sayings

1399. NAJIKANDILE JUMONDA.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile bhukandi bho bhusu bho ngano. Olihoyi munhu uyo okandaga bhusu bho ngano ub’o bhugakandwa mpaga bhomonda na wigelelwa guzugwa mandazi, chapati na migate. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agayombaga giki “najikandandilile jumonda.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alindamu ugutumama milimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi na bhukamu bhutale kunguno ya bhutungilija bhokwe mpaga onamhala naonaga lulu uguitumama imilimo yiniyo. Uweyi agapandikaga matwajo mingi aha kaya yakwe kunguno ya bhukamu bhunubho ubho gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agakanda bhusu bho ngano mpaga bhumonda bho gwikoma guzugwa mandazi, chapati na migate, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe mpaga opandika matwajo mingi, umuwikaji bhokwe. “hunagwene agayombaga giki, “najikandile jumonda.”

Akahahile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gwigulambija gutumama milimo yabho bho nguvu ningi, kugiki bhadule kupandika matwajo gagubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Yahana 21:18.

 KISWAHILI: NIMEUKANDA UKALAINIKA.

Chanzo cha msemo huo huongelea juu ya unga wa ngano.  Alikuwepo mtu aliyekuwa akitengeneza unga huo wa ngano kwa kuukanda mpaka ukalainika kiasi cha kutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkakamavu wa kufanya kazi katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi na kwa bidii kubwa kwa sababu ya uaminifu wake huo, mpaga anazeeka ndipo anachoka kuzifanya kazi hizo. Yeye hupata mafanikio mengi katika familia yake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na yule aliyekanda unga wa ngano mpaga ukalainika kiasi chakutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate, kwa sababu naye hufanya kazi zake kwa nguvu mpaka anapata mafanikio mengi maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao kwa nguvu nyingi, ili waweze kupata mafanikio mengi ya kuwasaidia katika kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Yahana 21:18.

ENGLISH: “I KNEADED IT UNTIL IT WAS SOFT.”

The origin of this saying is about wheat flour. There was a person who was making wheat flour by kneading it until it was soft enough to be used for baking buns, and bread. That is why he said that, “I kneaded it until it was soft.”

This saying is matched to a person who is hardworking in his life. This person, exerts himself to do his work with great strength and diligence because of his loyalty, when he gets old he gets tired of doing those jobs. He achieves a lot of success in his family because of his diligence in doing his works with great strength, in his life.

This person resembles the one who kneaded wheat flour until it was soft enough to be used for baking buns, and bread, because he also works hard until he achieves a lot of success in his life. That is why he says that, “I kneaded it until it was soft.”

This saying instills in people a clue of being honest and hard working enough to nicely fulfill their responsibilities, so that they can achieve countless successes which can help them in developing their family lives.

John 21:18.

1398. UMUNHU UYU AGIMINYAGA WEYI NG’WINIKILI.

Olihoyi munhu uyo olina nguzu ningi umuchalo ja Ngeme. Umunhu ng’wunuyo abhuchaga miligo midito mpaga oyukoya ugusiminza kunguno ya wihadikija bhokwe bhunubho. Uweyi agayukeleja nose ugumisha kunguno ya bhunoge bho gubhucha miligo midito yiniyo. Hunagwene nose abhanhu bhagayuyomba giki, “umunhu uyu agiminyaga weyi ng’winikili.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo midito bho nduhu ugugusatwa umili gokwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga milimo midito gwingila diyu mpaga mhindi kunguno ya gukija ugugusatwa umili gokwe gunuyo, umubhutumami bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga anogile bhuli makanza kunguno ya gutumama milimo midimu yiniyo bho nduhu ugugusatwa umili gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo obhuchaga miligo midito mpaga oyukoya ugumisha, kunguno nuweyi agatumamaga milimo midimu mpaga olala anogile, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagahayaga giki, “umunhu uyu agiminyaga weyi ng’winikili.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guilanhana chiza imimili yabho umubhutumami bho milimo yabho yiniyo, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

KISWAHILI: MTU HUYU HUJIUMIZA YEYE MWENYEWE.

Alikuwepo mtu aliyekuwa na nguvu nyingi katika kijiji cha Ngeme. Mtu huyo alikuwa akibeba mizigo mizito mpaka anaanza kutembea kwa shida kwa sababu ya kujilazimisha kubeba mizigo hiyo. Yeye alifikia hatua ya kuchelewa kuamuka asubuhi kwa sababu ya uchovu huo wa kubeba mizigo mizito, katika maisha yake. Ndiyo maana mwishowe watu walisema kwamba, “mtu huyo hujiumiza yeye mwenyewe.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi bila ya kuuhurumia mwili wake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi nzito kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu ya kukosa umakini wa kuuhurumia mwili wake huo, katika kazi zake. Yeye huwa ana uchovu kila wakati kwa sababu ya kufanya kazi hizo ngumu bila ya kuuhurumia mwili wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyebeba mizigo mizito mpaka akaanza kutembea kwa shida, kwa sababu naye hufanya kazi ngumu mpaka analala akiwa amechoka sana, katika maisha yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu hujiumiza yeye mwenyewe.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuilinda miili yao wanapofanya kazi zao, ili waweze kuishi kwa furaha katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

 

ENGLISH: THIS MAN HURTS HIMSELF.

There was a man who was so strong in the village of Ngeme. He used to carry heavy maize sacks until he started walking with difficulty because of forcing himself to carry those sacks. He reached the point of waking up late in the morning because of the fatigue of carrying those heavy maize sacks, in his life. That is why people said about him that, “this man hurts himself.”

This saying is equated to a person who works without pitying his body, in his life. This person, does heavy works from morning to evening because of the lack of decent attention enough to pity his body, in his works. He is always tired because of doing those hard jobs without pitying his body, in his life.

This person resembles the one who carried heavy maize sacks until he started walking with difficulty, because he also works hard until he goes to bed very tired, in his life. That is why people say about him that, “this man hurts himself.”

This saying instills in people an idea of being watchful enough to protect their bodies while doing their jobs, so that they can live happily in their families, in their lives.

Genesis 9:21.

Job 3:17.

 

 

1397. OLALILA UYU.

Aho kale olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo ja Sanjo. Umunhu ng’wunuyo, ujimalaga wangu ijiliwa jakwe kunguno ya gugayiwa witegeleja bho gujilanhana chiza umukikalile kakwe kenako. Uweyi wikalaga na bhusunduhasi kunguno ya gugayila jilliwe aha kaya yakwe mpaga olala bho nduhu gulya jiliwa aha ng’wakwe, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “olalila uyu.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agajitumilaga sagara isabho ijo agajipandikaga umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo apajipandikaga isabho jakwe ujitumamila sagala bho gujigulia majikolo ayo gadina solobho aha kaya yakwe, kunguno ya gugayiwa witegeleja bho gujitumamila chiza isabho jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agajimalaga isabho ijo agajipandikaga mpaga oyulala nzala aha kaya yakwe kunguno ya gugayiwa witegeleja bho gujilanhana chiza isabho jakwe jinijo, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ojimalaga wangu ijiliwa jakwe mpaga olala bho nduhu gulya jiliwa aha kaya yakwe, kunguno nuweyi agajimalaga bho gujitumamila sagala isabho jakwe mpaga olala bho nduhu gulya jiliwa, aha kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “olalila uyu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujilanhana chiza isabho ijo bhagajipandikaga, kugiki bhadule gwikala na jiliwa ja gulya chiza umukaya jabho.

Mwanzo 41:54.

Luka 12:16-18.

Mathayo 6:25-26.

KISWAHILI: KALALA NJAA HUYU.

Hapo zamani alikuwepo mtu aliyeishi kwenye kijiji cha Sanjo. Mtu huyo, alikuwa akikimaliza haraka chakula alichokipata kwa sababu ya kukosa umakini wa kuvitunza vizuri vyakula hivyo. Yeye alikuwa na huzuni kwa sababu ya kukosa chakula kwenye familia yake hiyo mpaga akafikia hatua ya kulala bila kula chakula, katika maisha yake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “kalala njaa huyu.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huzitumia hovyo mali anazozipata, katika maisha yake. Mtu huyo, hupata mali zake na kuzitumia hovyo kwa kuzinunulia vitu visivyo na faida kwenye familia yake, kwa sababu ya kukosa umakini wa kuzitumia vizuri mali zake hizo, maishani mwake. Yeye huzimaliza mali zake hiyo mpaka anafikia hatua ya kulala bila kula chakula kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya kukosa umakini huo wa kuzitunza vizuri mali anazozipata, katika maisha yake.

Mtu huyo hufanana na yule aliyekimaliza haraka chakula chake mpaka akafikia hatua ya kulala bila kula chakula katika familia yake hiyo, kwa sababu naye huzitumia hovyo mali zake mpaka anaishiwa na kulala bila kula chakula katika familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “kalala njaa huyu.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuzitunza vizuri mali zao, ili waweze kuwa na chakula cha kutosha kula vizuri, katika familia zao.

Mwanzo 41:54.

Luka 12:16-18.

Mathayo 6:25-26.

ENGLISH: THIS ONE HAS SLEEP HUNGRY.

Once upon a time, there was a man who lived in the village of Sanjo. That man used to quickly finish food which he got because he was not careful enough to take decent care of it. He was so sad because of food shortage in his family that he went to bed without eating food in his life. That is why people said about him that, “This one has slept hungry.”

This saying is compared to a person who spends his money in a wasteful way. This person earns his money and spends it in a wasteful way by buying useless things for his family, because he is not careful enough to take virtuous care of the money which he gets, in his life. He spends his money until he reaches the point of going to bed without eating food in his family, because of not being careful enough to take decent care of his money in his life.

This person is like the one who quickly finished his food until he reached the point of going to bed without eating food in his family, because he also spends his wealth in such a way that he runs out and goes to bed without eating food in his family, in his life. That is why people say about him that, “this one has slept hungry.”

This saying imparts in people an idea of being careful enough to take respectable care of their wealth, so that they can have enough food to eat, in their families.

Genesis 41:54.

Luke 12:16-18.

Matthew 6:25-26.

1396. NI B’ULI ALIB’AKIJA?

Olihoyi munhu uyo oling’wi o walwa uyo ob’ung’waga noyi umkikalile kakwe. Uwalwa bhunubho bhugagubhakijaga umili gokwe kunguno ya bhukoji bhobho bhunubho. Umunhu ng’wunuyo, agakumuka noyi umuchalo jakwe kunguno ya bhung’wi bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagayibhuja nose giki, “ni b’uli alib’akija?”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agagukenagulaga umili gokwe bho gwita mihayo iyo igang’wenhelaga makoye, umukikalile kakwe. umunhu ng’wunuyo, agalyaga jiliwa mpaga osata kunguno ya gugayiwa witegeleja umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agagulab’ulaga umili gokwe kunguno ya gugayiwa witegeleja bhunubho umukatumamile ka jikolo jakwe jinijo, umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo ong’waga walwa mpaga ogulabhula umili gokwe, kunguno nuweyi agalyaga jiliwa ja gugukenagula umili gokwe umikikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagamujaga giki “ni b’uli alib’akija?”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujitumamila chiza ijikolo jabho, kugiki bhadule guyilanhana chiza imimili yabho yiniyo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

KISWAHILI: KWA NINI UNAJIUNGUZA?

Alikuwepo mtu aliyekuwa mlevi wa pombe kali katika maisha yake. Pombe hiyo iliuharibu mwili wake kwa sababu ya ukali wake huo. Mtu huyo, alijulikana sana kwenye kijiji chake kwa sababu ya ulevi wake huo. Ndiyo maana watu walimuuliza kwamba “kwa nini anajiunguza?”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huudhuru mwili wake kwa kutenda matendo ambayo humletea matatizo, katika maisha yake. Mtu huyo, hula chakula kupita kiasi mpaga anaugua kwa sababu ya kukosa umakini wa kuwa na kiasi maishani mwake. Yeye huuharibu mwili wake huo kwa sababu ya kukosa umakini huo wa kuwa na kiasi katika matumizi ya vitu vyake katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyelewa pombe kali mpaka akaiharibu afya yake, kwa sababu naye hula chakula kupita kiasi mpaka anaugua, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuuliza kwamba, “kwa nini anajiunguza?”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuvitumia vitu vyao kwa kiasi kizuri, ili waweze kuzilinza vizuri afya zao, katika maisha yao hayo.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

ENGLISH: WHY DO YOU HURT YOURSELF?

There was a man who was a heavy drinker of alcohol in his life. The alcohol destroyed his body because of its intensity. Such man became so well known in his village because of his alcoholism. That is why people asked him that, “Why do you hurt yourself?”

This saying is equaled to a person who harms his body by doing deeds that cause him hitches in his life. This man eats too much food to the point of getting sick because of a lack of attention to moderation in his life. He destroys his body because of his lack of attention to such moderation in using of his belongings in life.

This man is similar to a person who drank too much alcohol to the point of ruining his health, because he also eats too much food until he gets sick, in his life. That is why people ask him that, “Why do you hurt yourself?”

This saying teaches people about being so careful enough to use their possessions in the right way, so that they can take respectable care of their health in their lives.

Genesis 9:21.

Job 3:17.

1395. LYAGI NAWE DUHU.

Olihoyi nigini uyo wikalaga aha kaya ya bhasab’i. Unigini ng’wunuyo agahaya gujulya na bhanhu bhatale aho jatengwa ijiliwa kunguno oliatuubhile. Abhanhu bhagayunemeja ugujilya ijiliwa jinijo kunguno jali jabhatale. Hunagwene unamhala oha kaya yiniyo agabhawila giki, “lyagi nawe duhu.”

Akakayile kenako kagalenganijiyagwa ku kaya ya bhanhu abho bhalibhizanholo umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagabhakaribhushaga pye abhanhu bhajilya ijiliwa jabho ulu japyaga kunguno ya wizanholo bhobho bhunubho umuwikaji bhobho. Abhoyi bhagapandikaga mbango ja gwikala bho mholele na bhanhu bhabho aha kaya yabho yiniyo, kunguno ya wizanholo bhobho bhunubho.

Ikaya ya bhanhu bhenabho igikolaga nu namhala uyo olyaga na bhanigini ijiliwa jakwe ulu japyaga, kunguno nabhoyi bhagabhakaribhushaga pye abhanhu bhajilya ijiliwa jabho ulu japyaga, aha kaya yabho yiniyo. Hunagwene bhagayombaga giki, “lyagi nawe duhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na wizanholo bho gubhambilija abhichabho abho bhalina makoye, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi bhutale umukaya jabho jinijo.

Yahone 6:31-33.

Mathayo 25:35.

Yohane 6: 55-56.

KISWAHILI: MLE NAYE TU.

Alikuwepo mtoto aliyekuwa akiishi kwenye familia tajiri. Mtoto huyo, alitaka kula na watu wazima kilipowekwa mezani chakula chao kwa sababu alikuwa na njaa. Watu walimzuia kukila chakula hicho kwa sababu kiliwa cha watu wazima. Ndiyo maana mzee wa familia hiyo aliwaambia kwamba, “mle naye tu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa familia ya watu wale ambao ni wakarimu katika maisha yao. Watu hao huwakaribisha watu wote kula chakula chao kinapoiva kwa sababu ya ukarimu wao huo, maishani mwao. Wao hupata Baraka za kuishi kwa furaha kubwa katika familia yao, kwa sababu ya ukarimu wao huo katika maisha yao.

Familia ya watu hao, hufanana na yule mzee aliyekula chakula chake pamoja na watoto kilipoiva, kwa sababu nao huwakaribisha watu wote kula chakula chao kinapoiva, katika familia yao. Ndiyo maana wao husema kwamba, “mle naye tu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na ukarimu wa kuwasaidia wenzao wanaokumbwa na matatizo mbalimbali, ili waweze kuishi kwa furaha kubwa katika familia zao.

Yahone 6:31-33.

Mathayo 25:35.

Yohane 6: 55-56.

ENGLISH: EAT ONLY WITH HIM.

There was a child who lived in a rich family. This child wanted to eat with adults when their food was placed on the table because he was hungry.  People prevented him from eating such food because it was for adults. That is why the elder of the family told them that, “eat only with him.”

This saying is related to the family of people who are generous in their lives. These people invite everyone to eat their food when it is ready because of their generosity in their lives. They receive blessings of living with great happiness in their family, because of their generosity in their lives.

This family of these people is like the old man who ate his food with children when it was ready, because they also invite everyone in their family to eat their food when it is ready. That is why they say that, “eat only with him.”

This saying imparts in people an idea of being generous enough to help their nobles who are facing various hitches, so that they can live with great happiness in their families.

John 6:31-33.

Matthew 25:35.

John 6: 55-56.