sayings

171. NVA NA NVA JIDIKAMILAGA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Mbuki ya lusumo lunulo ililola nva. Inva iyene ulu yukamilwa idiko gulya mujiseme jimo na ng’wichayo. Buli yene igalilaga bho ng’wi binghi, yalya bho nduhu ugwisangija lihamo. Nulu ab’ize ali ng’wana oyo idulya kihamo ung’wibinghi limo. Inva jili na kab’uyiyene umuwikaji bhojo.

Ulusumo lunulo lugalenganijiyagwa kulimunhu uyo aliminholo umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’unuyo adahayile ugwigunana na b’iye, ku nguno ya nhungwa jakwe ijagutogwa gwikala yiyene.

Ulusumo lunulo lodulanga higulya ya kuleka nhungwa ja kutogwa gwikala yiyene. Ilichiza gwikala na kajile kagwigunana chiza na bhanhu b’igisu. Ubhusangi bhugabhambilijaga abhanhu umugwikala bho mholele na b’ichab’o.

Ijinagongeja, ulusumo lunulo lolanga bhanhu higulya ya kuleka gub’iza na kajile ka nyawa. Ilichiza abhanhu bhab’ize ni lonjo na witogwi umuwikaji bhobho umuchalo jabho, nulu umujuiya jabho.

KISWAHILI: MBWA NA MBWA HAWASHIRIKI CHAKULA KWA KUTUMIA CHOMBO KIMOJA

Chanzo cha methali hiyo chaangalia mbwa. Mbwa ana ubinafsi kwa sababu yeye hayuko tayari kula chakula kwenye chombo kimoja na mwenzake. Kila mmoja hulia kwenye chombo malumu kwa ajili yake tu.

Hawawezi kulia chombo kimoja kwa kuchangia. Hata awe mtoto wake atamkatalia kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kuwa na ubinafsi maishani mwake. Mbwa wana ubinafsi wa hali ya juu katika maisha yao.

Methali hiyo hulinganishwa kwa mtu ambaye ni mchoyo katika maisha yake. Mtu huyo hataki kusaidiana na wenzake, kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kukaa peke yake. Mtu huyo atawaliwa na ubinafsi katika maisha yake.

Methali hiyo hufundisha watu juu ya kuacha tabia ya ubinafsi. Tabia hiyo ni ile ya kupenda kukaa peke yao katika maisha yao. Ni vizuri kuwa pamoja na wenzao kwa kujijengea tabia ya kusaidiana nao. Umoja huo husaidia watu katika kuishi kwa amani na wenzao katika jumuiya au kijiji chao.

Zaidi ya hayo, methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuachana na tabia za mbwa, yaani ubinafsi. Wao wanatakiwa kujijengea tabia ya kuwajali wenzao katika maisha yao kwa ajili ya kuwawezesha kuleta maendeleo katika jumuiya zao. Inawabidi wawajali wenzao kwa kukubali kusaidiana na kushirikiana nao kwa upendo.

Zaburi 10: 3-4.

Isaya 56:11.

Luka 12:15-21.

Wafilipi 2:4-6.

1Petro 4:7-11.

1Wakorintho 3:4-8.

dog

 DOGS CANNOT SHARE FOOD IN ONE BOWL

The above proverb looks at the selfish nature of dogs. A dog cannot share food in one bowl with a fellow dog because of their selfishness. Each has a separate bowl to itself.

They cannot share one plate, even with their puppies, because of their high degree of selfishness.dog-

The overhead proverb is likened to the character of a selfish person. Such a person is not supportive to others, and has a tendency to live in isolation. He/she is controlled by selfishness in his/her life.

The proverb teaches people against selfish behavior in their lives, and against seclusion. Instead, people are advised to embrace unity, which helps them co-exist in peace with their colleagues in their community.

Above all, the proverb cautions people to shun dog character: selfishness. They should instead possess self-sacrifice, which empowers communities. Similarly, they should support and co-operate with each other in a loving way.

Psalm 10: 3-4.

Isaiah 56:11.

Luke 12: 15-21.

Philippians 2: 4-6.

1 Peter 4: 7-11.

1 Corinthians 3: 4-8.

170. GASHI DUGUKOYELAGA ISHALEKWA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya kahayile kenako ililola bhanhu abho bhagukoyelaga ginhu, nulu nimo uyo gub’izile guti gupya ijigugulola. Aliyo ubhunghana bhogo ukubhanhu abho bhagudeb’ile guligukulukulu.

Ligashigaga ikanza ilya gubhudeb’a ubhunghana bho nimo, nulu ginhu jinijo ukubhanhu bhenebho abho b’agujikoyelaga kulwa nguno ya bhoyi gub’iza bhalibhageni ukuginhu jinijo. Ulu bhumana chena, bhagayombaga giki ‘gashi dugukoyelaga ishalekwa.’

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo yakwe bho nduhu ugub’iza na bhukengeji bho guimana chiza imilimo yiniyo. Agisangaga onogaga sagara, kulwa gujimara inguzu jakwe kumilimo iyo idina solobho ya kub’eja kaya, nulu jumuiya yakwe. Ilichiza umunhu agudeb’e chiza unimo gokwe, hayo adinagwandya ugugutumama.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gwita bhukengeji bho gudula guideb’a chiza imilimo yabho, hayo bhatali ugwandya uguitumama. Ulub’ita chene, bhagudula uguitumama imilimo iyagubhenhela solobho, umuwikaji bhobho, na guileka iyo itina solobho.

Kuyiniyo lulu, akahayile kenako agayombaga munhu uyo alitumama nimo uyo gudinayo isolobho. Guti gugwita nimo gosegose uyogoiwa ugudililwa na bhiye.

KISWAHILI: KUMBE TWAHANGAIKIA KILICHOACHWA

 Chanzo cha msemo huo chaangalia watu wahangaikiao kitu ambacho kwa macho huonekana kama kipya. Lakini ukweli wa kitu hicho kwa wale wakifahamuo ni kikuukuu.

Hufika wakati wa kuufahamu ukweli wa kitu hicho ambacho watu hao hukihangaikia kwa sababu ya ugeni wao kwenye kitu hicho. Wakisha fahamu hivyo, watu hao husema hivi ‘kumbe twahangaikia kilichoachwa.’

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu afanyaye kazi zake bila kufanya utafiti wa kutosha kuzifahamu vizuri kazi hizo. Mtu huyo hujikuta amechoka kwa kuzimalizia nguvu zake kwenye kazi hizo zisizo na faida kwenye familia au Jumuiya yake. Yafaa mtu aifahamu vizuri kazi yake kabla ya kuanza kuifanya.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kufanya utafiti wa kazi zao kabla hawajaanza kuzifanya. Wakifanya hivyo, wataweza kuzigundua na kuzifanya kazi zile ziwezazo kuwaletea maendeleo na kuziacha zile ambazo haziwezi kuwaletea maendeleo hayo.

Kwa hiyo basi, msemo huo huusema mtu afanyaye kazi isiyo na faida, kama vile kujishugulisha na kazi yoyote ambayo wenzake waliashaiacha kuifanya.

2 Kor 5:17

Wagalatia 5:4.

people-catechist

ENGLISH: EXPENDING ENERGY ON NOTHING WORTHWHILE

The above saying is about people who spend so much energy chasing after what their eyes perceive to be new, yet in reality it is completely worthless, according to those who are aware of it.

A time comes when the truth dawns on the people as they understand how naive they were about their deceptive perception. With this realization, they would say, ‘so we are losing energy on nothing worthwhile’

The saying is likened to a person who performs his/her work without carrying out sufficient research to determine its worth. Such a person wears himself/herself down by focusing all his/her energy on unprofitable tasks in the family or in the community. It is advisable for a person to be adequately familiar with his/her job before attempting it.

The saying teaches people about the need for due diligence before embarking on anyteacher2 assignment. That would not only guarantee profitable engagements that can bring about development in families but also help shun those worthless ones that cannot lead to progress.

Thus, the saying advises people to conduct sufficient research before settling on any job. That helps ensure that they engage in profitable ones for the sake of developing the family and the community.

2 Cor. 5:17

Galatians 5: 4.

169. SEGA SEGA IGABYALAGA MIDIIMU, MIDIIMU IGABYALAGA SEGASEGA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Mbuki ya kahayile kenako ililola milimo yose iyo ilimidimu, kulwa nguno ligikalaga liliho likanza idimu ilyagukoyakoya, aliyo uluugushisha unimo gunuyo ugwasha hela kulwa wiyumilija wenubho.

Akahayike kenako kagalenganijiyagwa kulimunhu uyo agiyumilijaga umuguitumama imilimo yakwe imidimu yiniyo mpaka oimala na opandika matwajo mingi na miza umuwikaji bhokwe. Umunhu ng’wunuyo agayegaga noi uluogapandika amatwajo ga milimo yakwe.

Ijinagongeja, akayayile kenako, kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagamanaga bhusega ulubhaligusha. Aliyo umuligusha linilo, umo obho adulile guminyika na gwandya gulila. Abhanhu bhaguyomba giki, sega sega igabyalaga lila lila, hi midimu iyiniyo.

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gub’iza na wiyumilija umu milimo imidimu, nguno igenhaga solobho ahabhutongi. Ilichiza uguitumama imilimo yiniyo na wiyumilija bhutale, kulwa nguno idulile gwenha bhuyegi bhutale ahabhutongi yaho.

Akahayile kenako hangi kalanga bhanhu higulya ya kuleka ilishinya ilya sagara. Kunguno, lishinya linilo lidulile gwenha bhusunduhazu bho gulabhuka munhu ose ose. Ilichiza ugwigusha bho masala.

KISWAHILI: CHEKA CHEKA, HUZAA MAGUMU, MAGUMU HUZAA CHEKA CHEKA

Chanzo cha msemo huo chaangalia kazi yoyote ambayo ni ngumu, kwa maana kuna wakati mgumu wa kuhangaka, hata hivyo ukisha imaliza kazi hiyo unapata faida kwa kuvumilia huko.

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu avumiliaye katika kufanya kazi zake ambazo ni ngumu mpaka kuzimaliza na kupata matokeo mazuri kwa uvumilivu wake. Mtu huyo hufurahi mno apatapo matunda ya kazi zake.

Zaidi ya hayo, msemo huo hulinganishwa kwa watu wachezao huku wakicheka kwa maana ya kufurahia. Lakini katika mchezo huo, mmoja wao huumia na kuanza kulia. Watu husema, cheka cheka huzaa kilio, hiyo ndiyo migumu kwa watu hao.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na uvumilivu katika kufanya kazi zao zilizongumu, kwa sababu kazi hizo huleta faida maishani mwao. Ni vizuri kuzifanya kazi hizo zilizo ngumu kwa uvumilivu mkubwa, kwa sababu hizo zaweza kuleta furaha kubwa wakati ujao.

Zaidi kwa hayo, msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha michezo iliyo ya hovyo, kwa sababu michezo hiyo, huweza kuleta huzuni itokanayo na kuumia kwa mtu yeyote. Ni vizuri kucheza kwa kutumia akili za kutosha kuepuka kupata matokeo mabaya.

Yohana 4:35-36.

Yakobo 5:7-10.

Zaburi 126:5-6.

2Timotheo 2:6.

smile

ENGLISH: LAUGHTER GIVES BIRTH TO DIFFICULTIES; DIFFICULTIES GIVE BIRTH TO LAUGHTER

The above proverb relates to tasks that are considered difficult and which are daunting to perform. However, once accomplished, one reaps the benefits of one’s endurance.

The overhead proverb is compared to a person who undertakes his/her work with diligence and endurance, resulting to effective completion of the exercise. That situation brings a satisfaction to the person as he/she reaps the fruits of his/her labour.

In addition, the proverb is likened to people who enjoy playing and reveling in excitement. However, in the same game, someone can get sick and start grieving. Thus, it said that, ‘laughter gives birth to difficulties; difficulties give birth to laughter.’

The proverb teaches people to exercise patience in doing their work. Hard work guarantees value in life. So, it is good to undertake those hard tasks with a lot of patience; that is a surety for a happy future.

In addition, such proverb cautions against engaging in dangerous games, because some games can bring about grief. It is advisable to play safe to avoid poor outcomes.

John 4: 35-36.woman6

James 5: 7-10.

Psalm 126: 5-6.

2 Timothy 2: 6.

168. LWIGUTO LWA NG’WI NZALA YA NTUNGWA

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Mbuki ya kahayile kenako ililola munhu uyo ali ng’wi owalwa. Ung’wi ng’wunuyo agamanaga uyomba mamihayo ga sagala guti: nabhung’waga bhukomile ng’ombe.

Aliyo bhaliho bhanhu bhangi abho bhatungilwe bhatina wiyabhi bho guja gujung’wa uwalwa bhunubho. Abhanhu bhenabho niyo bhagakalalagwa ulu bhamona munhu uyo ong’waga walwa bhab’iza na nzala nh’ale ya gubhung’wa.

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo atogilwa gwita mihayo ya sagara iyo idina solobho uko kaya yakwe. Imihayo yiniyo igakenagulaga sabho ya hakaya yakwe.

Akahayile kenako kulangaga bhanhu higulya ya kuleka ugwita imihayo ya sagala umuwikaji bhobho. Ilichiza abhanhu ugoya ugwikumilija mugwita yabhubhi kunguno iyiniyo igakenagulaga kaya na chalo jabho.

Hangi akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya goya gwikumva ya musi iyo ikomile gulisanya kaya, na nulu bhananzengo. Ilichiza abhanhu bhakalalile mihayo iyo iliya wiza ijinagubheja kaya na chalo jabho.

KISWAHILI: KUSHIBA KWA MLEVI NJAA KWA ALIYEFUNGWA

Chanzo cha msemo huo kinaangalia mtu anayekunywa pombe. Mtu huyo huzungumumza maneno ya hovyo hovyo mfano: nimekunywa yenye kipimo sawa na ng’ombe.

Hata hivyo kuna watu wengine ambao wamefungwa ambao hawana uhuru wa kwenda kunywa pombe. Watu hao hupata hamu ya kunywa pombe wanapomuona mtu aliyekunywa pombe hiyo. Huwa wanakuwa na njaa kubwa ya kuinywa.

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu ambaye hupenda kufanya matendo ya hovyo hovyo ambayo hayana maana katika ujenzi wa familia yake. Matendo hayo hubaribu familia yake.

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuacha kufanya matendo yasiyofaa katika ujenzi wa familia zao maishani mwao. Huwataka watu hao kuacha kutenda matendo yaliyomabaya kwa sababu matendo hayo huharibu familia na vijiji vyao.

Zaidi ya hayo, msemo huo hufundisha watu juu ya kukoma kutamani mabaya yaliyomo duniani, kwa sababu hayo husambalatisha familia na vijiji vyao. Watu hao hutakiwa kutamani yale yaliyo mema kwa ajili ya kuwawezesha kuzijenga vizuri  familia na vijiji vyao.

Mathayo 7:13-14.

Mathayo 24:37-44.

Luka 13:22-24.

Waebrania 10:24-25.

drunkard

ENGLISH: A SATISFIED DRUNK; A HUNGRY OF A PRISONER

The above proverb talks about the attitude and behavior of a drunkard. Such a person speaks carelessly, for example he/she would boast: I have drunk the same quantity as that of a cow.arms

On the other hand, people who are incarcerated do not have the freedom to drink, despite the craving for it whenever they see someone who has taken alcohol. They develop great desire for the drink.

Such proverb is likened to the irresponsible character in some people, for example those who behave in a careless manner. Such sloppy conduct destroys families.

The same principle is used to teach people against engaging in destructive activities that can wreck their families and the community.

In addition, the proverb discourages people against craving worldly things because they destroy families and communities. They are instead encouraged to crave pleasant things that can help bring about development in their societies.

Matthew 7: 13-14.

Matthew 24: 37-44.

Luke 13: 22-24.

Hebrews 10: 24-25.

167. MAKONO NINA O MUNHU

Research sponsored by: Don Sybertz, with special thanks to Rev Joe Healey (African Proverbs, Sayings and Stories)

Imbuki ya lusumo lunulo ililola makono na Munhu. Umunhu ulu atali ng’wana ndoo agambilijiyagwa bhogub’uchiwa mumakono ga ng’wa nina, nulu ga b’akongi bhakwe. Aliyo lulu umunhu ulu ukula agab’izaga na bhudula bho gwilisha wei bho gutumila makono gakwe.

Gashinaga lulu, imbuki ya lusumo lunulo yalomela giki umunhu ulukula agilishiga ng’winikili bho gutumila makono gakwe. Amakono genayo hayo gagabhizaga myaji okwe.

Amakono gagalenganijiyagwa kuli myaji wa ng’wa munhu uyo amanile ugubhalanghana abhana bhakwe. Umyaji uojigongo agabhalanghanaga chiza abhana bhakwe.

Umyaji ng’wunuyo agatumilaga makono ugub’alanga bhutumami ubho milimo abhana bhenabho. Hunagwene b’agakulaga ukunu bhalilanga uguitumama imilimo yiniyo.

Uluukula umunhu aguyutumama weyi ng’winikili imilimo ya gwilisha umukaji bhokwe. Ichene guhaya giki, amakono gali nina o ng’wa munhu.

Ulusumo lunulo lulilanga bhanhu higulya ya gugatumila chiza amakono gabho, kugiki gadule gubhapandikila matwajo mingi umuwikaji bhobho. Ilichiza abhanhu bhuleke ubhugokolo.

Ijinagongeja, ulusumo lunulo lulilanga bhanhu higulya ya gufunya ilange lya wiza kubhana jumuiya ilya gutumama milimo iyo idulile gub’enhela matwajo ga wiza umuwikaji bhobho.

KISWAHILI: MIKONO NI MZAZI WA MTU

Chanzo cha methali hiyo kinaangalia mikono na mtu. Mtu akiwa mtoto mdogo husaidiwa kwa kubebwa mikononi mwa mama yake au mikononi mwa walezi wake. Lakini mtu huyo akikua huwa na uwezo wa kujilisha mwenyewe kwa kutumia mikono yake. Ndiyo kusema kwamba, ‘mikono ni mzazi wa mtu.’

Mikono hulinganishwa kwa mzazi wa mtu anayefahamu kumtunza mwanae. Mzazi mwenye huruma huwafundisha vizuri watoto wake namna ya kuitumia mikono yao kwa kulijiletea maendeleo.

Mzazi huyo hutumia mikono yake katika kuwafundisha watoto wake hao namna ya kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuifikia hatua ya kupata mafanikio ya kujilisha wenyewe na kuwatunza wenzao maishani mwao. Ndiyo maana watoto hao hukua wakiwa na ufahamu wa kuitumia vizuri mikono yao katika kujipatia mahitaji yao ya kila siku na ya wenzao.

Ndiyo kusema kuna ukweli kwamba ‘mikono ni mzazi wa mtu,’ kwa sababu ya utunzaji anaoupata mtu huyo kutoka kwenye mikono yake.

Methali hiyo huwafundisha watu juu ya kuitumia vizuri mikono yao ili iweze kuwapatia maendeleo maishani mwao. Inapiga vita tabia ya uvivu au ile ya kuwa na utegemezi katika kufanya kazi zile ambayo mtu huyo anaziweza kuzitekeleza mwenyewe.

Zaidi ya hayo, methali hiyo huwafundisha watu juu ya kuwapatia wanafamilia, au wanajumuiya na wananchi wote kwa ujumla, malezi mema yawezayo kuwaletea maendeleo maishani mwao.

Mithali 10:4.

 

girl3

 ENGLISH: HANDS ARE A PERSON’S MOTHER

The overhead proverb relates to a human being’s hands. While still in infancy, a baby is taken care of in his/her mother’s hands, or in the hands of the babysitters. But when he/she grows up, the adult is able to feed himself/herself using his/her own hands. As such, ‘hands are a person’s mother.’baby1

Such proverb is likened to a parent who knows how to take care of his/her child. A compassionate parent teaches his/her children how to be self-reliant or how to use their hands to bring them development.

Such a parent uses his/her hands to teach the children to work hard and achieve their own goals, and to care for fellow human beings. That is why the children would grow up with the good habit of using their hands to provide themselves and their peers with daily needs.help

In essence, it is a fact that ‘hands are a person’s mother’ because of the care that he/she gets from the mother’s hands.

The proverb teaches people on how to use their hands in a resourceful way in order to improve their lives. It discourages the tendency of being lazy or dependent upon others in undertaking tasks that can be accomplished by them alone.share

Furthermore, the proverb instills in people the importance of proper training of family members, the community and society in general for the sake of bringing about progress in their lives.

Proverbs 10: 4.