37. Mnangala

Collected by: Don Sybertz, Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs,Sayings and stories)

Namhala wali na bhana bhadatu. Namhala ng’wenuyo wali ni bhonde lya maguwa. Akayubhawila kujugalinda abhana bhakwe kunguno galiwagwa shinu. Usabho agabhawila giki, ulu bhalilinda bhiya ukulya amagua. Bhagita giko shiku ningi, nduhu ukulya amagua.

Lushiku na lushiku, ung’waniki uumo ubhihindanya abhiye ukabhinza wandya kulya. Aha wamala ukulya ugabhisa amafefa mumafa. Aha washoka, bhumuja abhiye wali waja he? Uyomba inakagalola amashinu uko magua ulu kadulyaga.

Ntondo yaho unamhala uja ukwibhonde lyakwe ukasanga amagua gabhinzile. Ubhabhuja abhalindi, “Nani walile amagua gane?” Bhalindi bhuyomba, “lmalulu” ubhawiia, “Yombagi ya ng’hana, nalihaya kusumba.” Aliyo bhatayombile uyo walile.

Namhala ushoka kaya, ukiza ni sumbi lya jisukuma lya nzule. Wiza ulitula ung’wibhonde, bhuyigasha umo umo ahi sumbi. Wandya kwimba, Nani wayilya mitumbi tumbi Nene nailile mitumbi tumbi. Ulu wamala ukwimba wabhuka.

Nu wakabhili, wigasha wandya ukwimba nigiko umu wimbilaga ung’wiye. Nu wa kadatu wigasha nang’hwe, aho wandya ukwimba, ili sumbi lyuyulibhila hasi, ulwalimalija ukwimba ulibhila hasi, ulibhila pye nilisumbi, lisi lilugala.

Namhala umana lulu uyo walyaga amagua gakwe. Ku mhindi abhaniki bhiyie abhabhili aha bhaja ikaya ukabhabhuja umayu wabho, “Ung’wiching’wi ali hali?” Nabho bhuyomba, “Ima lulu uko wajaga, twangayiwagwa.”

Aha gwashila ung’waka gwenuyo umujidiku unamhala ulima ngunda bihi nuko kwibhonde. Kuyubhita ka Jiji kajile ukwibhonde lyakwe. Kangisha, “Madilo bhabha” wazunya, “Madilo Jiji.” Bhigisha bhamala kang’wila giki, “Nabhite kunu nano” wakabhuja, “Ujile he? “Kuyomba, najile kunu duhu.” Kajiji kenako guja.

Gashi akanoni kenako gajaga kagadaha minzi, kandya kumumba ung`waniki aho walibhilila. Kagashada shiku idatu kagubhitaga. Nose unamhala ukabhuja, “Gwa ukubhitaga ukujaga heshi igete Jiji?” kuhaya, “Nagujaga kunu duhu.” Bhulekana, kukandya kumumba.

Aha kamala kuchimika loya logo aha ntwe gati ya bhulolo. Ng’waniki nsumba no. kajiji kung’wila ung`waniki ng`wenuyo “Nakutole lulu.” Ng’waniki uzunya. Kubhiza kansola kunchala kung’wago.

Aho kaganshisha ikaya kubokelwa na bhabyaji bhago. Bhigasha nu ng’waniki ng`wenuyo. Kikalile gakwe kagabhiza kawiza no. Kungulila myenda misoga, bhudodi wa mumagulu, jilatu jisoga.

Bhagigasha bhumala ng’waka kushila. Aha bhamala ng’waka ng’waniki ung’wila ungoshi Jiji, bhakagishe kung’wawe wa ng’waniki. Jiji uzunya bhuja ukujugisha ukubhukwiye.

Aha bhashika ukubhukwiye wa Jiji bhusumbilwa. Ngikulu utogwa no, ugumona ng’wana wakwe. Wina makanza malihu atumonaga. Aha bhigasha shiku ningi Jiji agankomiga unke bhashoke kaya.

Ng’waniki ulemejiwa nu Nina. Aho walemejiwa, nang’hwe ung’wila jiji giki, “Jaga duhu ubhebhe, nene natujaga.” Aha wawilwa giko Jiji wifukula uja, aha wakashika uko ng’wawe, ubhujiwa nu Nina, “Wakaneka he ung’winga wane? Jiji uyomba walemile atizaga ukunu.”

Aho wawilwa chene, ngikulu usatwa uhaya, “Jilaga imyenda yako ugantaje.” Ntondo diyu wipuna ujiji ajile, ukansanga unke alisha. Jiji wapelanaga ugagwa halugutu duhu wandya kwimba.

Mnangala yii! Mnangala,
Ninhe myenda yane mnangala,
Naje kaya yise mnangala

Ng’waniki ubhuka witunganya pye imyenda ifulushi lidi gete, umponegeja uyomba, “Gaya amamyenda gako.” Jiji ubhucha ilifulushi lya myenda uja akugwaga gwaga lyamunaga. Ntondo hangi unyamuka ujiji ugwa hangi aha lugutu wandya kwimba;

Mnangala yii! Munangala,
Ninhe bhudodi wane munangala.

Ng’waniki uyomba, “Mabhudodi duhu gayo.”
Jiji ubhucha bhudodi wakwe ajile kaya. Ntondo hangi ujiji ubhuka izile, ukashika naha akashigilaga wandya kwimba hangi;

Munangala yii! Munangala,
Ninhe loya lone munangala,
Naje kaya yise munangala.

Ngikulu wandya kumuja ng’wana wakwe giki, “Uloya hangi lulihe!” ng’waniki wihimangija wandya gusha duhu lulu bhufu. Jiji akishogela ukwimba hangi nduhu atinhagwa uloya lokwe. Jiji nose upelana gete wakalala Jiji ugankwala ung’waniki hagati ya ntwe. Jiji uludubula uloya lokwe. Ng’waniki usesaguka.

Kiswahili: Mnangala

Mzee alikuwa na watoto watatu. Mzee huyo pia alikuwa na shamba la miwa. Akawaambia watoto wake kwenda kulinda miwa iliyokuwa inaliwa na wadudu. Baba yao aliwaambia hivi, wakiwa wanalinda wasile miwa. Walifanya hivyo kwa muda wa siku nyingi, bila kula miwa.

Siku moja msichana mmoja aliwazunguka akaenda kuvunja miwa akaanza kula. Alipomaliza kula aliyafika maganda ya miwa kwenye majani. Aliporudi, walimuuliza wenzake “ulikuwa umeenda wapi?” Alisema, “nilienda kuyaangalia madudu kwenye miwa kama hayali.”

Kesho yake mzee alienda kwenye bustani yake akakuta miwa imevunjwa. Akawauliza walinzi, “Nani alikuja kuvunja miwa yangu.? Walinzi walisema, “Hatujui.” Akawaambia, “Semeni ya ukweli, nataka kutega dawa.” Lakini hawakusema yule aliyekula.

Mzee alirudi nyumbani, akaja na kiti cha kisukuma cha Nzule. Akaja akakiweka kwenye bustani, wakawa wanakaa mmoja mmoja kwenye kiti hicho. Akaanza kuimba, “Nani alikula pingili pingili Mimi nilikula pingili pingili.” Akimaliza kuimba anasimama.

Na wapili alikaa akaanza kuimba hivyo alivyoimba mwenzake. Na watatu alikaa naye, alipoanza kuimba kile kiti kikaanza kudidimia aridhini, alipomaliza kuimba alididimia ardhini, alididimia pamoja na kiti, ardhi ilijifunga.

Basi mzee akajua yule aliyekula miwa yake. Jioni walipoenda wale wasichana wenzake wawili nyumbani, mama yao akawauliza, “Mwenzenu yuko wapi?” Nao walisema, “Hatujui alikoenda, tumemkosa.”

Ulipoisha mwaka huo, mzee alilima shamba karibu na kwenye bustani yake. Kakawa kanapita ka Jiji (Jina la ndege) kanaenda kwenye bustani yake. Kanamsalimu, “Habari za jioni baba” anakubali, “Habari za jioni Jiji.”  Wanamaliza kusalimiana, kanamwambia hivi, “Nipite huku kwenye unafuu” anauliza, “Unaenda wapi?’ Kanasema, “naenda huku tu.” Kajiji hako kakaenda.

Kumbe kandege hako kalikuwa kanaenda kumuumba msichana pale alipodidimia. Kalitumia siku chache kakiwa kanapita. Mwishowe mzee akauliza, “Kila siku unapita ukienda wapi kweli Jiji? Kakasema, “Naenda huku tu. Wakaachana, kakaenda kuanza kumuumba.

Kalipomaliza kuchomeka unyoya wa kenyewe kwenye utosi wa kichwa cha udongo. Msichana mzuri mno akatokea. Kajiji kalimwambia msichana huyo “nikuoe basi.” Msichana alikubali. Kakawa kamemuoa kakampeleka nyumbani kaliko.

 Kalimfikisha nyumbani kakapokelewa na wazazi wa kenyewe. Wakakaa na yule msichana. Kuishi kwake kulikuwa kuzuri mno. Kakamnunulia nguo nzuri, ya mapambo na mabangili mazuri ya miguuni, na viatu vizuri.

Walikaa wakamaliza mwaka. Walipomaliza mwaka msichana alimwambia mumewe Jiji, wakawasalimie kwa wazazi wake msichana, Jiji alikubali, wakaenda kusalimia, kwa wakwe zake.

Walipofika kwa wakwe zake Jiji, walipokelewa. Mama mkwe alifurahi mno, kumuona mwanae. Alikuwa na muda mrefu bila kumuuona. Walipokaa siku nyingi Jiji alimwambia mke wake, warudi nyumbani.

Msichana alikatazwa na mama yake. Alikatazwa, naye akamwambia Jiji hivi, “Nenda tu wewe, mimi siendi.” Alipoambiwa hivyo, jiji alizila akaenda. Alipofika nyumbani kwao, aliulizwa na mama yake, “Umeenda kumuacha wapi mkamwana wangu” Jiji alisema, “Amekataa kurudi huku.”

Alipoambiwa hivyo, mama yake, aliumia akasema,  “Fuata nguo zako ukamnyang’anye.” Kesho yake asubuhi, Jiji alijihimu akaenda, akamkuta mke wake anasaga. Jiji akiwa amekasilika alienda kuanguka zizini tu, akaanza kuimba.

Mnangala Yii! Mnangala,

Nipe nguo zangu Mnangala,

Nienda nyumbani kwetu Mnangala.

Msichana akasimama akazifunga nguo zote kwenye furushi kubwa kabisa, akamtupia akisema, “Haya manguo yako.” Jiji alibeba lile furushi la nguo akaenda huku akianguka anguka na furushi likiwa limemzidi. Kesho yake tena Jili alirudi akaanguka kwenye zizi akaanza kuimba:

Mnangala yii! Mnangala,

Nipe udodi wangu Mnangala.

Msichana akasema, “Mabudodi (bangili za shanga) tu hayo hapo.” Jiji akabeba budodi wake akaenda nyumbani. Kesho yake tena Jiji alianza safari akirudi, akafika pale anapofikia akaanza kuimba tena:

Mnangala yii! Mnangala,

Nipe unyoya wangu mnangala,

Niende nyumbani kwetu Mnangala.

Mama yake akaanza kuuliza mtoto wake hivi, “Unyoya tena uko wapi!” Msichana, akajifanya hasikii, akaanza kusaga unga tu. Jiji alirudia kuimba lakini hapana, hakupewa unyoya wake. Mwishowe Jiji alikasilika akaruka na kwenda kumkwaluza msichana utosini kwa kucha zake. Jiji aliung’oa unyoya wake kwa kucha zake. Msichana akasambaa.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.