heritage

1416. IGEMBE NAGEMA NG’WELELE.

Aho kale olihoyi nhimi uyo olimilaga ligembe lya makono. Unhimi ng’wunuyo olialisanije iligembe lyakwe linilo kunguno olilimilaga chiza mpaga lyang’wenhela jiliwa aha kaya yakwe. Uweyi olidimilaga china iligembe linilo guti numo agabhukikaja ng’wana ng’welele, umuwikaji bhokwe. Hunagwene agayomba giki, “igembe nagema ng’welele.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina bhutungilija bho gwihanda gutumama chiza nimo uyo gugang’wenhelaga jiliwa, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agihandaga gugudumama unimo gokwe bho gubhalanga abhanhu bhakwe higulya ya gwigulambija kugugutumama chiza mpaga gobhapandikila jiliwa, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agapandikaga jiliwa ja gulya chiza bhuli ng’waka aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya bhutungilija bhokwe bhunubho ubho gwigulambija gugutumama chiza unimo gokwe gunuyo, umukikalile kakwe kenako.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu nhimi uyo olilimilaga chiza iligembe lyakwe mpaga lya ng’wenhela jiliwa aha kaya yakwe, kunguno nuweyi agagudimilaga chiza unimo gokwe gunuyo bho gwigulambija gugutumama chiza mpaga opandika jiliwa ja gulya chiza aha kaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene agayombaga giki, “igembe nagema ng’welele.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gwigulambija guyitumama chiza imilimo yabho iyo igabhenhelaga jiliwa, kugiki bhadule gupandika sabho ja gutumamila chiza umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mwanzo 3:19.

Mithali 24:27.

KISWAHILI: JEMBE NIMEJARIBU MTOTO MCHANGA

Hapo zamani alikuwepo mkulima aliyelimia jembe la mkono. Mkuliwa huyo alilitegemea jembe lake hilo kwa sababu ya kulilimia vizuri mpaka linamletea chakula kwenye familia yake. Yeye alilishikilia vizuri jembe hilo kama anavyobeba mtoto mchanga, maishani mwake. Ndiyo maana alisema kwamba, “jembe nimejaribu mtoto mchanga.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujikaza kuifanya vizuri kazi ile ambayo humletea chakula, katika maisha yake. Mtu huyo, huishikilia kazi yake hiyo kwa kuwafundisha watu juu ya kujibidisha kuitekeleza vizuri mpaka inawapatia chakula, kwa sababu ya uaminifu wake huo, maishani mwake. Yeye hupata chakula cha kula vizuri kila mwaka kwenye familia yake kwa sababu ya uaminifu wake huo wa kujibidisha kuitekeleza vizuri kazi yake hiyo, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo hufanana na yule mkulima aliyelilimia vizuri jembe lake mpaka likamletea chakula kwenye familia yake, kwa sababu naye hujibidisha kuitekeleza vizuri kazi yake hiyo mpaka inamletea chakula cha kula kila mwaka kwenye familia yake, maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “jembe nimejaribu mtoto mchanga.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kujibidisha kuzitekeleza vizuri kazi zao zinazowaletea chakula, ili waweze kupata mali za kutumia vizuri katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 3:19.

Mithali 24:27.

ENGLISH: A HOE HAS TESTED A BABY.

Once upon a time, there was a farmer who cultivated farms by using a hand hoe. This farmer relied on his hoe because it worked well until it brought food to his family. He held the hoe tightly like he was carrying a baby, in his life. That is why he said that, “a hoe has tested a baby.”

This saying is equaled to a person who strives to do well the work that brings him food, in his life. Such person holds on to his work by teaching people about working hard enough to do it well until it provides them with food, because of his loyalty, in his life. He gets good food to eat every year for his family because of his loyalty to work hard enough to finish well his work in his life.

This person resembles the farmer who cultivated his farm until it brought food to his family, because he also strives to carry out his work well until it brings food to his family every year, in his life. That is why he says that, “a hoe has tested a baby.”

This proverb teaches people about being honest enough to carry out their work well that brings them food, so that they can obtain wealth for using well in their families, in their lives.

Genesis 3:19.

Proverbs 24:27.

1409. NASUGAMBAGA NASUMBYAGA MAKONO.

Olihoyi munhu uyo wikalaga muchalo ja Wimate. Umunhu ng’wunuyo agikenya na ng’wiye uyo bhali bhuzenganwa nanghwe kunguno ya gwishogeja shib’i. Uweyi agiyangula gulomba bhulekejiwa ukuli ng’wiye ng’wunuyo. Hunagwene agayomba giki, “nasugambaga nasumbyaga makono.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alina widohya bho gulomba bhulekejiwa ulu ohubhaga, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agalombaga bhulekejiwa ulu widumaga nabhiye kunguno ya widohya bhokwe bhunubho ubho gwikala chiza nabhiye, umuwikaji bhokwe. Uweyi agayilelaga chiza ikaya yakwe kunguno ya widohya bhokwe ubho gwikala chiza na bhanhu bhakwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agalomba bhulekejiwa aho widuma nu nzenganwa okwe, kunguno nuweyi alina widohya bho kulomba bhulekejiwa ukubhiye ulu widumaga nabho, umuwikaji bhobho. Hunagwene agayombaga giki, “nasugambaga nasumbyaga makono.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na widohya bho gwikala na bhanhu chiza na gulomba bhulekejiwa ukubhichabho ulu bhidumaga nabho, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Hebabu 14:19.

Zaburi 78:38.

Mathayo 6:12.

Mathayo 6:15.

Luka 15:3-7.

Luka 17:4.

KISWAHILI: NIMEPIGA MAGOTI NAKUFUMBA MIKONO.

Alikuwepo mtu aliyeishi kwenye kijiji cha Wimate. Mtu huyo aligombana na mwenzake aliyekuwa jirani yake kwa sababu ya kujibizana vibaya. Yeye aliamua kuomba msamaha kwa mwenzake huyo. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimepiga magoti nakufumba mikono.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana unyeyekevu wa kuomba msamaha anapokosea, katika maisha yake. Mtu huyo, huomba msamaha anapokesana na wenzake kwa sababu ya unyenyekevu wake huo wa kuishi vizuri na wenzake, maishani mwake. Yeye huilea vyema familia yake kwa sababu ya unyenyekevu wake huo wa kuishi vizuri na watu wake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyeomba msamaha alipokosana na jirani yake, kwa sababu naye ana unyenyekevu wa kuomba msamaha kwa wenzake anakosana nao. Ndiyo maana husema kwamba, “nimepiga magoti nakufumba mikono.”

Msemo huo hufundisha watu juu ya kuwa na unyenyekevu wa kuishi na watu vizuri na kuomba msamaha kwa wenzao wanakosana, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Hebabu 14:19.

Zaburi 78:38.

Mathayo 6:12.

Mathayo 6:15.

Luka 15:3-7.

Luka 17:4.

ENGLISH: I HAVE KNELT DOWN AND FOLDED MY HANDS.

There was a man who lived in the village of Wimate. This man had a fight with his neighbor because of evil argument. He decided to apologize to his neighbor. That is why he said that, “I have knelt down and folded my hands.”

This saying is related to a person who has humility to apologize when he makes a mistake in his life. Such person apologizes when he makes a mistake with his friends because of his humility to live well with his friends in his life. He takes virtuous care of his family because of his humility to live well with his people in his life.

This person is like the one who apologized when he made a mistake with his neighbor, because he also has the humility to apologize to his friends with whom he makes a mistake. That is why he says that, “I have knelt down and folded my hands.”

This saying teaches people about being humble by living well with people and asking for forgiveness from their earls who have differences, so that they can raise their families well, in their lives.

Hebrews 14:19.

Psalm 78:38.

Matthew 6:12.

Matthew 6:15.

Luke 15:3-7.

Luke 17:4.

1399. NAJIKANDILE JUMONDA.

Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile bhukandi bho bhusu bho ngano. Olihoyi munhu uyo okandaga bhusu bho ngano ub’o bhugakandwa mpaga bhomonda na wigelelwa guzugwa mandazi, chapati na migate. Hunagwene umunhu ng’wunuyo agayombaga giki “najikandandilile jumonda.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alindamu ugutumama milimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agigulambijaga gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi na bhukamu bhutale kunguno ya bhutungilija bhokwe mpaga onamhala naonaga lulu uguitumama imilimo yiniyo. Uweyi agapandikaga matwajo mingi aha kaya yakwe kunguno ya bhukamu bhunubho ubho gutumama milimo yakwe bho nguvu ningi, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agakanda bhusu bho ngano mpaga bhumonda bho gwikoma guzugwa mandazi, chapati na migate, kunguno nuweyi agatumamaga milimo yakwe mpaga opandika matwajo mingi, umuwikaji bhokwe. “hunagwene agayombaga giki, “najikandile jumonda.”

Akahahile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na bhutungilija bho gwigulambija gutumama milimo yabho bho nguvu ningi, kugiki bhadule kupandika matwajo gagubhambilija ugujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Yahana 21:18.

 KISWAHILI: NIMEUKANDA UKALAINIKA.

Chanzo cha msemo huo huongelea juu ya unga wa ngano.  Alikuwepo mtu aliyekuwa akitengeneza unga huo wa ngano kwa kuukanda mpaka ukalainika kiasi cha kutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate. Ndiyo maana alisema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mkakamavu wa kufanya kazi katika maisha yake. Mtu huyo, hujibidisha kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi na kwa bidii kubwa kwa sababu ya uaminifu wake huo, mpaga anazeeka ndipo anachoka kuzifanya kazi hizo. Yeye hupata mafanikio mengi katika familia yake kwa sababu ya bidii yake hiyo ya kufanya kazi zake kwa nguvu nyingi, maishani mwake.

Mtu huyo hufanana na yule aliyekanda unga wa ngano mpaga ukalainika kiasi chakutosha kutumika kwa kupikia maandazi, chapati na mikate, kwa sababu naye hufanya kazi zake kwa nguvu mpaka anapata mafanikio mengi maishani mwake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimeukanda ukalainika.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na uaminifu wa kujibidisha kuyatekeleza majukumu yao kwa nguvu nyingi, ili waweze kupata mafanikio mengi ya kuwasaidia katika kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Yahana 21:18.

ENGLISH: “I KNEADED IT UNTIL IT WAS SOFT.”

The origin of this saying is about wheat flour. There was a person who was making wheat flour by kneading it until it was soft enough to be used for baking buns, and bread. That is why he said that, “I kneaded it until it was soft.”

This saying is matched to a person who is hardworking in his life. This person, exerts himself to do his work with great strength and diligence because of his loyalty, when he gets old he gets tired of doing those jobs. He achieves a lot of success in his family because of his diligence in doing his works with great strength, in his life.

This person resembles the one who kneaded wheat flour until it was soft enough to be used for baking buns, and bread, because he also works hard until he achieves a lot of success in his life. That is why he says that, “I kneaded it until it was soft.”

This saying instills in people a clue of being honest and hard working enough to nicely fulfill their responsibilities, so that they can achieve countless successes which can help them in developing their family lives.

John 21:18.

1398. UMUNHU UYU AGIMINYAGA WEYI NG’WINIKILI.

Olihoyi munhu uyo olina nguzu ningi umuchalo ja Ngeme. Umunhu ng’wunuyo abhuchaga miligo midito mpaga oyukoya ugusiminza kunguno ya wihadikija bhokwe bhunubho. Uweyi agayukeleja nose ugumisha kunguno ya bhunoge bho gubhucha miligo midito yiniyo. Hunagwene nose abhanhu bhagayuyomba giki, “umunhu uyu agiminyaga weyi ng’winikili.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agatumamaga milimo midito bho nduhu ugugusatwa umili gokwe. Umunhu ng’wunuyo, agatumamaga milimo midito gwingila diyu mpaga mhindi kunguno ya gukija ugugusatwa umili gokwe gunuyo, umubhutumami bhokwe bhunubho. Uweyi agikalaga anogile bhuli makanza kunguno ya gutumama milimo midimu yiniyo bho nduhu ugugusatwa umili gokwe gunuyo, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo obhuchaga miligo midito mpaga oyukoya ugumisha, kunguno nuweyi agatumamaga milimo midimu mpaga olala anogile, umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagahayaga giki, “umunhu uyu agiminyaga weyi ng’winikili.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza na witegeleja bho guilanhana chiza imimili yabho umubhutumami bho milimo yabho yiniyo, kugiki bhadule gwikala na bhuyegi umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

KISWAHILI: MTU HUYU HUJIUMIZA YEYE MWENYEWE.

Alikuwepo mtu aliyekuwa na nguvu nyingi katika kijiji cha Ngeme. Mtu huyo alikuwa akibeba mizigo mizito mpaka anaanza kutembea kwa shida kwa sababu ya kujilazimisha kubeba mizigo hiyo. Yeye alifikia hatua ya kuchelewa kuamuka asubuhi kwa sababu ya uchovu huo wa kubeba mizigo mizito, katika maisha yake. Ndiyo maana mwishowe watu walisema kwamba, “mtu huyo hujiumiza yeye mwenyewe.”

Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hufanya kazi bila ya kuuhurumia mwili wake, katika maisha yake. Mtu huyo, hufanya kazi nzito kuanzia asubuhi hadi jioni kwa sababu ya kukosa umakini wa kuuhurumia mwili wake huo, katika kazi zake. Yeye huwa ana uchovu kila wakati kwa sababu ya kufanya kazi hizo ngumu bila ya kuuhurumia mwili wake huo, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyebeba mizigo mizito mpaka akaanza kutembea kwa shida, kwa sababu naye hufanya kazi ngumu mpaka analala akiwa amechoka sana, katika maisha yake. Ndiyo maana watu husema kwamba, “mtu huyu hujiumiza yeye mwenyewe.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na umakini wa kuilinda miili yao wanapofanya kazi zao, ili waweze kuishi kwa furaha katika familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 9:21.

Ayubu 3:17.

 

ENGLISH: THIS MAN HURTS HIMSELF.

There was a man who was so strong in the village of Ngeme. He used to carry heavy maize sacks until he started walking with difficulty because of forcing himself to carry those sacks. He reached the point of waking up late in the morning because of the fatigue of carrying those heavy maize sacks, in his life. That is why people said about him that, “this man hurts himself.”

This saying is equated to a person who works without pitying his body, in his life. This person, does heavy works from morning to evening because of the lack of decent attention enough to pity his body, in his works. He is always tired because of doing those hard jobs without pitying his body, in his life.

This person resembles the one who carried heavy maize sacks until he started walking with difficulty, because he also works hard until he goes to bed very tired, in his life. That is why people say about him that, “this man hurts himself.”

This saying instills in people an idea of being watchful enough to protect their bodies while doing their jobs, so that they can live happily in their families, in their lives.

Genesis 9:21.

Job 3:17.

 

 

1391. AGALILAGA ULU WIZA HA WELELO.

Akahayile kenako kingilile kuli ng’wana uyo obyalagwa. Ung’wana ng’wunuyo agalilaga ulu obyalwa kunguno wingilaga muweja umo adamanilile. Uweyi agalombaga wambilijiwa kuli msumbi okwe kunguno wandyaga wikaji bhupya kugiki adule gwikala mhola. Hunagwene abhanhu bhagahaga giki, “agalilaga ulu wiza ha welelo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agalombaga wambilija kuli Mulungu ulu wandyaga nimo gupya umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agandyaga imilimo yakwe imipya bho gunomba Mulungu kunguno ya guzunya gokwe gutale ukubhudula bho Nsumbi okwe, umuwikaji bhokwe. Uweyi apandikaga matwajo mingi umumilimo yakwe imipya yiniyo, kunguno ya kunomba Mulungu aho alandya uguitumama, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu ng’wana uyo agalombaga wambilijiwa kuli nsumbi okwe bho gulila ulu obyalwa, kunguno nuweyi agalombaga wambilijiwa kuli Mulungu ulu alandya uguitumama imilimo yakwe imipya yiniyo, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “agalilaga ulu wiza ha welelo.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya kulomba wambilijiwa kuli Mulungu ulu bhalandya uguitumama imilimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umutumami bho milimo yabho yiniyo, umuwikaji bhobho.

1 Wakorintho 13:11.

KISWAHILI: HULIA ANAPOKUJA DUNIANI.

Msemo huo ulianzia kwa mtoto aliyezaliwa. Mtoto huyo hulia baada ya kuzaliwa kwa sababu ameingia ulimwengu ambamo hajazoea. Yeye huomba msaada kwa muumba wake kwa sababu ameanza maisha mpya kwake ili aweze kuyamudu vizuri. Ndiyo maana watu husema kwamba, “hulia anapokuja duniani.”

Msema huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huomba msaada kwa Mungu anapoanza kazi mpya, katika maisha yake. Mtu huyo, huanza kazi mpya kwa kumuomba Mungu kwa sababu ya imani yake kubwa kwenye uwezo wa Muumba wake maishani mwake. Yeye hupata mafanikio mengi katika kazi zake hizo mpya, kwa sababu ya kumuomba Mungu anapoanza kuzifanya kazi zake hizo, katika maisha yake.

Mtu huyo hufanana na yule mtoto ambaye huomba msaada kwa Muumba wake kwa kulia baada ya kuzaliwa, kwa sababu naye huomba msaada kwa Muumba wake anapoanza kufanya kazi zake hizo mpya, maishani mwake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hulia anapokuja duniani.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuomba msaada kwa Mungu wanapoanza kuyatekeleza majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi katika utendaji wao wa kazi, maishani mwao.

1 Wakorintho 13:11.

 

ENGLISH: HE CRIES WHEN HE COMES INTO THE WORLD.

This saying is originated from a newborn baby. The newborn baby cries after birth because of entering into new world which it is not used to. It asks for help from the creator because of starting a new independent life so that it can nicely cope with it. That is why people say that, “he cries when he comes into the world.”

This saying is associated to a person who asks for help from God when he starts a new job, in his life. Such person, starts a new job by asking God because of his great faith in the power of his Creator in his life. He achieves great success in his new jobs, because of depending on God when he starts doing them, in his life.

This person resembles the child who asks for help from his Creator by crying after birth, because he also asks for help from his Creator when he starts doing new jobs, in his life. That is why people say to him that, “he cries when he comes into the world.”

This proverb teaches people about asking God for help when they begin to carry out their duties, so that they can achieve great success in their lives.

1 Corinthians 13:11.