatuka akiwa na chupi na soksi miguuni, akakimbia mbio hadi kijiji fulani ambako alifika huko yapata saa sita usiku, akaota moto uliokuwa ukiwaka nje ya nyumba.

Aliamua kuingia kwenye kibanda kilichokuwa wazi, lakini hakuweza kulala kwa sababu ya maumivu ya kipigo na majeraha yaliyo yapata toka kwa majambazi.

Akakesha huku ameketi na kuegemea ukuta. Baadaye alisikia sauti za watu waliotarajia pia kuja hapo kijijini. Alipowachungulia, akawaona wana baiskeli na sanduku ambavyo ni mali ile ile waliyomnyang’anya majambazi.

Walibisha hodi kwenye moja ya nyumba zile. Mara baba yao hao majambazi alifungua mlango na kutoka nje. Baba akawauliza, “Je, mmepata nini na nini?” Watoto wakajibu, “Tumepata baiskeli hii mpya na sanduku hili.” “Je, ndani ya sanduku  kuna nini?” baba alidadisi. “Hatujalifungua bado,” watoto walimjibu baba yao. Baiskeli na lile sanduku wakahifadhi katika  nyumba maalumu ya kuficha mali zao na kuufunga mlango kwa kufuri.

Yule mtu alisikiliza mazungumzo yote. Yakamjia mawazo ya kwenda kuomba msaada nyumbani  kwa balozi. Alipofika kwenye nyumba moja, walimhurumia, wakampa nguo, suruali na shati na wakamwonesha nyumbani  kwa balozi. Alipofika nyumbani kwa balozi, alimweleza yote yaliyompata. Balozi akasema, “Twende kituo cha polisi, tukatoe taarifa.” Polisi walielezwa na mwenye mali kuwa alinyang’anywa baiskeli mpya na sanduku. Pia alifafanua vitu vyote alivyoviweka ndani ya sanduku hilo. Akaonesha funguo na risiti ya kununulia mali zile.

Polisi walichukua gari na kwenda kuuvamia mji ule. Walipofika huko wakawakamata wale majambazi, baba na zile mali za wizi. Walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kuandikisha na kufunguliwa mashitaka. Baadaye walipofikishwa mahakamani, walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kazi ngumu.

bike

police

ENGLISH: THE MAN WHO BOUGHT A BICYCLE

There was a man who went on a trip to buy a bicycle in Nyanga. When he got there, he bought a bicycle. Then he bought some other things including a box, three bed sheets, two spanners for his cart, adjustable spanner and a vice from Germany.

After finishing buying all these items, he missed the transport back home. The car that was depended on had sent football players to another region. He decided to go home using his new bike.

At three o’clock, he began his journey. When it was six o’clock in the evening, he realized that he could not get home. He decided to go to sleep to his relatives about thirty kilometers away.

Before he came to his relatives’ house, he was attacked by three robbers who had various weapons. The robbers beat him up and took from him the bike and the box.

Fortunately, he escaped them in his the underwear and socks on his feet. He ran to a village where he arrived at about twelve o’clock midnight. He started warming himself at the fire that had been left burning outside the house.

He decided to go into an open hut. But he could not sleep because of the pain sustained from the blows and injuries caused by those robbers.

He spent the night sitting and leaning against the wall of that hut he had encroached. Later, he heard the voices the people who were also   coming to that village. When he looked at them, he saw the people with the bicycle and the box. They were the same properties they had robbed him.

They knocked at one of those houses. Their father opened the door and they entered. Their father asked, “What have you got today?” They replied, “We have found this new bike and this box.” “What is in the box?”, their father asked.They said, “We haven’t opened it yet. The bicycle and the box were kept in a special house. To hide their properties they shut the door with a lock.

The man listened to all the conversations very carefully. He got the idea of ​​ asking for help from the ten-cell leader. When the man came to one house, they felt sorry for him and  gave him clothes, pants and a shirt and showed him the home of the the ten-cell leader. When he came to the the home of the ten-cell leader, he told him all that had happened to him. The ten-cell leader said, “Let us go to the police station and report the matter.” The police were told.The property owner said that he was robbed a new bike and a box. He also mentioned all the things he had put in the box. He showed the keys and the receipt for the purchase.

The police took the car and went to arrest the robbers. When they arrived, they arrested the robbers, the father and the property of theft. They were taken to the police station to register and later they were prosecuted. Finally, when they were brought to court, they were sentenced five years in prison and hard work.

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.