1170. YAPYAGA INDULU.

Ulusumo lunulo, luhoyelile higulya ya ndulu iyo yapyaga. Indulu yiniyo igikalaga munda ya mitugo nulu ndimu iyo agailujaga inyama yayo ulu yutinikila mumho mugati ahikanza ilya guibhaga inyama yiniyo. Iyoyi igaikenagulaga chiniko inyama ya ndugo gunuyo ulu yubhagwa bho nduhu witegeleja. Hunagwene abhanhu bhagayombaga giki, “yapyaga indulu.”

Ulusumo lunulo, lugalenganijiyagwa kuli munhu uyo agapelanaga bho nduhu uguyangulwa nulu okenyiyagwa hadoo duhu, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agapelanaga wangu nulu ukenyiyagwa bho kamhayo kadoo duhu, kunguno ya bhukali bhokwe bhunubho. Uweyi agabhakoyaga abhanhu bha ha kaya yakwe kunguno ya gulema guyangulwa bhuli makanza ulu upelanaga, umuwikaji bhokwe.

Umunhu ng’wunuyo, agikolaga ni ndulu iyo igakumiyaga hadoo duhu yatanduka mpaga yayiluja pye inyama, kunguno nuweyi agakenyiyagwa hadoo duhu opelana mpaga olema uguyangulwa umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’wilaga giki, “yapyaga indulu.”

Ulusumo lunulo, lolanga bhanhu higulya ya kuleka upelanu bho gulema guyangulya ulu bhakenyiyagwa nulu hadoo duhu, kugiki bhadule gujilela chiza ikaya jabho, umuwikaji bhobho.

Luka 19:45-48.

Luka 22:47-50.

Luka 14:21.

KISWAHILI: NYONGO IMEIVA.

Methali hiyo, huongelea juu ya nyongo iliyoiva. Nyongo hiyo, hupatikana tumboni mwa mifugo ambayo hufanya nyama iwe chungu endapo itapasukia ndani wakati wa kumchuna huyo mnyama. Yenyewe huiharibu hivyo hiyo nyama yote, asipokuwa na uangalifu mchunaji wa mnyama huyo. Ndiyo maana watu husema kwamba, “nyongo imeiva.”

Methali hiyo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hukasirika upesi mpaka kufikia hatua ya kukataa kuamriwa hata anapokesowa kwa jambo dogo tu, katika maisha yake. Mtu huyo, hukasirishwa haraka na hata kwa jambo dogo tu, na kukataa kuamriwa kwa sababu ya hasira yake hiyo. Yeye huwahangaisha watu wa kwenye familia yake hiyo, kwa sababu ya ukali wake huo wa kukataa kuamriwa na wenzake, maishani mwake.

Mtu huyo, hufanana na ile nyongo ambayo huguswa kidogo na kupasuka mpaka inaiharibu nyama yote, kwa sababu naye hukasirishwa hata na jambo dogo tu, na kukataa kuamriwa, katika maisha yake. Ndiyo maana watu humwambia kwamba, “nyongo imeiva.”

Methali hiyo, hufundisha watu juu ya kuacha hasira ya kukasirika upesi kwa sababu ya jambo dogo tu na kukataa kuamriwa, ili waweze kuzilea vizuri familia zao, maishani mwao.

Luka 19:45-48.

Luka 22:47-50.

Luka 14:21.

ENGLISH: THE GALL IS RIPE.

This proverb speaks of a ripen gall. The gall is found in a stomach of livestock, which makes the meat bitter if it bursts inside while slaughtering the animal. It itself destroys all the meat, if the slaughterer of such animal is not so careful. That is why people say that, “the gall is ripe.”

This proverb is compared to the person who gets angry quickly to the point of refusing to be ordered even when he is wronged in a small thing, in his life. Such person, gets angry quickly and even in a small thing that he refuses to be ordered because of his anger. He worries the people in his family, because of his harshness in refusing to be ordered by his colleagues, in his life.

This person is like the gall that is touched a little and bursts until it destroys all the meat, because he also gets angry even in a small thing to the point of refusing to be ordered, in his life. That is why people speak about him that, “the gall is ripe.”

This proverb teaches people about stopping getting angry quickly because of a small thing to the point of refusing to be ordered by others, so that they can raise their families well, in their lives.

Luke 19:45-48.

Luke 22:47-50.

Luke 14:21.

 

 

stick-fight-412666__480

One comment

  1. Ni kweli kabisa, kilichoandikwa katika methali hii kina mafunzo mazuri sana hasa kwa jamii zetu za sasa hivi.

    Like

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.