Ugwisengekela ili gubhucha nulu guzega michimu na masonga. Amachimu jili jilanga ja guchimila. Amasonga gali jilanga ja gulasila ginhu nulu bhanishi bho gutumila bhuta.
Ulihoyi munhu uyo agazega jilanga jakwe kunguno ojaga gujitula na bhanishi bhakwe. Hunagwene abhanhu obhawilaga giki, “nisengekelaga machimu na masonga.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agasolaga jilanga ja gutumamila milimo yakwe chiza umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo agikalaga higiki bhuli makanza bho gutumamila jilanga jawiza umumilimo yakwe kunguno ya witegeleja bhokwe bhunubho. Uweyi agapandikaga sabho ningi umubhutumami bhokwe kunguno ya gutumila jilanga ja wiza umumilimo yakwe yiniyo, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agabhucha machimu na masonga aho ajile kubhulugu, kunguno nuweyi agasolaga jitumamilo jawiza umubhutumami bhokwe. Hunagwene agayombaga giki, “nisengekelaga machimu na masonga.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gutumamila jilanga jawiza umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.
Luka 14:31.
KISWAHILI: NIMEBEBA MIKUKI NA MISHALE.
Mikuki ni silaha za kuchomea kitu fulani. Mishale nazo ni silaha za kuchomea kitu au adui kwa kutumia upinde. Alikuwepo mtu aliyebeba silaha zake hizo kwenda kupigana na adui zake. Ndiyo maana aliwaambia watu kwamba, “nimebeba mikuki na mishale.”
Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hubeba silaha nzuri za kufanyia kazi zake katika maisha yake. Mtu huyo, huwa tayari kila wakati kwa kubeba na kutumia silaha zitakiwazo katika utekelezaji wa majukumu yakwe, kwa sababu ya umakini wake huo. Yeye hupata mafanikio mengi katika kazi zake kwa sababu ya kutumia silaha nzuri katika kazi zake hizo, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na yule mtu aliyebeba mikuki na mishale alipokuwa akienda vitani, kwa sababu naye huchukua zana nzuri za kufanyia kazi zake, katika utekelezaji wa majukumu yake. Ndiyo maana yeye huwaambia watu kwamba, “nimebeba mikuki na mishale.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kutumia silaha nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kupata mafanikio mengi, maishani mwao.
Luka 14:31.
ENGLISH: I HAVE CARRIED SPEARS AND ARROWS.
Spears are weapons for chopping something. Arrows are also weapons for slicing something or an enemy by using a bow. There was a man who carried his weapons in fighting against his enemies. That is why he told the people that, “I have carried spears and arrows.”
This saying is compared to a person who carries good weapons enough to do his works in his life. Such person is always ready to carry and use the necessary weapons in the execution of his duties, because of his attention. He gets a lot of successes in his works because of using good weapons in fulfilling his daily responsibilities.
This person resembles to the person who carried spears and arrows when he was going to war, because he also takes good tools for doing well his works in fulfilling his duties. That is why he tells people that, “I have carried spears and arrows.”
This saying teaches people about using good weapons in the execution of their duties, so that they can get a lot of successes in their families.
Luke 14:31.
