1114. NAHINJAGA NIGUNAGI.

Olihoyi munhu uyo ukilaga mongo umuchalo ja Ng’watuma. Umunhu ng’wunuyo wiganikaga giki agudula ugugukila umongo gunuyo kunguno ya bhumani bho guhega bhokwe. Ohaimanila goyunhebha umongo gunuyo mpaga nose uyulomba bhanhu bhanguhe hoyi gung’wambilija, kunguno gugayumaja inguzu jakwe. Hunagwene agayomba giki, “nahinjaga nigunagi.”

Akahayile kenako, kagalenganijiyagwa kuli munhu uyo agitulaga bhumani bho bhuli mhayo bho gubhadalaha abhiye, umukikalile kakwe. Umunhu ng’wunuyo, agiganikaga giki alina masala mingi gulebha abhiye kunguno ya libhengwe lyakwe linilo. Uweyi apandikaga makoye ga gumala jiliwa aha ng’wake henaho, kunguno ya gubhadalaha abhanhu abho bhadulile gung’wambilija umuwikaji bhokwe bhunubho.

Umunhu ng’wunuyo agikolaga nuyo agagudalaha umongo uyo gugahaya gunjana gunuyo, kunguno nuweyi agabhadalahaga abhiye abho bhadulile gung’wambilija mpaga olemelwa na wandwa gubhitana giki bhang’wambilije. Hunagwene agayombaga giki, “Nahinjaga nigunagi.”

Akahayile kenako kalanga bhanhu higulya ya gubhiza nikujo ukubhanhu bho kuleka gubhabyeda abhiye, kugiki bhuli ng’wene adule ugubhushigila uwitanwa bhokwe, kugiki bhadule gupandika matwajo mingi umuwikaji bhobho.

Zaburi 69:1-5.

Luka 1: 68 – 71.

Zaburi 77:2-4.

 

KISWAHILI: NIMEZIDIWA NISAIDIENI.

Alikuwepo mtu mmoja aliyekuwa akivuka mto kwenye kijiji cha Mwatuma. Mtu huyo, alikuwa akifikiri kwamba angeweza kuuvuka mto huo kwa sababu ya utalaam wake wa kuogelea. Alishtukia ule mto ukaanza kumzidi nguvu mpata mwishowe alilazimika kuomba msaada kutoka kwa watu wengine kwa sababu ya yeye kuanza kuishiwa nguvu.  Ndiyo maana alisema kwamba, “nimezidiwa nisaidieni.”

Msemo huo, hulinganishwa kwa mtu yule ambaye hujidai kujua kila kitu kwa kuwadharau wenzake, katika maisha yake. Mtu huyo, hujifikiria kwamba ana akili nyingi kuliko wenzake wote kwa sababu ya dharau yake hiyo kwa watu. Yeye hupata matatizo ya kuishiwa chakula kwenye familia yake, kwa sababu ya kuwadharau watu wale ambao wangemsaidia, katika maisha hake.

Mtu huyo, hufanana na yule aliyetaka kuvuka mto uliotaka kumpeleka mpata akasaidiwa na watu, kwa sababu naye huwadharau wenzake ambao wanaweza kumsaidia katika maisha yake. Ndiyo maana yeye husema kwamba, “nimezidiwa nisaidieni.”

Msemo huo, hufundisha watu juu ya kuwa na heshima kwa watu kwa kuachana na dharau kwa wenzao, ili kila mmoja aweze kuufikia wito wake, na kupata mafanikio mengi, katika maisha yake.

Zaburi 69:1-5.

Luka 1: 68 – 71.

Zaburi 77:2-4.

 

ENGLISH: I HAVE BEEN OVERWHELMED, HELP ME.

There was a man who was crossing the river in the village of Mwatuma. He thought that he could manage crossing it because of his swimming skills. He was shocked that the river started to overpower him until he finally had to ask for help from other people because he started losing his strength. That is why he said, “I have been overwhelmed, help me.”

This saying is equated to a person who claims to know everything by despising his colleagues, in his life. Such person thinks that he is more intelligent than all his nobles because of his contempt to them. He experiences problems of running out of food in his family, because of despising the people who could help him, in his life.

This person resembles the one who wanted to cross the river that overhelmed him until he got help from people, because he also despises his colleagues who can help him in his life. That is why he says, “I have been overwhelmed, help me.”

This saying teaches people about having respect to people by stopping despising them, so that they can get a lot of successes in their lives.

Psalm 69:1-5.

Luke 1: 68 – 71.

Psalm 77:2-4.

 

river-trading-4215417__480

elephants-250663__480

boat-1982943__480

Leave a comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.