Imbuki ya kahayile kenako iholelile hela ijo alinajo munhu nhebhe. Ihela jinijo akikalaga najo umunhu ng’wunuyo muli likanza liguhi duhu kunguno jigashilaga ulu wandya ugujitumamile bho gujigulile majikolo malebhe. Hunagwene umunhu ng’wunuyo, agayombaga giki, “nalinajo aliyo jijile.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajitumamilaga chiza ijikolo jakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agajitumamilaga isabho jakwe bho gudebha igiki jilashila ulu lyushiga ilikanza kunguno ya kubhiza ni lange lya wiza, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadujaga uguibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya lilange lyakwe ilya weza linilo, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo oliadebhile igiki ihela jakwe jigushila ulu wandya ugujitumamila, kunguno nuweyi agajitumamilaga chiza isabho jakwe haho jitali ugushila umukaya yakwe. Hunagwene agayombaga giki, “nalinajo aliyo jijile.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujitumamila chiza isabho jabho haho jitali ugushila, kugiki bhadule gujibheja chiza ikaya jabho, umubhulamu bhobho bhunubho.
Maombolezo 4:18.
Mathayo 13:49.
KISHAHILI: NINAZO LAKINI ZINAENDA.
Chanzo cha msemo huo huongelea pesa alizonazo mtu fulani. Pesa hizo huwa nazo mtu huyo kwa muda mfupi tu kwa sababu zenyewe huisha akianza kuzitumia kwa kuzinunulia vitu mbalimbali. Ndiyo maana mtu huyo husema kwamba, “ninazo lakini zinaenda.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huvitumia vizuri vitu vyake katika maisha yake. Mtu huyo, huzitumia mali zake kwa kuelewa kuwa huwa zinaisha ukifika muda kwa sababu ya malezi yake mema yamwezeshayo kuelewa kula kila kitu kina mwisho wake. Yeye hufanikiwa kuiendeleza vizuri familia yake kwa sababu ya malezi yake hayo mema ya kuzitumia vizuri mali zake, maishani mwake.
Mtu huyo hufanana na yule aliyeelewa kwamba pesa zake zitaisha akianza kuzitumia, kwa sababu naye huzitumia vizuri mali zake kabla hazijaisha. Ndiyo maana husema kwamba, “ninazo lakini zinaenda.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzitumia vizuri mali zao kabla hazijaisha, wakielewa kuwa, zina mwisho, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.
Maombolezo 4:18.
Mathayo 13:49.
ENGLISH: I HAVE THEM BUT THEY ARE GOING.
The origin of an overhead saying refers to money which someone has. A person possess the money only for a short period of time because it ends when he starts using it by buying various things. That is why such person says, “I have them but they are going.”
This saying is paralleled to a man who uses his possessions well in his life. Such person uses his possessions with good understanding that they end when the time of using them comes because of his good upbringing that enables him to recognize that in taking everything has an end. He manages to soundly cultivate his family because of his good upbringing enough to use his resources well, in his life.
This person reminds us of the one who understood that his money would run out when he starts using it, because he also uses his properties well before they run out. That is why he says that, “I have them but they are going.”
This saying instills in people an idea of being careful enough to use well their belongings before they run out, understanding that they have an end, so that they can nicely improve their families, in their lives.
Lamentations 4:18.
Matthew 13:49.












