Imbuki ya kahayile kenako ihoyelile linzwi ilo ligakulaga bho guja hasi mpaga lyabhiza na matambi agagulidimila ilinti ilitale ilo lilina matambi galyo. Ilinzwi linilo ligabhizaga na nguzu ja gudula gugudimila unti intale pye na matambi gago kunguno ya bhujamu bholyo. Hunagwene abhanhu bhagalitanaga giki, “linzwi lilina matambi.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo atolile mpaga upandika bhana bhingi, bhizukuru na bhizimbili bhakwe, umuwikaji bhokwe bhunubho. Umunhu ung’wunuyo agayilelaga chiza ikaya yakwe bho guilanga gutumama milimo ya gubhapandikila matwajo gaguyilanhanila chiza ikaya yiniyo kunguno ya witegelecha bhokwe bhunubho, umukikalile kakwe kenako. Uweyi agapandikaga matwajo mingi noyi akaya yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho ubho guyilela chiza ikaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga ni linzwi ilo lilina matambi ga gugudimila unti na matambi gago, kunguno nu weyi alina nanguzu na witegeleja bhutale ubho guyilela na guyilanhana chiza ikaya yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe bhunubho. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “linzwi lilina matambi.”
Akahayile kenako kalanga bhitoji higulya ya gubhiza na witegeleja bho gujilela chiza ikaya jabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umukaya jabho jinijo, umuwikaji bhobho.
Mwanzo 17:7.
2 Samweli 5:12.
Yohana 15:1-9.
KISWAHILI: MZIZI WENYE MATAWI.
Chanzo cha msemo huo huongelea juu ya mzizi unaokua kwa kwenda chini ya ardhi mpaka unapata matawi ya kuweza kuushikiria mti mkubwa wenye matawi. Mzizi huo huwa na nguvu za kuweza kuushikiria mti mkubwa wenye matawi yake kwa sababu ya uimara wake huo. Ndiyo maana watu huuita jina la “mzizi wenye matawi.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule aliyeoa akapata watoto wengi, wajukuu na vilembe, katika maisha yake. Mtu huyo, huilea vyema familia yake hiyo kwa kuifundisha kufanya kazi za kuwapatia mahitaji ya kutosha kutumia kwa sababu ya uaminifu wake huo maishani mwake. Yeye hupata mafanikio mengi sana kwenye familia yake kwa sababu ya uaminifu wake huo wa kuilea vyema familia hiyo, maishani mwake.
Mtu huyo hufanana na ule mzizi wenye matawi ya kuushikiria mti wenye matawi, kwa sababu naye ana nguvu na uaminifu wa kuilinda vyema familia yake hiyo, maishani mwake. Ndiyo maana watu humuita jina la “mzizi wenye matawi.”
Msemo huo hufundisha wana ndoa juu ya kuwa na uaminifu wa kuzilea vyema familia zao, ili waweze kupata maendeleo mengi katika familia zao, maishani mwao.
Mwanzo 17:7.
2 Samweli 5:12.
Yohana 15:1-9.


