21. Sabho Ja Musi Nani Ajitogilwe Kukila Ho- Ngosha Nulu Nkima?

Collected by: Don Sybertz,   Scanned by: Cephas Yao Agbemenu

With special thanks to Rev Joe Healey (African proverbs, Sayings and stories)

Banhu bhabhili bhakihalalija nani atogilwe sabho, bhangi bhuhaya giki, “Bhagosha tujitogilwe.” Bhangi bhuhaya bha mayu bhajitogilwe kukila ho.”

Mu halali yabho bhung’witana ngosha umo, ntumami wabho bhung’wila, twagayiwa maninga ga nkima ga kusanja mu bhugota. (nulu lubhango nulu ki) giko bhung`wila umulage nke wako, tukwinhe shikolo.”

Ngosha uzunya nahene. Aho washika kukaya usumbhilwa na nke, ugishiwa chiza chiza, winhwa minzi ga koga, uzugilwa na shiliwa shawiza wiza.

Aho wamala kulya wandya kwidedeng’hanya, “Nke wane wanitila chiza, namulage, yaya no, ulu kunipeja mu milimo bhanipejage.” Huna lulu ubhuka ushika hangi kumilimo yake. Ushika ung’wila ngonzo wakwe. “Bhabha naduma kumulaga nke wane bhuhaya. Bhasi ati na mhayo ya shilaga, bhubhona kuli ngosha tatindwa.

Tulole kwipande lya bhakima. Bhung’witana nkima aliyela yela haho, bhung’wila, “Twagayiwa mininga ga ngosha ga kusanja mu bhugota.” Nu bhebhe mayu ulibhona kinahe udugije kumulaga ngoshi wako. Utenhele mininga tukwinhe shikolo.

Ubhuja giki iki igosha nakulibhulaga kinahe? Tukukwinha mawalwa makoji, ulu ugang`wa ulu ukumona gankola. Unsinza na kunsinza.” Bhasi, nkima uzunya winhwa walwa wenubho. Untwalila ngoshi, aho wabhung’wa bhunkola ng`hana, usola lushu ubhuta ntwe. Bhasi, ukingilija amininga huna ugabhucha ubhatwalila mininga nu ntwe. Kihamo bhagosha nabho bhung’wanukula. Wabeja mayu huna lulu uwilwa nzugu wigashe kunu mayu, tukwenhele shikolo shako. Ulekwa kuchumba, bhanikili bhutula simu ku polisi.

Kiswahili: Mali Za Duniani Nani Anazipenda Zaidi- Mwanaume Au Mwanamke?

Watu wawili walibishana juu ya nani anapenda mali zaidi kati ya wanaume na wanawake. Wengine walisema kwamba, “Wanaume wanapenda mali zaidi kuliko wanawake. Lakini wengine walisema, kuwa, “Wanawake wanapenda mali kuliko wanaume.”

Katika mabishano hayo, walimwita mwanamume mmoja, mfanyakazi wao, wakamwambia, “tumekosa damu ya mwanamke ya kuchanganya kwenye dawa.” (Au Baraka au nini), hivyo wakamwambia, amuue mke wake, wampe mali au kitu.

Mwanamume huyo alikubali, “sawa.” Alipofika nyumbani, alipokelewa na mke wake, akasalimiwa vizuri, akapewa maji ya kuoga, akapikiwa chakula kizuri.

Alipomaliza kula, alianza kufikiri, “Mke wangu amenifanyia vizuri, nimuue, hapana kabisa, kama nikunifukuza kazini wanifukuze.” Ndipo akafika tena kwenye kazi yake. Akafika na kumwambia mwajiri wake. “Baba nimeshindwa kumuua mke wangu,” wakasema, basi “haina neno yameisha.” Wakaona kwamba, kwa mwanamume wameshindwa.

Tuangalie kwa upande wa akina mama. Wakamwita mwanamke aliyekuwa akitembea tembea hapo, wakamwambia, “Tumekosa damu ya mwamume ya kuchanganya kwenye dawa. Na wewe mama unaonaje unaweza kumuua mume wako, utuletee damu tukupe mali au kitu?”

Akauliza kwamba, “kwa vile ni mwanamume nitamuuaje?” Wakamwambia, “tutakupa pombe kali, akinywa na kama ukimuona amelewa. Umchinje.” Basi yule mwanamke akakubali, akapewa pombe hiyo.

Alimpelekea mmewe, alipokung’wa ikamlewesha kweli, alichukua kisu akamkata kichwa. Basi, alikinga damu ndipo akabeba akawapelekea damu na kichwa pamoja, na wanaume nao wakampokea.

Wakasema, “asante mama wakamwambia njoo ukae huku mama, tukuletee mali yako.” Akaachwa chumbani, wenyewe wakapiga simu ya kuita polisi.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.