Author: Sukuma legacy

1228. KOLAGA BHUGILIMILAGA UKO ALIJA.

Olihoyi munhu uyo omanaga usamila muchalo jingi ijo bhaponaga jiliwa abhanhu. Umunhu ng’wunuyo, obhizaga giki, ulu ogakela uko chalo ijo osamilaga jinijo osamilaga kuchalo jingi hangi uko wigwaga giki bhaponile ijiliwa. Uweyi okelaga ijiliwa kunguno ya gukija uguidilila chiza imigunda iyo oilimaga bho guilimila ingese pye iyose. Hunagwene abhanhu bhagaiwila giki, “kolaga bhugilimilaga uko alija.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu ngokolo ugutumama imilimo yakwe, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunyo, agalimaga migunda yakwe okija ugumala uguilimila ingese kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agikalaga ukoya na nzala aha kaya yakwe yiniyo, kunguno ya bhugokolo bhokwe bhunubho, ubhoguduma uguilimila pye ngese ya mumigunda yakwe, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo okelaga ijiliwa osamila muchalo jingi, ijo bhaponaga, kunguno nuweyi agalimaga imigunda yakwe oduuma uguilimila ingese pye iyose, umuwikaji bhokwe. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “kolaga bhugilimilaga uko alija.”

Akahayile kenako, kalanga bhanhu higulya ya gwigulambija gutumama milimo yabho bho bhukamu bhutale, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umukaya jabho.

Methali 27: 11-15.

Mhubiri 10:18.

KISWAHILI: KWANI PALIZI HUJIPALILIA ANAKOENDA!

Alikuwepo mtu ambaye alikuwa akihamia kwenye kijiji walichopata chakula vizuri kwa mwaka huo. Mtu huyo, alikuwa akikosa chakula kwenye kijiji hicho kwa mwaka huo alihamia kwenye kijiji kingine alichosikia kuwa watu wake walipata mazao mengi ya chakula. Yeye alikuwa akikosa chakula katika familia yake kwa sababu ya kutoyatunza vizuri mashamba yake aliyoyalima kwa kuipalilia palizi mpaka kuimaliza. Ndiyo maana watu walisema juu yake kwamba, “kwani palizi hujipalilia anakoenda!

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ni mvivu kufanya zake, katika maisha yake. Mtu huyo, hulima mashamba ya chakula na kuacha bila kuyapalilia palizi kwa sababu ya uvivu wake huo, maishani mwake. Yeye alikuwa akihangaika na tatizo na njaa katika familia yake hiyo, kwa sababu ya uvivu wake huo, wa kushindwa kupalilia palizi yote ya kwenye mashamba yake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyekosa chakula katika kijiji chake na kuhamia kwenye kijiji kingine, ambacho wakazi wake walipata chakula, kwa sababu naye hukosa chakula kwa hulima mashamba na kuyaacha bila kuyapalilia palizi zake, maishani mwake. Ndiyo maana watu huongea juu yake kwamba “kwani palizi hujipalilia anakoenda!

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kujibidisha kufanya kazi zao kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao, maishani mwao.

Methali 27: 11-15.

Mhubiri 10:18.

ENGLISH: DOES IT MEAN THAT WEEDS ARE WED BY THEMSELVES WHERE HE IS GOING!

There was a person who was moving to a village where they had good food in that year. This man lacked food in his village in that year. Then he moved to another village where he heard that his people got a lot of food crops. He was lacking food in his family because of not taking good care of his cultivated fields. He did not finish weeding them. That is why people said about him that, “does it mean that weeds are wed by themselves where he is going!”

This saying is compared to a person who is lazy in doing his own works, in his life. That person, cultivates food fields and leaves without weeding them because of his laziness. He was struggling with problems and hunger in his family, because of his laziness, of not being able to weed all the weeds in his fields.

This person resembles the one who lacked food in his village and moved to another village where its inhabitants got food, because he also lacks food because he cultivates the fields and leaves them without weeding his weeds, in his life. That is why people talk about him that “does it mean that weeds are wed by themselves where he is going!”

This saying imparts in people an idea about forcing themselves to do their works with great effort, so that they can get a lot of success, in their families.

Proverbs 27: 11-15.

Ecclesiastes 10:18.

hope-3467922__480

1227. PANDULAGA MIHAYO.

Oliyohi munhu uyo uyombaga mihayo yakwe bho lilaka lidoni umumahoya gakwe. Umunhu ng’wunuyo, wikalaga muchalo ja bhanhu bhingi abho bhadumaga uguigwa chiza imihayo yakwe yiniyo kunguno ya guiyomba bho lilaka lidoni, umumahoya gakwe genayo. Hunagwene abhanhu bhenabho, bhagang’wila giki, “pandulaga mihayo.”

Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agayombaga mihayo bho guyigondya, umukikalile kakwe kenako. Umunhu ng’wunuyo, adaiyigololaga chiza umihayo ya mumahoya gakwe genayo, kunguno ya gubhisa ginhu ijo agikalaga adahayile igiki abhiye bhajimane, umuwikaji bhokwe bhunubho. Uweyi agadumaga ugubhalela chiza abhanhu bha aha kaya yake kunguno ya guduma guigolola chiza imihayo ya mumahoya yakwe genayo, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo oyombaga mihayo yakwe bho lilaka lidoni, kunguno nuweyi agayomba mihayo yakwe bho nduhu uguigolola chiza, umumahoya gakwe genayo, aha kaya yakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “pandulaga mihayo.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higlya ya guyomba bhunhana bho guigolola chiza imihayo ya mumahoya yabho, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho bhunubho.

Mathayo 10:16.

Luka 12:2-3.

KISWAHILI: PASUA MANENO.

Alikuwepo mtu aliyekuwa akiongea maneno yake kwa sauti ndogo katika maongezi yake. Mtu huyo, aliishi kwenye kijiji cha watu wengi, ambao walishindwa kuyasikia vizuri maneno yake kwa sababu ya kuyaongea kwa kutumia sauti ndogo. Ndiyo maana watu hao walimwambia kwamba, “pasua maneno.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye huongea maneno yake kwa kuyapindisha, katika maisha yake. Mtu huyo, huwa hayanyoshi vizuri maneno yake hayo, kwa sababu ya kuficha kitu fulani ambacho huwa hataki watu wengine wakielewe, maishani mwake. Yeye hushindwa kuiendeleza vizuri familia yake kwa sababu ya yeye kushindwa kuyanyoosha vizuri maneno yake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyesema maneno yakwe kwa sauti ndogo mpaka wenzake wakashindwa kuyasikia, kwa sababu naye huongea maneno bila kuyanyosha vizuri mpaka watu wanashindwa kuyaelewa vizuri, katika maongezi yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “pasua maneno.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kusema ukweli kwa kuyanyosha vizuri maneno yao, katika maongezi yao, ili waweze kuzilea vyema familia zao, maishani mwao.

Mathayo 10:16.

Luka 12:2-3.

ENGLISH: BREAK THE WORDS.

There was a man who was speaking words in a low voice in his speech. Such person lived in a village of many people who failed to hear his words properly because he spoke them in a low voice. That is why those people told him that, “break the words.”

This saying is likened to a person who speaks his words by twisting them, in his life. Such person does not speak correctly his words, because he hides something that he does not want other people to understand, in his life. He fails to develop his family properly because of failing to properly stretch his words, in his life.

This person is similar to the one who said his words in a low voice until his colleagues could not hear them, because he also speaks words without stretching them properly until people are unable to understand them properly, in his speech. That is why people tell him that, “break the words.”

This saying teaches people about telling the truth by stretching their words properly, in their speech, so that they can raise their families well, in their lives.

Matthew 10:16.

Luke 12:2-3.

old-3391298_1280

1226. WIZUKA NG’WENDA GWA GWIKUMBA IKANZA WELAGA.

Oliyohi munhu uyo wikalaga muchalo jilebhe. Umunhu ng’wunuyo, agingila gulala umuchumba jakwe ukija ugwikumba ung’wenda mpaga wela aliyo imbeho yali nhali noyi. Uweyi akalala mpaga wela ubhujiku na wizuka gwikumba ng’wenda gokwe kunguno ya wiyibhu bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “wizuka ng’wenda gwa gwikumba ikanza welaga.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu ngosha uyo odila gutola nose unamhala na wiganika mhayo gwa gutola, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, wiganikaga mihayo yingi habhuyanda bhokwe mpaga nose unamhala na wandya gwiganika mhayo gwa gutola, kunguno ya gudilila milimo iyo idinasolobho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agadumaga ugubhuyegela ubhutoji bhokwe kunguno ya wiyibhu bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, akikolaga nuyo agiyibha gwikumba ng’wenda mpaga wela ubhujiku na wizuka ugugwikumba ung’wenda gunuyo, kunguno nuweyi igiyibha ugutola mpaga nose unamhala na wizuka gutola, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “wizuka ng’wenda gwa gwikumba ikanza welaga.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gwanguha gutumama milimo yabho iyasolobho bho gwigulambija na bhukamu bhutale ahikanza lya milimo yabho linilo, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi, umuwikaji bhobho.

Yoshua Bin Sira 25:3.

KISWAHILI: UMEKUMBUKA SHUKA YA KUJIFUNIKA WAKATI KUMEKUCHA.

Alikuwepo mtu aliyekuwa akiishi kwenye kijiji fulani. Mtu huyo, aliingia chumbani mwake kulala bila kujifunika shuka wakati baridi ilikuwa kali sana. Yeye alilala mpaka asubuhi ndipo akakumbuka kujifunika shuka kwa sababu ya usahaurifu wake huo. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umekumbuka shuka ya kujifunika wakati kumekucha.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mwanamume yule aliyechelewa kuoa mpaka akazeeka ndipo akafikiria kuoa, katika maisha yake. Mtu huyo, alikuwa akifikiria mambo mengine wakati wa ujana wake mpaka akazeeka ndipo akaanza kufikiria kuoa, kwa sababu ya kujali mambo yasiyo na faida, maishani mwake. Yeye alishindwa kuifurahia ndoa yake hiyo kwa sababu ya kujisahau kwake huko, wakati wa ujana wake, katika maisha yake hayo.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejisahau kujifunika shuka wakati wa baridi kali, mpaka asubuhi ndipo akakumbuka kujifunika, kwa sababu naye alijisahau kuoa mpaka akazeeka, ndipo akakumbuka kuoa, maishani mwake. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “umekumbuka shuka ya kujifunika wakati kumekucha.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuwahi kuyatekeleza majukumu yao ambayo ni muhimu kwa bidii kubwa unapofika wakati wake, ili waweze kuyafikia malengo yao vizuri na kupata mafanikio mengi, maishani mwao.

Yoshua Bin Sira 25:3.

ENGLISH: YOU HAVE REMEMBERED THE SHEET TO COVER YOURSELF WHEN IT WAS MORNING.

There was a man who lived in a certain village. He went into his room to sleep without covering himself with a sheet when it was very cold. He slept until morning then he remembered to cover himself with a sheet because of his forgetfulness. That is why people told him that, “you have remembered the sheet to cover yourself when it was morning.”

This proverb is related to the man who delayed marrying until he was old and then he thought about marrying, in his life. Such man was thinking about other things during his youth until he got old and then he started thinking about getting married, because he cared about useless things in his life. He failed to enjoy his marriage because of his self-forgetfulness there, during his youth, in his life.

This is like the one who forgot to cover himself with a sheet during the cold winter, until morning then he remembered to cover himself, because he also forgot to marry until he was old, then he remembered to marry, in his life. That is why people told him that, “you have remembered the sheet to cover yourself when it was morning.”

This proverb imparts in people an idea of carrying out their duties which are important with great effort when the time comes, so that they can achieve their goals well and achieve many successes in their lives.

Joshua Bin Sira 25:3.

girl-347850_1280

1225. DAGELALA GUBHONA KALYETO DUHU.

Bhalihoyi bhanhu abho bhalibhaja gujunlola ngeni uyo obhitilaga umuchalo jabho. Abhanhu bhenabho bhagaduma ugumona na gundebha chiza ungeni ng’wunuyo, kunguno agabhita wangu wangu aho bhasangwa bhiyebhaga. Hunagwene bhagayomba giki, “dagelela gubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kubhanhu abho bhagiyebhaga ugutumama imilimo yabho, umukikalile kabho. Abhanhu bhenabho, bhagajaga ugujutumama imilimo yabho bhagalendela yingi duhu iyo idina solobho kunguno ya wiyebhu bhobho bhunubho, umubhutumami bho milimo yabho. Abhoyi bhagakelaga bhuli ng’waka umukaya jabho kunguno ya gwiyebha kutumama milimo yabho yiniyo, bho gulendela yingi iyo idina solobho yoseyose, umuwikaji bhobho.

Abhanhu bhenabho, bhagikolaga nabho bhagaja gujunola ngeni bhugiyebha mpaga ubhita bhadamonile chiza, kunguno nabhoyi bhagajaga ugutumama imilimo yabho bhagiyibha bho gulendela iyo idina solobho yoseyose umuwikaji bhobho. Hunagwene bhagayombaga giki, “dagelega kubhona kalyeto duhu.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka gwiyebha gutumama milimo yabho bho gwigulambija guitumama na bhukamu bhutale, kugiki bhadule kupandima matwajo mingi, umukaya jabho.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

KISWAHILI: TUMEKOMEA KUONA NUSU TU.

Walikuwepo watu walioenda kumuona mgeni aliyekuwa akipita katika kijiji chao. Watu hao, hawakuweza kumuona na kumfahamu vizuri mgeni huyo kwa sababu yeye alipita haraka wakati wao wakiwa wamejisahamu. Ndiyo maana walisema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa watu wale ambao hujisahau kufanya kazi zao, katika maisha yao. Watu hao, huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote kwao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko, katika utekelezaji wa majukumu yao. Wao hukosa chakula kila mwaka kwenye mashamba yao, kwa sababu ya kujisahamu kwao huko kufanya kazi zao, maishani mwao.

Watu hao, hufanana na wale walioenda kumuona mgeni wakajisahau na kukomea kumuona nusu, kwa sababu nao pia huenda kufanya kazi zao na kupoteza muda wao kwa kujali vitu visivyo na faida yoyote, maishani mwao. Ndiyo maana wao husema kwamba, “tumekomea kuona nusu tu.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuacha kujisahau katika kuyatekeleza majukumu yao kwa kujibidisha kuzifanya kazi hizo kwa bidii kubwa, ili waweze kupata mafanikio mengi, katika familia zao.

Habakuki 1:11.

Luka 19:1-3.

ENGLISH: WE HAVE ONLY SEEN HALF.

There were people who went to see a stranger who was passing through their village. Those people could not see and get to know the stranger well because he passed quickly while they were busy. That is why they said that, “we have only seen half.”

This saying is compared to people who forget to do their works, in their lives. Those people go to do their works by wasting their time caring about things that are of no benefit to them, because of their self-indulgence in the implementation of their duties. They lack food every year in their fields, because of their indulgence in doing their works, in their lives.

Those people are like those who went to see a stranger and forgot themselves by wasting their time in useless things until they ended up seeing him only half way, because they also go to do their works and waste their time worrying about things that have no benefit in their lives. That is why they say that, “we have only seen half.”

This saying imparts in people an idea of stopping from wasting their time in useless things themselves enough to carry out their responsibilities by forcing themselves to do those tasks with great effort, so that they can get a lot of success, in their families.

Habakkuk 1:11.

Luke 19:1-3.

africa-5274086_1280

 

 

 

1224. BHUYENZE BHUDIZILAGA KULI MUNHU UWENE KU NDIMU DUHU.

Olihoyi munhu uyo wihayaga giki alina bhuyenze. Umunhu ng’wunuyo, wilenganijaga na Ndimu guti Shimba kunguno oliadamanile akalekanije ka munhu ni ndimu. Aliyo lulu, indimu jilina bhuyenze lelo umunhu atina bhuyenze. Hunagwene abhanhu bhagang’wila giki, “bhuyenze bhudizilaga kuli munhu uwene ku ndimu duhu.”

Ulusummo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo adadebhile ugwikala chiza na bhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga abhadalahile abhanhu bha aha kaya yakwe guti giki bhadi bhanhu kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho, umuwikaji bhokwe. Uweyi agaikenagulaga ikaya yakwe bho guduma uguilela chiza kunguno ya bhudoshi bhokwe bhunubho ubho gumana ubhakalihila sagala abhiye, umukikalile kakwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga nuyo wilenganijaga na Shimba, kunguno nuweyi agaikenagulaga sagala ikaya yakwe bho gumana ubhakalihila sagala abhiye guti giki bhadibhanhu, umukikalile kakwe kenako. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “bhuyenze bhudizilaga kuli munhu uwene ku ndimu duhu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya gudebha gwikala chiza na bhichabho bho guleka gubhakalihila sagala abhichabho bhenabho, kugiki bhadule kujibheja chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Mwanzo 1:24-26.

KISWAHILI: MANYOYA HAYAOTI KWA MTU ILA KWA WANYAMA TU.

Alikuwepo mtu aliyejisema kuwa ana manyoa. Mtu huyo, alikuwa akijifananisha na wanyama kama simba kwa sababu hakujua tofauti ya mtu na wanyama. Lakini basi, wanyama wana manyoa bali mtu hana manyoa. Ndiyo maana watu walimwambia kwamba, “manyoya hayaoti kwa mtu ila kwa wanyama tu.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hafahamu kuishi vizuri na wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, huwadharau watu wa kwenye familia yake kana kwamba siyo watu kwa sababu ya majivuno na dharau zake hizo, maishani mwake. Yeye huiharibu kwa kuisambatisha familia yake kwa sababu ya majivuno yake hayo ya kuwakaripia hovyo wenzake, katika maisha yake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyejifananisha na Simba, kwa sababu naye huisambaratisha familia yake kwa kuwakaripia hovyo wenzake kana kwamba siyo binadamu, katika maisha yake hayo. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “manyoya hayaoti kwa mtu ila kwa wanyama tu.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kufahamu namna ya kuishi vizuri na wenzao kwa kuacha kuwakaripia hovyo, ili waweze kuziendeleza vizuri familia zao, maishani mwao.

Mwanzo 1:24-26.

ENGLISH: FEATHERS DO NOT GROW ON HUMAN BEINGS BUT ONLY ON ANIMALS.

There was a man who said that he had feathers. This man was likening himself to animals like lions because he did not know the difference between man and animals. But then, animals have feathers but human beings do not. That is why people told him that, “feathers do not grow on human beings but only on animals.”

This proverb is equaled to a person who does not know how to live well with his colleagues, in his life. Such person despises people who live in his family as if they are not human beings because of his pride and contempt in his life. He destroys his family by disuniting its members because of his pride in reprimanding his colleagues carelessly in his life.

This person is similar to the one who compared himself to a lion, because he also destroys his family by scolding his colleagues carelessly as if they are not human beings in his life. That is why people tell him that, “feathers do not grow on human beings but only on animals.”

This proverb teaches people to know how to live well with their family members by stopping scolding them carelessly, so that they can develop their families well in their lives.

Genesis 1:24-26.

woman-1320103_1280