Akahayile kenako kahoyelile bhululu bho nshishi. Imishishi ili habhili, iyingi ili mipolo alii yingi igikalaga milulu. Abhanhu ulu bhuja gujuyotona bhushishi bhagabhonjaga tamu kugiki bhadule guyidebha imishishi iminonu na guyiyob’a lulu. Aliyo lulu ulu bhuyibhona giki ili milulu bhagalekaga ugubhutona ubhushishi bhunubho kunguno ya ubhululu bhogo bhunubho. Hunagwene bhagwitanaga unshishi gunuyo giki, “nshishi nulu.”
Akahayile kenako kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo obhalemela abhiye kunguno ya nhinda jakwe umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agikalaga abhatab’anije abhiye umunhungwa jakwe kunguno ya nhani ya kashokeje kakwe ukubhiye. Uweyi agadumaga ugwikala chiza na bhanhu kunguno ya bhulambu na libhengwe lwakwe linilo ukubhiye, umuwikaji bhokwe.
Umunhu ng’wunuyo agikolaga nu nshishi unulu uyo gubhalemelile abhanhu ugubhung’wa ubhushishi bhogo, kunguno nuweyi abhalemelile abhiye umukikalile kakwe. Hunagwene abhanhu bhagang’witanaga giki, “nshishi nulu.”
Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya guleka nhungwa ja bhulambu, na nhani umubhutumami bho milimo yabho, kugiki bhadule gwikala chiza na bhichabho umukaya jabho.
Warumi 13: 10.
Mathayo 5:43-45.
KISWAHILI: MCHAJU MCHUNGU.
Msemo huo, huongelea uchungu wa mkwaju. Mikwaji iko katika aina mbili, mingine ni mtamu lakini mingine ni michungu. Watu wakitaka kuchuma ukwaju huuonja kwanza ili waweze kufahamu kama ule mti ni mtamu kwa ajili ya kuyachuma matunda yake. Lakini watu hao wakionja na kuona kwamba ule mkwaju ni mchungu, huacha kuyachuma matunda ya mti huo. Ndiyo maana watu hao huuita mti huo kuwa ni “mkwaju mchungu.”
Msemo huo hulinganishwa kwa mtu yule ambaye ameshindikana kwa wenzake kwa sababu ya kiburi chake katika maisha yake. Mtu huyo, hukataa kutungwa na wenzake kwa sababu ya kiburi chake hicho, katika utekelezaji wa kazi zake. Yeye hushindwa kuishi na watu kwa sababu ya dharau zake hizo kwa wenzake, maishani mwake.
Mtu huyo, hufanana na ule mkwaju mchungu uliowashinda watu kuyatumia matunda yake, kwa sababu naye ana kiburi cha kukataa kutumwa na wenzake katika maisha yake. Ndiyo maana watu humuita kwamba ni “mkwaju mchungu.”
Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuachana na kiburi na dharau katika utekelezaji wa majukumu yao, ili waweze kuishi vizuri na wenzao katika familia zao.
Warumi 13: 10.
Mathayo 5: 43-45.

ENGLISH: BITTER TAMERAND.
The overhead saying speaks about a bitterness of tamerand tree. There are two types of tamerand tree namely, the sweet one and bitter one. If people want to pick the nectar, they taste it first so that they can know if it is sweet for picking its fruit or not. But when they taste and see that its fruits are bitter, they stop picking them. That is why these people call it a “bitter tamerand.”
This saying is equated to a person who has become an impossible to his colleagues because of his pride in his life. This person refuses to help his colleagues because of his pride, in the implementation of his tasks. He fails to live peacefully with people because of his contempt for his colleagues, in his life.
This person resembles the bitter tamerand that people could not eat its fruits, because he also has pride that cause him to refuse to help his colleagues in his life. That is why people call him a “bitter tamerand.”
This saying imparts in people an idea of abandon pride and contempt in performing their duties, so that they can live well with their societal members in their families.
Romans 13:10.
Matthew 5: 43-45.