Author: Sukuma legacy

1208. ULIGALINZULA YAKI INGOB’O YA NKWILIMA?

Imbuki ya kahayile kenako ilolile Nkwilima na nina bhukwi okwe. Unina bhukwi ng’winuyo, goli ngilo ugwidima ingob’o ya nkwilima okwe. Aliyo lulu umayu ng’wunuyo, agandya guidimagula ingob’o ya nkwilima okwe ng’winuyo. Hunagwene abhanhu bhagamuja giki, “uligalinzula yaki ingob’o ya nkwilima?”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo alinibhengwe ukubhanhu abho agikalaga nabho, aha kaya yakwe. Umunhu ng’wunuyo, alina bhutoshi bho gubhadalaha abhanhu bhakwe kunguno ya gwibhona giki aliosolobho nhale gukila abhiye, umuwikaji bhokwe. Uweyi agaikenakulaga ikaya yakwe kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho ubho gubhitila libhengwe abhiye, aha kaya yakwe.

Umunhu ng’wunuyo, akikolaga nu nina bhukwi uyo agaminzila ikujo unkwilima okwe bho guidimagula ingob’o yakwe, kunguno nuweyi agabhabhinzila ikujo abhanhu bhakwe bho gubhitila libhengwe, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagamujaga giki, “uligalinzula yaki ingob’o ya nkwilima?”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya kubhiza ni kujo ukubhichabho bho ndugu ugwisendeja lwande lumo ijinagufunya bhuyanguji, kugiki bhadule kujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

1Petro 2:17a.

1Yohana 3:11.

1Yohana 4:11-12.

KISWAHILI: UNAIPEKUA YA NINI NGUO YA MKWILIMA?

Chanzo cha msemo huo chaangalia Mkwilima na mama mkwe wake. Mama mkwe huyo, ilikuwa ni mwiko kuishika nguo ya mkwilima wake. Lakini mama huyo, alianza kuishikashika nguo hiyo ya mkwilima wake huyo. Ndiyo maana watu walimuuliza kwamba, “unaipekua ya nini nguo ya mkwilima?”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ana dharau kwa watu wale anaoishi nao, katika maisha yake. Mtu huyo, ana majivuno ya kuwadharau watu wake hao kwa sababu ya kujiona kuwa yeye ana thamani kubwa zaidi kuliko hao wenzake, maishani mwake. Yeye huivuruga familia yake hiyo kwa sababu ya majivuno yake hayo ya kuwafanyia dharau wenzake, katika familia yake.

Mtu huo, hufanana na yule mama mkwe aliyemvunjia heshima mkwilima wake kwa kuishikashika nguo yake, kwa sababu naye huwavunjia heshiwa watu wake kwa kuwadharau, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuuliza kwamba, “unaipekua ya nini nguo ya mkwilima?”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na heshima kwa watu wote bila ya kuwafanyia dharau kwa kuegemea upande mmoja, katika utoaji wa maamuzi, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

1Petro 2:17a.

1Yohana 3:11.

1Yohana 4:11-12.

 

ENGLISH: WHY ARE YOU SEARCHING THE CLOTHES OF THE SON IN LAW?

The cradle of the above saying is about a mother in law who touched clothes of her son-in-law. The mother-in-law was a taboo to hold clothes of her son in law. But she started holding the clothes of her son in law. That is why people asked her that, “Why are you searching the clothes of the son in law?”

This saying is compared to a person who has contempt for people whom he lives with in his life. Such person is proud enough to look down on his people because he thinks that he has more value than his colleagues in his life. He disturbs his family because of his pride in disrespecting his colleagues.

This person is similar to the mother-in-law who dishonored her son in law by grabbing his clothes, because he also dishonored his people by disrespecting them in his life. That is why people ask him that, “Why are you searching the clothes of the son in law?”

This saying teaches people about having respect for all people without insulting them by leaning on one side, in making decisions, so that they can raise their families well, in their lives.

1 Peter 2:17a.

1 John 3:11.

1 John 4:11-12.

 

man-5966217_1280

1207. KALAGU  –  KIZE.ONKONDYA BHULI UNKWILIMA? – LUSHINGE.

Imbuki ya kalagu yiniyo, ililola lushinge ulo luli na milimo mingi. Ulushinge lunulo, lugatumamilagwa bhuli makanza bho kumanusumila myenda kihamo nu bhudololo bholo. Huna gwene lugalenganijigwa kuli nkwilima kunguno ya wei gumanutumama milimo mingi bhuli makanza niyo bho nduhu ugucha isoni. Uweyi nulu agatung’wa ungi agifunyaga ogagutumama unimo uyo gohayiyagwa mpaga nose agakondaga obhiza guti lushinge. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga bho gubhuja giki, “onkondya bhuli umkwilima? – Lushinge.”

Ikalagu yiniyo, ikalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhalekanijaga bhiye uguyitumama imilimo ya ha kaya yakwe, mpaga nose bhakonda, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, adabhasadagwa abhatumami bha milimo yakwe yiniyo, kunguno ya gwiiganika weyi duhu bho nduhu ugubhadilila abhanhu bhakwe bhenabho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agabhapambulaga nose abhageni uja aha kaya  yakwe kunguno ya gubhalubhya bho gutumama milimo midimu ulu bhangeniha chiniko a haka kaya yake yiniyo.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo agantumamya milimo umkwilima okwe mpaga ukonda guti lushinge, kunguno nuweyi agabhatumamyaga milimo abhanhu bhake mbaga bhakonda bho nduhu ugubhadilila, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanbu bhagamujaga giki, “onkondya bhuli umkwilima? – Lushinge.”

Ikalagu yiniyo, yalanga bhanhu higulya ya gwiyambilija gutumama milimo yabho kihamo bho nduhu ugwilekanija, kugiki bhadule kupandika sabho ningi umukaya jabho.

Waebrania 13:1-3.

1 Petro 1:22.

Yohane 13:34.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

KWA NINI UMEMKONDESHA MKWILIMA? – SINDANO.

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia Sindano inayotumika kwa kufanya kazi nyingi. Sindano hiyo, hutumiwa kwa kushonea nguo na magodolo pamoja na wembamba wake huo.

Ndiyo maana watu huifananishwa Sindano hiyo na mkwilima kwa sababu naye hufanya kazi nyingi kila wakati, bila hata ya kuona aibu. Yeye hujitolea kufanya kazi hata zile ambazo ni za wengine, mpaga mwishowe hukonda kutokana na mateso ya kufanya kazi nyingi hizo. Ndiyo maana watu huhadithiana kwa kuulizana kwamba “kwa nini umemkondesha mkwilima? – Sindano.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hutegea kufanya kazi kwa kuwaachia wengine kazi za kwenye familia yake, mpaga mwishowe watu wake hao hukonda. Mtu huyo, huwa hawaonei huruma wafanya kazi wake hao, kwa sababu ya kujijali yeye mwenyewe tu bila ya kuwajali watu wake hao, maishani mwake. Yeye huwaogopesha hata wageni wake kumtembelea katika familia yake kwa sababu ya kuwafanyisha kazi nyingi na ngumu kila wanapomtembelea, kwenye familia yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyemtumikisha kazi mkwilima wake mpaka akakonda kama Sindano, kwa sababu naye huwafanyisha kazi ngumu watu wake mpaka wanakonda bila hata ya kuwajali wake hao. Ndiyo maana watu, humuuliza kwamba, “kwa nini umemkondesha mkwilima? – Sindano.”

Kitendawili hicho, huwafundisha watu juu ya kufanya kazi zao kwa ushirikiano wa pamoja bila ya kutegea kwa kuwaachia wenzao, ili waweze kupata mafanikio ya kupata mali nyingi, katika familia zao.

Waebrania 13:1-3.

1 Petro 1:22.

Yohane 13:34.

 

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

WHY DID YOU MAKE THIN THE SON IN LAW? – NEEDLE.

The foundation of this paradox looks at the Multitasking Needle. The needle is used for sewing clothes and mattresses with its thinness.

That is why people liken it to a son in law who he does a lot of works all the time, without even feeling ashamed. He dedicates himself to work even those that belong to others to the point of losing weight at the end due to the suffering of doing so many jobs. That is why people talk to each other by asking “why did you make thin the son in law?” – Needle.”

This riddle is compared to a person who relies on working by leaving the works in his family to others, but in the end, those people become weak. That person does not feel sorry for his workers, because he only cares about himself without caring about his people in his life. He even scares his guests to visit him in his family because he makes them do a lot of hard works every time when they visit him, in his family.

This person is similar to the one who made his son in law work until he was as thin as a needle, because he also makes his people work hard until they become thin without even caring about them. That is why people ask him that, “why did you make thin the son in law?” – Needle.”

This riddle imparts in people an idea of doing their works in cooperation without relying on others, so that they can achieve success in getting more wealth in their families.

Hebrews 13:1-3.

1 Peter 1:22.

John 13:34.

 

 

african-3416695_1280

1206. KALAGU – KIZE. MUMO UGANENGELA UDUNASA UNG’WANA NG’WUNUYO – BHUNYENYA.

Imbuki ya kalagu yiniyo ililola kabhunyenya ako kali kadoo noyi nulu ugiyina kugalasa udukadula kunguno ya bhudoni bhogo bhunubho. Ubhunyenya bhunubho  bhuli bhudodo aliyo bhukikalaga bhunoyi noyi ugubhulya. Ukwene huguhaya giki, iginhu jigikalaga na solobho yajo mumho jigadohela. Hunagwene abhanhu bhagiganilaga giki, “mumo uganengela udunasa ung’wana ng’wunuyo – kabhunyenya.”

Ikalagu yuniyo, igalenganijiyagwa kuli munhu uyo agabhadahalaga abhanhu kunguno ya bhudoni bho mimili yabho umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo adaibhonaga isolobho ya bhanhu abho bhali hasilili yakwe, kunguno ya libhengwe yakwe linilo umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga uguyibheja chiza ikaya yakwe kunguno ya gubhadalaha sagala abhanhu bhakwe bhenabho, aha kaya yakwe yiniyo.

Umunhu ng’wunyo, agikolaga nuyo abhudalaha ubhunyenya bho gulola bhudoni bhobho, kunguno nu weyi agabhadalahaga abhanhu abho bhali hasilili yakwe, umuwikaji bhokwe mpaga oduma uguibhona isolobho yabho, aha kaya yakwe yiniyo. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “mumo uganengela udunasa ung’wana ng’wunuyo – kabhunyenya.”

Ikalagu yiniyo yalanga bhanhu higulya ya kuleka libhengwe lya gubhadalaha sagala abhanhu abho bhali hasilili yabho, kugiki bhadule kupandika matwajo mingi umubhutumami bho milimo yabho, umukaya jabho.

Marko 4:30-32.

1Wakorintho 1:27-28.

KISWAHILI: KITENDAWILI – TEGA.

HATA UJITAHIDI KUMLENGA KWA MSHALE NAMNA GANI MTOTO HUYO HUTAMPIGA – UFUTA.”

Chanzo cha kitendawili hicho, chaangalia ufuta ambao ni mdogo sana. Ufuta hata mtu ajitahidi kuulenga kwa mshale ili aupige hataweza, kwa sababu ya udogo wake huo. Wenyewe ni mdogo lakini ni mtamu kwa kuula. Ndiyo kusema kwamba, kitu hata kikiwa kidogo namna gani, kinafaida yake katika maisha ya mwanadamu. Ndiyo maana watu huhadithiana kwamba, “hata ujitahidi kumlenga kwa mshale namna gani mtoto huyo hutampiga – ufuta.”

Kitendawili hicho, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huwadharau watu walioko chini yake kwa sababu ya udogo wa miili yao. Mtu huyo, huwa haioni faida ya watu walioko chini yake, kwa sababu ya dharau aliyo nayo kwao, maishani mwake. Yeye hushindwa kuilea vyema familia yake kwa sababu ya kuwadharau hovyo watu waliopo kwenye familiya yake hiyo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliudahau ututa kwa kuangalia udogo wa umbo la zao hilo, hata akashindwa kuona faida yake, kwa sababu naye huwadharau watu walioko chini yake mpaga anashindwa kuona faida yao kwenye familia yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “hata ujitahidi kumlenga kwa mshale namna gani  mtoto huyo hutampiga – ufuta.”

Kitendawili hicho, hufundisha watu juu ya kuacha kuwadharau hovyo watu walioko chini yao, ili waweze kupata mafanikio mengi katika utekelezaji wa majukuku yao, katika familia zao.

Marko 4:30-32.

1Wakorintho 1:27-28.

ENGLISH: I HAVE A RIDDLE – LET IT COME.

EVEN IF YOU TRY TO TARGET WITH AN ARROW YOU WILL NOT HIT THAT CHILD – SAMSAM.

The basis of this paradox looks at a very small crop which is known as samsam. Even if someone tries to aim at it with an arrow, he will not be able to hit it, because of its small size. They themselves are small but they are sweet to eat. That is to say that, no matter how small something is, it is useful to human life. That is why people tell each other that, “even if you try to target with an arrow, you will not hit that child – Samsam.”

This puzzle is equated to a person who despises people who are under him because of smallness of their bodies. Such person never sees benefit of people who are under him, because of a contempt that he has to them, in his life. He fails to raise his family well because of his carelessness to his people.

This person relates to the one who underestimated the small size of that small crop, until he failed to see its benefit, because he also despises the people who are under him to the point of failing to see their benefit in his family. That is why people tell him that, “even if you try to target with an arrow, you will not hit that child – Samsam.”

This riddle teaches people about stopping belittling the people who are under them, so that they can achieve a lot of success in raising their children, in their families.

Mark 4:30-32.

1 Corinthians 1:27-28.

family-2563889_1280

mother-and-daughter-668167_1280

woman-1320103_1280

1205. VIDEO OF TLRS FROM NDELELEJI RESEARCH GROUP

YOU INVITED TO WATCH THE NDELELEJI RESEARCH GROUP  VIDEO BY CLICKING THE LINK BELOW:Waimbaji waliomo kwenye video hiyo hapo juu, ni wanakikundi cha utafiti kinachoitwa Traditional Legacy Research Society (TLRS), chenye makao makuu yake Mkoani Shinyanga, kwenye wilaya ya Kishapu, katika parokia ya Ndoleleji. Kikundi hicho, kilianzishwa na marehemu Pd. Donald Sybertz, MM, (ng’wanahelena). Aliitwa Ng’wanahelena kwa heshima ya mama mazazi wake ambaye ni HELENA, wakimaanisha kwamba yeye ni mtoto wa Helena. Mmisionari huyo wa shirika la Maryknoll, alifanya kazi ya kuhubiri Injili kwa miaka zaidi ya hamsini katika jimbo la shinyanga. Alitumia zaidi lugha ya kisukuma, katika kuongea na wazee, na wanavikundi mbalimbali, kwa upendo na bidii ya hali ya juu sana, kwa lengo la kuifikisha vizuri habari njema wa watu hao aliopenda sana mmisionari huyo. Wimbo huo, ni kuombeleza kifo chake na kumuombea kwa Mungu, ili Mungu amuweke mahali pema peponi, apumzike kwa amani na kuufurahia uzima wa milele. 

(The singers in the above above are members of a research group which is called Traditional Legacy Research Society (TLRS), with its headquartered in Shinyanga Region, in Kishapu district, at Ndoleleji parish. The group was founded by the late Pd. Donald Sybertz, MM, (Ng’wanahelena). He was called Ng’wanahelena in honor of his mother whose name is HELENA, meaning that he is the son of Helena.  He is the missionary of the Maryknoll society who worked hard in preaching the Gospel for more than fifty years in Shinyanga diocese. He mostly used the Sukuma language in speaking to elders, and members of various groups, with love and diligence of a very high level, with the aim of conveying the good news of Jesus to those people whom the missionary loved so much. The singers pray for his death and to pray for him, so that God may welcome him in heaven enough to rest in peace and enjoy eternal life.)

Wimbo unaofuata umeimbwa na wanakikundi cha utafiti cha Ndoleleji, kilichoanziswa na Marehemu Padri Donald Sybertz, MM. Kikundi hicho kwa sasa kinaitwa Traditional Legacy Research Socierty (TLRS). Wimbo huo unahusu maisha ya mbinguni ya watu wanaotenda mema hapa duniani. Unatualika kutenda mema ili tuweze kuyapata maisha hayo ya Mbinguni baada ya kuaga dunia. Unaeleza kwamba wale watendao maovu watapata mateso yakuchomwa moto. Waimbaji wanamuomba Yesu mwana wa Maria awasaidie kumshinda shetani ili waendelee kutenda mema mpaka waupate uzima wa milele mbinguni baada ya maisha haya. (the following song has been sung by members of the Ndoleleji research group that was started by the late Father Donald Sybertz, MM. The group is currently called the Traditional Legacy Research Society (TLRS). This song is about the heavenly life of people who do good on earth. It invites us to do good so that we can find that life in Heaven after passing away. It also explains that those who do evil will suffer the torment of being burned. The singers ask to Jesus, the son of Mary, to help them enough to defeat the devil so that they can carry on doing good until they find eternal life in heaven after this life.

VIDEO

1204. SHOGAGA NIGINI

Akahayile kenako kahoyelile higulya ya guwilwa nigini gushaga uko wikalo bhokwe. Ulihoyi nigini uyo agaja Shinyinga aliganika giki agujupandika wikaji bho wiza koyi. Ohayugashika koyi uyupandika makoye ga gugayiwa ijiliwa pye ni jizwalo. Abhiye abho agabhaleka ukuchalo jakwe, bhaganchola mpaga bhumhona na gumana umo okoyelelaga. Hunagwene bhagang’wila giki, “shogaga nigini.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kubhabyaji abho bhagabhashoshaga mulilange lya wiza abhana bhabho abho bhagalilekaga bho gubhadililaga chiza, umuwikaji bhobho. Abhabyaji bhenabho bhagabhadililaga abhana bhabho bhenabho bho gwikala nabho chiza, mpaga bhalidebha ililange lya gwikala na bhanhu chiza. Abhoyi bhagabhakujaga bho lilange liza abhana bhenabho bho gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Abhabyaji bhenabho bhagalenganijiyagwa kubhanigini abho bhaganchola ng’wichabho uyo upandikaga makoyi Shinyinga mpaga bhumpandika na gung’wila ashoke kaya, kunguno nabhoyi bhagabhashoshaga abhana abha nhungwa jabhubhi, bho kubhalanga nhungwa jawiza, umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagabhawilaga giki, “shogaga nigini.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gubhalanga ilange lya wiza abhichabho abha nhungwa jabhubhi, bho gwikala labho chiza, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Waefeso 6:4.

Methali 22:26.

1Thimotheo 5:10.

KISWAHILI: RUDI MTOTO.

Msemo huo, huongelea juu ya mtoto alieambiwa arudi kwenye makazi yake. Alikuwepo mtoto mmoja aliyeenda Shinyanga mjini akifikiri kwamba atapata maisha mazuri huko. Alipofika kule alianza kupata matatizo ya kukosa chakula na mavazi. Wenzake alioowaacha kijijini mwake, walimtafuta mpaka wakamuona na kufahamu alivyokuwa akihangaika. Ndiyo maana walimwambia kwamba, “rudi mtoto.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa wazazi wale ambao huwarudisha kwenye malezi mema watoto wao waliokiuka maadili yao kwa kuwajali vizuri maishani mwao. Wazazi hao, huwajali watoto hao hao kwa kuishi nao vizuri, mpaga wanaweza kuyaishi maadili yao vizuri. Wao huwakuza vizuri watoto wao hao kwa kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.”

Wazazi hao, hulinganishwa kwa watoto wale waliomjali mwenzao kwa kumtafuta na kumwambia arudi kwake, kwa sababu nao huwarudisha watoto wao waliokiuka malezi mema, kwa kuwalea vizuri. Ndiyo maana huwaombia kwamba, “rudi mtoto.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwalea wenzao katika maadili mema kwa kuishi nao vizuri, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Waefeso 6:4.

Methali 22:26.

1Timotheo 5:10.

ENGLISH: COME BACK CHILD.

This saying speaks of a child who was told to return to his home. There was one child who went to Shinyanga town thinking that he would have a good life there. When he got there, he started having problems such as lack of food and clothing. His friends, whom he left in his village, looked for him until they saw him and realized that he was facing problems. That is why they told him that, “come back child.”

This saying is compared to parents who return their children who have violated their values to a good upbringing by taking good care of them in their lives. These parents, take care of those children by living well with them within their values. They raise their children well by raising their families well, in their lives.

These parents are compared to children who cared for their partner by looking for him and telling him to return back to his home, because they also bring back their children who violated good upbringing, by raising them well. That is why the tell them, “come back child.”

This saying, teaches people about raising their people in good values by living well with them, so that they can raise their families well, in their lives.

Ephesians 6:4.

Proverbs 22:26.

1 Timothy 5:10.

child-2428546__480